The way how I know Mr. Zitto Kabwe

Kila mtu ana nafasi yake na uwezo wake. Sidhani kama mleta huu uzi alimaanisha kutafuta mshindi. Anyways, hawa wote ni viongozi wetu, kwa hiyo tuwapendeni wote, utakapofika wakati wa kuwachagua kuwapa madaraka fulani fulani, tutaamua nani akae wapi. Ikumbukwe sisi wapiga kura ndo tuna nguvu ya kuamua nani akae wapi kupitia taratibu na chaguzi zetu ndani ya chama.
Huyu ameja kutuchagulia mshindi!!which is hogwash.
 
Mkuu SG8, hii kauli imenistua kidogo!, unamaanisha wale watakaosababisha CCM ishinde tena, Watanzania hatuta wasamehe?, hao watakaipa ushindi hiyo CCM jee watakuwa ni kina nani?.

Wakati tukijiandaa kutowasamehe watakaosababisha CCM ishinde mwaka 2015, jee tutawafanya nini hawa ambao tangu leo wanatamka wazi kuwa ili Chadema ishinde 2015, ni lazima ifanye a,b,c,na d!, na kutoa angalizo, isipofanya hivyo , 2015 ni CCM tena!. Mpaka sasa, Chadema bado haijafanya, wala haijaonyesha kufanya!. Ikitokea ni kweli 2015, CCM ikashinda tena kwa sababu Chadema haikufanya a,b,c,na d, itamaanisha, waliofanya CCM ishinde tena 2015 ni Chadema, jee hao nakuuliza mkuu SG8, jee mtawafanya nini hawa Chadema wataosababisha CCM ishinde tena 2015?.

By the way nimelipenda sana lile jina la utangulizi la rais wa ...Ford wa Marekani, just curious what does "S" stand for?.

P.

Mkuu Pasco,
Nimependa uchambuzi wako murua.
 
Last edited by a moderator:
Busara busara, uzee uzee, kijana kijana, udini mdini, sisi tunahitaji mtu kwa sifa za kuwa kiongozi bora na mwenye kupenda mapinduzi ya kweli na si sifa za kijinga! Yangu macho na masikio, 2015 Mungu niweke hai! Inshallah!
 
zitto kabwe ni mtaji ndani ya ccm, chaumma na adc wanatumika.wamepewa fungu kubwa kumaliza kabisa nguvu za upinzani nchini adc wanadili kuidhoofisha cuf na chaumma kudhoofisha nccr na chadema. Alama zao za bendera zinajieleza zitto anafanya kazi maalumu kutangaza nia ni njia sahihi kuimaliza chadema ili asipopitishwa kugombea ataasi chama na kujiunga chaumma mchange atamtangulia na atawaambia wananchi wamenikata kwa sbbu si wa kaskazini na kwa sbbu ya uislamu wake.

nina uhakika asilimia mia atagombea urais 2015 lakini sio kupitia chadema na wala sio kwa nia yake bali matakwa ya ccm na atapewa nafasi ya uwaziri ndani ya serikali ya ccm. jiulize urais anaoutaka zitto bila kushiriki kukipeleka chama mashinani ni upi.
 
maneno ni jambo lingine na matendo ni jambo lingine, pamoja na kwamba mtu hupimwa pia kwa maneno/busara aliyonayo- hayo hayakamilishi ubora wa mtu. kuna watu ni hodari mno katika kupanga maneno, lakini njoo kwenye vitendo, anayoongea na anayotenda havishabihiani. mmesahau kampeni za 2005? tuliweweseka watu wanatoa ahadi kem kem, ''mkinichagua, nitarudisha nyumba za serikali zilizomilikishwa kwa watu binafsi, bla bla kibao na yale maneno yalituvuta wengi, tukasema tumepata mkombozi. haya ameingia amefanya nini, sana sana pengine naye kachukua si moja zaidi ya hiyo moja.
kwa hiyo mkimsifu mtu kwa kuongea kwake, mbona hiyo ni fani ya watu wengine,speech tu! utashindwa wewe. tujaribu pia kuwa na sababu za msingi -kwa nini huyu anafaa na kwa nini yule hafai
 
Sasa mleta mada mbona umeishia kutoa mtazamo wako badala ya kutueleza unavyomfahamu?
 
