The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

mimi nadhani mweshimiwa mbowe ana haki ya kujibu au kuacha kujibu haya maswali kama anaona sio apriapriate hapa forum yameandikwa machafu zaidi kuhusu watu; haya maswali mimi naona ni laini tu kwa mweshimiwa mbowe. mbowe katoa nafasi kuulizwa maswali nadhani ni mjinga tu ambaye hatatumia nafasi hiyi kuuliza na kutoa nafasi ya huyu kiongozi kukanusha yanayosemwa juu yake kwenye circles hapa bongo.
 
Kwa staili hii hata kama kulikuwa na viongozi na watawala wengine walitaka kuja humu basi wataingia mitini kabisa. Suala la watoto wake sijui wanapassport, sijui wanasoma wapi yana maana gani? Tungeweza kuyaelewa kama kuwepo kwao huko kunahusiana na kodi ya Watanzania. Tutakuwa wajinga vilelvile JK akija humu tukaanza kumwuliza ati Amina Chifupa kapata ubunge kwa sababu tunasikia ni nanihii ... Ama kweli tuna safari ndefu
 
KWA NINI SISI SIYO WA BUNIFU
Imetokea katika vyama vya upinzani kuanzisha sera au kitu fulani kwa mfano Muh. Mbowe kutumia Helikopta ,sera, Mbowe kutumia tekinolojia ya habari na mawasiliano kuongea na wananchi ,inakuwa kero, Sasa Muh.Mbowe ameanza kampeni ya 2010 kwa kutumia njia ya mtandao wakomputa ama kweli Mbowe anatupiga bao

Chama changu CCM kina wasomi wengi inamaana wahaujui huu mtandao JAMANI MNANIANGUSHA namkiingia katika mtandao huu msikashifu mtu yeyote haya ni maoni ya watu muwe wapole soma kwanza kabla ujachangia alafu changiueni HOJA Msilumbane na mtu mnampa umaarufu tutaonaonekaka tumeshindwa na tuna tumia nguvu siyo akili.

Muh. Mbowe anajua mahali akitushika tunalia bila majibu sasa mimi nina amini hatuwezi tukiwa na hasira tumeanguka kwa uso.

Nikama unamtaka mwana...... badala ya wewe kwenda vikwako unaanza kutoa maneno machafu kwa mtu aliye kuwa naye kabla, siyo vizuri {samahani kwa mfano nilioutumia kama nita kuwa nime wakwaza wengi}.

Ninatumaini tuna weza kujibu hoja za kila haina hata kama ni za nani.. sasa njia Mbowe anayotumia ina mvuto watu wana msubiri ajibu ANAONGEA NAO LIVE LIVE !!! kila saa kuna watu maelfu kwenye komputer wana subiri tamko la Muh.MBOWE , sasa kwa kutumia mtandao huu sisi CCM tuanzishe mjadala ambao katibu mkuu wa CCM atatoa tamko kwa wanahama wa CCM ,WABUNGE,WANASIASA WETU WANAFUNZI WA CHUO KIKUU, MAPROFESA, MAWAKILI WA CCM, kujibu hoja asitembee tu mikoani anzishe IT CENTER KWA WANA CCM tupo wengi tunaju COMPUTER
tuweze kupambana na wapinzani wana tupiga bao.

Niko South Africa mkiniitaji kusaidia chama nikotayari,

INAKUWAJE WASOMI WA CCM HAWAIJUI HUU MTANDAO AU NI KWA SABABU YA DIGIRII ZAO FEKI, zao PhD,Dr,
 
Mzee King,
Unadhani Amina Chifupa atakuwa na muda wa kuingia katika mtandao huu? Na wasomi unaowazungumzia wa CCM ni akina nani Akina Dr. Nchimbi? Hawa bado wanajiweka kisawa katika mtandao, sidhani wana muda huo.
 
10. ushiriki wako hapa forum. a strategic mistake, ungekuwa unasoma tu.

Very true, in fact "strategic mistake" is rather a friendly phrase. By joining this forum openly, Mr Mbowe is, in all senses, attempting to commit a "political suicide."

There are lots of good things this forum can offer to a leader like Mbowe, but along come with factual manipulations, hatrage, speculations, personal attacks, conspiracy based-arguments, and other ills that one requires a nickname to tolerate, compose and respond to.

