The Second Door (Tamthilia)

Ipigie kura simuizi hii

  • Nzuri Sana

    Votes: 9 56.3%
  • Inafaa Kusomwa

    Votes: 5 31.3%
  • Yakawaida

    Votes: 0 0.0%
  • Sijaisoma

    Votes: 2 12.5%

  • Total voters
    16
Yap! uhondo unaendelea na kuanzia Episode ya 14 au 15 nahisi ndio utakuwa mwanzo wa utamu kamili wa Tamthilia hii nashukuru wooooote kwa sapport. Lakini shukrani zangu za kipekee ziwafikie prospa, everlenk na beth ambao wamekuwa watu wa kwanza kutoa michango yao kwaajili ya kuisapot Tamthilia hii naamini wasomaji wangu wengine wanaonipa nguvu kubwa kabisa kwa kufatilia tamthilia hii wasomaji kama ram, xfactor,davidson689, Mrembo by Nature, Mbimbinho, Kyenju na wengine wengi sana zaidi ya 5000 siwezi kuwataja woote naamini pia wapo njiani kusapot kazi hii kwa kuichangia hata kidogo

Kama kawaida brother.Hii simulizi inanipa feelings kama zile nazopata nikiwa naangalia TV series za action.

Umenifurahisha ulivyoingiza matukio ya computer hacking maana ndio eneo langu la kujidai japo terms ulizotumia sio sahihi sana ila imeeleweka na inafariji kuona mwandishi ukiwa na upeo wa haya mambo maana ndio dunia yetu ilipo sasa,watu hawapigani kwa bunduki ila kwa teknolojia ya computer.

Big up sana,nipo mguu kwa mguu.
 
tunashukuru sana kutupa kitu cha maana na mafunzo ya kusisimu , mi najifunza mengi sana hapa sijui wenzanguu
 
Ushaur wangu kwa watunzi wote. Leten uhondo jumatatu mpaka ijumaa, thn jmoc na jpil mupumzike. Mnachosha. Hongera kwa kaz nzuri
 
Ushaur wangu kwa watunzi wote. Leten uhondo jumatatu mpaka ijumaa, thn jmoc na jpil mupumzike. Mnachosha. Hongera kwa kaz nzuri

from tommorow itakua hivyo for you. but mimi nilikuwa natoa kila baada ya siku moja.
 
The Second Door- Episode 13

Habari gani marafiki? Ni wasaha mwingine murua tunaoungana pamoja katika mkasa wa tamthilia ya kuvutia, si nyingine bali ni Tamthilia ya The second door.

Jana katika episode namba 12 tuliishia makaburini ambako Tarick na Roby walifika kwa ajili ya kusindikiza safari ya mwisho ya mpendwa wao Frank. Baada ya kutoka eneo lile la mazishi, sasa kwa Roby ilikuwa ni zamu ya kumalizia kibarua cha kumkabidhi Brenda kwa Rweyemamu. Hili halikuonekana kama lilikuwa zoezi kubwa kwa Roby. Roby anamrudisha Tarick nyumbani kisha anaelekea hospitali kwa ajili ya kuangalia utaratibu ambao atautumia kumpeleka Brenda kwa Rweyemamu bila kumsababishia matatizo. Roby akiwa ofisini kwakwe anajaribu kuweka mambo ya kikazi vizuri huku akiplan jinsi ya kumrudisha Brenda kwa Rweyemamu.

Muda wa masaa ya kazi unaisha Roby akiwa anarudi nyumbani anaamua kupitia kwa wakala wa usajili wa namba za simu akiwa na malengo ya kwenda kusajili line atakayoitumia kuwasiliana na Rweyemamu, Roby anafanikiwa kusajili namba kwa utambulisho feki, kisha kutokana na muda kuwa umeenda sana anaamua kurudi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani wakiwa pamoja na Tarick Roby anasema, “Tarick ujue umefanya uamuzi mgumi sana, na laiti ingekuwa hiari yangu ningekusafirisha hata kwa viboko ukaishi nje ya nchi”, Tarick anajibu, “nikweli kabisa unachosema dokta, lakini kunamsukumo mkubwa sana kutoka moyoni mwangu ukinilazimisha niendelee kuishi Tanzaia”. Roby anashusha pumzi na kusema, “ok! Tatizo linakuja, ni jinsi gani tutaficha identity yako” baada ya swali hilo Tarick anajibu, “Naweza hata kutumia ndevu za bandia ili nibadilishe muonekano wangu.” Baada ya Tarick kuongea maneno hayo Roby anatikisa kichwa akiashiria kutokubaliana nae kisha anasema, “Tarick! Utambulisho wako ni muhimu kuliko sura unayoifikiria. Jina lako, umezaliwa wapi, umesomea wapi, wazazi wako, passpot, vitambulisho navitu vingine vyote lazima vikutambue, ukishindwa kuonesha vidhibitisho hivyo kunamambo mawili, pengine sio mtanzania au utajilikana kuwa ni wewe unaetafutwa umeamua kuficha utambulisho wako.” Roby na Tarick wanajadili kwa muda mrefu bila kupata jibu.

