Binti Nusume Mlinzi wa kaka zake.

OscarkambonaJr

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
1,592
2,567
Ilikua Jioni majira ya saa 12 Mwaka 1995 Mkoani Mbeya alibishwa hodi nyumbani kwetu na mdogo wangu Asubisye Alitoka kwenda kuitikia wito na kumkaribisha mgeni.Alikua ni mama wa makamo amebeba begi na mfuko mkononi. Alikua,alipoingia malangoni kwetu Nilitoka jikoni nilipokua naandaa mlo wa mchana kwaajili ya familia na kuelekea sebureni na kupokelewa na sauti ya kilio huku nikikumbatiwa na mama Yule,Aliniita Nusume pole shangazi yangu,tumebaki peke yetu huku akinikalisha kwenye kochi. Alikua ni shangazi yangu mdogo wa wa baba yetu Tupilike akitokea Morogoro Kilombero.

Ghafla machozi yalitililika mashavuni mwangu baada akili kunijia kuwa mama yangu mzazi Tupokigwe hatunaye duniani maana alienda na baba kwaaliji ya kuuguzwa kijijini kwa baba na mama yetu. Nikiwa binti wa miaka 13 ,Mtoto wa kike pekee kwenye familia ya watoto wanne. Kaka yetu wa kwanza anaitwa Athur, wa pili ni Kulwa ambae ni pacha wangu na mwisho ni Asubisye ambae ni mdogo wetu.
Nilianza kuwaza Maisha bila mama yangu kipenzi ambaye alikua mwalimu wa shule ya msingi Iwambi wakati huo mbeya haijawa jiji.Baba yetu alikua afisa misitu Wilaya ya Kawetele.

Hata chakula nilichokua naandaa kilikosa maana tena majirani wakaanza kuja kujua nini kinaendelea,Kama kawaida viti vilitolewa nje na mikeka maandalizi ya msiba na taratibu nyingine zilianza kupangwa na watu wazima waliofika pale.Walimu na wafanyakazi we zake na baba wakawasili nyumbani kupanga mikakati ya mazishi huko kijijini kwetu Isoko wilaya ya Ileje. Kaka yangu nae aliporudi shule alikuta Hali ya msiba tukajumuika Kama familia nikiwa napelekwa tu maana kwa umri wangu ni tukio geni kabisa,Hata kaka yangu pia hakuwa na cha kufanya maana alikua mdogo pia.Kiufupi ilikua familia changa maana watoto wote tulikua under 18

Kesho yake zilikuja gari za serikali kutuchukua na baadhi ya majirani kuelekea Kijijini kwaajili ya mazishi.

Tulifika na kumkuta Baba na ndugu wengine hakika baba alikua na uchungu sana kupoteza kipenz chake alitukumbatia akalia kwa uchungu nakumbuka akasema nawapenda wanangu nitawatunza.

Baada ya mazishi tulibaki muda wa wiki mbili kijijini ndipo tukarudi nyumbani ili maisha mengine yaendelee. Nilifika nikakuta picha zote za marehem mama zimetolewa sebureni,Nilifanikiwa kupata picha moja tu ambayo mama yetu alipiga na Sisi tukiwa watoto wote wanne.

Hakika Maisha yalibadilika ghafla bila mama yangu kipenzi,afya ya mdogo wetu Asubisye wa miaka mine ilidhoofu.Baba alishindwa kuhikili kile kishindo kabisa.
Baba akamua kuomba msaada wa kutafutiwa dada wa kazi walau asaidie baadhi ya majukumu pale nyumbani ikiwemo kukuangalia mdogo wetu.Baada ya miezi kadhaa Hali ya mdogo wetu haikutengemaa,Shangazi yetu aliomba kumchukua kukaa nae kwakuwa alikua na watoto wa lika lake hivyo angechangamka akiwa huko.

ITAENDELEA……..
 
Pole kwa msiba wa mama, mbele yake nyuma yetu
 
NUSUME:SEHEM YA PILI

Baada ya Mdogo wangu kuchukuliwa na shangazi yangu nilibaki mpweke maana nilimpenda sana, sikuwa na jinsi ya kuamua tofauti ukizingatia nilitakiwa kwenda shule pia,Nilikua nikimkumbuka Mara kwa mara.Sisi familia ya chini hatukua na Simu wala njia ya kuwasiliana kwa haraka zaidi ya barua,mbaya zaidi hakuwa anajua kusoma na sikujua pia barua zinatumwaje

Maisha mapya yalianza bila mama nikiwa na dada wa kazi lakini baba hakuwa mbali zaidi alizididha ukaribu.