As a matter of fact we at jambo forum are fighting on who should have the first punch,,ooops, the first question to Mr Mbowe. I'm pretty much sure the lowest point of Mr Mbowe's political career is about to be marked. His critics are standing ready to jolt down humiliating quotes that will make him regret if he is to further his political ambitions.
 
Guys we are jumping the point here, kama mnataka CCM wajiunge na huu mtandao basi anzisheni topic nyingine ya kuhamasisha hilo. Hii ni topic aliyoanzisha Mr Mbowe ni kwa yeye kuwasiliana nasi kwa njia ya maswali na majibu. Kama CCM mnataka nafasi hiyo basi fanyeni kivyenu.

Siungi mkono personal questions kwa Mr Mbowe; ila naona tunakuwa kama hatuna ustaraabu kwa nini tusimwache Mr Mbowe ajibu mwenyewe na kama tukiona mtu anangania kuuliza maswali yasiyo na msingi basi Admin ndio aingilie kati na kurekebisha wanaforum. I get tired of reading numbers of comments kutoka kwa wanabodi wengine just to find out wanakosoana wao kwa wao, tumieni PM kufanya hivyo. Hapa weka mawe, personal issues hazitakiwi ila muhusika yupo so let him answer.

I still think this isn't going to work; Mr Mbowe you may want to take my advice and use Pen Name Let JJ be here to represent Chadema and himself, he's a young man...with a pretty clean history...so nothing much to loose.
 
mi pia mgeni hapa naiepnda Chadema na nina mambo kadhaa nataka kuongea:

1. eti ni kweli anna komu bibi yako ndio maana akawa mgombea mwenza baada ya kufa yule mzenji na vilevile akawa kwenye nafasi ya kuwa mbunge viti vya wanawake chadema

2. naomba maelezo kuhusu sakata la wagombea viti maalum chadema manake kamati kuu yenu ilitaka kukuondoa lakini wazee wa busara kina makani, mtei na wengineo wakaingilia wanasema eti mmechagua mabibi zenu tu zitto na muhonga, wewe na anna komu na kiwelu na halima mdee na yule binti wa ndesamburo. what happened?

Habari za siku nyingi?
Mimi naomba kwa ufupi nitoe maelezo kuhuusu hili suala la viti maalumu maana linaibuliwa na kuzimika na kisha kuibuliwa tena na tena. Naomba radhi kuwa imenibidi nijibu hoja hii tu maana ndio nimetoka hospitali ambako nililazwa kwa siku mbili tatu hivi. Ninaendelea vizuri sana.
Kwa wale wasiojua, viti maalumu vya ubunge kwa chama vinapatikana kutokana na idadi ya kura ambazo kila chama kimepata katika uchaguzi ili mradi tu chama hicho kiwe kimefikisha asilimia 5 ya kura zote.

CCM walipata asilmia 69, hivyo viti 58, CUF walipata asilimia 14 hivyo viti 11 na CHADEMA asilimia 8 na hivo kupata viti 6.

CHADEMA kama chama cha siasa, na kama mwenyekiti wake alivyosema kuwa ni chama asasi, kina taratibu zake za kupata wabunge wa viti maalumu. Sio lazima utaratibu wa CHADEMA uwe kama wa CCM au CUF. Ninavyoelewa mimi na kufuatia utafiti wangu niliofanya kama mwananchama wa CHADEMA utaratibu ulikuwa nimzuri na ulizingatia matokeo ya uchaguzi.
1. Mkoa wa Kilimanjaro ndio mkoa uliotoa kura nyingi zaidi kwa CHADEMA katika uchaguzi wa 2005 (www.chadema.net/matokeo). Ulikuwa mkoa wa kwanza. Katika viti 6, Kilimanjaro ikapewa viti 2 - Grace KIWELU ambae alikuwa Mbunge na alitunukiwa heshima na Kamati Kuu ya Chama kwa utendaji mzuri na kuheshimu maagizo ya chama alipokuwa Mbunge) na Lucy Owenya ambae ni mwanachama wa CHADEMA toka 1992 na amekuwa akisaidia sana chama kimali nyakati zote za kampeni. Pia aligombea na kushinda mkoani Kilimanjaro.
2. Mkoa wa Dar es Salaam ulitoa kura nyingi ukiwa wa pili. Wakapewa viti 2 - Halima Mdee, mwanasheria kijana ambae alijiuunga na CHADEMA mara baada ya kumaliza chuo kikuu na licha ya kuwa mfanyakazi wa serikali alikuwa akitumia muda wake kufanya kazi za chama mpaka pale alipopata likizo baada ya kuwa Mbunge. Nafasi nyingine ikaenda kwa dada wa Chuo KIkuu cha Dar, Susan Lyimo, na kila mtu anajua jinsi CHADEMA ilivyopata kura nyingi kutoka jumuiya ya chuo kikuu na umuhimu wa kufanya recruitment kutoka chuo kikuu.
3. Mkoa wa kigoma ulikuwa wa tatu kwa idadi ya kura kwa chadema. Wakapata kiti kimoja - Mhonga ruhwanya. Huyu baada t ya kumaliza chuo alijiunga na CHADEMA akiwa afisa maendeleo ya chama. Pia aliongoza katika kura za Kigoma.
4. Anna Komu - Unapokuwa na Mgombea mwenza mwanamke, halafu mnashindwa hawi makamu wa Rais, halafu hawi Mbunge, jamii ingawaelewa nini chadema?

