The Second Door (Tamthilia)

The Second Door (Tamthilia)

Ipigie kura simuizi hii

  • Nzuri Sana

    Votes: 9 56.3%
  • Inafaa Kusomwa

    Votes: 5 31.3%
  • Yakawaida

    Votes: 0 0.0%
  • Sijaisoma

    Votes: 2 12.5%

  • Total voters
    16
On wattpad mkuu vip tena, kule nlkua nakupata vzur but kmyaa

Daa niko Tanga bosi wangu, kidogo mazingira yananiyumbisha, Lakini nakuahidi kabla siku ya leo haijaisha nitapost episode hizi zote kaka. samahani sana.
 
Nlkusoma ila nlkua busy nikajua nikchungulia ntazkuta mana wattpad patupu name huku patupu.
 
yaani nimesoma usingizi umekata kabisa imenifanya nikae kwa wasiwasi na uwoga at last nikakumbuka ni story napata ahueni. unatisha kwa hii story kali.
 
Msamiati nilikuwa mbali sana kwa majukumu flani hongera naona kitu kimenoga waiting for the ep 17.
 
Msamiati yaani matumbo yashaanza umia sasa,, maana tumengoja sana!!
 
Last edited by a moderator:
Gunda Wekend hii namalizia episode ya mwisho ya season one. Kuanzia wiki ijayo tunaendelea
 
Inakuja kwa fujo sana bosi wangu naomba mnisamehe kwa kuichelewesha. Wasomaji wangu Blaki Womani, everlenk na prospa nawengineo kaeni mkao wa kula naweka mazingira vizuri zaidi. Then Mpoooo! mbona kimya sana! nimewamis

Aiseee!!! Msamiati uje tu umalizie hadithi yetu mbona kimya sanaaa?? Au mtu amepanda dau nini???? Weekend ilishaisha siku nyingi
 
Last edited by a moderator:

MHESHIMIWAgclick, MHESHIMIWA Kongosho, MHESHIMIWAHeavenSent, MHESHIMIWAEnnie, MHESHIMIWADaudi1, MHESHIMIWAeverlenk, MHESHIMIWAjembeafrika, MHESHIMIWAHARUFU, MHESHIMIWAmahirtwahir, MHESHIMIWAKasonsoS., MHESHIMIWAprospa, MHESHIMIWAPayer, MHESHIMIWAPhenomenonLady, MHESHIMIWAMfagio, beth, MHESHIMIWAMwadunda, MHESHIMIWAannabubelwa, MHESHIMIWAram, MHESHIMIWAdreadnaughty, MHESHIMIWAObe, MHESHIMIWAwangewange, MHESHIMIWALunoG, MHESHIMIWAMremboby Nature, MHESHIMIWAGunda66,MHESHIMIWALolipop,MHESHIMIWABlakiWomani, MHESHIMIWAGiti,MHESHIMIWAKhantwe, MHESHIMIWAKyenju,MHESHIMIWAKaunga,MHESHIMIWAEnnie, MHESHIMIWAtoghocho, MHESHIMIWAtwin'sisy, MHESHIMIWAArnooy1206, MHESHIMIWAMbimbinho, MHESHIMIWAMeljons, MHESHIMIWAdavidson689, MHESHIMIWAxfactor, MHESHIMIWAkifagio.Na waheshimiwa woooooote, ndugu, jamaa, marafiki wagenina wasomaji wangu... Asalaam aleikum.

Siwezi kutumia maneno meeengi kuomba radhi kwa utovu wa nidhamu wa hali ya juu nilioufanyakwenu lakini naomba nirekebishe makosa kwa vitendo kamaifatavyo.

Kusimama kwa simulizi ya tamthilia yetu kwa muda ambao haujatarajiwa kumetokana na kushindwa kuiendelezea kwasababu nilijikuta nimesahau mtiririko wa matukio jambo ambalo lilinilazimu nianze kusoma simulizi nzima kuanzia mwanzo hapo ndio uvivu ulinishika na kujikuta nimesimama.

Nawaomba nianze tenataratibu, sitaweza kuisoma tena riwaya hii kuanzia mwanzo hivyonaamini mtakuwa mkinivumilia makosa madogo madogo ya kiuandishi namtiririko wa matukio nitakayokuwa nikiyafanya.

TheSecond Door- Episode 16

Baada ya Rweyemamu kumpata Brenda nakugundua kuwa alikuwa anahitilafu za kiafya, anaamua kuingia gharamana kushirikiana na familia ya Brenda kumsafirisha Brenda mpaka Nchiniuingereza kwa ajili ya matibabu ya haraka.

Siku ya jumapili ikiwa ni siku moja tuiliyosalia kabla ya Tarick kwenda kujipandikiza kwenye familia mpya,ambapo atatakiwa kwenda kuishi kama Ramson Sanga. Wakiwa kwenyemaandalizi ya mwisho mwisho, Tarick, Roby na Zubery wanajaribukumvalisha Tarick baadhi ya mavazi aliyokuwa akipendelea kuvaaRamsoni, zoezi hilo lilienda sambamba kabisa na mazoezi mengine yakuiga mitingo ya uongeaji, na vitendo vya Ramson, yote hii ni katikakuhakikisha kuwa Familia ya Ramsoni kwa namna yoyote ile hawamgunduiTarick kuwa sio Ramson ndugu yao.

