Sam GM
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 535
- 30
Leo katika taarifa ya jioni ya BBC wametangaza kuwa mahakama ya kimataifa ya the Hague iko mbioni kutoa warrant ya kumkamata rais wa Sudan bwana Bashir kutokana na uhalifu na maovu juu ya binadamu katika eneo la Darfur na maeneo mengine ya Sudan. Pamoja na kuwa uovu mwingi umefanyika Darfur na bado watu wanaendelea kufa, wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanafikiria itakuwa vigumu sana kumkamata bwana Bashir, nani kwanza anayeweza kumkamata? pili viongozi wa Afrika wanaweza wasikubali kuona mwenzao anakamatwa na kuburuzwa mahakamani, kwa kuhofia kuwa wakiruhusu na wao pia wanaweza kamatwa siku moja.
Pia kuna wale wanaofikia kuwa mahakama ina double standards, kwa sababu watu kama Bush ndio walitakiwa wafikishwe The Hague kwanza! Swali ni kwamba kwa kumkamata Mr Bashir na kumuacha George Bush mahakama inakuwa fair?