The Second Door (Tamthilia)

The Second Door (Tamthilia)

Ipigie kura simuizi hii

  • Nzuri Sana

    Votes: 9 56.3%
  • Inafaa Kusomwa

    Votes: 5 31.3%
  • Yakawaida

    Votes: 0 0.0%
  • Sijaisoma

    Votes: 2 12.5%

  • Total voters
    16
Umetishaaaaaaaaaaaa nilijua ndo mwisho unataka kutuacha njia panda.
 
THE SECOND DOOR- Episode 10

Naam mpenzi msomaji, Niwakati maridhawa, tunaokwenda kukutana kwa ajili ya kuendelea na Tamthilia yetu ya the Second Door katika sehemu ya 10.

Mara ya mwisho katika Episode Ya 9, tulimuona Frank mapema alfajiri akiwa anawahi kuelekea Unix Network ambako mara ya mwisho alivyoenda alikubaliana nao kuwa angerudi leo kwa lengo la kufanya ukaguzi kama network yao ilikuwa salama kwa ajili ya usafirishaji wa hiyo database. Frank akiwa njiani baada ya kugundua kuwa Jina lake lilikuwa kwenye most wanted list ya polisi, analazimika kuongeza umakini mkubwa kwenye kila hatua anayopiga. Akiwa njiani anahakikisha macho yake hayagongani na ya mtu yoyote, lakini pia sasa hivi anaona ni vyema kuacha kabisa kupita njia zenye msongamano wa watu ikiwa ni pamoja na kutumia usafiri wa uma. Safari ya Frank inampeleka mpaka kwenye ofisi za Unix Network, tofauti na alivyokuja awali safari hii anapokelewa vizuri kama mgeni wa heshima. Frank anafika kwenye chumba cha maengeneer, na kutoa Laptop yake na Kifaa ambacho hakuna mtu ambae aligundua kuwa kilikuwa na kazi gani. Lakini kama unavyojua ingekuwa aibu sana kwa maingeneer wale kuanza kuuliza kuwa kile kilikuwa ni kifaa cha nini. Kilikuwa ni kifaa chenye umbo Fulani hivi la mraba na antenna ndogo, kifaa hiki Frank atakitumia kuhakikisha hakuna mtu yoyote ambae anaweza kugundua nini alikuwa anafanya pale, kilikuwa na uwezo wa kuzuia conection yoyote ambayo pengine ingetumika kutrack(kufatilia) vitu anavyofanya Frank muda ule.

Kama ilivyo kawaida hususan kwenye miji mikubwa kama Dar Es Salaam Taarifa za anatafutwa huwa sio ngeni kwenye kurasa za magaazeti, watu husoma na kwakutumia mazoea huzipuuzia, lakini kutokana na Donge nono la kiasi cha shilling million 5 zilizo tangazwa, zinafanya kila mmoja ajute kwanini hamfahamu huyo mtu anaetafutwa. Zikiwa zimesalia siku tano tu kabla ya hukumu ya Tariki na kundi la magaidi wengine 9 kunyongwa, Rweyemamu mheshimiwa ambaye moyo wake ulishindwa kabisa kupata U-turn ya mahaba dhidi ya mrembo Brenda, baada ya kuset Plan Kabambe ya kutumia jeshi la polisi kumnasa mtu anaemchezea akili na kukinasa kipenzi chake anaamua kuvuta pumzi ili atizame kama mpango huo utazaa matunda, akiwa ametulia Ofisini kwake, anamwita secretary wake na kumwambia, amwandikie Bosko Barua ya likizo ya mwezi mzima ili ashughulikie afya yake vizuri.

Frank Huku akiwa anaamini kabisa kuwa hata pale alipo hapakuwa salama hata kidogo, anaamua kufanya alicho kuwa anafanya chapchap. Akiwa anaendelea kufanya mambo, anaingia Engeneer mmoja akiwa ameshikilia Gazeti la udaku, anasalimia kila mmoja na kukaa sentimita chache kando ya Frank, anakunjua gazeti lake na kuanza kusoma. Akiwa amekunjuwa gazeti hilo, kwenye kurasa ya nyuma kabisa Frank anaona maandishi makubwa yakiwa yanasema Jasusi La kimataifa kutoka Kongo lakimbilia Dar. Gazeti hilo linapamba habari hiyo kwa picha kubwa ya Frank ambayo haina muonekano ang'avu kutokana na waandishi wa gazezi hilo kutumia picha ya paspotsize ambayo ilikuwa imetolea na polisi na kuikuza kisha kuipamba kwa nakshi nakshi za milipuko na maganda ya Risasi. Halikuishia hapo gazeti hilo, habari hiyo inaendelea kwa subtitle zilizokuwa zinasema, Laishi Dar kwa zaidi ya wiki 3. Atakae Likamata Kutajirika. Polisi waapa kulinasa. Gazeti hili linamfanya Frank akose amani, Jasho linamtoka katika jitihada za kufunga funga na kumalizia alichokuwa akifanya.