Kati ya wabunge sita wa chadema wa viti maalumu, watatu elimu yao ni shahada za uzamili, mmoja shahada moja ya kwanza na wawili elimu ya sekondari. Hivyo nusu ya wabunge wanawake wa CHADEMA ni wasomi wa posgraduate, theluthi mbili wasomi wa ngazi yaa chuo kikuu. Hebu fuatilieni wa ccm muone.

Sasa mgongo mgongo, nakujua, ulitaka nani awe mbunge wa viti maalumu chadema? maana hoja hii umeishika sana wewe!

Ngoja nipumzike............. nisijerejeshwa hospitali
 
Mzee Ndabita,

Kwanza heshima yako mkuu, ninashukuru kwa kuchukua muda wa kuyajibu maswali ya kimsimgi kwa chama chako yaani Chadema, sasa kati yetu kama kuna asiyeridhika basi aendelee na ya nyongeza,

(1). But, with all that said, sikubaliani na kauli ya kaangalieni CCM, kwa sababu wabunge wa chama chako viti maalumu wengi ni wasomi, NO! take that back, CCM ina wabunge wanaofanana na jamiii, yaani kila mwananchi anawakilishwa kuanzia, wasiosoma ambao ndio wananchi wengi na halisi wa Tanzania, wenye elimu kidogo, na wenye elimu ya juuu kidogo, na elimu ya juu kabisa, sidhani hapa kama kuna argument against kwenye hili,

(2). The matter of fact ni chama chako na TLP, ndivyo bado mpaka leo viko mstari wa nyuma kwa kuwa na wenyeviti wasiokuwa na elimu ya kutosha, yaani elimu duni, na pia ndivyo vyama pekee ambavyo kwenye uchaguzi wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, nchi yetu, vilikuwa na wagombea urais huo wenye elimu duni, kulinganisha na vyama vyote vingine vilivyoshiriki.

(3). Kwa ndugu zangu wengine wa forum hii, ninaomba tuwe na subira na wavumilivu, badala ya kurushiana rushiana maneno yasiyostahili, kuna mpaka anayeshauri kuwa kuja kwa viongozi hapa ni ku-commit political suicide! toka kuanzishwa kwa forum zote za wabongo, hii ni kwa mara ya kwanza kiongozi mkuu wa kisiasa bongo, ameingia mzima mzima, sasa lazima baadhi ya wananchi watakuwa excited, lakini isichukuliwe kama ni sababu ya baadhi yetu kukata taamaa na kuanza kutoa maneno ambayo kwakweli hayajengi, ila ni kubomoa, yaani sasa hivi mtashauri kuwa maswali yaandikwe pembeni na kupitiwa kabla hajauliwa Ndugu Freeman, kama Mzee JK, alivyofanya NY, please!

(4). Waacheni wananchi wamfurahie kiongozi wao, Mwalimu siku zote alikuwa akiwaambia waandishi wa habari kuwa atajibu yale tu anayoyaona ya maana na ndivyo alivyofanya siku zote, tena pale Hoteli Kilimanjaro, mtakumbuka jinsi alivyowatukana waandishi kwa kumuuuliza maswali ya Mrema, sasa tusiwakatishe tamaa wananchi wanaotaka kuuliza maswali, hata kama ni low au high kiasi gani, tuwaachie viongozi wote watakaoingia hapa wachague yapi watayajibu na yapi hawatayajibu, ndio siasa, Ditopile kule Kizota alimuuliza swali Mwalimu, ambalo wajumbe wote walifikiri ataishia jela, lakini akapewa uwaziri mdogo wa mawasiliano na ujenzi, Mitume wetu wote wawili kuanzia Muahammad, mpaka nabii Isaya, hawakuwahi kuwafokea wafuasi wao kwa sababu ya kuuliza maswali ya kijinga, tena mfuasi Peter, alikuwa siku zote na maswali ya kuudhi kwa nabii Isaya(Yesu), mapaka akamwambia Peter kuwa kwako wewe nitajenga ngome ya imani, pamoja na kwamba wanafunzi wengi kati ya 12 walikuwa wakimchukia Peter kutokana na maswali waliyoyaona kuwa ni upuuuzi, lakini kwake nabii yalikuwa ni muhimu mno kuliko yale waliyoyaona wanafunzi wake kuwa ni muhimu.