Baada ya kufanya maandalizi hayo kwatakribani siku nzima, Zubery anaamua kuaga haraka haraka na kuondokakwenda kukutana na kamanda Mwamkonge ili akakamilishe dili lakumkamatisha Tarick na kuchukuwa Mshiko wake.

Nchini Uingereza kwenye matibabu yaBrenda, Madaktari bingwa wanagundua kuwa Baada ya tukio la Brendakunywa sumu, Kiasi kikubwa cha kemikali kiliingia kwenye ubongo nakupelekea tatizo hilo la kuchanganyikiwa akili. Madokta wanaipafamilia ya Brenda Taarifa hizo na kuwaambia kuwa watamfanyiaoparesheni ya ubongo, lakini Brenda atapata tatizo la kupotezakumbukumbu za matukio mengi ya nyuma. Tatizo hilo halitakuwa shidasana kwa familia ya Brenda hivyo wanasign na kuwaruhusu madaktariwaendelee na oparation.

Zubery akiwa na Kamanda mwamkongeanapanga nae na kukubaliana mpango mzima wa kumtia mikononi Tarick.Ili asijulikane kama yeye ndiye aliyemkamatisha, Zubery anaamuakumchomesha Tarick siku ya kwanza tu atakayoingia kwenye maisha mapyaakiwa kama Ramson sanga. Mpango huo unaiva kisha kikosi maalum chapolisi kinaundwa na kufanya maandalizi ya aina yake kwaajili yakufanya uvamizi wa kumtia nguvuni Tarick siku ya jumanne.

Jumatatu alfajiri Roby anaamkia kazini,kisha anawasiliana na Zubery kuwa zoezi la kuondoka Tarick inabidiwalifanye usiku ili isiwe rahisi kwa ndugu wa familia hiyo kumtiliashaka. Jioni inaingia, Roby anarudi na kukuta Tarick amejiandaavyakutosha. Muda huo Zubery alikuwa makao makuu Polisi akikamilishamipango ya mwisho mwisho ya kujiingizia mamilion.

Mungu anasaidia Oparation ya Brendainaenda vizuri, anapona kabisa, lakini kama madaktari walivyokuwawamesema, Brenda sasa amepoteza kumbukumbu za matukio mengi sanayaliyowahi kutokea kipindi cha nyuma cha maisha yake. Hivi sasahakumbuki tena kua aliwahi kunywa sumu, wala kukumbuka kama kulikuwana mwanaume ambaye alikuwa akimpenda sana ambaye ni Tarick. Madaktariwanamkabidhi mgonjwa kwa wanafamilia na kuwapa masharti mengi ikiwemona sharti la kutomuacha Brenda akae kwenye mazingira yoyote ambayoyatampa msongo wa mawazo pia wahakikishe hawamsimulii tukio lolotelililopita ambalo litamuumiza. Wanandugu hao wanapokea maagizo yoteya Wataalamu na kumchukuwa mgonjwa wao tayari kwa safari ya kurejeaTanzania.

Baada ya kutoka kituo cha polisi,Zubery anarudi haraka kwaajli ya kumuwahi Roby na Tarick, safari yaZubery inamfikisha nyumbani kwa kaka yake wanasalimiana kisha Zuberyanauliza, "Brother nini kinaendelea ! " Roby anamjibu, "NahisiTarick atakuwa ameshaenda maana mimi mwnyewe nimerudi kazinisijamkuta". Maneno hayo yanamstua Zubery, "Kha! Ameondokajemwenyewe wakati tulikubaliana tukutane hapa kwanza?" Roby hukuakiwa hana wasi wasi kabisa anasema, " Tulishampa information zote,hakuna sababu ya kuwa na wasi wasi, yule ni mtu mzima, penginealipoona tumechelewa kuja akaamua aende tu". Baada ya mazungumzohayo Zubery anaona hata hivyo hakuna kilichoharibika anamuaga kakayake na kurudi nyumbani akisubiri kesho saa nne kwenda kumchomeshaTarick kama alivyokuwa amepanga na kamanda Mwamkonge.

Kesho yake alfajiri askari wanafanyamaandalizi ya mwisho, inafika saa nne wanajikusanya na kwenda mpakakwenye nyumba waliyoelekezwa na Tarick lakini baada ya kufika hapowanakuta mtu waliyetarajia kumtia nguvuni hayupo.

Marafiki, naomba niishie hapa, keshonitajitahidi nikamilishe Season One ya Tamthilia hii kwa kusamarizeseason nzima na hitimisho lake ili nianze season two kwa Nguvu mpyahali mpya na kasi mpya, Season two ndio funga kazi ya Tamthilia hiimikasa mizito na ya kusisimua ya kimapenzi na maisha kwa ujumla kaamkao wa kula. Nawapenda sana
 
Back
Top Bottom