Jackline Mahulwa Masanja: Nyota iliyozimwa kabla ya kuangaza

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Na Malisa GJ,

Mara ya kwanza nilifahamiana naye nikiwa Lusaka, Zambia mwaka 2012. Alijitambulisha kuwa ni Mtanzania, mwanaharakati na mzalendo. Alikua mwanachama hai wa CHADEMA. Ndiye aliyenipa habari za kifo cha mwandishi Mwangosi aliyeuawa kikatili na Jeshi la Polisi.

Baadae nikaja kumsikia kupitia kipindi cha 'Njia Panda' cha Clouds Fm akielezea namna alivyopata maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Sikushtuka kumsikia 'NjiaPanda' maana kabla ya hapo aliwahi kunieleza kuwa alikua akiishi na virusi vya UKIMWI kwa miaka 10 hadi wakati huo.

Nilipenda ujasiri wake wa kujikubali hali yake bila hakujificha. Angeamua kuficha basi angeweza kuua watu wengi sana maana alikua msichana mrembo, mpole, mwenye akili nyingi, na mwenye umbo na sura ya kuvutia.!

Baadae tukaja kukutana Arusha akiwa kwenye harakati za chama, nikamuona kavaa gwanda yupo na Kamanda James Ole Millya. Hapa ndipo nilipojua ni mwanachama wa CHADEMA. Awali nilijua ni mwanaharakati na mpenda demokrasia wa kawaida tu, kumbe alikuwa pia mwanachama hai wa chama cha siasa. Alinionesha kadi yake ya uanachama iliyolipiwa ada kwa kipindi chote. Kuanzia hapa nikaanza kumuita "kamanda"

Baadae akanijulisha yupo Arusha. Aliamua kuanzisha maisha yake mapya huko. Alifungua biashara ya nafaka. Alianzisha kampuni yake ndogo iliyo-deal na kuzalisha bidhaa za nafaka na kuzipack vizuri na kusambaza kwenye supermarket na maduka ya kawaida.

Wakazi wa Arusha bila shaka wamenunua sana bidhaa zake zenye nembo ya "Mahulwa Investment" kama unga safi wa sembe, unga wa lishe, mchele, etc. Ni nyota iliyoanza kuchomoza vizuri. Nilipenda sana spirit yake ya utafutaji licha ya kuwa alikua na maambukizi ya HIV.

Kwake HIV haikua kifo, ilikua sehemu ya maisha yake na aliikubali hali hiyo. Alijua kuna maisha baada ya HIV. Nakumbuka siku moja nilikutana nae Singida, mimi nikiwa kwenye basi kutoka Mwanza yeye akielekea Dodoma kutafuta fursa za biashara zake. Nilishangaa alivyokuwa akichakarika na ujasiriamali while alijua ana maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Dakika 10 nilizokaa nae pale Singida nilijifunza mengi. Aliniambia "Malisa HIV sio UKIMWI na UKIMWI si kifo. Nimeishi na HIV kwa miaka 10 sasa na maisha bado yanaendelea. Nimeikubali hali yangu, siwezi kukata tamaa"

Mwaka 2013 niliandaa kongamano kubwa la kujadili maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Mgeni Rasmi alikua Wazirii wa Afya Mhe.Hussein Mwinyi na mgeni wa heshima alikua Mhe.James Mbatia.

Nilimkaribisha pia Jack kwenye kongamano hilo aongee na vijana wenzie namna alivyoweza kuishi na HIV miaka yote hiyo. Bahati mbaya alishindwa kushiriki maana alikua Dar kufuatilia mambo yake ya kibiashara.

Siku ya kongamano alinitumia ujumbe wa simu (sms) akisema "Malisa nilitamani sana kushiriki nanyi. Ningefurahi kupata fursa ya kuelezea hali yangu mbele ya vijana wenzangu na wengine wanaodhani kuambukizwa HIV ni kifo. Lakini bahati mbaya nimeikosa fursa hiyo kutokana na ratiba kunibana. Nawatakia kila la heri"

Baada ya hapo tukaendelea kuwasiliana na kujuliana hali. Mwaka juzi (2013) wakati "Waraka wa siri" wa ZZK, Prof.Kitila Mkumbo na wengineo ulipokamatwa, Jack alisikitika sana maana ZZK alikuwa "role model" wake.

Aliniambia "nimeusoma waraka wa siri sioni kosa lolote maana ule ni mkakati wa kushinda. Siasa yoyote lazima iwe na mkakati. Bahati mbaya mkakati wao umevuja kabla ya wakati".

Nakumbuka nilibishana nae sana juu ya suala hilo lakini aliendelea kushikilia msimamo wake. Mwishowe nikamwambia "Lets agree to disagree".