(5). Kiongozi wa siasa na wananchi, ni lazima iwe established kwamba anayo character inayokubalika na jamii, yaani wananchi hawatakuwa na wasi wasi naye katika kuamua maamuzi ya taifa yanahusu character, kwa mfano kama si mzinzi, hatakuwa na tatizo zitakapopitishwa sheria za kuwabana wanaokwepa watoto wao wa nje, na zikipitishwa na bunge atazisaini bila tatizo, sasa kama ni mzinzi ina maana kesi ya nyani hatutampelekea ngedele! Na tutamjuaje? ni kwa kumuuuliza maswali mapak ya nguoni, asipojibu ni uamuzi wetu wananchi kuamua tumuweke wapi katika kumhukumu huyu kiongozi, as far as character is concerned. Lakini hiyo haina maana kwamba aulizwe maswali yasiyokuwa na kichwa wa miguu, lakini tumuachie kiongozi aamue ni swali gani atajibu au hatajibu!

(6). Character ikiwa established, basi tutajua kuwa huyu kiongozi hata akiletewa vimwana na makampuni ya madini, ili ayape msamaha wa kodi hatakubali maana tunamjua, huyu hayumbi yumbi na viimwana. Tusiwakatishe taama wananchi kwa maneno mengi ya kejeli, waacheni wananchi waulize maswali, na Mzee Freeman ninakuhakikishia kuwa hakuna lolote la kujimaliza kisiasa hapa, kama kuna viongozi wanakwenda Bagamoyo kutafuta uchawi bado hawajamlizika kisiasa na tunawajua, kama tuna viongozi wauza unga na tunawajua, kama tuna viongozi waliokuwa wakilala uchi pale Namanga kwa ajili ya uchawi wa kuchaguliwa urais na bado wapo mpaka leo serikalini wanatungoza itakuwa wewe unayetaka kuwaelimisha wananchi kuhusu taifa lao?

(7). Ndugu zangu acheni hizo, aliyewapeni nyinyi, ndie huyo huyo aliyewanyima mnaowakejeli kwa ajili ya maswali yao. CCM tayari imeshaarifiwa yanayoendelea hapa kwa hiyo wanakuja hapa hapa nao, na ndio tulichokuwa tunakitaka siku zote viongozi waje hapa wabebe misalaba yao, ndugu zangu tujaribu kutumia hii nafasi kwa faida ya umma, na tuheshimiane pia sio wote tuliosoma, halafu at the end of the day, hii ni bulogu tu ya burudani kama alivyosem, Mzee Mwanakijiji ninatrudia kuwa hii ni bulogu ya burudani Mzee Freeman, hii nafasi yako muafaka kumaliza mzizi wa fitina kwa kujibu kila swali ikibidi, maan hapa ndio kuna wabongo wenyewe waliosoma na wasiosoma.

Wasaalam ndugu zangu, na forum idumu!
 
Ndugu zangu watanzania,
kuna msemo unasema katika kila msitu haukosi kuwa na mbwa mwitu, kwahiyo ni kama hapa kwenye hii forum, kunawatu wa kila aina hapa...,
mheshimiwa mbowe ameongea jambo la msingi sana, kuwa sisi watu wachache tunao kuwa na access ya mtandao kama hivi tunaweza kuwakilisha maoni ya mamilion ya watanzania wanaoteseka kule vijijini,sisi tunaweza kuwa cream ya watanzania.

