The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Hapo ndio umuhimu wa katiba kubadilishwa unapokuja, katiba ya nchi bado imekaa kichama kimoja sana (mambo ya kushika hatamu).

nani atabadilisha katiba kama ccm hawataki?
 
anaijua siasa ya Tz? anatakiwa tu aliyeko bongo ambaye anaiweza misukosuko. Say Mnyika?
LoL,

Mnyika hapana mama! Huyu atinge tena kwenye kinyang'anyiro cha Ubungo na sasa tunamhakikishia ushindi kwa udi na uvumba...! Anahitajika Bungeni huyu
 
nani atabadilisha katiba kama ccm hawataki?

Suala la katiba naona liko gumu sana mama Mary Nagu aliisha sema katiba ya sasa haina tatizo na hakuna sababu ya kubadilisha!! akiwa waziri wa sheria unategemea nini hapo?
 
Mabadiliko ya katiba yatakuja pale tu tutakapokuwa na Rais ambaye yuko tayari kufanya mabadiliko hayo. Kwa sababu hawa watu wana njia zao za kuchelewesha maamuzi mbambali hata kama yametolewa na mahakama. Kwa hiyo ni muhimu sana kuhakikisha pamoja na kuing'oa CCM kwenye viti vya ubunge ni muhimu pia kuwang'oa kwenye Urais.

Nyani mimi sijamsoma/kumsikia John Mashaka kwa hiyo ndio maana inaniwia vigumu kujua uwezo wake katika utendaji na yapi ana uwezo wa kuyatekeleza akiwa kama kiongozi.
 
nani atabadilisha katiba kama ccm hawataki?

Itabadilika tuu, huku kuumbuka kwa mafisadi ndio mwanzo,tunaweza kufanya hata petition iwe signed pia na wananchi. Cha muhimu ni kupeleka elimu hii kwa watanzania walio wengi huko vijijini ili kupata support ya wengi, . Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Iko siku yatakuwa, sooner than later
 
Qeeque kaanzisha mjadala mzuri, lakini kama ilvyo kawaida ya JF, tayari umekwishapindishwa.

Pendekezo limetolewa Dr. Slaa agombee 2010. Bado sijasoma hoja nzito inayopinga pendekezo.
 
LoL,

Mnyika hapana mama! Huyu atinge tena kwenye kinyang'anyiro cha Ubungo na sasa tunamhakikishia ushindi kwa udi na uvumba...! Anahitajika Bungeni huyu

Basi nguvu ielekezwe kwenye viti vya ubunge, baada ya kupata wabunge wengi itakuwa rahisi kumpin point mgombea katika hao watakaoupata ubunge
 
Swala hapa ni kuhakikisha wapinzani wanapata wabunge wengi at least kuwe na balance.....lakini kusema mambo ya ccm ina wabunge 200 wapinzani 50 hakuna chochote kitakachofanikiwa.
 
Qeeque kaanzisha mjadala mzuri, lakini kama ilvyo kawaida ya JF, tayari umekwishapindishwa.

Pendekezo limetolewa Dr. Slaa agombee 2010. Bado sijasoma hoja nzito inayopinga pendekezo.

Naona kama mjadala unajadiliwa, haujapindishwa
 
Geeque,
Katiba haiwezi kubadilishwa kwa kuipigia magoti CCM ikubali kuibadili. Kenya walifanikiwa kuanza mchakato wa kuibadili katiba yao kwa kumlazimisha Moi.

Wapinzani, Civic organizations, na wananchi wanahitaji viongozi tu wa ushawishi mkubwa kuwafanya CCM wasalim amri.
 
Ndo maana nimesema mchango wa NGO katika kuakikisha Tanzania inakuwa nchi yenye good governance bado ni mdogo, hizi ndo zinatakiwa kuwaelimisha wananchi vijijini lakini wamekaa mjini tu.
 
Ndo maana nimesema mchango wa NGO katika kuakikisha Tanzania inakuwa nchi yenye good governance bado ni mdogo, hizi ndo zinatakiwa kuwaelimisha wananchi vijijini lakini wamekaa mjini tu.

