Kubwajinga,
Hayo mawazo yako ya kukatisha tamaa vyama vya upinzani nilikuwa nayo sana, kabla ya Kikwete haja-prove beyond doubt kwamba hana uwezo wa kuleta mabadiliko ya maana Tanzania.
Kwa taarifa yako, nadhani haitapata kutokea tena wakati mzuri kwa wapinzani kama wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mwingine hapo 2010. Yaani wapinzani wasitegemee tena kuwepo na udhaifu mkubwa katika chama cha CCM pamoja na serikali yake kama ulivyo wakati huu. Kazi tu inayowakabiri wapinzani wakati huu ni kuwapata viongozi wenye uwezo na ushawishi wa kuwavuta wananchi wakubali kuwatelekeza CCM. We need our own Railas now, the rest would be history.
Kusema kwamba CCM haiwezi kung'olewa hata kwenye urais, sio kweli hata kidogo. Kuna mifano mingi na mizuri tu inayopingana na hiyo dhana yako. Chama cha PRI kule Mexico ilikuwa kama ni 'institution' tena iliyoimarika zaidi kuliko hii CCM yetu hapa. Lakini waling'olewa, tena hata 2006 wakaendelea kucharazwa na Felipe Calderon.
Ni juzi tu, kule Paraguay - Chama cha ASUNCIO, chama kilichotawala nchi hiyo miongo sita mfululizo kiling'olewa madarakani na kumchagua Fernando Lugo(askofu aliyeng'atuka) kuwa rais wa nchi hiyo.
CCM si lolote, hasa wakati huu ambapo imekuwa dhahiri kabisa kuwa kimekuwa ni chama cha wenye pesa na wanachama wanaochagua viongozi kwa kukubali hongo.
Akipatikana kiongozi mwenye kuaminika huko kwenye wapinzani, na mtu ambaye atakuwa na uwezo wa ku-articulate vizuri matatizo yanayowakabili wananchi, na ambayo CCM imeshindwa kuyasimamia, CCM wataanguka vibaya mno! Ndio maana sisi wengine tunakazania ajitokeze/wajitokeze viongozi huko kwenye upinzani (akiwemo na Dr. Slaa ambaye amependekezwa hapa) ili tuweze kuangalia wasifu zao na kuwashawishi wajitokeze kugombea urais hapo 2010.
Bila hawa watu kujitokeza, bila shaka, ninakubaliana na wewe kwamba 'we are stuck with these CCMs eternaly.'
Asante kitila,Ndio uzuri wenyewe, kwamba tulipewa uwezo tofauti wa kuona mambo. Sasa utashindaje kama unataka watu imara na wazuri wasigombee urais? Halafu tunaongea kwenye anga tofauti sana ndio maana hatuelewani. Wewe mwenzetu unaamini kwamba CCM haiwezekani kuishinda katika urais. Sisi tunaamini kwamba ni vigumu lakini inawezekana. Na kwa sababu ni kazi ngumu ndio maana tunaifanya. Wengine hatuamini katika kufanya mambo rahisi tu; mambo rahisi kila mtu anaweza kuyafanya. Zaidi ya yote siasa haijawahi kuwa kazi rahisi na ni sababu hiyo ndiyo maana wengine tupo huko. Ni kwa sababu ya kurahisha kazi ya siasa ndio maana wenzetu wa CCM wamejikuta wanafikiri kazi ya siasa ni kujichumia na kujiondokea zako, matokeo yake wameingia huko wasio wanasiasa na walio wanasiasa wapo nje ya fence wamejikatia tamaa.
So, man we know it is hard and difficult to uproot CCM out of power and that is exactly why we're doing it. You don't consider yourself to have made an achievement by doing an easy task that everybody can do; an achievement is attained by accomplishing a difficult task such as removing CCM from power! Next please!
Hakuna cha kungoja wakati ni huu, CCM imeshavurunda vya kutosha, CCM has to go, Hatuwezi kukubali kuendelea kuongozwa na Mafisadi na Majambazi. Kwa hiyo nadhani 2010 ni muda muafaka kabisa wa kutumia kila mbinu kuwatoa madarakani CCM. Dr. Slaa for President.Asante kitila,
Kwa kukubali CCM ina mizizi ambayo ni vigumu kung'oleka,sio kwamba na mie nafurahia CCM kuwa madarakani ila nacho washauri wainzani ni wajipange kwanza..
tuanzie Chini kwanza,hata hatyua ya udiwani kwa 2010 na 2015 Muingie katika wabunge 2020 muingie katika kuweka spika kutoka upinzania na 2025 muweke Rais wa Umoja wa kitaifa.ila kwa kutaka makuu kwanza hii ni ngumu naitawasumbua sana
Hakuna cha kungoja wakati ni huu, CCM imeshavurunda vya kutosha, CCM has to go, Hatuwezi kukubali kuendelea kuongozwa na Mafisadi na Majambazi. Kwa hiyo nadhani 2010 ni muda muafaka kabisa wa kutumia kila mbinu kuwatoa madarakani CCM. Dr. Slaa for President.