Inanishangaza na kunisikitisha sana wakati kuna issue nyingi sana za kitaifa za kuzijadili,mfano suala la umeme, maji,afya,ajira,mustakabli wa demokrasia nchini,jumuiyaya afrika mashariki,oic,mahakama ya kadhi.......,lakini kuna watu wachache hapa wanataka kutupotezea malengo,
tunawaomba nyinyi vibaraka mliotumwa muondoke hapa, hapa si mahala pa wajinga kama nyinyi, hapa tuko watu serious ambao tunapenda mambo yabadilike katika taifa hili,
keshokutwa taifa letu linasheherekea miaka 45 ya uhuru tukiwa gizani, hakuna maji safi na salama, hakuna ajira, bajeti ya taifa ni tegemezi kwa zaidi ya asilimia hamsini,

huu ni wakati wa sisi kukaa chini na kuangalia tulikotoka, tulipo, na tunakokwenda,
niwakati wa kuangalia ni wapi tulikosea ili tujifunze ili makosa yale yasijirudie tena,

wakati binafsi nikiendelea kutafakari uhuru wetu wa miaka 45 ningependa niwakumbushe jambo muhimu.
Mnafahamu kuwa nchi hii baada ya uhuru ilikuwa katika mfumo wa chama kimoja kwa zaidi ya miaka ishirini, sitapenda kuuzungumzia sana mfumo huu ila, kwanza nakubaliana kabisa na mtazamo wa mwalimu nyerere kwa wakati huo, mfumo wa chama kimoja,siasa ya ujamaa,pamoja na lugha yetu ya kiswahili, vimesaidia kutransform makabila zaidi ya 100 kutufanya kuwa taifa moja la tanzania.
Lakini pamoja na mazuri yote ya mfumo huu ni wazi kuwa ulishindwa kwenda na wakati, ilifika mahari ilikuwa ni lazima mfumo ubadirike, yeye mwenyewe mwalimu alikubali kuwa chama kama ccm,kinapokuwa madarakani kwa muda mrefu sana kinakuwa kinajiamini kupita kiasi, na matokeo yake ni chama kinapoteza muelekeo na ndio kama tunavyoona sasa, ccm inanuka rushwa na kimsingi ccm sasa hivi haina ubavu tena wa kuwa sauti ya mnyonge, kwasababu kimeshikwa na wafanyabiashara na watu wenye pesa, kazi kubwa ya ccm sasa hivi ni kuhakikisha inaendelea kukaa madarakani kulinda maslahi ya wale wachache ambao wanafaidika na mfumo uliopo,
mfumo wa demokrasia ya vyama vingi tulioanza nao miaka ya tisini ulikuwa ni nafasi nyingine ya kutuweza kama taifa kurejea katika marengo yetu ya awali baada ya uhuru,
lakini miaka 15 imepita bado mfumo huu ni mchanga na kwa asilimia kubwa serikali ya ccm ndio inachangia kudumaza mfumo huu.
Kwa mtazamo wangu nafikiri sasa ni wakati muhimu sana kwa watanzania kufanya upembezi yakinifu na kuchukua maamuzi ya ujasiri,
ccm imeshaweka dhahiri malengo yake ni kuumaliza kabisa mfumo wa demokrasia ya nvyama vingi na kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja, ndio maana unaona kuanzia waziri mkuu anavyo wabana wabinge wake wa ccm, spika sitta jinsi anavyowanyanyasa wabunge wa upinzani, pamoja na matumizi mabaya ya dola katika kudhoofisha mfumo huu.
Sasa mimi naamini ccm hawatutakii mema,.kwasababu watanzania wenzangu lazima tufahamu mfumo wa chama kimoja huwa unaishia kwenye udikteta,
mimi ninawahusia watanzania wenzangu kwa pamoja tupinge vikali kupelekwa kwenye mfumo wa chama komoja na badala yake tuamue kukijenga chama kingine,
tanzania tunahitaji vyama viwili tu vya kubadilishana dola, baada yapo tutakuwa na ahueni, na tutajenga heshimwa kwa vizazi vijavyo kwani tutakuwa tumewaachia taifa huru,makini na lenye kujiletea maendeleo.
naomba kutoa hoja.
 
ndabita,

Pole kwa kuumwa.

Nimesoma hayo maelezo yako ya uteuzi wenu wa wabunge wa kuteuliwa, somehow convincing, ila nimebakiwa na maswali mawili:

1. Je kuvigawa hivi viti kwa mikoa kwa kufuatana na kura mlizopata .. ndio utaratibu rasmi ulio katika vitabu vyenu?

2. Katika kuvigawa viti hivi kwa wahusika kutoka hiyo mikoa, zilipigwa kura au iliamuliwa amuliwa vipi kuwa flani na flani ndio tutawapa nafasi za mkoa flani?