Tukifika siku ya kutafuta mgombea wa Uraisi tutawatathimini sasa tunatathimi anayejenga Chama kwanza. Swala la kuongea na kutenda ni vitu viwili tofauti sana, ukisoma yale makarabrashia ya maprofesa wetu ni mazuri sana utendaji ndio unatupashida. Duniani watu hawawezi kufanana na kulingana kwa kila kitu.

Ndani ya Chadema viongozi wetu wote wana input na tunaziheshimu sana kazi zao kwani kila aliyefanya kwa moyo wa kuwasaidia watanzania na chama tutamwenzi. Waacheni wafanye kazi ya kujenga chama msiwatoe kwenye hilo kwa sasa na wale wanaofanya kampeni za uraisi waacheni wafanye msiwatoe kwenye hilo na wale wanaounganisha watanzania waacheni wafanye na wale wanaovuruga chama vile vile waacheni, Acheni ngano na magugu viote pamoja ili wakati wa palizi usije ukachanganya ukang'oa ngano badala ya magugu.

Busara za Chief Mkwawa wa kalenga
Hawawezi kutulia kama maji mtungini vilevile hawawezi kuvunja mtungi kwani kama wana akili wanajua wanauhitaji sana mtungi ili kuweza kuishi humo ndani. Kuna wakati joto linazidi na baridi inazidi vyote ni vipindi wao wanaita Demokrasia.

Well done Mkwawa, imejitosheleza
 
Last edited by a moderator:
Haswa mkuuu. Wanaotaka urais wajitokeze mapema tuwafahamu. Tuanze kuwasoma na kuwapima taratibu siyo ati wanajificha na kusema mchakato bado. Ukiwa umebaki mwezi mmoja ndio wanajitokeza matokeo yake tunaweza kuchagua mtu asiyefaa kwa kuwa tu katufanyia surprise. Eti ukijitokeza unahatarisha mshikamano ndani ya chama! Ina maana watu ndani ya chama hawajui kwamba kuna urais 2015? Hii ni akili ya mbuni kuficha kichwa kwenye mchanga wakati mwili mzima upo hadharani.
mkuu leo umefikiri kwa kutumia masaburi,.jk amefukuzia urais tokea 1995 na kila mtu alilijua hilo na wakamchagua kwa kishindo,lakini chini ya miezi 6 aliiharibu nchi beyond repair!!!!miaka yote mitatu unataka kumjua mtu kuhusu mambo gani?miezi mitatu ya kampeni inatosha kuchimba habari za mtu na kumfahamu vizuri...labda wewe hiyo miaka mitatu unataka kujua kama mgombea aliendelea kukojoa kitandani hadi miaka mingapi!!!!
 
Yaani maara hii Mbowe amekuwa Mzee? Ndio maana wenye busara wanasema kutangaza nia ya kugombea Urais sasa ni kutengeneza makundi ndani ya Chama. Leo Habib Mchange kaandika makala ndefu sana kwenye gazeti la Raia Mwema akimnadi na kumtetea Zitto, Kitila Mkumbo naye katoa msimamo wake (sijui kama amemtetea pia au la) na baadae Mchange kamnukuu Kitila Mkumbo na kuweka kwenye ukurasa wake wa facebook. Haikuishia hapo ZZK naye kaandika kuwajibu kwa pamoja Mayage S. Mayage, Mbwambo na Chahali akilalamika kwamba makala tatu za toleo lililopita zilimlenga yeye. Bahati mbaya leo makala tatu pia kwenye gazeti hilo hilo leo zimmtetea yeye....Makundi!!!! Zitto kama binadamu na kama Mwanasiasa aneweza kuwa na nia dhabiti ya kusukuma mbele gurudumu la mabadiliko lakini hofu yangu ni wafuasi wake. Wapo wanaodhani Zitto lazima awe Rais kupitia Chadema jua liwake mvua inyeshe. Hawa ni hatari kuliko ukoma na watanzania hatutawasamehe wakisababisha CCM ishinde mwaka 2015

Ni jambo la kusikitisha kiongozi wa ngazi ya juu kutoa taarifa ambazo zinalenga kukudhoofisha chama. Japo ana haki ya kugombea lakini si wakati muafaka kutoa hilo tamko. Busara za Mbowe ni hazina kubwa ya CHADEMA.
 
