Waungwana, hivi huyu Maximo ni hakuna halichotufanyia watanzania au tulikuwa tumeweka IMANI KUBWA SANA KWAKE. Nadhani tujaribu kuangalia mahali alipotukuta ndipo tulipo? kama jibu ni ndiyo BASI HANA JIPYA, kama jibu ni hapana, je ametusogeza mbele au ameturudisha nyuma. nadhani kama ameturudisha nyuma basi hana sababu hata ya kuaga ni kuchapa lapa kwa kwenda mbele kama ametusogeza mbele basi tunayo sababu ya kuangalia hiyo hatua utuliyosogea tulistahili kwa hiyo hatua au la. Haisaidii kila siku kuhoji swala la kaseja, boban na chuji kuwezpo stars, sitaki kuamini kwamba matokeo mabaya inayoyapata stars ni kukosekana kwa hao wachezaji watatu. Naamini kila kocha anachagua wachezaji kutoka na mfumo anaotaka kuutumia, na vilevile hakuna kocha ambaye atachagua wachezaji ili timu ikose ushindi.
Tujaribu kunyoosha vidole kwenye vilabu vyetu kwanza, vipi mafanikio ya vilabu vyetu katika michezo ya kimataifa? Kama vilabu havifanyi vizuri sidhani kama timu ya taifa itafanya vizuri kwani ndio hao hao wacheza tutakaokuwa nao kwenye national team.
nadiriki kusema huyu mtu ni mshenzi....
Nimepata ukumbi wa kutolea pongezi zangu kwa Zanzibar. Mlistahili kuchukua ubingwa kabisayote kwa yote... Hongera Zanzibar
Usimsahau na 'Kapu' vilivile yumo katika hao wababaishaji wa soka.Maximo ni mpiga kelele anaendesha soka kiswahili-swahili kuliko waswahili wenyewe, nimeamini kweli wabrazil wengi ni matokeo ya biashara ya utumwa wa Afrika mashariki, yaani kitabia anafanana sana na ndolaga, Rage na Waendesha soka wengine hapa Dar es salaamaambiliki, ni kiziwi na mtu anayepigania sifa ambazo mwisho wa siku tumekua mabingwa wa kushinda mechi nyingi za krafiki kuliko za kimashindano.
Maximo hawezi kuleta jipya aliyoleta katika soka letu yanatosha kwa uwezo wake kiufundi ,kimawazo na kiakil.
Very interesting hii story ina ukweli?Mwanzoni wakati mheshimiwa anaukwaa urais aliwaahidi wa tz kuwa atawaletea kocha wa kimatiafa na mwenye utaalam mkubwa wa soka. Na kweli muda si mrefu Maximo aliwasili. Siku za mwanzoni wakati Maximo alipokuwa anawapa mazoezi wachezaji wa taifa stars katika uwanja wa taifa na mheshimiwa naye alikwenda kushuhudia mazoezi. wakati mheshimiwa anaondoka uwanjani aliongea na vyombo vya habari, Aliongea nini? namnukuu ambapo nilimsikia live katika itv nadhani hata humu jamvini kuna watu wanaweza kukumbuka kauli yake, alisema:" kocha amenifurahisha sana, huyu kocha yuko uwanjani anafundisha huku anatumia laptop! hii ni tofauti kabisa na makocha wetu wa hapa, huyu kocha yuko makini na kazi kwa sababu anatumia laptop" kwa upande wangu hii kauli ilinipa wasiwasi sana kuona mkuu wa nchi anastaajabu juu ya laptop, hapo ndipo nikasema ama kweli watz wameingia mkenge kumchagua kwa kufata upepo!
Mwanzoni wakati mheshimiwa anaukwaa urais aliwaahidi wa tz kuwa atawaletea kocha wa kimatiafa na mwenye utaalam mkubwa wa soka. Na kweli muda si mrefu Maximo aliwasili. Siku za mwanzoni wakati Maximo alipokuwa anawapa mazoezi wachezaji wa taifa stars katika uwanja wa taifa na mheshimiwa naye alikwenda kushuhudia mazoezi. wakati mheshimiwa anaondoka uwanjani aliongea na vyombo vya habari, Aliongea nini? namnukuu ambapo nilimsikia live katika itv nadhani hata humu jamvini kuna watu wanaweza kukumbuka kauli yake, alisema:" kocha amenifurahisha sana, huyu kocha yuko uwanjani anafundisha huku anatumia laptop! hii ni tofauti kabisa na makocha wetu wa hapa, huyu kocha yuko makini na kazi kwa sababu anatumia laptop" kwa upande wangu hii kauli ilinipa wasiwasi sana kuona mkuu wa nchi anastaajabu juu ya laptop, hapo ndipo nikasema ama kweli watz wameingia mkenge kumchagua kwa kufata upepo!
aisee hapo gambler umenena, hiyo kitu hata mimi nakumbuka alisema, ni ulimbukeni kwa president kushangaa na laptop
Ni kweli hata mimi nilimsikia JK...Maximo alikuwa akitaja majina ya wachezaji aliokuwa amewachagua akawa anasoma kutoka kwenye laptop badala ya mikaratasi kama wengi wanavyo fanya basi kitendo kile kilimfanya JK amwamini kuwa Maximo ni mbongo la kocha kumbe ni mbonge la msani kama yeye..Very interesting hii story ina ukweli?