Kimsingi najaribu kudodosa ili kujua whether hizi ni 'justifications' au ni utaratibu rasmi wa chama ambao tuutarajia hata 2010 ndio utakaotumika.
 
Dr.WHO,
Ndugu yangu swali lako zito sana na halibebeki, kama ningekuwa Mbowe ninge -ingia mitini pia kwa sababu hii ni Political suicide bob kama alivyosema Mgonjwa Ukimwi...
Mshikaji that's a leading question na Umeshahukumu!
 
ahhh basi bwana

i thought so

kwa sababu nilikuwa nashangaa iweje huyu Mheshimiwa hataki kunijibu? I hope watakuja wengine au atanijibu baada ya kusoma hiyo MBA yake

i think we should move on na mengineyo

th_150px-Arsenal_FC.png
 
DrWHO,
Mbona umeshikilia ujibiwe maswali yako? Kuwa na subira. Mzee ES, Kumbe na wewe Biblia unaimanya? Sikujua unayajua yale ya St. Petro. Mhe. Mbowe ameshaamua kuingia hapa, ambapo kwa maoni yangu ni uamuzi wa busara, na wala si suicide kama walivyosema baadhi. Katika forum hii kuna mengi negative yamesemwa kuhusu Chadema na upinzani kwa ujumla, ama kwa kubeza tu upinzani au kwa kutoelewa hali halisi ambapo upinzani umejikuta nchini Tanzania. Kwa hiyo ni jambo zuri na la busara kwa viongozi wa upinzani kuweza kuwasiliana nasi moja kwa moja na wala si kujimaliza. Mimi ningependelea pia msomi wetu Prof. Lipumba aingize pua yake humu na kuwasiliana nasi moja kwa moja. Kwa hiyo tumpe muda Free atakapokuwa tayari atayajibu maswali yetu pamoja na kutuweka sawa pale tunapofikiria Chadema imeboronga, hasa katika suala la majimbo, kama alivyotaja kijana wangu Mkandara.
 
Nukuulize Mukandara na DrWHO, maana naona mko online. Do you think you have the right people on this forum? Upeo wao baadhi yao unashangaza! Unaona wanavyojadili masuala? Kama walevi vile? No coordination, no order....uswahili swahili! Can we be serious this way? Or do you think we can discuss something serious? This way?
 
Mzee Kichwamaji,

Poa bro, utaji-frustrate bure na watu usiowafahamu katika siasa kuna short terms issues na long term issues, halafu time ni kitu muhimu sana kwenye siasa I mean timing, Freeeman ana washauri sio kwamba ankuja tu kichwa kichwa, ambao wanajua the excitement ya wananchi wanyonge,

Sijui uko nchi gani, lakini waulize kule NY Jk alipoingia kuonana na wabongo kwa mara ya kwanza jinsi baadhi yao walivyojikanyaga, na pale kuna wasomi haijapata kutokea kuna watu kama Professor Mtui au Professor Lwiza hao ni moto wa kuotea mbali, lakini ninakuhakikishia leo kuwa akienda tena atalia na maswali ya kweli, ndio siasa na wananchi ilivyo,

Hii blah! blah! itaisha na kadri tunvyoendelea NONESENSE zitatoka na issue zitasimama, calm down bro after all, hii ni bulogu tu,

Hayo ni maoni yangu binafsi, Freeman hawezi kukimbia maana kabla ya kuja hapa alichunguza wapi kuna moto akaja hapa, forum ipo haiendi kokote na trust me they are coming.............., subiri uone!

Yaani Mzee Jasusi,

Kumbe hunitakii mema, unataka nikale mawe ya moto jehanamu na kina Osama na Bush? au? Off course nina Mungu bro! ha! ha! ha!
 
Kwanza nianze kwa kuwashukuru wajumbe wote kwa kutoa haoja madhubuti , Jamani ni lazima tukubali ya kuwa jambo lililofanywa na mheshimiwa mbowe ni jambo la kijasiri . Ni kweli kwamba watu wana maswali mengi kwa huyu muheshimiwa kwa sasa , ila ni lazima tujue kitu kimoja tabia tutakayoonyesha kwa huyu muheshimiwa inaweza kujenga au kubomoa hii forum , namaanisha kama watu tutauliza concrete questions trust me waheshimiwa wengine watakuja hapa , ila kama tukiendelea kuuliza maswali kama kwenye blogu ya michuzi basi hakuna mtu atakayekuja hapa .