Hapo kwenye bluu, maadui wa kweli wa rafiki yangu Zitto anao mabegani mwake mwenye hivi sasa wakimtembeza jina kila mahala kama karanga lakini wakitumia mbinu chukizo kweli kweli tena zile za miaka ya 47.

Yaani maara hii Mbowe amekuwa Mzee?

Ndio maana wenye busara wanasema kutangaza nia ya kugombea Urais sasa ni kutengeneza makundi ndani ya Chama. Leo Habib Mchange kaandika makala ndefu sana kwenye gazeti la Raia Mwema akimnadi na kumtetea Zitto, Kitila Mkumbo naye katoa msimamo wake (sijui kama amemtetea pia au la) na baadae Mchange kamnukuu Kitila Mkumbo na kuweka kwenye ukurasa wake wa facebook. Haikuishia hapo ZZK naye kaandika kuwajibu kwa pamoja Mayage S. Mayage, Mbwambo na Chahali akilalamika kwamba makala tatu za toleo lililopita zilimlenga yeye. Bahati mbaya leo makala tatu pia kwenye gazeti hilo hilo leo zimmtetea yeye....Makundi!!!! Zitto kama binadamu na kama Mwanasiasa aneweza kuwa na nia dhabiti ya kusukuma mbele gurudumu la mabadiliko lakini hofu yangu ni wafuasi wake. Wapo wanaodhani Zitto lazima awe Rais kupitia Chadema jua liwake mvua inyeshe. Hawa ni hatari kuliko ukoma na watanzania hatutawasamehe wakisababisha CCM ishinde mwaka 2015
 
  • Thanks
Reactions: SG8
hivi Habib Mchange mbona huwa hampendi Dr.Slaa?[/QUOTE
Si unajua Dr Slaa na rushwa ni mbingu na nchi? Sasa dogo alitembeza MPESA halafu Mzee akamuumbua na kumfutilia mbali. Hili nadhani dogo hatasahau maisha yake yote na si ajabu akigombea tena Slaa Urais dogo na watu wake watapigia kura CCM
 
Mkuu SG8, hii kauli imenistua kidogo!, unamaanisha wale watakaosababisha CCM ishinde tena, Watanzania hatuta wasamehe?, hao watakaipa ushindi hiyo CCM jee watakuwa ni kina nani?.

Wakati tukijiandaa kutowasamehe watakaosababisha CCM ishinde mwaka 2015, jee tutawafanya nini hawa ambao tangu leo wanatamka wazi kuwa ili Chadema ishinde 2015, ni lazima ifanye a,b,c,na d!, na kutoa angalizo, isipofanya hivyo , 2015 ni CCM tena!. Mpaka sasa, Chadema bado haijafanya, wala haijaonyesha kufanya!. Ikitokea ni kweli 2015, CCM ikashinda tena kwa sababu Chadema haikufanya a,b,c,na d, itamaanisha, waliofanya CCM ishinde tena 2015 ni Chadema, jee hao nakuuliza mkuu SG8, jee mtawafanya nini hawa Chadema wataosababisha CCM ishinde tena 2015?.

By the way nimelipenda sana lile jina la utangulizi la rais wa ...Ford wa Marekani, just curious what does "S" stand for?.

P.
Ha ha ha Mkuu Pasco,
heshima yako. Leo nimerudi kutoka kwa ofisi nikiwa hoi sana, niwie radhi kwamba leo sitajibu hoja zako (Naamini ni hoja nzito) lakini S kwenye SG8 inasimama badala ya jina langu la kwanza, tehe, tehe!!! Usiku mwema
 
Last edited by a moderator:
labda mambo ya uzinzi wa padri,huwezi jua bana!!!!!!!!
Ha ha ha hapa ndio ulipoishia katika kufikiri kwako? Kama ndivyo basi nchi yetu ina safari ndefu sana...Baada ya ushirikina kinachofuata kwenye akili ya Mtanzania ni Uzinzi yaani ngono... Tutasubiri miaka mia kupata mabadiliko ya kweli lukatony
 
Last edited by a moderator:
nia si kitendo, wala kitendo siyo pato, na si kila pato ni faida.Mwambieni ZZKna mwingine mwenye nia maneno haya machache tu.mengi hatafuatilia!
 