Ni siku nyingine tena Asubuhi na mapema mheshimiwa Proffesa Rweyemamu akiwa ofisini kwake anapokea simu kutoka kwa mtu asie mfahamu, simu hiyo anayopokea Rweyemamu inampa taarifa za kumtaka afike kwenye jengo la Haidary Plazza posta kwa ajili ja kuchukua mzigo na taarifa za muhimu. Rweyemamu anauliza maswali mengi na kuhoji sana juu ya wito huo lakini hakuna hata swali moja linalopata jibu. Mwisho simu hiyo inamuelekeza kuhakikisha anafika hapo akiwa peke yake. Kutokana na msisitizo uliooneshwa na simu ile Rweyemamu anaamua kumtuma mfanyakazi wake kwenda kusikiliza wito huo, na kwakuwa hakuwa na uhakika kuwa wito huo ulikuwa unahusiana na nini Rweyemamu anahofia kumtuma peke yake mfanyakazi wake hivyo anaagiza na askari wawili ili wawe wanamfatilia mjumbe huyo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wake.

Mpenzi msomaji wito huu wa ghafla aliokuwa ameupokea Rweyemamu ilikuwa unatoka kwa Roby na ulikuwa na lengo la kumkabidhi Brenda. Bila kujua Rweyemamu anamuelekeza mfanyakazi wake mpaka kwenye sehemu ya juu ya jengo hilo ambako aliambiwa angekutana na mtu anaempigia simu na kumkabidhi vitu alivyo muahidi. Roby kwa kuwa alikuwa hajulikani na mtu aliekuwa akiongea nae kwenye simu anaamua kutumia ujanja wa kumtanguliza eneo la juu kwenye jengo hilo sehemu ambayo inamgahawa, baada ya kuwasiliana na Rweyemamu, na Rweyemamu kumhakikishia kuwa tayari alikuwa amefika eneo hilo, Roby nae anapandisha ili kukutana nae. Kabla hajatokeza, Rweyemamu anawatumia meseji wale askari waliokuwa wakiongozana kwa siri na mtu aliyemtuma na kuwapa namba aliyokuwa akitumia Roby kisha anawaambia waibip ikiita wamkamate, na kumpeleka kituoni kisha wamtaarifu.

Huku nyumbani alikoachwa Tarick, Roby alikuwa amemuagiza Zubery afike nyumbani hapo kwa ajili ya kuchukua Pesa azipeleke kwa mama, maagizo ya pesa hizo Roby alikuwa amemuachia Tarick, Zubery anafika nyumbani kwa Roby na kupokelewa na Tarick, kwakuwa Tarick alikuwa peke yake ndani ya nyumba hiyo Zubery anaamua kukaa kidogo ili kumpa kampani, Tarick. Zubery hakuwa mgeni kabisa ndani ya nyumba hiyo, anaweka movie kisha wanaendelea kutizama na Tarick huku wakipiga story. Baada ya story za hapa na pale walijikuta wakizungumzia kutafutwa kwa Tarick. Tarick haoneshi wasiwasi wowote kwa Zubery kwani aliamini kwa moyo alionao kaka yake sio rahisi Zubery akafanya jambo lolote baya.