Kwako mbowe naomba jibu maswali ya wanachizaidi suala la umeme !
 
HELLO WATU

NAFIKIRI WOTE WAZIMA

NIMESOMA THREAD NZIMA BASI NA MIMI NAOMBA NICHANGIE ANGALABU KIDOGO MIMI SIO MWANASIASA NA SIJAWAHI KUWA MWANASIASA LAKINI NIMEKULIA KATIKA FAMILIA NA JAMII ZA WASHAURI WA WANASIASA KAMA HUYO MBOWE ALIYEJILETA MWENYEWE

KWANZA NAPENDA KUMKARIBISHA MBOWE KATIKA FORUM HII NA WANASIASA WENGINE WOTE WALIOKUWA HUMU KAMA JOHN MNYIKA NA KADHALIKA , NINGEPENDA KUMGUSIA JOHN MNYIKA KWAMBA SASA NI WAKATI WA KUTOA SERA ZAKE NA KUCHANGIA MADA KWA WINGI ZAIDI ILI TUMJUE UWEZO WAKE WA KUTATULIA WANANCHI MATATIZO YAO NA ISHHU ZAO MIMI NI MWENYEJI WA UBUNGO KWAHIYO NINACHOONGEA HAPA NINA EXPERIANCE NACHO , JOHN MNYIKA UMESHAKUFA KISIASA TOKEA MWAKA 2005 , SASA UNATAKIWA UFUFUKE UPYA TENA KWA KUTUMIA FORUMS KAMA HIZI NA NYINGINE KUELEZEA SERA ZAKO NA MAMBO MENGINE KWA WANANCHI SIO KUFUKUZANA NA WAKINA DADA PALE HILL PARK .

HAYA HAYA , NIMEONA PALE MBOWE ANAOMBA WATU WATUMIE MAJINA YAO ORIGINAL AU SIO ? KWANI TATIZO LA KUTUMIA NICKNAME NI NINI ? SIONI TATIZO LOLOTE SEMA TU UZURI WAKE NI KUFICHA PRIVACY YAKO NA VILE VILE TU KWA HUJUI KWA WALE WATAALAMU WA MTANDAO KAMA MIMI HATA KAMA UKIJIFUCHA KWA NICKNAME NA UNATUMIA COMPUTER ZA OOFICE KUTUMA KASHFA ZAKO NAKUONGEA UWONGO UNAWEZA KUFUATILIWA ASIKUAMBIE MTU KILA COMPUTER ILIYOKUWA CONNECTED KATIKA MTANDAO INAJULIKANA KWAHIYO HATA UKIWA NA NICKNAME SERIKALI INAWEZA KUOMBA TAARIFA ZAKO TOKA WA ADMINS WA FORUM NA WAKATOA AU KAMA WAO WAKIGOMA AU HAWAJUI WANAWEZA KUONGEA NA THIRD PARTIES AMBAO KAZI YAO NI UCHUNGUZI NA TAARIFA ZA MTANDAO NA WAKAPATA TAARIFA ZAKO HIYO MOJA

MWISHO WA YOTE NAWAKUMBUSHA KITU FULANI TU KATIKA www.ethinktanktz.org KUNA JAMAA MMOJA ANAITWA TOSSY ALIKUWA ANATUMIA JINA LAKE ORIGINAL AKADANGANYA UMMA KWAMBA ANASOMEA PHD KUMBE NI UWONGO KATIKA FORUM HIYO HATA BOSI WAKE YUKO KWAHIYO SASA HIVI ANA PAMBANA NA BOSI WAKE KWA TAARIFA ZA UWONGO KATIKA FORUMS NA CHATROOMS

HAYA MADA IKO WAZI HICHI NI KIJEWE HURU SEMA CHOCHOTE NA CHANGIA CHOCHOTE ILA TU KISIWE NA MDHARA KWA JAMII HUSIKA AU USIFANYE PERSONAL ATTACKS KWA MTU -- MIMI KUNA MTU KULE ALINIITA ROSEBANJI LAKINI SIJAFANYA LOLOTE NAJUA NI FORUM NA YUKO HURU KUSEMA CHOCHOTE

AHSANTE
 
MWENDAPOLE
Mwendapole karibu sana katika forum hii ya watanzania wasema kweli wanao penda taifa lao na wanaopenda kujenga nchi yao, wanao taka hoja zao msingi zipate uvumbuzi.