Tena na baadhi ya hizi NGO zimekuwa ni za kifisadi tu. Nguvu ya NGO and civic societies kwa Tanzania bado kabisa, hizi ndio zilitakiwa zifanye kazi kubwa kuwaelimisha wananchi wa vijijini umuhimu wa kubadili katiba na pia umuhimu wa upinzani.
 
wacha ndoto za Alinacha....
 
Mimi naona wazo la Dr Slaa kuwa raisi ni wazo zuri kwani linatimiza jukumu la kikatiba kwamba kila mwana wa nchi anashiriki shughuli za maendeleo ya nchi kiasiasa na kuendeleza jamii ya watanzania kijamii na kiuchumi.

Ila mtazamo wangu mimi ni kwamba viongozi wote wa upinzani inabidi waunde chama kimoja madhubuti cha kusimama na CCM ili kutimiza ile hoja ya kuwepo mabadiliko ya kisiasa nchini mwetu.

Moja ya kazi kubwa ya upinzani ni kuwashawishi wananchi kwamba ni kwanini wapinzani wapewe madaraka kuongoza nchi badala ya chama kinachotawala.

Ukiangalia sana kwa makini utaona kwamba ukiondoa Mheshimiwa Mbatia, wengi wa viongozi hawa ni ama walikuwa CCM au wamekuwemo serikalini kwa hio moja ya mbinu za ushindi ambazo ni uhamasishaji tayari wanayo.

Kwa hio mimi naona wakiunda chama hicho ndio wamchague kiongozi wao ambae nduie atakiongoza na kuhakikisha anawafahamu watu wake wote akaoingia nao serikalini ikiwa wananchi watakubali kufanza mabadiliko katika fikra zao huo mwaka 2010.

La sivo hadithi zitaendelea kuwa zilezile siku zote na mimi sasa itabidi niwe mgombea binafsi halafu nikishinda nitawateua wabunge wengi wa upinzani na sio CCM labda ntamfikiria Dr Shein ambae hana madoa ya rushwa.

Si mnajua kama hauko kwenye siasa kuna mambo yakitokea ndio unakuwa na "interest"!

Kama ambavo huwa wanaonesha mshikamano wao kama huo hapo juu, basi wakiungana pamoja na kuunda chama kipya basi muda bado upo wa kujitayarisha na sisi wapambe tupo tayari kusaidia kimawazo.
 
Kama ambavo huwa wanaonesha mshikamano wao kama huo hapo juu, basi wakiungana pamoja na kuunda chama kipya basi muda bado upo wa kujitayarisha na sisi wapambe tupo tayari kusaidia kimawazo.

ingeleta bonge la upinzani na CCM wangetoka jasho viganjani. Bado umuhimu wa kuelimisha wananchi wa vijijini maana halisi ya upinzani na umuhimu wake.

Waeleweshwe kuwa hali zao duni kimaisha ni matunda ya serikali ya CCM so itakuwa vema na haki kutowapa kura katika chaguzi zijazo. Wananchi wakipata elimu hii na wakaelimika mambo yatakuwa rahisi, vinginevyo mchezo utakuwa ule ule.
 
Wanashirikiana sasa hivi uchaguzi ukikalibia kila chama kivyake
 
Wanashirikiana sasa hivi uchaguzi ukikalibia kila chama kivyake

Basi inaonyesha hata wao hawana nia na maendeleo ya nchi hii, labda na wao wana njaa vile vile, kwa nini kila mmoja wao anataka kuwa Rais? labda na wenyewe wana cysts za ufisadi na mara waingiapo madarakani hizo cysts zitagrow na yatakuwa yale yale. Kazi ipo ya kumtafuta mtu hasa mwenye uchungu na Tanzania..vijana hasa, hawa wazee basi sasa kwani wote ni products za CCM.
 
Wanashirikiana sasa hivi uchaguzi ukikalibia kila chama kivyake

siku hao viongozi wa upinzani wakipopigwa picha inayoonekana kwenye thread hii,waliahidi kusimamisha mgombea mmoja wa urais ifikapo 2010.
 
siku hao viongozi wa upinzani wakipopigwa picha inayoonekana kwenye thread hii,waliahidi kusimamisha mgombea mmoja wa urais ifikapo 2010.

Okay, basi itakuwa vizuri. Lakini huyo mgombea asiwe kati ya hao, nadhani wapo wenye uwezo zaidi ya hawa na wengine kama kina Lipunba imekuwa too much!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…