The founder: Machache niliyojifunza

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
May 30, 2021
333
673
Habarini wadau wa ukurasa huu.

Nikiwa kati ya watu wenye shauku ya kuona vijana tunajikomboa kiuchumi, nimeona leo nije nishee kitu nilichojifunza.

Binafsi nilikuwa na biashara home Mwanza ya huduma za kifedha, iliyumba hivyo nikaamua kuja Dar kuongeza wigo wa utafutaji, mambo hayakwenda vizuri na sjasimama bado.

Ila ofisi yangu ya Mwanza sikuiua kabisa nilimuacha mama asimamie kifup siitegemei.

Nimekuwa na mgogoro wa kimawazo pia, namna ya kujikomboa katika vita hii ya kiuchumi.

Kitu ambacho nimejifunza ni hiki.

i/ Ni ngumu kufanya kazi pekeako, mfano unataka kuuza nafaka, wewe huyo huyo ukafate nafaka mashambani, wewe huyohuyo uulete mjini, huyohuyo ukatafute masoko, huhuyo urudi ubebe nafaka zako huyohuyo upelekee wateja, huyohuyo wakuahidi baada ya sku tatu ufate pesa. Ni ngumu sana kufanya kazi kwa namna hii inabidi utafute team.

ii/ Jinsi ya kufanya biashara katika mfumo mzuri na namna ya kuiendesha.

Kingine jana nilitembelea kampuni ya kilimo malembo farm nimeogeza maarifa zaidi kwa kujifunza vitu vingi, nilibahatika kupata simulizi kutoka kwa watu wa ndani kabisa wanaomiliki kampuni hio, nikawaza kama ni vyema tuunde club maalum kwa wale walio na maono juu ya maisha yao. Katika club hii tutakua tunakumbushana na kushaurina ili kufikia malengo.

Nawasilisha

IMG_20220228_151548_6.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom