CCM Simiyu inakaaje kimya?

CCM Simiyu inakaaje kimya?

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
150
Reaction score
148
Inazua maswali kuona viongozi wa chama wakitukanwa kwenye baadhi ya makundi ya WhatsApp yanayodaiwa kuhusisha wanachama, huku kukiwa hakuna hatua za wazi za kinidhamu zinazoonekana kuchukuliwa.

Je, ukimya huo unatokana na tahadhari kuelekea uchaguzi wa ndani wa chama mwakani, au ni dalili ya changamoto za umoja na mshikamano ndani ya uongozi?

Wanachama wengi wanaamini kuwa nidhamu ndiyo msingi wa uhai wa chama chochote cha siasa. Endapo viongozi wa chama, wakiwemo Mwenyekiti wa Mkoa, Mwenyekiti wa Wilaya au wabunge, wanashambuliwa kwa lugha za matusi na uongozi hauonekani kuchukua hatua, ni kawaida wananchi kuhoji kama kanuni za chama zinatumika kwa usawa.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba makosa ya watu binafsi hayapaswi kutafsiriwa kuwa ndiyo taswira ya taasisi nzima. Kama ilivyo msemo usemao, udhaifu wa mchungaji si udhaifu wa Ukristo, na udhaifu wa Imamu si udhaifu wa Uislamu. Vivyo hivyo, makosa ya baadhi ya wanachama hayapaswi kuwa kipimo cha chama kizima.

Kinachotarajiwa ni uongozi kutoa msimamo unaolinda heshima ya chama, kuimarisha nidhamu na kuonyesha kuwa tofauti za maoni zinaweza kujadiliwa kwa ustaarabu bila matusi au kejeli.
 
Huo ni mgogoro mzuri na wenye afya kwani unakwenda kumaliza zile zama za uungumtu huko ccm! Bamizaneni kibabeli mpaka kila mmoja wenu anene kwa lugha ili ile lugha iliyozoeleka ya wananchi wangu ifutike!
 
Back
Top Bottom