Sekta ya madini inavyofungua fursa za biashara, uchumi

I wish i have

Senior Member
Nov 2, 2021
136
62
Na Tito Mselem

Tanzania ni miongoni mwa mataifa Duniani yaliyobarikiwa zaidi kwa rasilimali za asili. Miongoni mwa rasilimali hizo ni pamoja na madini ambayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza vipato vya Watanzania na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Shughuli za uchimbaji wa madini nchini zimekuwa zikivutia Kampuni kutoka mataifa mbalimbali kuwekeza kwenye shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini hivyo kuchochea ukuaji wa sekta nyingine kiuchumi.

Baadhi ya kampuni hizo ni kutoka katika nchi za Australia, Afrika ya Kusini, China na Canada ambapo kupitia uwekezaji wao umeifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazozalisha dhahabu kwa wingi barani Afrika.

Licha ya kampuni za kigeni kuwekeza, pia, wazawa wamekuwa wakipewa kipaumbele zaidi ambapo Serikali inaendelea kuwawezesha wananchi kuwa sehemu ya umiliki wa rasilimali madini kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Miongoni mwa mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali kwa siku za karibuni katika Sekta ya Madini ni pamoja na uboreshwaji wa miundombinu muhimu katika maeneo ya migodi kwa kuchukua hatua mbalimbali ili kuchochea shughuli za madini zifanyike kwa ufanisi. Serikali imeendelea kuhamasisha uwajibikaji wa Kampuni katika huduma za kijamii (CSR) ambapo Kampuni zimejenga miundombinu ya barabara, madarasa, madawati, vituo vya afya katikamaeneo yanayozunguka migodi hiyo.

Pia, katika kuhakikisha wachimbaji wa madini wanaendelea kunufaika, Serikali imeanzisha masoko ya madini katika mikoa mbalimbali nchi nzima ambapo mchimbaji mdogo ana fursa ya kwenda kuuza madini yake kwa uwazi na kwa faida.

Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeendelea kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wa madini kufanya shughuli zao kwa uhuru ili waweze kupata faida na kukuza uchumi wa Nchi.

Hili linakwenda sambamba na namna serikali ilivyodhamiria kufungua fursa za kibiashara kupitia Sekta ya Madini baada ya kuanzisha Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery Limited kilichogharimu shilingi bilioni 12.2.

Wakati wa ufunguzi wa Kiwanda hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anaeleza kuwa kiwanda hicho kitasaidia kuchochea shughuli za uchimbaji madini kwenye Ukanda wa Ziwa Victoria ikiwa ni pamoja na kutoa ajira 120 za moja kwa moja na 400 zisizo za moja kwa moja. Pia, kiwanda hiki kuchangia mapato ya Serikali kupitia mrabaha, tozo za ukaguzi na ushuru wa huduma pamoja na kuchochea shughuli nyininge za kiuchumi.

Vilevile, anasema mtambo huo na mingine miwili iliyopo katika Mikoa ya Dodoma na Geita na masoko ya madini ni matokeo ya mabadiliko ya sheria iliyofanywa na Serikali katika Sekta ya Madini ambayo imeongeza makusanyo ya maduhuli kwa mwaka 2020/2021 na kufikia jumla ya shilingi bilioni 584.83

Aidha, Serikali imeendelea kuonesha fursa za kibiashara zilizopo kwenye Sekta ya Madini kupitia Maonesho ya madini yanayoandaliwa na Mikoa mbalimbali yenye shughuli za madini. Lengo ni kuhakikisha wananchi na wadau wanafahamishwa kuhusu fursa mbali mbali zilizopo.

Akizungumza wakati akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini, Mkoa wa Shinyanga Waziri wa Madini Doto Biteko anasema maonesho hayo ni kielelezo cha kuwafanya watanzania kujijengea uwezo wa ndani na kuchangamkia fursa katika Sekta ya Madini. Aidha, maonesho hayo yanalenga kutangaza fursa zilizopo katika Mikoa husika kupitia Sekta ya Madini.

Wakati akitembelea maonesho hayo, Waziri Biteko anatoa wito kwa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya fundi Stadi (VETA) kuchangamkia fursa ya kutengeneza mitambo inayotumia teknolojia rahisi kwa ajili ya shughuli za uchimbaji baada ya kuona mitambo iliyotengenezwa na taasisi hizo. Lengo ni kutaka manufaa hayo yabaki nchini na kukuza sekta nyingine.

Biteko anawataka watanzania kuona fursa zilizopo katika mnyororo mzima wa Sekta ya Madini na kuzitumia. Anaongeza kuwa, ushiriki wa vikundi mbalimbali katika maonesho hayo unafanya Taifa kuwa na Wajasiliamali wakubwa ikiwemo kutoa msukumo wa kuwafanya kuwa wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji kwenye nchi yao.

“Huko ndiko kufungamanisha uchumi wa madini na sekta nyingine kwa kufanya hivyo tutakuwa tumefungua fursa za kibiashara kwa watanzania,’’ anasema Waziri Biteko.

download.jpg
 
Back
Top Bottom