Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,495
- 5,529
Marko 4:25"Kwa maana aliye na kitu ataongezewa, na asiye na kitu atanyang'anywa hata kile kidogo alicho nacho."
Nianze kwa kusema kwamba sihubiri injili nataka niwafundishe siri ndog tu ya ulimwengu.
Na kwa wale waliosoma Science ya maumbo-A body remains in a state of rest or uniform motion unless an external force compels it to act otherwise.Na pia kuna laws kama vile Law of conservation of energy,Momentum n.k ambazo zote zinaendeleza universal dynamics.
Sasa leo nataka nilete siri ambayo najua kuna wanaoijua na kuna wasoijua na hata ukiijua bado unaweza usiifanyie kazi. Ni siri inayohusu the Power of Giving.
What is Giving-Giving is the act of transferring what you have/own to another person who needs it.Giving becomes meaningful and powerful when the person we are giving has no ability nor intention of giving us something in return.It is called charity.
Kwa Kiswahili chepesi, kutoa ni ile hali ya kuhamisha kile ulichonacho kwenda kwa mtu mwingine anayekihitaji. Utoaji unakuwa na maana zaidi pale ambapo yule unayepatia anakuwa hana uwezo au ni ya kukupatia kitu kingine na wewe.
Unapotoa unapata zaidi na maradufu.Kwa nini?kwa sababu hakuna cha bure.Unapopokea lazima pia utoe hivyo usisahau kurudisha wema.
Kwa mfano:
Watu wenye tabia/desturi ya kuomba omba huwa utawakuta miaka mingi wanakuwa katika hali ile ile ya unyonge na umaskini kwa nini?-Watu wanaotoa sana hujikuta wakiongezeka katika utajiri maradufu kwa nini? Watu wachoyo hujikuta wakipungukiwa na kufilisika sana kwa nini? Kama unafikiri nakosea jaribu kuangalia watu wanaokuzunguka, matajiri wengi wakarimu huendelea kuwa matajiri. Matajiri wachoyo hufilisika, maskini wakarimu hupata utajiri, maskini wachoyo hutopea katika lindi la umaskini.
Ufunguo upo katika kutoa na hii ni kwa mujibu wa kanuni zilizodumu karne nyingi.
Najua kuna anayeuliza: Nitoe nini? Sina cha kutoa. Sio kweli unayo mengi sana ya kutoa na sio lazima iwe pesa, pesa ni namna tu ya ku-exchange.
Karibisha mtu au watu chakula nyumbani mwako,Tembelea wagonjwa hospitalini. Jitolee katika shughuli mbalimbali katika jamii yako, mtaa wako. Unapotoa chochote iwe muda wako, pesa yako, talanta yako n.k. Toa kwa kadiri ya uwezo wako na Mungu atakujazia. Toa kwa Upendo.
Tazama, kipimo kile upimacho ndicho utapiwa na kujaziwa na kusukwasukwa.
Uwezo uliopewa wewe, uwe wa kifedha, kielimu, talanta, sio kwa ajili ya kukufaidisha wewe tu ni lazima na wana jamii wengine pia wafaidike nao ndio uweze kuzaa matunda maradufu. Tazama jamii inayokuzunguka uone nguvu ya utoaji inavyofanya kazi.
Mfano Rahisi ni uhusiano wa Baba na mtoto. Mtoto anapopewa matunzo na mzazi huwa anapokea tu bila kutoa,anapofikisha umri wa kuanza kujitegemea na bado akaendelea kuwa tegemezi basi anaanza kupoteza mibaraka. Ulipokuwa mdogo mzazi wako alibarikiwa kwa kukupatia wewe mahitaji kwa kuwa hukuwa na uwezo wa kujitegemea.
Unapkuwa mtu mzima unayeweza kujitegemea basi hali inabadilika pale unapoendelea kupokea kutoka kwa wazazi badala ya kujitegemea, unaanza kupoteza. Ndio maana vijana wengiwanajikuta mpaka wakiwa wana miaka arobaini bado wanaanza na Dady kafanya hivi, kafanya vile kwa sababu wamekuwa tegemezi mpaka wakatopea. Matokeo yake mzee akifa wanaishia kugawana mali na kuzitumbua kisha kubaki katika umaskini kwa sababu mzee wao alishawanyonya kila kitu wakati akiwatunza wakiwa na ndevu zao.
Ila tazama pale ambapo mzazi ni kauzu, ametiimua watoto watafute maisha, huwa anawafungulia baraka, watakula msoto ila baada ya muda hutasikia "dady kanunua nyumba sijui dady kaoa mke mwingine"
Ninachotaka kusisitiza ni kwamba pale unapotoa lazima upokee maradufu.
Anza sasa kutoa katika kidogo ulicho nacho na uone utapokea kiasi gani,toa upendo na utapokea upendo.
Kila la heri