Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 297
Wakuu hebu tuliangalie bara letu kwa mapana kidogo.
Bwan Al BASHIR, Rais wa Sudan, leo ameshtakiwa Rasmi kama "war criminal" na mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa (ICC) ya The Hague bwana Luis Moreno Ocampo.
Kifupi kama majaji wataridhia hiyo application ya Ocampo, basi Rais wa Sudan atakuwa on wanted list kama Marehemu Milosevic na Charles Taylor. Na most likely watakubali..evidence are overwhelming!
Swala langu ni je, sisi kama waafrika hiki kitendo cha hii mahakama ku-deal na RAIS ALIYEKO MADARAKANI..bila longo longo tuliyozoea ya "UN DIPLOMACY" tukichukulieje? inaweza kuwa mwanzo mzuri kwamba hawa viongozi wetu wa kiafrika ambao wamekataa kuwasikiliza na kuwahudumia raia wao waende wakakae huko The Hague, sisi tuhangaike na mustakabali wa bara letu au vipi?
Maana kweli waafrika tumenyanyasika na hawa viongozi ndugu zetu kuliko hata wazungu walivyotunyanyasa. Je wakipelekwa The Hague itasaidia viongozi wengine kuamka na kuwa responsible?
Personally nimeshindwa kutoa msimamo wangu...maana viongozi wa Afrika watasema tunaingiliwa na wazungu, lakini nikiangalia Darfur inavyowaka moto, sina budi kusema, Al BASHIR AENDE AKAOZEE HUKO THE HAGUE.
Watakao sema kwamba ashtakiwe Sudan, asipelekwe The Hague, naomba waangalie uwezo wa mahakama za kiafrika kuwashtaki "wakulu wetu'. IT IS IMPOSSIBLE.
So is it the right decision for Al BASHIR to be indicted by the ICC?
Mkuu Masanja,
Umeliweka hili suala vizuri sana. Binafsi hupenda sana kuangalia kwa undani nia za wenzetu wa magharibi wanapochukua hatua hasa pale matamko yao yanapoonyesha 'nia' ya kutusaidia. Ni mara chache sana haya mataifa makubwa yanafanya mambo bila kuangalia maslahi yao kwanza. Hili la Daffur nalo kama tujuavyo kuwa lina maslahi ya wote, wa magharibi na wa mashariki, kwa hiyo ni muhimu kuwa makini kusoma matamko yao vizuri.
Hata hivyo, kila ninachoangalia cha kumkingia Bashir kwenye hili sikioni maana karibu kila kitu kibaya kinaelekea kuhusishwa na utawala wake. Ushahidi wa wazi tu ndio unaotakiwa kuhitimisha kesi.
Kwa hiyo ingawa ni precedence mbaya kwa Africa, kwani siasa zinaweza kutumiwa kuwatingisha maraisi wa Africa watakaokuwa tofauti na wakuu kwa kuwatisha kuwapeleka ICC, k.m. Mugabe, lakini nafikiri ni vema tu Bashi akawajibika kwa aliyopandikiza. Ninashangaa kwa TZ kuikandia Zim na kumtetea Bashir. Kwa kweli tumeishiwa.