Mpenzi msomaji, alichokuwa akifanya Frank Ndani ya Kampuni hii ya Unix Telecom haikuwa Kuchunguza Usalama Wa network kama alivyodai Bali ilikuwa ni kupekenyua mwanya wa kupata access na Database za magereza ili afanye mpango wa kuzihack na ikiwezekana uharibifu huo utumike kumsaidia Rafiki yake ama, usaidie kutimiza adhma hiyo. Akiwa anasubiri baadhi ya taarifa zijisevu ili kumalizia shughuli yake, yule jamaa aliekuwa na gaazeti anafikia kurasa moja kabla ya kudondokea kwenye kurasa yenye taarifa ya Frank. Frank anaamua kuomba kipande cha mwisho ili asome. Cha ajabu ni kwamba, moja kwa moja Frank analigeuza gaazeti lile nyuma mbele ili wasione ile taarifa ambayo ilikuwa inamuelezea yeye, kisha anaanza kuzuga kama anaisoma bila kusoma hata herufi moja. Ndani ya wakati huo Frank hakuwa akifahamu kuwa mwenzie alikuwa akiifatilia habari kamili kwenye kurasa ya ndani, Frank anaamua kwenda chooni ili kuweka kipande kile cha gaazeti mbali na eneo hilo. Anauliza choo kiko wapi, anaelekezwa na kutoka kwenda chooni, choo hicho kilikuwa humo humo ndani hatua kadhaa tu ukutoka kwenye chumba cha ofisi ya maengeneer. Kitendo cha Frank kutoka tu, huku akiwa ameacha begi na computer yake, Yule jamaa aliekuwa akisoma gaazeti anasimama mbio mbio pembeni kidogo na kupiga simu kituo cha polisi. Huku chooni Frank akiwa hana hata moja, kumbe ndani ya muda huo General maneger nae alishaliona tangazo la kutafutwa Frank, kisha akawasiliana na askari ili kuhakiki taarifa hizo na jinsi atakavyopata malipo yake halafu akawaelekeza mahali ofisi zao zilipo.

Mpenzi msomaji Upande mwingine, Mbali na kwamba mama yake na Tariki alikuwa ameondolewa wasi wasi kabisa na Frank kuwa Tarick Lazima atarudi na mipango yote ye kumrudisha ipo sawa, lakini kwa kuzingatia usemi wa Kiswahili unaosema uchungu wa mwana aujuae mzazi, leo mama huyu anashindwa kuvumilia na kuamua kwenda moja kwa moja kwa moja gerezani angalau akamuone mwanae, Kufika gerezani mama huyu kama kawaida anakutana na kizuizi kutokana na lile Karatasi. Yule mama anaangua kilio kwa uchungu mbele ya wale maafisa magereza, Wakati akiendelea kulia, mara mkuu wa gereza hilo anatokea na kuuliza shida ya mama huyo kisha anaelezewa, huruma inamjaa ofisa huyo na kuwaambia wamruhusu aingie. Moja kwa moja askari anamuongoza mpaka pale alipofungwa Tarick. Tariki kusikia nyayo za mtu akiwa anamsogelea kwa mbali, anazigundua nyayo za mama yake, Uchungu unamkamta Tarick kwani hakutaka mama yake kipenzi amuone akiwa katika hali aliyo nayo, alikuwa amepururuka mwili mzima, kila kona ya mwili wake ilikuwa na jeraha lililokuwa likitokana na mateso aliyokuwa akipewa kila kukicha, Sehemu ya juu jicho lake iliyokuwa inashikilia kope inaonekana kutunga usaa, macho yanacheza cheza na kuonesha kama mtu anae dhurika na nuru ya jua. Nondo za gereza zilizo kuwa zikimtenganisha na mtu yoyote aliekuwa akienda kumsalimia zinashindwa kumzuia kumkumbatia mama yake, Anakumbatiana na mama yake na wote wawili wanalia kwa uchungu. Wanatumia muda mrefu huku wote wawili wakiwa wanashindwa hata kutoa sauti, mama anajikaza na kusema huku akilia," la ilaha illallah….. Alhamdulillah Mwenyezi Mungu atawalipa, wote walionifanyia hivi mwanangu watalipiwa na mwenyezi Mungu, hata wasipolipiwa leo, inshallah muhukumu wa haki atawalipia hata kiama kwa mola" mama anaendelea kuongea maneno hayo kwa uchungu na maumivu makubwa moyoni mwake, frank anashindwa kabisa kuongea na kuishia kulia kwa uchungu. Tukio hilo linamtia huzuni hata Mwanadada askari aliemsindikiza mama eneo lile. Hatimae Dakika tano za mama kumuona Frank zinakatika, kisha askari anamsindikiza mama kutoka eneo hilo.

Tukirudi Unix Telecom, askari walioletwa na general maneger wanafika maramoja na kuingia mkumku mkumku. Frank akiwa chooni anajaribu kupitia kile kipande cha gazeti na kugundua kuwa habari kamili ilikuwa ukurasa wa ndani, Anapata picha moja kwa moja kuwa ndio maana yule engeneer alikuwa bize akisoma kurasa ya ndani.Frank anapata picha kuwa lazima yeye alipotoka yule engeneer atakuwa ameita polisi. Frank anaamua kutoka mle chooni, ila anagundua purukushani kubwa ndani ya kile chumba cha ofisi ya Maengeneer. Askari mmoja anasikika akisema kwa amri ya ukali,"Kila mmoja alale chini kisha aweke mikono kichwani, ukijaribu kufanya kitendo chochote ambacho sijakuelekeza hata kupiga chafya nakupasua kichwa, ni sekunde moja tu. Hatujaja kuwinda sungura hapa", maneno haya yakiwa yanazingumzwa wote walikuwa wamelala chini huku bunduki zikiwa vichwani mwao.