Ndani ya muda huu kwenye jengo la Hidary Plaza, Roby anatokeza juu walipokuwa askari wale na ndani ya sekunde hiyohiyo yule askari anapiga ile namba kwa siri, bila kuweka simu sikioni kisha wote wana zungusha macho huku na kule kuangalia simu itakayoita. Roby naye akiwa ndio anatokeza pale juu macho yake yanazunguka haraka haraka kumtizama Rweyemamu, lakini anashtuka kugundua kuwa Rweyemamu hakuwa amefika eneo hilo. Wakati wale askari wamepiga simu ya Roby, inakuwa kama bahati Roby alikuwa ameiwekea simu yake vibration, hivyo simu hiyo ilivyoanza tu kuita Roby hakuangaika kuipokea wala kuitazama yeye ananyoosha moja kwa moja kuelekea kwa wahudumu wa vinywaji kwenye mgahawa huo huku akitizama sura ya kila mmoja ilia one ni nani aliekuwa akimpigia. Yule askari aliyekuwa akipiga simu baada ya kuona hakuna simu inayoita eneo hilo anaamua kutoa simu mfukoni nakupiga tena, Roby anatizama kitendo hicho na kugundua kuwa Rweyemamu aliamua kumuwekea mtego. Kitendo cha simu ya Roby kuita kwa mara ya kwanza, ilinavyoita kwa mara ya pili inaita sambamba na simu ya mfanyabiashara mmoja wa spare za magari aliyekuwa ameketi eneo hilo akisubiria chakula. Askari hao wanamkamata kwa fujo na kumfunga pingu kisha, wanashuka nae kwenye jengo hilo chap chap na kwenda nae kituoni.

Kila mmoja anashangaa tukio hilo, Roby akiwa ameshaagiza juice ya matunda na ameshalipia pesa, anaondoka eneo hilo na kuacha kila kitu, anaenda mpaka alipopaki gari yake, anaingia ndani na kumtazama Brenda ambaye alikuwa amempakia kwenye siti ya nyuma, kisha anaegemea stering ili kusubiri mapigo ya moyo yapungue. Haimchukui muda mrefu Roby anawasha gari na kuondoka eneo hilo. Baada ya kuhakikisha amefika mbali kidogo anapaki gari vizuri na kumpigia tena simu Rweyemamu, kisha anasema,”Umepoteza nafasi ya kupata zawadi yako, ulikuwa unafikiria nini?” Rweyemamu anajibu huku akiwa amepaniki, “wewe -------- unajua kuwa mimi ni mtumishi wa serikali!? Ninashughuli nyingi sana za kufanya, usijilazimishe kuingia kwenye matatizo” Roby anajibu kauri hiyo taratibu kwa kusema, “Unashughuli nyingi sana ikiwemo na ya kumtafuta Brenda!?” Kauli hiyo inamfanya Rweyemamu apigwe na bumbuwazi kisha anaduwaa kimya akiwaza imekuaje mtu huyu asiyemfahamu azungumzie kuhusiana na Brenda, Roby bila kujali anasema, “Kama jibu ni ndio, umejiongezea ukubwa wa shughuli hiyo. Jioni njema”. Baada ya kauli hii Roby anakata simu na kuizima.

Muda huu akiwa anaongea na Roby , Rweyemamu alikuwa kituoni akimtizama mtu aliyekuwa amekamatwa na askari wake. Jamaa huyo mfanya biashara alikuwa ameshapokea kipigo cha kutosha wakimlazimisha akubari kuwa yeye ndiye aliyekuwa akimpigia simu mheshimiwa Rweyemamu. Rweyemamu mara baada ya kupokea simu hiyo anaingia haraka haraka ndani katika chumba alichokuwa akiadhibiwa mtuhumiwa huyo na kusababisha kila mmoja ashangae kwa kasi aliyoingia nayo, baada ya kufika sehemu hiyo, Rweyemamu anamtizama kila mmoja usoni, kisha mwisho anashangaa kuona jinsi yule jamaa alivyokuwa amepigwa bila kosa. Pamoja na ukatili mkubwa aliokuwa nao Rweyemamu anamtizama yule mfanya biashara na kumuonea huruma kisha kwa upole anawaambia,” muachieni……” mmoja kati ya askari walioshiriki kumkamata anasema, “Lakini proffesa… ! anakiri kuwa yeye ndie aliekuwa akikupigia simu”, proffesa akiwa amechukia kweli kweli kwa kitendo cha askari hao kumkamata mtu ambae hakuwa na hatia na kumpiga, anasema kwa ukali, “Nimesema Muachieni……. ! wajinga wakubwa, polisigani nyinyi” Baada ya kufoka kwa ukali Rweyemamu anawaamuru wale askari wachukue namba alizotumia Roby kuwasiliana nae, kisha wamtafute mtu huyo mpaka wampate, na kuwaambia kuwa ndie aliemteka nyara Brenda.

