Kila kiongozi na utaratibu wake..jakaya amepita na sasa ni huyu..jakaya alikuwa na uzuri na ubaya wake..uzuri wake ulizidiwa na ubaya(katika maamuzi)...
Wakati wa mwisho wa utawala wake aliyumba katika maamuzi na haya ni yupi awe successor wake...hata huko taasisini aliwayumbisha..hakuwa anaeleweka sana mpaka wazee anaowasema
Pasco wakakutana mbeya(mahali salama) kwa siku tatu na wakaamua wametengeneze magufuli...mchezo wote na fomula zote za yaliyojiri dodoma zilitengenezwa na kikao hiki..yote yaliyotokea dodoma yaliandaliwa hapo...
Lakinj wakati wa maandalizi na mipango ikiwekwa sawa ni watu wawili walipitishwa..huyu aliyekalia kiti na makongoro...ilikuwa piga ua mmoja wao akalie kiti...
Na hata pale dodoma siku ile waziri mkuu mstaafu anakatwa..jina lililokuwa na maksi nyingi toka kamati ya maadili lilikuwa la makongoro...huyu akiyekalia kiti alikuwa wa tatu...na wala membe hakuwepo kwenye list..kwa kifupi membe na lowassa walikatwa...mwenyekiti wa chama akalalama kwa wazee washauro wa chama kina mkapa kwamba yeye kama mwenyekiti mbona hana meno..mtu wake amekatwa...akapewa karatasi yenye majina..katika haki ya kustaajabu mwenyekiti akakata jina la makongoro na kuweka la membe....
Hilo lilikuwa kosa lenye heri kama alifanya yuda kumsaliti yesu ili ulimwengu ukombolewe...magufuli akapitia dirishani na kuingia kwenye ufalme...hizi zote ni fomula za wazee walizotengeneza huko mbeya na kusimamiwa na mkapa hapo dodoma...