Believe me or not; mwaka 2010 [endapo wapinzani hawataleta products zinazouzika] CCM watapata ushindi wa kishindo tu.Nakwambia. Mimi sijui watu wengine wanataka CCM waharibu kiasi gani ndio wafukuzwe madarakani!
Hakuna cha kungoja wakati ni huu, CCM imeshavurunda vya kutosha, CCM has to go, Hatuwezi kukubali kuendelea kuongozwa na Mafisadi na Majambazi. Kwa hiyo nadhani 2010 ni muda muafaka kabisa wa kutumia kila mbinu kuwatoa madarakani CCM. Dr. Slaa for President.
Tatizo watu mkiwa nje ya nchi mnadhani Tanzania mambo yamebadilika sana. Kisha mnakuwa na nguvu kubwa sana ya kutaka kubadilisha mambo. Ni kweli CCM na serikali yake wanakera sana. Kuanzia Bunge la maigizo (pale Bungeni huwa wanafanaya maigizo tu) mpaka serikali ya mafisadi.
Kama kweli kuna nia ya kuwatoa hawa jamaa madarakani, inatakiwa kujua mahali pa kuanzia. Pa kuanzia ni kwa Watanzania wapiga kura wenyewe. Wengi wao wako vijijini, hawana uhakika hata wa mlo mmoja kwa siku, hawapati magazeti, hawana hata maji safi ya kunywa. Mbaya zaidi hao ndio wapiga kura halisi wa Tanzania na ndio walio wengi. Je mkakati wa kuwapata hawa ni wa staili ya zimamoto? Hapana! Unahitajika mpango wa muda mrefu katika hili. Sio kelele za kwenye magazeti na tovuti.
CCM wanalijua hilo, na ndio maana mnaona kwamba wana mizizi isiyong'oleka. Jipangeni!
teh teh teh, live on the blue side of life!Khee!! Na wewe hayo mabluu ndio nini sasa? Au na nyie mnawaiga CCM na mikijani na minjano yao?
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Kalamu,
Kwanza naomba unielewe kuwa sijasema CCM hawawezekaniki ila nimesema hawatawezekana kama vyama fya upinzani vitaingia katika uchaguzi na mgawanyiko wao wa hivi sasa pamoja na baadhi ya matatizo yaliyomo ndani yao. Hata hivyo nimeorodhesha sababu chache ambazo nafikiri zikifuatwa zinaweza kusaidia kuiondoa CCM. Angalia post yangu ya hapo awali.
Kwa hiyo, ingawa ni vizuri kuwa optimistic lakini ni uzembe kuwa hivyo wakati hujadadisi na kuyafanyia kazi mazingira yanayokufanya wewe kuwa na hayo matumaini. Kwa vile Paraquay waliweza kutwaa madaraka haina maana kuwa automatically itakuwa hivyo TZ. Siasa na watu wake ni tofauti kabisa. Wapinzani wanatakiwa wajiangalie na kupanga mikakati tokea mapema, ikiwa ni pamoja kuunda muungano wa vyama mapema, ili uzoeleke kwa wananchi.
Kwa bahati mbaya, wao hadi hivi sasa wamelala kama vile wao ndo wako madarakani, halafu mwaka 2010 ukifika ndio utaanza kuwasikia wakianza mikakati na kuishia kugombana, this is stupid. Hata Obama alijua kuwa ili aweze kupambana na Mrs. Clinton, ilibidi aanze kampeni 2006 na sio 2008.
Kama kuna anayefikiria kuwa ufisadi umekiua CCM, atakuwa anajitakia mabaya mwenyewe. Mwaka 1995 wapinzani walikuwa na nguvu kuliko wakati mwingine wowote. Mrema alikuwa fresh na wananchi walimjua na kumpenda. Lakini kwa sababu ya kukosa mipangilio na migawanyiko, NCCR ikashindwa na kugawanyika. Hii ndio mifano ya kuangalia na sio ile ya S.Amerika.