Tukaendelea kuwasiliana ktk namna ya kawaida hasa ktk mambo yahusuyo chama na issues za biashara. Baadae akaniambia anatishiwa maisha kwa kuwa amejipambanua kuwa mwanachama wa chama cha upinzami. Nikamtia moyo kuwa asihofu hiyo ni kawaida ktk maisha ya siasa.

Mara ya mwisho tulipowasiliana alinieleza juu ya mpango wake wa kusajili kampuni yake ili awe na wigo mpana zaidi wa kufanya biashara zake. Alinieleza kuwa licha ya biashara yake ya nafaka anataka kuongeza bidhaa nyingine kama Mafuta ya kupikia, Juice na Maji ya kunywa vyote vikiwa na nembo yake.

Lakini alilalamika kuwa alipata changamoto ya kusajili kampuni hiyo kwa sababu za kisiasa.

Mwezi October mwaka jana nilimuuliza "mbona upo kimya sana siku hizi kamanda?", akanijibu "kamanda nafuatilia usajili wa kampuni yangu na kuongeza products mpya sokoni. Nikimaliza nitarudi tena kwenye harakati"

Baada ya hapo hatukuwasiliana tena hadi jana nilipopewa taarifa kuwa amefariki Dunia. Nilishtuka japo si sana maana niijua alikua akiishi na maambukizi ya VVU. So nikajua labda aliugua na kufariki dunia.

Lakini nilipofuatilia habari za kifo chake nikajikuta natokwa na machozi na kuamini kweli dunia hii imejaa ukatili. Jack hakufa kwa ugonjwa bali aliuawa. Tena aliuawa kikatili mno na watu "wasiojulikana"

Gazeti la UWAZI la November mwaka jana liliripoti juu ya kifo cha Jack na wakaweka picha yake kwenye ukurasa wa Mwanzo na maandishi 'Dar si salama tena'. Bahati mbaya sikuliona hilo gazeti, hivyo wala sikujua kama Jack amefariki.

Msimu wa Xmass nilimtext kumtakia heri ya Xmass lakini hakujibu, nikadhani yupo 'busy' nikamuacha. Mwaka mpya pia nikamtext kumtakia heri lakini hakujibu. Nikaconclude kuwa yupo busy atanijibu akipata muda.

Maskini kumbe nilikua natext maiti. Nilipomtumia ujumbe wa X-mas mwaka jana, kumbe Jack alikua ana mwezi mmoja kaburini. X-mas yake ilikuwa akhera mimi huku duniani nahangaika kumtumia sms.!!

Taarifa za gazeti la UWAZI lililoripoti kifo chake zinasema Jack alitekwa na wanaume wanne wasiojulikana akiwa na rafiki yake maeneo ya Mlimani City mwishoni mwa November mwaka jana. Wote wawili walitekwa na kuingizwa kwenye gari aina ya Toyota Noah na watekaji kupotea nao.

Jack alifanikiwa kutuma ujumbe kwa familia yake kuwa ametekwa. Familia ilitaharuki na kuanza kumpigia simu. Lakini kitu cha kusikitisha ni kuwa watekaji walichukua simu yake na kuanza kuwasiliana na ndugu zake kwa sms kuwa hawajatekwa hivyo wasiwe na hofu.

Yani watekaji walimnyang'anya simu Jack na mwenzie, kisha kuwatext ndugu zao wakijifanya wao ndio Jack wakisema "msiwe na wasiwasi hatujatekwa, nilikua natania tu. Tuko salama"

Baada ya siku mbili mwili wa Jack uliokotwa maeneo ya Temeke akiwa ameuawa kikatili kwa kupigwa na kitu kizito kichwani. Na mwili wa rafiki yake ukaokotwa mtaroni huko maeneo ya Airport. Wote wawili waliuawa kikatili na "watu wasiojulikana".

Hakuna ajuaye sababu za watekaji hao kuwaua kikatili hivyo. Ni wivu wa kimapenzi? Ni sababu za siasa? Ni mambo ya biashara? Hakuna ajuaye zaidi ya Mungu wa mbinguni ajuaye mambo ya sirini.

Vifo vya mabinti hawa vimenisikitisha sana. Pamoja na mambo mengine nimegundua kuwa nchi hii si salama kama tunavyodhania. Waliomuua Jack na mwenzie hadi leo hawajakamatwa kwa kigezo eti ni "watu wasiojulikana".

Kuna madai kuwa watu hao walikua wakiwasiliana nae kwa simu. Na inadaiwa kwenye hilo kundi lililomteka alikuwepo pia boyfriend wake. Sasa hao kweli ni "watu wasiojulikana?"

TCRA wako wapi? Kwanini wasitrace mawasiliano ya mwisho ya marehemu ili kujua aliwasiliana na nani na kuisaidia Polisi? Usajili wa simu una maana gani kama mtu anaweza kuwasiliana na wewe na akakuua bila kujulikana?