Turudi nyuma sasa tumesha kukaribisha tumachokuomba usifundishe watu nini chakufanya katika forum hii Muh. Mbowe kabla ajaingia katika forum hii alipata ushauri kwa timu yake nzima na anasababu zake za msingi na muhimu ni kiongozi wa kitaifa na kimataifa Muh. huyu aendi kichwa kichwa wewe unajuaje kuwa ushauri ameupata kutoka kwa wapiga kura wake .

Muh. Mbowe ni kiongozi wa kwanza Afrika kuongea na wananchi kwa kutumia tekinolojia ya habari na mawasiliano kwa muda mfupi ameweza kuwafikia mamilion ya wananchi wa Tanzania na majirani zetu walioko ndani na nje ya nchi.

Pili ameamua kuwa muwazi na kujitabulisha kwa jina na cheo chak, sasa sisi tusubiri 2010 tuone jinsi tekinolojia hii ya habari na mawasiliano ya komputer itakavyo kuwa imesambaa tanzania nzima CCM haita mkamata
Hii ni maarifa anatumia tekinolojia hii kwa kufikisha ujumbe kwa wa piga kura wake na atafanya watu wengi kujua komputa kwa kusoma habari zake, watanzania wengi hawata enda kwenye mikutano ya hazara kusimama kwenye jua kali na vumbi nzito. wananchi watafuatilia kampeni kupitia njia ya mtandao wa Internet.

kwa hiyo huyu bwana anaona mbali sana atatumia RADIO,MAGAZETI,TV,MIKUTANO,INTERNET kupata wapiga kura pia atapata ushauri kwa watu wasioipenda CCM na wako ndani ya chama hicho kwa kuficha majina yao kutoa siri ya chama.

Mimi ni CCM damu lakini tuna kuwa wazito kuamua mambo yetu mpaka wapinzani waanzishe ndiyo sisi tufuate,
Mtandao huu unanjia tofauti za kuwasiliana bila kuonekana katika forum hii PRIVATE MESSAGE kwahiyo kuna faida nyingi sana kuijiunga katika chombo hichi cha habari Mahiri ukiwa na shida post hapa utasaidiwa.

Jingine kuongea na watu au jambo usilolijua ,kufahamiana na watu usio wajua nchi mbalimbali kuna faida nyingi sana katika forum hii Muh. huyu ana akili timamu

Hii ndiyo FUTURE ya CHADEMA karibia kila wilaya sasa hivi Tanzania ina INTERNET huyu Muh.Mbowe anaona mbali, ataweza kuwafikia maelifu ya watu kwa mara moja.

Jinsi ambavyo Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano inavyofanya kazi kwasasa Muh. MBOWE YUPO MASOMONI UINGEREZA NA HAPO HAPO ANAONGEA NA WATANZANIA ''LIVE'' !!!HAPA NYUMBANI na sehemu nyingine duniani. RAIS KIKWETE ALIPO KUWA SAFARINI AKUWEZA KUONGEA NA WANANCHI,MPAKA TUSUBIRI MAGAZETI NA TV KESHO YAKE HATA WEBSITE YA STATE HUOSE ''IKULU'' www.statehuose.go.tz HAIPO TANGIA JK AINGIE MADARAKANI, 21 Desemba 2005. Jamani CCM tumieni ICT

Ameanza kipindi kizuri sasa kazi kwetu sisi CCM mimi nina shauri chama changu tuamke katika tekinolojia hii inayo kwenda haraka kuliko maisha yetu.

Muh. Mbowe ameamua kutumia tekinolojia hii kuwasiliana na watanzania kwa sababu ukiandika kitu huku kina kaa milele siyo kama MAGAZETI,TV NA RADIO Ambayo ikiandikwa leo airudi tena imetoka ,kwahiyo watu wata fuatilia sera za CHADEMA milele akiziandika humu azitafutika ,

Watalamu wa tekinolojia wana sema INTERNET itakuwa namba moja katika kutoa habari kuliko MAGAZETI,RADIO,na TV kwa sababu ukiweka tangazo kwenye TV kama uko kazi basi uwezi kuliona lakini ukiweka kwenye INTERNET halifutiki wala haliondoki, linakaa kwa muda mrefu, sasa huyu kaona mbali

Mwendapole samahani kama nitakuwa nimekukwaza kwa hili pia ni kwa faida ya wengine

asanteni
 
Back
Top Bottom