Baada ya Roby kufanikiwa kuwaponyoka wale askari anaamua kurudi hospitali na Brenda, kisha anamkabidhi kwenye kitengo cha madaktari wa matatizo ya akili na kuahidi kuwa atakuja kesho kumchukua. Baada ya hapo Roby anaelekea ofisini kwake na kukuta barua kutoka kwa mwajiri wake iliyokuwa ikimpa onyo kali kutokana na maudhurio na ufanisi usioridhisha katika kazi. Roby anakuna kichwa na kutafakari kidogo lakini anaumiza kichwa zaidi kwa kuwaza ni jinsi gani atakavyo mkabidhi Brenda kwa Rweyemamu bila yeye kuangukia kwenye matatizo. Baadaya ya Roby kumaliza masaa yake ya kazi, Roby anarudi nyumbani na kumkuta Tarick akiwa anaangalia movie. Wanasalimiana na Roby anafurahi kumkuta Tarick akiwa hana majonzi tofauti na sikuzote. Katika mazungumzo ya hapa na pale, Tarick anasema, “alikufika hapa mdogo wako nikampa zile pesa, ni mkarimu sana…” Roby anapata wasiwasi kwani hakutarajia kuwa Zubery angekaa hata kidogo, anauliza, “Alikaa!?” Tarick anajibu, “andio nimekaa nae sana, akawa ananisimulia jinsi mlivyohangaika na Frank kuwakimbia askari kutoka Hosteli”. Kwa mshtuko Roby anauliza, “ulimwambia chochote kuhusiana na swala lako?” Tarick anajibu, “Mbona anajua kila kitu, amenielezea jinsi swala hili lilivyokuwa gumzo nchi nzima” Moyo wa Roby unampasuka na kugundua kuwa alikuwa amefanya kosa kubwa kumuagiza Zubery afike eneo hilo, kama unavyojua mpenzi msomaji kichwa kinapokuwa na mlundikano wa mambo, ni rahisi sana kupoteza umakini na kufanya uamuzi unaoweza kuwa na madhara makubwa.

Baada ya Roby kuonesha hofu, Tarick anamuuliza, “vipi dokta! Kwani kuna tatizo lolote…..?” Roby akiwa amedhamiria kutomueleza chochote Tarick anajibu, “Hapana, ila sitaki kumuamini mtu yoyote kwenye swala hili kwani inaweza kutuletea shida” Tarick anamjibu Roby kwa kusema, “lakini mdogo wako ni mtu mzuri sana” kauli hiyo ya Tarick inamfanya Roby amtazame usoni kisha anasema, “simuamini hata mama yangu mzazi katika swala hili”. Baada ya mazungumzo hayo Roby anasema, “Nimeumiza sana kichwa nikiwaza nini tunaweza kufanya ili uishi kwa amani bila kujulikana…..” Anakaa kimya kidogo kisha anamalizia , “Kichwa kimestack kabisa... au wewe umepata wazo lolote?” Tarick anajibu kwa kutikisa kichwa kisha anasema, “Hapana sijapata jibu tutafanyaje”. Kitendo cha Tarick kumaliza kauli yake hiyo ghafla mlango unasukumwa kisha anaingia mtu…………….

Wapenzi marafiki na wasomaji wangu wapendwa… maji yanazidi unga kwa Roby, mambo yameanza kumuendea mrama kazini kwake lakini pia swala la kumkabidhi Brenda kwa Rweyemamu na kumfanya Tarick aendelee kuishi dar es salaam bila kujulikana na mtu yeyote vinakuwa kama utando mkubwa wa kiza kwenye tamthilia hii ya the second door, Wacha mimi niishie hapa. Mpaka tutakapo onana tena katika Episode no 14 ya Burudani hii uipendayo Bye

g click, Kongosho, Heaven Sent, Ennie, Daudi1, everlenk, jembe afrika, HARUFU, mahirtwahir, Kasonso S., prospa, Payer, Phenomenon Lady, Mfagio, beth, Mwadunda, anna bubelwa, ram, dreadnaughty, Obe, wangewange, Luno G,Mrembo by Nature, Gunda66, Lolipop, Blaki Womani, Giti, Khantwe, Kyenju, Kaunga, Ennie, toghocho, twin'sisy, Arnooy1206, Mbimbinho, Meljons,davidson689, xfactor, kifagio.