Wewe Joshua Bukuru ndio umeahidiwa ukuu wa wilaya na huyo Zitto au ubunge wa kuteuliwa?
Hatutaki majanga sie janga JK tumejifunza haturudii makosa tena.. Kama mchukueni agombee urais wa LEKA DUTIGITE
 
Last edited by a moderator:
Unajua ni lazima tujifunze vizuri kelewa nini maana ya demokrasia, haiwezekani katika demokrasia ya kweli watu wasitoe mawazo yao au mitizamo yao hasa juu ya kauli mbalimbali kuhusu mustakabali wa taifa letu kwani huo ni UPUUZI. Sioni tatizo watu kuwa na mawazo tofauti juu ya kauli ya ZITTO kuhusu kugombea uraisi wa nchi hii kiasi kwamba kila kukicha watu kutumia muda wenu sijui ni kwa utashi binafsi au kwa kutumwa kuanza kujibu hoja ambazo haziwahusu. Maoni yote yanayotolewa na watu ndio kipimo cha kuona kama kweli ZITTO akisimamishwa na CDM ataleta mabadiliko katika nchi hii ambao kwa sasa ina changamoto kubwa sana. Mtoa mada umejitahidi sana kufanya uchambuzi wako ambao ki msingi nauheshimu sana kwan pia ni mtazamo wako juu ya ZITTO ingawa sikupenda sana zako za ingawa mimi ni wa Kigoma lakini simfahamu ZITTO kiasi kwamba naanza kupata mashaka na wewe hasa kwenye suala la ukabila. Nashukuru sana mpaka sasa viongozi wa chama hawajaingilia hili hasa hii kauli ya mwenzetu kuhusu suala la Uraisi ingawa kuna watu wa OVYO OVYO kama hawa ambao kazi yao ni kuchochea mjadala wa ZITTO tena kwa maana ya kumpambapamba tu tena kwa mambo ambayo ni ya kawaida kwa kulinganisha na nafasi ya Uraisi ili tu ikija kutokea kama akashindwa kupitishwa na Chama kwa sababu ya kutokidhi mahitaji ya chama na ya watanzania ionekane kama ameonewa. Chama kina taratibu zake na vigezo vyake vyenye kuzingatia tafiti, mazingira, aina ya siasa na uhitaji wa watanzania na si kuangalia tu eti ujana na vigezo vingine vya ovyo ovyo ambavyo havilingani na nafasi ya uraisi. Nakumbuko kauli za mara kwa mara za huyu kijana kama "uwezona sifa wa kuwa amiri jeshi mkuu ninao" alivyokuwa anazungumza siku fulani pale bungeni nilimuondoa kabisa katika mawazo yangu na nafasi anayozungumzia, kwanza alikuwa anaongea kwa JEURI, KIBRI na kama vile anawaambia watu fulani anaopigana nao vikumbo katika kuhangaikia nafasi hii. ZITTO babo hana sifa za kuwa Raisi wa nchi hii na kama CDM ikisubutu kumsimamisha wasahau habari ya uraisi. Huyu kijana CCM wameshamteka tayari na skendo zake mbovu ambazo CCM wanamshirikisha wanazo tena kwa evidence na ndio ngao yao ya kuishindwa CDM 2015
 
time for Operation sangara.

tuna kampeni za uchaguzi all over Tanzania,kindly can you bring the same kind of topics??????

Tumewasikia,tumewaelewa.Basi tupambane kumuandalia mazingira.otherwise hata hizo ndoto zenu zitakuwa za alinacha.

Greetings.
 
time for Operation sangara.

tuna kampeni za uchaguzi all over Tanzania,kindly can you bring the same kind of topics??????

Tumewasikia,tumewaelewa.Basi tupambane kumuandalia mazingira.otherwise hata hizo ndoto zenu zitakuwa za alinacha.

Greetings.

hellow firstlady in making!
 
Back
Top Bottom