Frank anatoka taratibu lakini kwenye mlango wa kutokea nje kuna askari mmoja amesimama na wengine wawali wapo kwa nje kwenye gari. Inakuwa kama bahati kabla ya frank hajatokeza kuna Dada mmoja anatokeza kutokea kwenye chumba kidogo cha Stoo huku akuwa amekumbatia kapu kubwa ambalo linaonekana likimzidia nguvu, haraka haraka Frank anampokea lile kapu na kulibeba kwa mtindo wa kulikumbatia. Lile kapu lilikua na mapanzia ya Jengo zima la ofisi na hawa waliokuja kuyachukua ni watu wa dry cleaner. Frank akiwa anaongozana na yule dada anatoka mpaka nje, baada ya kupita pale mlangoni yule askari anatilia shaka watu waliotoka nje, anamuuliza yule dada wa reception, "ni wakina nani wale?" kutokana kutiwa hofu na hali iliyokuwa ikiendelea yule dada anajikuta akipiteza kumbu kumbu kuwa msichana wa Dry cleaner aliingia store peke yake na wametoka wawili anajibu swali alilokuwa ameulizwa kwa kusema,"Ni watu wa DryCleaner". Yule askari anaitikia kwa mdomo na kutikisa kichwa lakini anaonekana kama hakuwa ameridhika vizuri. Kidogo maaskari waliokuwa kwenye ukaguzi kule kwenye chumba cha ofisi ya Maengeneer wanatawanyika ovyo mle ndani nakupekua kila chumba baada ya kuambiwa huyomtu wanae mtafuta alikuwa ametoka hapo sekunde chache tu zilizopita na kuingia chooni, askari wanamtizama chooni na umkosa hatimae wanakagua jengo zima. Wakati zoezi hilo likiendelea, yule dada wa DryCleaner alietoka na frank anarudi kwani alikuwa amejisahau na kuondoka na funguo za stoo. Anazikabidhi na Kuondoka.

Pamoja na Frank kuwaponyoka Askari hao, lakini wanafanikiwa kuitia mikononi Computer yake na begi lake na kuondoka navyo moja kwa moja kuelekea kwa wataalamu wa usalama wa taifa TIS(Tanganyika Intelligency Service) wakiwa na Engeneer Mmoja wa Unix Telecom. Huku nyuma General maneger ana waweka kikao cha dharura na wale maengeneer na kuanza kuwauliza kama hajafanya uhalibifu wowote, Mwisho anawaambia endapo ikionekana kuna hasara yoyote amesababisha watawajibishwa wote wanaofanya kazi katika chumba chao kwa uzembe. Baada ya hapo anatoa amri ya kubadilishwa kwa security setting za kila eneo. Frank anaenda moja kwa moja mpaka kwenye mgahawa waliko Dokta Roby na Brender, akiwa anataka kuingia ndani ya mgahawa huo mara simu yake intoa notification kuasilia Email mpya ilikuwa imeingia. Email hiyo ilikuwa imetoka SouthAfria kwa Bosi wake na ilikuwa ikimuuliza vipi kuhusiana na matatizo yake na endapo anahitaji msaada wa aina yoyote. Frank anajibu ile Email kwa kusema Anamshukuru mungu kwani kila kitu kipo poa na siku ya nne kuanzia leo atakuwa SouthAfrica. Baada ya kutoka Kwenye Ofisi za Unix Frank aliamini kabisa kuwa kila kitu kilikuwa kimemalizika. Anafika chumba walichokuwa kisha baada ya salamu Frank anaulizia hali ya mgonjwa na kuendelea kumtizama. Wakati huu Brenda alizikuonesha matumaini, anakuwa kama mtu aliekuwa anataka kusema neno Lakini kinywa chake kinakuwa kizito. Frank anamsogelea na kujaribu kumuongelesha,"Brender Frank nipo hapa!" Brenda ananyanyua mdomo lakini inashindikana kutoa sauti, Frank anashusha pumzi na kukata tamaa. Anageuka upande wa pili analiona Gaazeti lenye tangazo la kutafutwa kwake.

Tangazo hilo linamfanya Frank apigwe na butwaa kwani dokta Roby hakuwa na kawaida kabisa ya kusoma magazeti, analisogelea na kuanza kulisoma, Robi anashtuka na kusema, "Kha! Zubery amesahau gazeti lake? ". Kauli hiyo inamstua Frank na kumuuliza Roby,"Ni la Zubery!? Yupo wapi" Rob anajibu, "alifika hapa mapema asubuhi tukapiga piga story kisha akaondoka, ila amenipigia simu kuwa kunadharura nirudi nyumbani haraka, hapa nilikuwa nakusubiri wewe tu ili nikuache mara moja". Maelezo hayo yanamtia shaka Frank, anamtizama Roby na kumpa lile tangazo asome. Akiwa anasoma tangazo hilo dokta Roby anapigwa na butwaa kisha kabla hajafungua mdomo kusema chochote Frank anamwambia,"anataka kuniuza?" Roby anajibu haraka haraka,"sio Rahisi" kisha wote wanakaa kimya kwa sekunde chache, halafu Roby anaendelea kwa kusema,"Lakini naweza kuwa na shaka, kwani alizungumza sana na simu kwa siri akiwa hapa, na mara ya mwisho alitumia simu yangu, ila kabla hajazungumza simu yake iliita akaongea nayo na kuniaga kuwa fundi anaetengeneza pikipiki yake amemwita halafu kuondoka". Frank anamwambia Roby,"Hebu nione simu yako!" Robi anampa kisha frank anasearch namba ya mwisho kutumika halafu anamuuliza Roby kama alikuwa akiifahamu ile namba Roby anakataa Frank anaamua kuipiga.