Nawengine nilio wasahau Tunaendelea.........

Comment, Like, Donnate.

New Donate copy.jpg

 
Mmmh!! Zubery kafanya mambo yake nini? Frank kamuachia Roby kazi nzito sana. Asante jamiiforum aka Msamiati,big up kweli huu ni msamiati mkubwa.
 
Last edited by a moderator:
What a fascinating story, shidA ni kwamba bado hatuna Directors na producers ambao they can put it on screen.
 
MAMBO VIPI MARAFIKI, NINAWATAKA RADHI SANA KUWATAARIFU KUWA NINASAFARI YA KUELEKEA TANGA KUANZIA J/3 AU J/4 KWA MUDA USIOZIDI WIKI MOJA HIVYO SITAKUWA NA NAFASI NZURI YA KUENDELEA KUANDIKA
RIWAYA HII. lAKINI NAAHIDI MUDA WOWOTE NIKIPATA KOMPUTER YOYOTE SAFARINI NA UPENYO WA
KUENDELEA KUANDIKA NITAIPOST KWANI SITAWEZA KWENDA INTERNET CAFE USIKU.
SITAKI MUDA MREFU UPITE BILA KUENDELEA KUWAPA BURUDANI HII.
NAOMBENI DUWA ZENU.

 
pouwa tunakutakia safari njema uende urudi salama maaana tanga bhana !!!!!!!!!!!!!!!
MAMBO VIPI MARAFIKI, NINAWATAKA RADHI SANA KUWATAARIFU KUWA NINASAFARI YA KUELEKEA TANGA KUANZIA J/3 AU J/4 KWA MUDA USIOZIDI WIKI MOJA HIVYO SITAKUWA NA NAFASI NZURI YA KUENDELEA KUANDIKA
RIWAYA HII. lAKINI NAAHIDI MUDA WOWOTE NIKIPATA KOMPUTER YOYOTE SAFARINI NA UPENYO WA
KUENDELEA KUANDIKA NITAIPOST KWANI SITAWEZA KWENDA INTERNET CAFE USIKU.
SITAKI MUDA MREFU UPITE BILA KUENDELEA KUWAPA BURUDANI HII.
NAOMBENI DUWA ZENU.

 
MAMBO VIPI MARAFIKI, NINAWATAKA RADHI SANA KUWATAARIFU KUWA NINASAFARI YA KUELEKEA TANGA KUANZIA J/3 AU J/4 KWA MUDA USIOZIDI WIKI MOJA HIVYO SITAKUWA NA NAFASI NZURI YA KUENDELEA KUANDIKA
RIWAYA HII. lAKINI NAAHIDI MUDA WOWOTE NIKIPATA KOMPUTER YOYOTE SAFARINI NA UPENYO WA
KUENDELEA KUANDIKA NITAIPOST KWANI SITAWEZA KWENDA INTERNET CAFE USIKU.
SITAKI MUDA MREFU UPITE BILA KUENDELEA KUWAPA BURUDANI HII.
NAOMBENI DUWA ZENU.


Safari njema mkuu si tupo tunakusubiri.
 
Safari njema Msamiati,Mungu akulinde,we will miss yoooooooo!!!!!!!


Wadau tuchange basi kijana apate Laptop na moderm burudani iwe inaendelea popote atakapokuwa.....au mnalionaje hili?????
 
Last edited by a moderator:
Ikiwezekana mtakuwa mmesaidia sana everlenk kwasababu hata computer ninayotumia nyumbani ni majanga matupu japokuwa inanisevu. Angalieni uwezekano wa wazo hili.
 
Safari njema Msamiati,Mungu akulinde,we will miss yoooooooo!!!!!!!


Wadau tuchange basi kijana apate Laptop na moderm burudani iwe inaendelea popote atakapokuwa.....au mnalionaje hili?????
Hahahahahaaa hii ndio ile waswahili walisema kuwa "ukionja asali utachonga mzinga"

Naunga mkono hoja
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom