Vijana wa kiume dhidi ya afya ya akili

Vijana wa kiume dhidi ya afya ya akili

verify

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2024
Posts
1,294
Reaction score
3,079
Kilio Kisichoonekana Afya ya Akili ya Vijana wa Kiume
Katika dunia ya leo, kuna kilio kikubwa kinachotokea kila siku… lakini hakuna anayekisikia Ni kilio cha vijana wa kiume.

Kijana wa kiume amefundishwa tangu utotoni kuwa mwanaume halisi halii, hasemi shida zake, haonyeshi udhaifu, na anatakiwa kubeba kila kitu kimya kimya amefundishwa kuwa machozi ni udhaifu, ukisema umechoka unaonekana dhaifu, ukiomba msaada unaonekana huna maana hivyo wengi wamejifunza kutabasamu mbele za watu huku ndani wakivunjika vipande vipande.

Wengi wanatembea mitaani wakiwa safi, wamevaa vizuri, wanacheka na marafiki zao… lakini ndani wana vita vikubwa Kuna anayelia usiku bila sauti kuna anayeshindwa kulala kwa mawazo kuna anayejiona hana thamani kuna anayehisi hakuna anayemuelewa. Kuna anayechoka kuigiza kuwa yuko sawa.

Jamii imezoea kuuliza kijana wa kiume: “Unafanya nini?” “Unaingiza kiasi gani?” “Umefanikiwa nini?” Lakini wachache sana huuliza, “Uko sawa kweli?” “Moyo wako ukoje?” “Una shida gani?” Watu wengi wanapima mwanaume kwa pesa, mafanikio, au uwezo wake wa kubeba wengine… lakini hawajui hata yeye mwenyewe anazama ndani kimya kimya.

Vijana wengi wa kiume wanapambana na msongo wa mawazo, depression, upweke, pressure ya maisha, mapenzi yaliyowaumiza, familia zilizowavunja moyo, ndoto zilizokufa, na hofu ya kushindwa lakini wanabaki kimya kwa sababu wanaogopa kuhukumiwa wanaogopa kuitwa dhaifu wanaogopa kuonekana sio “wanaume wa kweli.”

Kuna vijana ambao walihitaji tu mtu mmoja wa kuwaambia, “Nakuona nakusikia Upo muhimu” lakini hawakupata mtu huyo wakaendelea kunyamaza wakaendelea kuoza ndani kwa ndani Wengine wakageukia pombe, bangi, hasira, ukatili, au kujitenga si kwa sababu ni wabaya… bali kwa sababu walikuwa wanaumia
Ni huzuni kubwa kuona kijana akifa ndani akiwa bado hai nje.

Wanaume wengi hawafi kwa risasi wala ajali kwanza… wanaanza kufa ndani taratibu. Kila disappointment, kila rejection, kila mzigo wa maisha, kila maneno ya kudharauliwa huondoa kipande cha roho yao na siku wakinyamaza kabisa, watu hushangaa Lakini hawakuona vilio vyao vya kimya vya miaka mingi.

Ukweli ni huu mwanaume pia ni binadamu Anaumia, Anaogopa, Anachoka, Anahitaji kupendwa ,Anahitaji kukumbatiwa, anahitaji kusikilizwa, anahitaji kuambiwa kuwa si lazima abebe dunia peke yake.

Kwa kijana wa kiume anayesoma hii akiwa amechoka… najua umejifanya strong muda mrefu. Najua umecheka wakati ulitaka kulia. Najua umejibu “niko poa” wakati moyo wako ulikuwa unavunjika. Najua umebeba mengi bila msaada.

Lakini tafadhali usife kimya kimya.

Ongea Tafuta msaada lia kama unataka kulia pumzika kama umechoka Kuomba msaada sio udhaifu — ni ujasiri kusema unaumia sio kushindwa — ni ukweli.

Na kwa jamii nzima: tuwasaidie vijana wa kiume kabla hawajapotea. Tuwasikilize kabla hawajanyamaza milele. Tuwapende kabla hawajaamini hawapendeki.

Kwa sababu nyuma ya ukimya wa mwanaume, mara nyingi kuna maumivu makubwa kuliko maneno yanaweza kueleza.
 
Afya ya akili Sasa umekuwa kama wimbo na umeanza kuboa .

Kitu ambacho kinapelekea tatizo la Afya ya akili kuwepo ni swala la uchumi au fedha , vijana kama wapo financial broke , jobless hawana opportunity za kuwapa kipato na muda huo huo wapo katika umri ambao wanabidi kuhudumia familia zao , unafikiri kwanini wasipate mental health problem.


So jikiteni na tatizo kuliko kukaa mnaandika andika hizi mambo za Afya akili ni kama upumbavu Fulani mnafanya .


Ebu rudisha miaka 15 nyuma na Sasa uone wakati vijana wanapata fursa na wakati hawana fursa Afya zao akili zilikuwaje .

Yaani hakuna bingwa yeyote hapa duniani anaweza kushinda stress ukipitia fucking days no money no food , madeni kibao huku familia inahitaji matumizi you will noticed kuwa shit happens.
 
Kitu kingine, kuanzia utotoni wanatusigina kama kiatu bila upendo wowote halafu tukishaanza kupata kidogo shida zote wanatuletea sisi. Yaani ukiwa mwanaume nchi hii unanyonywa damu bila huruma mpaka ufe.
 
Back
Top Bottom