Askari waliokuwa wametoka Unix wakiwa na Engeneer mmoja wa kampuni hiyo, wanaenda mpaka kwenye TIS ndani ya kitengo cha Technohama, na kuanza kuifanyia uchunguzi ile Komputer na kupekua pekua begi la frank. Ndani ya begi wanakuta kamera ndogo ya Samsung, modem, Bisibisi ndogo na Gloves. sanjari na hivyo wanakuta vifaa vingine ambavyo hata mimi mpenzi msomaji nashindwa kuvielewa. Baada ya hapo wanajaribu kuwasha computer lakini kabla ya kuwaka komputa hiyo inadai password. Wanakuja wataalamu wa Forensic zaidi ya watatu kujaribu kuicrack ile password lakini inashindikana. Baada ya kupoteza masaa 5 kwenye zoezi hilo jamaa wa forensic wizarani hapo wanaanza kudai kuwa hakuna haja ya kuendelea kuhangaika, Waifungue kisha watoe hard disk na baadhi ya vifaa kutoka ndani ya hiyo computer halafu watumie vitu hivyo kupata Taarifa zote za hiyo computer. Wanamaliza kuifungua, lakini ndani wanakutana na kitu cha ajabu, kwani muundo wa ndani wa computer hiyo ulikuwa ni wa tofauti kabisa na komputa wanazo zijua, na kikubwa zaidi computer hiyo haikuwa na HardDisk(kifaa cha kutunzia taarifa ndani ya komputer). Kila mmoja anapata mshangao huku akiwa haamini anachokiona.
Hapo wanapata jibu kuwa ile ilikuwa ni toy na sio computer halisi. Askari hawa Wanashindwa kujua kuwa, Frank hakuwa akitumia hiyo computer, Bali aliitumia computer hiyo kama remote control iliyokuwa ikimuwezesha kutumia computer ya ofisini kwake nchini south Africa. Kwa kutumia technolojia hii inayofahamika kama (RCA) remote Computer Access, Frank alikuwa akihitaji computer yoyote ile ili kuaccess computer yake ambayo ndio alikuwa akiitumia kufanya kila kitu, na komputa waliyokuwa wameikamata wale askari, ilikuwa ni computer maalum kabisa kwa ajili ya kazi hiyo na ilimfaa sana frank katika kudhibiti usalama wa taarifa za kazi zake huko south Africa. Magamba ya mlimani ya maengeneer wetu yanashindwa kufua Dafu dhidi ya Technolojia hiyo ya kitoto na kuishia kudai kuwa ile haikuwa computer bali ni toy tu ambalo Gaidi alilitumia kufanikisha shughuli zake ndani ya ofisi za Unix, madai hayo ya polisi yanaishia hapo bila kusema kuwa shuguli alizokuwa akifanikisha Gaidi huyo ndani ya Ofisi za Unix network zilikuwa ni shughuli gani.

Tukirudi huku kwa Kwenye mgahawa wa wahindi, Frank baada ya kupiga ile namba ambayo ndio ilionekana kuwa namba ya mwisho kutumiwa na Zubery kabla hajaondoka mahali pale, ile namba inapokelewa na askari. Kumbe ndani ya muda huo kijana zubery alikuwa ameshavutiwa na dau la kiasi cha Tsh 5m zilizokuwa zimetangazwa na Jeshi la polisi. Na simu hii aliyopiga frank, ilikuwa ni ya afisa mmoja wa polisi ambaye alikuwa akishirikiana na Zubery kutengeneza channel hiyo. Kumbuka kuwa Zubery alipochukua simu ya kaka yake na kutaka kupiga, simu yake iliita na kuahirisha zoezi hilo, hivyo simu ya huyu askari inavyoita hakuweza kuigundua ile namba kuwa ni ya kaka yake na Zubery. Anapokea ile simu na kusema, "Inspector Ziki naongea, nani mwenzangu?" Frank baada ya kusikia hivyo na kugundua kuwa ile ilikuwa ni namba ya askari, anakata simu mara moja na kusema,"Ni polisi!". Kwa hasira dokta roby anasema, "-------!" Frank anasema ,"Acha mimi niondoke nyinyi bakini hapa", Roby kwa msituko na mshangao anasema,"Kha! Si watanikamata mimi?" frank anamtazama na kumwambia, "Hawakutafuti wewe" Roby anaishia kuduwaa huku akiwa hakubaliani kabisa na maneno ya Frank, anawaza kuwa pengine Frank anataka kumuuzia msala. Roby anaona ni vema kumuacha Frank aondoke ila akisha toka tu na yeye achomoke na kumtelekeza Brenda.