Jana Comrade Msando Alberto alihoji juu ya dhumuni la kusajili simu ikiwa bado uhalifu wa mitandaoni unaendelea. Hivi TCRA mmeshindwa kazi kiasi hiki?

Kingine nilichojifunza kwenye kifo hiki ni kuwa hakuna ajuaye mwisho wake. Jack alijua ana maambukizi ya HIV na pengine alidhani UKIMWI ndio utakaomuua, lakini amekuja kufa kifo tofauti kabisa na alichotegemea.

Ameishi na HIV miaka 10 lakini hakukata tamaa, ametafuta fursa za kiuchumi, amejiingiza kwenye harakati za siasa, ameamua kujilinda na kulinda wengine asiwaambukize, ameamua kutumia ARV, kufanya mazoezi na kula vizuri ili aishi maisha marefu, Lakini anakuja kuuawa kama kondoo na watu "wasiojulikana".

Jack ktk maisha yake alikua mwanaharakati wa kweli. Kwa haraka naweza kusema alipambania mambo makuu matatu. La kwanza ni AFYA. Alipambana sana kuilinda afya yake baada ya kujua ameathirika.

Pili ni UCHUMI. Alitumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi na kukuza maendeleo yake na jamii kwa ujumla. Wapo watu wazima kiafya (wasio na HIV kama Jack) lakini hawawezi hata kuona fursa zinazowazunguka. Na hata wakiziona hawawezi kuzitumia.

Tatu ni SIASA. Jack alipambana kupigania haki za watanzania wenzake ambazo zimekuwa zikididimizwa na tabaka tawala. Alichagua chama alichoamini kitamfaa kupaza sauti yake. Alichagua CHADEMA.

Lakini pamoja na changamoto za kiafya, kiuchumi na kisiasa alizokua nazo bado watu wasio na huruma wameamua kukatisha uhai wake wakijificha kwenye mwavuli uitwao "watu wasiojulikana"

Nachukia sana hili neno "watu wasiojulikama"... Polisi wote, askari wa upelelezi, maofisa wa usalama wa taifa, where are you hadi nchi hii iwe na "watu wasiojulikana??". Huu ni udhaifu mkubwa unaotumika kupalilia uhalifu.

Maalbino wanauawa na "watu wasiojulikana", ndugu zetu wanatekwa na kuuawa na "watu wasiojulikana".. halafu polisi mnasimama kwenye media na kukiri ni "watu wasiojulikana".

I hate this phrase. Ikiwa siku moja wataniua na mimi please don't use "watu wasiojulikana" kuripoti kifo changu, maana nitakanusha nikiwa huko ahera.!

Nimeumizwa sana, nimefadhaika sana na nimemhurumia sana Jack. Sijui ni mateso kiasi gani alipata hadi kukata roho ila ninachojua ni kuwa Jack angekuwa taswira kubwa kwa vijana wengi wa Tanzania siku za usoni.

Alikua dada mwenye upeo na maono. Alikuwa hodari, mchapakazi, Mzalendo, mwenye bidii, na asiyekata tamaa. Kwa umri mdogo aliokuwa nao aliweza kuanzisha kampuni ndogo na kutoa fursa ya ajira kwa vijana wachache. Laiti angeishi miaka mingi angetoa fursa nyingi zaidi za ajira kwa vijana wengi baada ya biashara yake kutanuka.

Naona ajira nyingi za watanzania zikipotea baada ya kifo chake. Naamini angekuwa hai angefanya mengi makubwa. Ange-invest na kuajiri vijana wengi kwenye hiyo kampuni yake, kwa maendeleo yao na nchi kwa ujumla.

Lakini yote yamezimwa na kikundi cha watu "wasiojulikana". Yote yamebaki kuwa historia. Yote yamepotea.!

Ile nyota ya mafanikio iliyoanza kuchomoza hatimaye imefifia na kupotea kabisa.

Buriani Jackline Mahulwa Masanja. Ulikuwa rafiki, ndugu, mshauri na mpenda demokrasia. Sitakusahsu kamwe ktk maisha yangu. Pumzika kwa amani. Naamini ipo siku tutakutana tena Paradiso.!

Malisa GJ.!
FB_IMG_1642147941521.jpg
 
Pole sana RIP Jackline na Mwenzie, ungeshare their numbers dont hold information as you have decide to speak up
 
Inasikitsha sana matukio kama haya kutokea na serikali kusema kukaa kimya bila kutoa tamko, ile kauli kwamba serikali ina mkono mrefu ilitakiwa ithibitishwe kwenye matukio kama haya tena kwa kuzuia tukio si kufanya uchunguzi baada ya tukio.RIP Jack.
 
Malisa GJ.!View attachment 2080530
Lengo la kusajili laini za simu lilikuwa ni la kufuatilia wafanyabiashara na wapinzani tu na halikugusa, halijagusa na halitagusa wahalifu wanaotusumbua.
 
Back
Top Bottom