Mimi nawashauri wapinzani kuwa, waanze hivi sasa kujisafisha na kujiimarisha, ili ikifika 2010 wawe wanajua kabisaa wapi watapata kura kiasi gani na wapi watawaachia CCM. Lakini kuingia kwenye uchaguzi kienyeji wakati tayari sayansi ipo na data za 2005 zipo ni uzembe na uvivu wa kufanya kazi. Sidhani Richmonduli na Radargate kama vitamuondoa JK unless naye ahusishwe moja kwa moja na hiyo miradi. Wenye masikio na wasikie.
Believe me or not; mwaka 2010 [endapo wapinzani hawataleta products zinazouzika] CCM watapata ushindi wa kishindo tu.
Wapinzani wanatakiwa kuleta vichwa vipya for God's sake. Think of it Kitila
Bila ya kuwa na mikakati kababe ya kuing'oa CCM na kutegemea tu kuwa hizi kelele za ufisadi na umaarufu wa Zito na Slaa vimeijenga Chadema kuipiku CCM, itakuwa ni kujidanganya, sawa na kusubiri nazi ambayo haijakauka ianguke.
Tatizo watu mkiwa nje ya nchi mnadhani Tanzania mambo yamebadilika sana. Kisha mnakuwa na nguvu kubwa sana ya kutaka kubadilisha mambo. Ni kweli CCM na serikali yake wanakera sana. Kuanzia Bunge la maigizo (pale Bungeni huwa wanafanaya maigizo tu) mpaka serikali ya mafisadi.
Kama kweli kuna nia ya kuwatoa hawa jamaa madarakani, inatakiwa kujua mahali pa kuanzia. Pa kuanzia ni kwa Watanzania wapiga kura wenyewe. Wengi wao wako vijijini, hawana uhakika hata wa mlo mmoja kwa siku, hawapati magazeti, hawana hata maji safi ya kunywa. Mbaya zaidi hao ndio wapiga kura halisi wa Tanzania na ndio walio wengi. Je mkakati wa kuwapata hawa ni wa staili ya zimamoto? Hapana! Unahitajika mpango wa muda mrefu katika hili. Sio kelele za kwenye magazeti na tovuti.
CCM wanalijua hilo, na ndio maana mnaona kwamba wana mizizi isiyong'oleka. Jipangeni!
Hakuna lolote hapa.
Linalotakiwa, iwe ni Mexico, Paraguay, Kenya, Zambia, Malawi, n.k., ni kumpata/kuwapata viongozi katika upinzani wenye 'charisma', ushawishi na kuaminiwa na wapiga kura. Tunataka wajitokeze akina Slaa na wengine, tumpate huyo kiongozi tutakayempa jukumu la kuwavuta wananchi.
Yote hayo unayoyasema kukosa ushirikiano na kufanya maandalizi kungali mapema, yote yanahusiana na kukosa kiongozi/viongozi hawa tunaowalilia wajitokeze mapema. Lakini wewe unawapinga wasijitokeze. Hueleweki msimamo wako upo wapi!
Ninakushangaa kama huoni somo lolote katika mifano ya Mexico na Paraguay! Nadhani unaishi katika dunia ya kipekee, au mambo ya siasa hunayo habari kabisa.
Tatizo sio product zinaouzika mkuu, tatizo ni ccm kutokuwa tayari kuachia madarakaa. Katika hili hakuna ubishi, muulize Chacha Wangwe akwambie kilichofanyika Tarime kabla msimamizi wa uchaguzi hajaamua kumtangaza Wangwe kama mbunge.
Wananchi waliamua kujichukulia sheria mkononi na wakadefy FFU na polisi ili kulinda ushindi wa Wangwe. Report zote za usalama zilionyesha kuwa Tarime ingewaka moto kama Wangwe asingetangazwa mshindi. Ilichukua masaa zaidi ya 24 kwa matokea kutangazwa na ndipo ccm wakagive up na kumtangaza Wangwe.
Wananchi wa majimbo mengine wao wanakubali tu yaishe na ndio maana ccm inashinda kwa "kishindo"
MwK'
Hili ni tatizo dogo na limekwishajulikana. Iliyobaki ni kwa wapinzani kuitangazia Tanzania yote kungali mapema kabisa kwamba upuuzi huu hauwezi kuendelea kuvumiliwa. Hayo yote na yaliyotokea Kiteto upinzani ni lazima wajiweke tayari kuyakabili kwa nguvu zote zinazowezekana. Wakati wa kulialia tu ili kuonewa huruma umepitwa na wakati.
Tatizo kubwa ni kuwaelimisha wananchi ili wawakatae CCM.