Frank Bila kusubilia kauli yoyote kutoka kwa Roby anatoka ndani ya chumba hicho kwa kasi, kabla hajafika popote, kasi yake inasimamishwa na Diffender 3 za polisi zinazopaki kwa fujo mbele ya mgahawa huo na kushusha timu ya makomando wa jeshi la polisi wakiwa na siraha za kila aina chini ya Kamanda machachari almaarufu kama ACP Kidevu. Wanatua morali hali ya juu eneo hilo na kuanza kazi mara moja. Frank anarudi kwa kasi mpaka ndani alikomuacha Dokta Roby. Roby na yeye akiwa ndio anataka kutoka anashtuka kumuona Frank akirudi kwa kasi, Roby anauliza kwa mshangao,"Vipi!?" Frank anajabu,"Polisi". Ndani ya muda huo Zubery alikuwa pamoja na inspector Ziki. Kabla ya kuwapa dili hilo zubery alidai kwanza apewe Sh 1,000,000 hapo hapo kisha zoezi likifanikiwa watammalizia million 4 zinazobaki. Polisi walimpa, lakini walimzuia kuondoka mpaka watakapothibitisha kuwa taarifa alizotoa ni sahihi.

Hapa kwenye mgahawa ACP Kidevu(ACP=Asistance Commisioner of Police) Anatoa amri kwa askari kuanzia pale mlangoni,"Nyie watatu mnasimama hapa hakikisha hata panya hakatishi kutoka nje" wote wanaitikia, "Sawa Kamanda", Kidevu anaongoza askari walio baki kupekua jengo zima. Frank pale ndani akiwa amesha sarenda anaamua kujaribu bahati ya mwisho. Mara moja anamfunua Brender shuka alilokuwa amefunikwa na kutatua Blauz aliyokuwa amevaa kisha anaivua. "Vua nguo haraka," Franka anamwambia Roby huku akimtazama usoni. Roby kwa mshtuko na mshangao anasema,"akha! Nivue nguo! Halafu iweje?", Frank anajibu" Mimi napanda juu ya dali wewe utalala na Brender kama wapenzi hapa kitandani, Fanya hivyo halaka" Roby akiwa hajiamini kabisa ana vua nguo zote na kubaki na nguo ya ndani, kisha anapanda kitandani na kuanza kuvuta shuka. Ni ndani ya sekunde hiyohiyo askari wanatoka ndani ya chumba kimoja na muda huu inakuwa ni zamu ya kukagua chumba cha kina Frank, Dokta Roby akiwa amesha lala anasahau kuhifadhi nguo alizovua na kuzitupia pale chini, Frank anaBuruza meza kidogo ili kuiweka usawa wa kimlango kidogo cha kuingilia juu ya paa la jengo hilo, Kwa bahati nzuri, kamlango hako kadogo hakakuwa kameshikizwa kwanguvu hapo juu, hivyo Frank anafanikiwa kukafungua, kisha anadandia hapo juu na kujivuta mpaka anapotelea kabisa juu ya dali. Kitendo cha Frank kurudishia tu kale ka mfuniko askari wanapiga mlango teke na kuingia humo ndani kwa fujo, kama askari hao wangekuwa makini kidogo tu kutizama juu wangeweza kuuona mfuniko huo ukiwa unarudishiwa. Fujo wanazoingia nazo wale askari zinapelekea dokta Roby ajifanye amekurupuka kutokea usingizini, wakati huo huku askari wengine wakiendelea kupekua chini ya uvungu, chooni nakila kona ya chumba hicho, Mmoja anamuinua kichwa Roby kwanguvu halafu wanajaribu kufananisha sura ya Roby na ile waliyokuwa nayo kwenye Kitabu. Wanagundua kuwa hakuwa yeye. ACP Kidevu anasema,"Hili ni Rituhumiwa la mungu linaonekana limechepuliwa njia kuu…… -------!" akiwa anamalizia kuongea maneno hayo anageuza shingo ilia toe amri ya kukagua chumba kinachofata, mara anagundua nyayo ya mtu ikiwa imekanyaga juu ya kitambaa cheupe cha meza ndogo ndani ya chumba hicho, macho yake hayaishii hapo anaitizama ile meza nakuona mburuziko kutoka pale ilipokuwa awali anaisukuma taratibu nakurudisha ilipokuwa awali kisha anasema, "mmoja apande na kukagua juu ya dali." Frank akiwa juu mle dalini anaona mfuniko wa dali ukifunuliwa, analala taratibu chini kabisa. Mpenzi msomaji, juu ya hilo dali ni sehemu ambayo hakuna binadamu anaeweza kukaa kwa zaidi ya dakika tatu au kuhimili dakika 10 akiwa hai, kwanza sehemu hiyo haina hewa ya kutosha, pili huko juu limepita bomba la kutolea moshi nje ya jiko la restaurant, bomba hilo linauwazi ambao unavujisha moshi na kuusambaza juu ya dali lote, mwisho juu ya dali hilo kulikuwa na joto kali sana na giza ambalo linasababisha Hata frank asione anachokishika wala sehemu anayokanyaga. Yule askari anabebwa na wenzie na kuchungulia juu kwa nusu Dakika tu, anapiga kelele ashushwe. Baada ya kushushwa anashindwa kusema kuwa kunagiza kubwa na ameshindwa kuona chochote akihofia kupandishwa tena na tochi, badala yake anasema kuwa wanaemtafuta hajapanda huko. Huo unakuwa mwisho wa ukaguzi wa chumba hicho, wanatoka na kuelekea vyumba vingine. Frank baada ya kugundua kuwa wale askari walikuwa wametoka ndani ya chumba hicho anajivuta taratibu na huku akiwa ameishiwa nguvu kabisa, anaongeza kasi ili awahi kupata hewa safi chini. Bila kugunduwa akiwa anazidi kujiburuza pale chini huku akiwa hoi Frank anagusa waya wa umeme ambao ulikuwa ukipitisha mkondo mkubwa wa nguvu za umeme kuelekea kwenye jengo la jirani. Frank anapigwa na shoti kali kidogo tu imkaushe kabisa pale juu lakini inakuwa bahati Socket Breacker inakata umeme wa jengo zima na kumnusuru licha ya shoti hiyo kumfanya awe na hali mbaya kabisa. Frank akifahamu wazi kuwa sasa yupo ukingoni mwa uhai wake anajitahidi hivyo hivyo mpaka anaufikia uwazi wa kushukia chini.