Baba hakuzoea ile Hali mapema kuwa mwenyewe ghafla.hivyo alikua anarudi nyumbani mapema na kujifungia chumbani.HakiKa nilisikia baba yangu akilia peke yake chumbani Mara kadhaa kisha anatoka kwenda kutembea.

Kaka zangu wao ni michezo na mpira ya Sodo wakitoka shule ni jioni.Mpaka wakikosea kitu baba akiwachapa Ndio wanamtaja mama Yao marehemu wakilia.

Shuleni walimu hawakututenga zaidi zaidi walitusimamia ukizingatia mama alikua mwenzao, Kuna muda nilihisi naonewa huruma mpaka namkumbuka mama yangu kipenzi,alijua kuniweka smart na hakika nilikua moja kati ya wanafunzi wasafi na wenye bidii darasani.

Siku moja Rafiki wa mama kipenz Anaitwa Mwalimu Kileo alinialika Nyumbani kwake,Mungu ambariki sana mama Yule,hakubarikiwa kuwa na mtoto wa kike Lakini alinifundisha Kama mwanae wa kumzaa.

Baba yangu alikua akituamsha kujiandaa kwenda kanisani akituambia Ndio njia pekee ya kumfurahisha mama yetu marehemu ili siku tukionanae mbinguni atupende zaidi.Hili somo niliniingia kwa uzuri zaidi maana nilimpenda sana mama.

Mama Kileo alinifundisha kujiweka Sawa Kama binti na kuzingatia usafi.Mara kadhaa baba yangu na Mama kileo walikutana kujadili maendeleo yetu ya shule na tabia. Mama huyu alikua mjane maana mume wake alifariki pia akimuachia watoto wawili wakiume.

Kuna siku baba alirudi Nyumbani Mwenye furaha akaniambia nioge twende kununua nguo za kanisani maana zilikua zimeanza kuniruka,

Baba:Nusume mwanangu

Mimi:Bee Baba,

Baba:Najua umekua ukienda kufanya manunuzi na mama lakini hayupo hivyo tutakua tunaenda wote kununua mahitaji yako, aliendelea kusema mimi ni baba yako sitaki upate shida nikiwepo,Pia usisite kuniambia shida Yoyote ukaogopa.
Hakika nilikua binti wa baba mpendwa.

Hongera kwa baba wanaopenda watoto wao wa kike na wakiume pia.
Basi tuliondoka na kwenda kununua nguo za kanisani na kurudi nyumbani.
Nilijaribu viwalo vyangu mbele ya kaka zangu mpaka wajakaona wivu, lakini Baba Ali Waambia ameanza na mimi kwani alikua na pesa kidogo muda unaokuja akipata ni zamu yao.
Nilimuliza baba Kama Mdogo wangu Asubisye amepata pia nguo za kanisani akaniambia ametuma pesa kwa shangazi kwaajili ya manunuzi ya nguo pia,Nilifutahi sana kwakua Mdogo wangu anakumbukwa Kama ninavyo mkumbuka.

Shule zilipofungwa baba alisema tunaenda kumsalimia shangazi ili tukamsalimie pia Mdogo wetu, Siku zilipowadia baba alituaga kuwa anaenda kukata tiketi kwaajili ya kwenda kwa shangazi,nilimsubiri baba lakini alikawia kurudi na haikua kawaida yake baba kurudi nyumbani zaidi ya saa usiku tangu mama alipotutoka.

ITAENDELEA….
 
NUSUME:Sehemu ya 3

Hatimaye Baba alirejea nyumbani saa 5 kasoro,Akiwa amelewa,nilishangaa maana kawaida yake ni kunywa anazozimudu,Haikua shida kwetu maana alimwita Kaka Athur na kumwambia kesho saa kumi tunaondoka tunaenda kwa shangazi,hivyo watoto wa mama Kileo watakuja kulala hapa kuanzia kesho kutazama nyumba yetu hivyo tuiache safi.

Baada ya muda mfupi baba kuingia chumbani kwake nilisikia sauti za mtu mzima kugumia kwa kulia,Huku akipiga godoro.Hakika Baba yangu alikua amemkumbuka mke wake haswa,

Dada wa kazi yetu Anaitwa Irene akaniambia baba yako anatakiwa aoe kapema,atapata shida sana Mwenyewe na utu uzima ule,walau apate mtu wa kubadilishana mawazo.Binafsi sikuelewa na sikutaka kuelewa kabisa Yaan baba yangu apate mke mwingine zaidi ya mama yangu.Nilimpinga vikali na nikaapa kumwambia baba kesho asisubutu kuoa mwanamke mwingine.

