The first KFC restaurant in Tanzania !


matangazo at work..
 
hiyo ya kisado niliioma mbele bongo ipo? kama ipo ni wapi wanaoffer such kind of a service?
 

hiyo ya kisado bongo inapatikana wap?
 
Mie zangu kwa Mpemba buguruni sheli, supu ya kuku wa kienyeji na chapati mbili, pilipili mbuzi na ndimu nalipa 3500 maisha yanasonga
 
Hawanipati ng'o, nani alishwe Farasi? waulizeni ulaya walivyowashtukia hawa meat supply dealers.
 
Nakuona mtani ha ha ha,

Naona umewapa A nandos, hao wanakubalika kila kona ni watamu sana kuku wao. Lakini hawa KFC kuku wao ukimla moyo unaenda mbio utasema yale mafuta yameenda kuziba mishipa ya damu ghafla

Yaani hao nawakubali kweli mtani wangu..nikipata chicken na spicy rice inayoogelea kwenye zile sauces zao, ooh mine!!Halafu dar kuna nandoz ya kuiga jina tu, khaah!!...
Mie sio mpenzi wa KFC na kweli futaz kibao..ila naona watapata wateja wengi sana bongo kama jf wanavyoupokea ujio wao.
 
11 herbs and spices secret recipe, ya hawa jamaa inayotengenezwa na watu wawili tu duniani na ambao hawaruhusiwi kusafiri pamoja watu wanaijua? Na ni kwanini kuku wao wakikaa nje ya jokofu hata wiki nzima hawaharibiki? Je tumboni ni salama?
 
hao kuku ni watamu balaa!! japo ni expensive ila ni watamu mnoooooo! nairobi huwa tunapanga na foleni kabisaaaaaaaa! japo full ni 4 thou kshs, ila hiyo nyomi ni balaaa!! nitakuwa mteja wao haswaaaaaaa, welkam kfc in bongo!

Utamu ni pickling spice au asili ya kuku? Eating places nyingi Nairobi hawatumi spices ni standard tomato sauce and salt for chips chicken. Dar make better chips and chicken hadi mitaani. Alternative to chips chicken vyakula vya mswahili at Malindi dishes Nairobi CBD, off Luthuli avenue. Food is good and prices fair. Frequent place since my student days.
 
Wenye kutaka kujisunda hizo vyakula-pepe vya Kimarekani waende tu, lakini waandae pia na pesa nyingi za kutibiwa matatizo (SIO MAGONJWA) ya moyo, figo, saratani, kisukari, n.k.

Kwa raha zenu. Mie ntashindia ugali wangu wa dona na samaki wa kuchemshwa. Tuone nani atawahi hospitali.
 
Sun wu...Nando si mchezo mi naweka mbali kisu na uma ni mikono tu!
 
Ahsante sana Mkuu saragossa...Mie mavyakula hayo hata hamu nayo sina!!! Nikipata ugali wangu wa samaki wa kukaanga na pembeni mchicha chukuchuku, pilau la kibongo, chapati na mchuzi wa kuku n.k. nafurahia msosi ile mbaya. Niliwahi kuyala hayo mavyakula sijayagusa tena.

Naona tumesogezewa cancer na ugumba karibu sasa! Mi ngoja niendelee na matembele yangu na dagaa pamoja na ngisi banaa!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…