Dokta Robi baada ya kuachiwa na wale askari anajifunika Shuka ghubighubi huku akiwa haamini kama amesarimika tena kwa mara ya pili. Akiwa anamalizia dua ya mwisho kumshukuru mwenyezi mungu kwa kumnusuru, Frank anajitupa mzima mzima kutoka juu ya dari na kudondokea pale chini. Roby anakurupushwa na kishindo kikubwa cha kudondoka Frank pale chini, Anapigwa na butwaa kuona frank akiwa amechakaa, mwili mzima amekuwa mweusi tiiii, Roby anatahamaki na kupigwa na Butwaa kisha anamkimbilia na kusahau hata kuvaa nguo, anauliza kwa mshangao,"Frank……. Frank! Nini kimetokea frank…. Mungu wangu…." Robi anaiangalia ngozi ya Frank na Kugundua kuwa alikuwa amepigwa na shoti kali sana ya umeme anakimbilia maji maalum yaliyokuwa kwenye mkoba wake na kumnywesha. Frank akiwa yupo hoi kabisa anamwambia Roby,"Roby ahsante, ahsante sana….. nashukuru, naomba nipe laptop yako na modem mara moja". Roby anamjibu frank, "Hapana achana na hivyo vitu niite Ambulance nikuwahishe hospitali hali yako ni mbaya sana",Frank anamjibu kwa kumwambia, "Mimi siwezi kupona Roby, ninakazi moja tu ya kumalizia kabla sijakata Roho" Roby kwa mshtuko anasema,"Acha kusema hivyo! Wewe sio Israeli na hata ungekuwa Israeli huwezi kujitoa roho mwenyewe. Ngoja kwanza…" Roby anatoa simu yake na kupiga kuita ambulance. Kumbuka Roby alikuwa ni Mkuu wa kitengo cha Upasuaji Kwenye hospitali ya Taifa, hivyo angeita ambulance mara moja ingefika eneo lile. Frank anamsimamisha Roby kupiga simu na kumsihi ampe laptop na modem amalizie kitu kimoja. Roby anamtizama Frank na kukosa la kufanya anaamua kumletea Laptop na modem alivyokuwa akihitaji.

Frank akiwa amelala pale chini anaconnect ile laptop kwenye internet na kuanza kufanya jambo moja. Wakati Frank alipoenda Unix Network alienda kwa lengo la kuiba taarifa za usalama za database ya gereza alilokuwa amefungwa Tarik, aliamua kufanya hivyo mara baada ya kujaribu kuivamia database hiyo na kukuta watu wa Unix wameiwekea usalama mkubwa, hapo akaona njia pekee ni kwenda kuiba taarifa za siri kule kule unix. Frank alifanikiwa kupata taarifa hizo kabla ya kuvamiwa na askari pale unix, na kama nilivyoelezea hapo awali kuwa dakika zote Frank alikuwa akifanya shuguli zake kwa kutumia computer iliyokuwa ofisini kwake southAfrica, na popote alipo kuwa alikuwa anaweza kutumia computer yoyote kama remote controll ya kuwasiliana na komputa yake. Anachokifanya sasa hivi ni kitendo kinachojulikana kama Database attacking, kitendo cha kuiingilia stoo ya kumbukumbu kwenye hifadhi ya kumbu kumbu ya Gereza alilokuwa amehifadhiwa Tarick. Frank akiwa yupo hoi huku nguvu zikimuishia kadri alivyokuwa akiendelea kufanya ileshuguli anamwambia Roby kwa sauti ya chini iliyokuwa ikikatakata."Roby, Tarick hana hatia sawa? Naomba unisaidie kumtorosha, hakikisha Serikali Dhalimu ya nchi yetu haimuoni tena". Roby anauliza kwa umshangao,"Nitawezaje kumtorosha mtu aliehukumiwa kifo gerezani?" Frank anaendelea kwa kujibu swali hilo huku akiendelea na uchokonoaji wa database ya gereza,"Nitafanya kila kitu na wewe utafanya patakaposalia... na kuhusu Brenda Nenda kamkabidhi kwa Rweyemamu mwambie ni zawadi yangu kwake" Roby anabaki kuduwaa huku akiona kama vile anaota kwa yale yanayotokea machoni pake muda huu, Baada ya kimya cha muda mfupi frank anatoa Tabasamu jepesi na kusema,"Nimefanikisha! Sasa utafanya kitu kimoja, nimebadilisha taarifa za wafungwa, taarifa ya Tarick na mtu anaeitwa Lucas Shehiza, kwahiyo fanya juu chini uhakikishe unampelekea Taarifa Tarick kuwa Jumatano ya Tarehe 16 atachukuliwa gerezani kama Lucas Shehiza na atapelekwa mahakamani kusikiliza kesi tofauti, wewe utafika hapo na kufatilia kesi yake mpya. Mwambie Tariki Asilie Juu ya kifo changu, Kwasababu mimi ninakufa na furaha ya kufanikisha kumuokoa".Frank anaanza kuvuta pumzi kwanguvu, pengine hii ilitokana na kupoteza kiasi kikubwa cha damu au maji kwenye ile shoti. Roby anapiga simu haraka Hospitali ya Taifa, lakini simu hiyo inachelewa kupokelewa, kabla hajampigia mtu mwengine Frank Anakata roho na kukauka pale pale. Tukio hilo linamtia simanzi kubwa Dokta Roby analia kwa uchungu huku akisema,"Frank amka Frank... Frank kwanini unakufa wakati hujamaliza kazi Frank.... Unakufa huna hatia Aaaaaaaa".

