The Radar Scandal: Investigation & Progress

kwanza walipo jua ana urai wa uk na tz hapo hapo wangemshikana kumshtaki kwa hilo kosa,then kama kifungo chake kingekuwa kimekwisha wange muweka chini ya uangalizi, na hii kazi ndugu zetu wa takukuru wamesomea, sasa mpaka sisi tuwakumbushe wajibu wao au walicho takiwa kufanya?
 
May be its time now to substatiate the statement ya Pesa Mbili Mramba. JF mwaikumbuka? It was an obvious insult to wabongo. Atajibu 2.
 
Kama ni kweli serikali (PCCB) imesema huyu jamaa ana uraia wa nchi mbili tunatakiwa kujua uraia wake wa nchi mbili ulijulikana lini, na ni nani walikuwa wanajua kuwa huyo Mtanzania ana uraia wa nchi mbili na kwanini walikaa kimya bila kuviarifu vyombo husika kuhusu hili jambo.
Na kama serikali(ikiwa ni pamoja na Mawaziri) ilijua hilo, ni kwanini ilishirikiana na mtu ambaye right from the begining alionekana kuwa ni mvunjaji wa Sheria, ni vizuri itueleze kwanini ina double standards.
 
Aaa wapi! Hakuna cha PCCB wala TAKUKURU longolongo tu... Jamaa si ajabu wamemsindikiza wenyewe airport vizuri tu tena kapitia VIP huyooo katimua zake...halafu ndio wanakuja na lame excuses eti ajitokeze... Mramba si yuko, ajitokeze na yeye awataje wote waliogawana hiyo $12,000,000
Hapa hata mazingaombwe ya Profesa Maji Marefu cha mtoto!
 
siasa za tanzania ni mazingaombwe tena kweli kweli.

mtu walikuwa nae wakamuachia sasa wanamsaka!! hii inadhihirisha kuwa hawakuwa na nia ya kumfikisha kwenye sheria kwa vile pesa zote hizo hajala peke yake. wakubwa wanamkingia kifua, na JK anajua. aibu kweli kweli
 
siasa za tanzania ni mazingaombwe tena kweli kweli. ....mtu walikuwa nae wakamuachia sasa wanamsaka!!

Nadhani ndiyo mazingaombwe yenyenwe hayo, sungura tunamwona akitolewa kwenye kofia!
 
May be its time now to substatiate the statement ya Pesa Mbili Mramba. JF mwaikumbuka? It was an obvious insult to wabongo. Atajibu 2.

Naam bado tunaikumbuka. Mramba alisema,"Tutakula hata majani, lakini rada lazima inunuliwe." Na bado anapeta kama waziri. Hivi mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri yaliyotabiriwa na wajuzi wa mambo ya siasa bado yapo au yameshakuwa history!?
 
Radar case in danger of becoming a farce: As Vithlani avoids corruption charges and gets slapped with perjury instead

PCCB director-general Edward Hosea: Despite the Bureau's highly-public announcement on Monday, it has now emerged that the case against Vithlani is not being handled by PCCB after all, but by the attorney-general's chambers

 
Thanks Bubu ataka kusema,

Now you're talking! Topics concerning this Radar issue have been merged to have a good flow. Edward Hosea topics also merged.

Karibu
 
Watu wanadai tumpe JK kipindi chake chote ndo tutaona matunda. Inashangaza sana kwani issue hii iiko ikulu lakini walianza kuiona imeoza au inahitaji kushughulikiwa ni watu walioko nje.
Hapa tutaletewa hekaya za Abunuasi.Hawawezi kumleta huyu Mhindi kwa ni wanajua wazi akishafikishwa mahakamani hataficha siri.
 
hakuna kesi hapo ni usanii tuu na tafadhari wasitupotezee muda na waendelee na speed hii hii,tunawasubiri 2010!
 
hakuna kesi hapo ni usanii tuu na tafadhari wasitupotezee muda na waendelee na speed hii hii,tunawasubiri 2010!

Kwa staili ya kesi za Danganyika, naungana na wewe kuwa hapo inatafutwa tiktak na mahali pa kukimbilia, kwani Vithlani akifikishwa mahakamani kwa kesi ya rada huenda tukayajua mengi mengine ambayo hatukuwa nayo. Kwa hiyo jamaa anashtakiwa kwa uongo, na sio kushiriki katika mlungula wa rada.

Mazingaombwe asubuhi subuhi.
 
Nitawawekea nakala ya mashtaka toka Mahakama ya Kisutu... dakika chache zijazo...
 
Bravo JF,
Ila some time ukiona haya madudu unakosa usingizi! kesi isha isha igizo karibia lina kamilika na pazia la jukwaa litafungwa!! Tumekwisha!
 
Lakini inavyoonekana hii kesi haikutoka PCCB, imetoka AG chambers, kwa kuwa chini imesainiwa na State Attorney... Huko ndiko alikotoka AG wa zamani, Andrew Chenge, ambaye ana mizizi mikuu na yeye ni muhusika wa kesi ya radar
 
This is absolutely silly. Nashangaa kwanini wasomi wetu waendesha mashtaka baada ya:

a. Kwamba alisema kampuni fulani si ya kwake, kampuni ambayo inatambulika kuwa ni ya kwake na akalipwa mabilioni ya shilingi kwa kutumia akaunti hiyo, swali: KWA nini hawakumshtaki kwa makosa ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu?

b. Kwenye kosa la pili ambapo alisema uongo kwa afisa wa PCCB kuhusu malipo aliyoyapata kwanini ameshtakiwa kwa kosa la kusema uongo kwa afisa wa serikali (kosa dogo) badala ya kosa la Obstruction of justice (I'm not sure kwenye Penal Code yetu tunalo kosa kama hilo. Ni sawa sawa na Polisi anakuja nyumbani ambako kumetokea uhalifu na kuuliza mtu "fulani yuko wapi" na yule mtu ilhali akijua amemficha chumbani kwake anamwambia afisa wa Polisi "alikuwa hapa lakini akaondoka". Baadaye ikijulikana alisema uongo ili kupinda utafutwaji wa haki, anashtakiwa kwa kosa la Obstruction na siyo kusema uongo.
 
Kwanini inaonekana kuwa mzizi wenyewe wa kosa umewekwa pembeni,na jamaa anatuhumiwa kudanganya. Kwanini ufisadi hauhusishiwi? Adhabu ya kudanganya si inaweza kuwa ni fine ya shilingi 5000 tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…