The SGR War: Wakati Kenya wakisuasua, Uganda wameamua kujenga SGR. Hii ni fursa kwa SGR ya Tanzania. Is it viable? Tuichangamkie?

Mkuu Rijali jandoni, thanks for this, huu ndio uzalendo!.
P
 
Sasa hiyo comparison uliyo ionyesha inatoka wapi juu ya Kenya? Kwani Tanzania tuna mashindano ya kiuchumi na Kenya?
 
Akisaini na asipotekeleza tutamfanya nini wakati Raisi wa nchi hii hashitakiwa na juzi tu wamepitisha sheria ya kuwalinda zaidi?
 
Wachumi wenzangu tungejitahidi kufanya synthesis analysis ya mradi huu kabla ya kuandika hasa figures. Matokeo yake ama tutakuwa wapotoshaji au hatuna uhakika na tunacho chambua.

Deni lolote muda unategemea na utakavyo structures loan repayments. Project inaweza ukaitafakari haraka haraka unaweza usipate ecomomic viability yake, lakini social viability ya huu mradi iko wazi kabisa.
Complex Consequential economic benefit analysis lazima uifanye ili upate usahihi wa economic viability. The Government is enabler, Haifanyi biashara.
 
Sasa hiyo comparison uliyo ionyesha inatoka wapi juu ya Kenya? Kwani Tanzania tuna mashindano ya kiuchumi na Kenya?
Huwezi kufanya comparison kwa kitu ambacho hakipo!, hivyo sijafanya comparison yoyote, nilichofanya ni kutoa angalizo la projected trends za SGR ya yetu, kwa kuitumia SGR ya Kenya. Japo hatuna mashindano ya wazi, like like entities zinashindana, Bandari ya Dar na Bandari ya Mombasa zinashindana kugombania wateja. Mzigo unaupita bandari ya Mombasa, ndio unailisha SGR ya Kenya, Kama bandari ya Mombasa, inapokea mzigo mkubwa kuliko bandari ya Dar, lakini SGR yao haishibi, sisi sasa tunapojenga SGR yetu, tusisubiri ije kushinda njaa, pia tujipange, tutaishibishaje SGR yetu?.
P
 
Bahati nzuri niko kwenye hii industry na kuna mambo mawili au matatu nayaelewa...kwa hapa nataka kusema Tanzania imelala usingizi wa pono kwenye kupigania shehena kubwa zaidi kupita Dar port, miundombinu ni mibovu mno na badala ya Magufuli kuhangaika na 10% zake kwenye biashara Kichaa ya ndege, ni heri angewekeza nguvu kuikamilisha SGR..

Lkn Sasa tumbo la mwanadamu halishibi, hadi Mhutu aje ashibishwe na 10% za dili za ndege Kenya watakuwa wameikamilisha SGR yao kuingia Uganda, Namibia Watakuwa wameifikisha SGR yao Zambia, na Angola Watakuwa wameifikisha SGR yao Lubumbashi.

Then Tanzania/dar port itaendelea tu kuwa ki-bandari kidogo kinachohudumiwa na bandari ya Mombasa
 
Brother Mayala Leo umetema madini ya maana kwenye Transport Economy, ubarikiwe sana kwa uwezo wa kuchambua masuala yenye tija na mshikamano kwa Nchi yetu Tanzania
 

Nime kuja kugundua kitu kuna mahusiano makubwa sana kati ya CCM na ujinga, simtukani mtu ila huo ndio ukweli tujitahidi sana kuwapa ndugu zetu somo Folded hands. madhara ya kukubali kumtegemea mtu kua kinga yako ndio hayo nilazima uwe kama zombie kila kitu unashabikia tuwasaidie wenzetu.
 
Wakati bandari yenu inapiga miayoo
 
Tanz is a sleeping giant km gesi tukiitumia vizuri kiuchumi tutakuwa economic power house shida hatujaukamilisha vizuri mradi huu. Tunayo mengi ya kujikwamua tayari tuko uchumi wa kati sawa na Kenya.
 
Hongera sana mkuu kwa somo zuri sana
 
Tanz is a sleeping giant km gesi tukiitumia vizuri kiuchumi tutakuwa economic power house shida hatujaukamilisha vizuri mradi huu. Tunayo mengi ya kujikwamua tayari tuko uchumi wa kati sawa na Kenya.
Unaizungumzia ges ipi hiyo?
 

Kwa katiba ipi ya kumbana rais atakayekuwa madarakani? Katiba yetu inampa rais uwezo wa kuamua ni mradi gani ni mzuri na sio mipango. Kwa katiba hii ya rais kuamua nani awe mbunge, na nani afungwe au asifungwe, sioni tukipiga hatua. Kama unataka Magufuli aongezewe muda sio kwasababu anayotekeleza sasa ni mazuri, bali una maslahi naye binafsi. Kama ni mazuri hata akitoka, uwe unaanzisha makala hata ikibidi kuuwawa ili hayo mazuri yatekelezwe. Sio leo tunaimbishwa kama watoto wadogo kuwa gas ndio muarubaini wa matatizo ya umeme, haijapita hata miaka 10, tunaambiwa gas tumepigwa, ila umeme wa maji ndio sahihi!
 
Na ni kweli pasco kutaja corona kama kikwazo kipande hicho cha km300 na kimeanza kujengwa miaka kadhaa nyuma huo ni uongo kama sio hoja ya kitoto kutoka kwa Pasco

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Nimepita sehemu kadhaa na kuna kazi kweli inafanyika, sina tatizo kabisa na kazi kufanyika, ninahoji muda wa kumalizika kwa mradi kutokana na ahadi zinazotoka. Dar-Moro ilikuwa ikamilike Nov 2019. Lakini sasa tunaambiwa itakamilika Aprili 2021. Na je kweli ni fedha za ndani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…