Hakukuchi kunakucha lilikuja gari la ofisini kwa baba tukapakia mizigo na kwenda stesheni ya treni tazara Mbeya,Mishele ya saa 10 jioni,safari ilianza nikikaa na Baba Upande mmoja wa siti kaka zangu wakakaa upande mwingine wa siti. Tukiwa tunatazamana, safari ilikua nzuri lakini ndefu.

Niliamua kumuuliza baba lile swali ambalo dada yangu aliniambia jana usiku,

Nusume:Baba eti nikuulize kitu

Baba alihamaki kidogo,akajibu niulize mwanangu
Kaka zangu wakatega sikio nasema nini mbele ya mshua wao

Nusume:Kwanin huwa unalia chumbani,eti unataka kuoa mke tena

Baba:Alishusha pumzi na kimya kikatawala kidogo huku kaka yangu Athur akinipiga mguuni,kupitia nafasi chini ya meza.

Baba akasema hapana mwanangu,Mimi ninampenda mama yenu mpaka leo,sitaweza kumpenda tena mama mwingine.

Nidhahiri lile swali lilimtoa jasho baba yangu mapaka akashusha tena pumzi baada ya kujibu alinivuta Karibu akanikumbatia ukimya ukatawala tukisikia Mlio wa magurudumu ya treni yakipokezana,

Tulipita steshen Kazaa lakini nilifurahi tulipofika kisaki,Baba alinunua kuku na chips hakika walikua kuku wakubwa wa nyama nilikula mpaka baba akamiambia atanifungia wengine tukirudi,
Nikamuomba baba amnunulie mdogo wetu nyama ya kuku pia tumpelekee,hakuwa na manna ya kutii amri yangu.

Safari ya Mbeya Morogoro ni mwendo wa siku moja na masaa kadhaa kwa gari moshi,Tulifika kesho yake saa Mbili usiku.

Shangazi alikuwepo stendi akitusubiri kwa muda,Huenda Waliagana sehem ya kukutana sikujua maana nilijiuliza shangazi alitukutaje hapa ,Hakika nilifurahi kufika Morogoro Mara ya kwanza nikiwa na shauku ya kukutana na mdogo wangu Asu,

Tulifika Nyumbani kwa shangazi nikimkimbilia mdogo wangu kwa furaha baada ya kusikia sauti ya Dadaaa,Hakika nilimshika kwa muda mrefu mapaka machozi yakanitoka,Nilikua na shauku ya kumuuliza maswali mengi lakini walikuja watoto wa shangazi tukajumuika na watoto wote.

Tukapata chakula cha jioni,na familia ya Mjomba yangu hakika nilipata faraja kumuona mdogo wangu Asu ameimarika kiafya,

Tulipokucha nikaanza kumuuliza mdogo wangu vipi shangazi anakupenda sana eeeh ile kumdodosa, akisema huwa Mjomba huwa anamletea zawadi na kumnunulia Nguo,alilalamika kuna mtoto mmoja jirani huwa anampiga anaitwa Juma,nilisema kimoyomoyo nitampiga makonzi huyu dogo anaemzingua mdogo wangu.

Nilitamani kuondoka na mdogo wangu Au nibaki pale kwa shangazi ili nimlinde mdogo wangu zaidi.

Tulikaa wiki moja na baba l kutuambia kuwa tutarudi home kesho kutwa,Akaisema safari ijayo watakuja kutusalimia Mbeya.

Mjomba wangu alikua mzungu sanaa,mpole na walielewana na shemeji yake vyema,Mara kadhaa walitoka kutembea kwenye sehem za kupata vinywaji.

Tuliludi Mbeya nikiwa na uhakika kua mdogo wangu yuko Sawa,sababu ya stori nilizosikia kuwa watoto wanateswa na watu baki wakienda kulelewa.

Tulifika nyumbani Mbeya tukakuta mazingira ya nyumbani yakiwa safi na chakula kimepikwa kwa Ustadi mkubwa,kitu ambacho niliona sio dada ameandaa maana naye alienda kusalimia kwao. Bila shaka yalikua ni maandalizi ya Mama Kileo.

Maisha yaliendelea kaka zangu wakipambana na masomo yao.Ukaribu wa Baba Mama Kileo uliongezeka huwa nawaza je Huyu Ndio atakua baba anataka kumuoa Au…

ITAENDELEA……
 
Back
Top Bottom