Ndani ya eneo hilo Polisi walipomaliza Kusachi Jengo zima na kukuta hakuna mtu waliemtafuta hayupo wanakasilishwa kweli kweli kwa kutumia nguvu kubwa na akili nyingi, kupoteza muda ndani ya jengo hilo. Kamanda ACP Kidevu anapiga simu Central na kusema kauli moja tu,"Arrest The Boy". Amri hiyo ilikuwa ikimaanisha kuwa Wamkamate na kumtia ndani Zubery ambae alionekana kutaka kufanya ujanja ujanja ili akamate zile millioni tano au hata moja ambayo alikuwa ameidai kabla ya kufanya kazi, na kuwaacha solemba wale askari. Roby pale hotelini anabeba mwili wa Frank na kuupakia kwenye gari yake, kisha anambeba Brenda naye anampakia anakusanya vifaa vyake vyote na moja kwa moja anaelekea hospitali ya taifa Muhimbili alipokuwa akifanyia kazi. Anafika muhimbili nakwenda moja kwa moja monchwari kuuacha mwili wa Frank, baada ya hapo anaenda kumkabidhi Brenda kwa madaktari wengine ambao wangeendelea kumfanyia matibabu na uchunguzi zaidi.

Mpenzi msomaji, kutokana na wadhifa wa Frank hospitalini hapo hakuna shida yoyote anayoipata wala kutiliwa mashaka na mtu yoyote, hata wakati anawakabidhi watu wa monchwari mwili wa Frank maelezo kuwa Ulikuwa ni mwili wa ndugu yake aliefariki kwa kupigwa na shoti ya umeme yalijitosheleza kabisa kumtambulisha marehemu. Huku akili yake ikiwa haijakaa sawa frank anaamua kurudi nyumbani kwake na kujipumzisha wakati akifikiria ni wapi pa kuanzia kwenda ili kujaribu kukamilisha zoezi la kumuokoa Tarick, Akiwa kajipumzisha nyumbani kwake dokta Roby anapokea simu kutoka kwa mama yake, simu hiyo inampa taarifa za kukamatwa kwa mdogo wake Zubery, Frank anapokea taarifa hizo na kuamua kuzipuuzia akidhamiria kumuacha kidogo ili agharamie malipo ya tamaa yake. Roby alishajua kuwa lazima wale askari watakuwa waliamua kumkamata mara baada ya kushindwa kumpata Frank pale kwenye mgahawa alipowaelekeza.
Kwa upande wa pili wa Tamthilia hii ya kuvutia, Upande wa Familia Ya Brenda, Baada kimya cha zaidi ya wiki nzima wanaanza kupada hofu kubwa. Dada yake na Brenda ambae alikuwa akiishi jijini Arusha, anarudi na kuungana na wazazi wake kwenda kwa Rweyemamu ili kufahamu kama alikuwa na Taarifa zozote. Familia hii ilikuwa ikimfahamu Rweyemamu kama mtu wa karibu sana na mtoto wao lakini pia ilikuwa ikijua mapenzi mazito aliyokuwa nayo mweshimiwa huyu dhidi ya mtoto wao, hivyo wote walikuwa wakiamini siku yoyote taratibu za ndoa zitakamilika na Profesa atachukua jiko.Isingekuwa busara sana kwa familia nzima kwenda kwa Rweyemamu, hivyo wanamtuma Dada yake na Brenda ambae yeye alikuwa akiitwa jestina ili akaonane nae. Jestina anafika kwa Rweyemamu na kupewa mkanda mzima wa matukio jinsi yalivyotokea mpaka kutoweka kwa Brenda, lakini Rweyemamu anaomba radhi kwa kutowataarifu kilichokuwa kikiendelea, na kudai kuwa alilazimika kufanya hivyo kwa kuhofia kuwaweka kwenye presha. Baada ya hapo Rweyemamu anamuahidi Jestina kuwa arudi nyumbani na kuwaambia wazazi wasiwe na shaka hata kidogo, kwani ndani ya siku 5 atakuwa amemkomboa Brenda kutoka mikononi mwa watu wabaya.

Baada ya Jitihada kubwa na za hali ya juu za pamoja kutoka kwa madaktari wa hospitali ya taifa, Brenda anapata nafuu, lakini anakumbwa na matatizo ya akili, anazungumza peke yake maneno yasiyoeleweka, nakufanya vitendo vilivyokuwa vikionesha wazi kuwa alikuwa ni mtu aliyekuwa amechanganyikiwa. Ikiwa ni siku nyingine tena, roby kabla ya kwenda kumuona Tarick na kumpa ujumbe aliopewa na Frank anaamua kwenda kumtazama mgonjwa wake na kuikuta hali halisi ikiwa sio nzuri. Anaamua kutoumiza kichwa kwa jambo hilo na ni vema kwa sasa akaenda Gerezani kumuona Tarick. Kesho siku ya jumatano, ndio siku ambayo Tarick atakuja kuchukuliwa kimakosa na kikosi maalum cha magereza ambacho huwa kinashughulilka na ukusanyaji wawafungwa wanaotakiwa kwenda kusikiliza kesi zao na kuwapeleka kwenye mahakama mbalimbali. Hivyo ilikuwa ni lazima Roby amuone Tarick leo na kumpa Taarifa kuwa atakuja kuchukuliwa na kwenda kusikiliza kesi tofauti na ile ya ugaidi iliyokuwa imemtia hatiani awali.
Roby anafika mpaka pale gerezani, nakujaribu kuangalia ni jinsi gani atamuona Tarick, Lakini kama kawaida anakutana na kikwazo kilekile cha list maalum kisha anaambiwa hawezi kumuona. Roby ni mtu mwenye hasira za karibu sana hivyo anajikuta akianza kuwabwatukia wale maafisa pale gerezani, lakini kabla hajaongea mengi anatokea Padri kisha anawasalimia wote na kuingia ndani, Kitendo cha padri huyo kupita kinamfanya Roby anyamaze na kuondoka eneo hilo.
Marafiki, Tumeweza kuona shujaa na mhusika machachari katika tamthilia hii akipoteza uhai wake katika harakati za kutetea haki ya Tarick, na sasa Kazi ya kukamilisha sehemu ndooogo ya kazi kubwa aliyoifanya marehemu Frank imekabidhiwa mikononi mwa daktari Roby na tayari kazi hiyo inaanza kwa mkosi mkubwa wa kizuizi cha kumuona Tarick, Je Roby anaweza akawa na akili nyingi kama Frank hatimaye akapata mwanya wa kumuona Tarick ? Kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi, utamu ndio kwanza unaanza usiache kufatilia Tamthilia hii yenye Raha za kila aina kwenye episode Namba 11.

Nawaaga wote kutoka kwenye Episode hii ya 10. Kwaherini.
Like & Comment napenda sana kujua watu wanaofatilia simulizi hii.

 
Jamani sio tunakazana kusoma tu, tangazo la DONATION mmeliona? mwenye 500, 1000, 10,000 tumchangieni apate nguvu ya kuendelea kutupa mauhondo. Jamiiforum mimi nimeshakucheck japokuwa ulinibania kuniuzia. hongera kwa kazi nzuri
 
duuuuuuuh, sasa ndo nini bana, frank hakutakiwa kufa banaaaaaaaaa, aaah kumbe ni hadith ila Jamii Forum Upo vizuri, japokuwa hapo baada ya frank kufa ukaanza kuchanganya kati ya Roby na Frank..
 
duuuuuuuh, sasa ndo nini bana, frank hakutakiwa kufa banaaaaaaaaa, aaah kumbe ni hadith ila Jamii Forum Upo vizuri, japokuwa hapo baada ya frank kufa ukaanza kuchanganya kati ya Roby na Frank..

Daaa! ujue mpaka mimi mwenyewe chozi limenitoka.... Ujue mpaka anakata roho nilikuwa sijui kama ndio anakufa. Ila Watch Out Kifo chake ndio mwanzo wa part Tamu zaidi ya hii Tamthilia.
 
I wonder! na mimi nilishtukia tu kafa? but I promice Ennie utafurahia sana kufa kwake kwani tamthilia itavutia zaidi.
 
Hadithi nzuri jaman nmeanza kuisoma leo, nmesoma yote yan natamani niendelee tu. Mungu amekujalia kipaji akuwezeshe kukitumia vizuri. Ila kifo cha Frank kimeniuma
 
Huo ni mwisho wa Episode No 9 namba 10 inakuja Juma 5. Mwisho bado kabisaaaaaa naziona kama Episode 50 hivi mbele.
Nilikua nabadilisha tu jinsi ya kumaliza Story. nashukuru kuona hii stori inasomwa na maprofessional wengine kama mizambwa I appreciating you kaka jaribu pia kuni advice how Can I Improve.

everlenk
,
Mrembo by Nature
Gunda66
Khantwe

na wasomaji wangu wote nawapenda sana.

Daaah, afadhali maana sijui ingekuwaje. Thanks mkuu, mwanzoni ilionekana kawaida ila now imekaa vizuri mkuu. Hongera.
 
Sterling hauwawi bwana...akifa ndio mwisho. Sina access na tigo wala mpesa ila nitachanga nikiwa na access navyo. Usjali we tyeena
 
Duh! JamiiForum nalia kwanini Frank,sina hata la kusema,ila majina umemix katikati na mwishoni. Big up nice story!!!
 
Last edited by a moderator:
Me najitolea kuwa mhamasishaji wa kuchangia hadithi hii.....Kama unajijua unapita hapa kujiburudisha iwe live au Kimya Kimya plssssss weka chochote kwenye mamba tajwa. Kumbukeni mhusika anatumia muda na akili kuhakikisha tunaburudika
 
Back
Top Bottom