The Bold & Nifah: Happy Six Months "Anniversary"!

The Bold & Nifah: Happy Six Months "Anniversary"!

Kufuta post dalili tosha kuwa jamaa mgaigai , tapeli na sio wa kuaminika na mtu wa kumtilia mashaka .

Bahati nzuri Jf watu usiwaone kimya wana akili wanaweza kukuchimba na kukufuatilia kiundani na kugundua janjajanja zako bila kukujua na wanaweza kukuumbua mpaka kuona Jf hii chungu na historia humu inaonyesha watu wengi matapeli na WA kufake life wameumbuliwa na wengine kukimbia Jf mazima.

Jamaa nilimuona kipindi Cha nyuma kwenye nyuzi kadhaa ni mtu wa Shari na baadhi ya members haswa wa Kike mpaka kufika stage za kuanikana privacy.
Jamaa anafuatilia sana maisha ya member wa kike humu...

ana tabia zote za kupoteza ubingwa...

hivi mwanaume uliyekamilika, mwenye mambo yako binafsi unaumia nini juu ya mahusiaono ya wanawake na watu wao?
 
Inasikitisha sana mkuu.

Ndio maana Mimi nimeridhika ya maisha ya ukapuku nafanya yangu tu tukikwaruzana na mtu kwenye nyuzi tunazichapa hapo hapo inaisha na sio kuhifadhi mpaka kufikia kwenye kufuatiliana personal life na privacy.
 
Sasa km hajapiga si angeonekana bwege nyuzi lote hili..!! 😹😹😹

Haya masijala una la kuongezea?
Mrs none kitengo chako hiki na mwenzio cocastic mbona mnaleta uzembe kazini? 😹
Tatizo ubuyu wa huyu N, Mie nilipewaga script 2 tofauti, hata sijui, lipi ni lipi. Lol
😂😂😂😂😂
 
Ile siku aliwapaka na coca nikabaki nacheka 😹😹😹
Zile nguvu zilitokana na mimba ndiomana nikatulia nisije kumuharibia mtoto udugu wangu, ninavyompenda alete baby girl 🥰🥰
Ampake nani? Shouzzz hawezi kunipakaa?
😂😂😂😂😂
 
Nchi za mashariki mwa bara la Asia kuna falsafa ya kale sana wanayoiamini kuhusiana na muunganiko na mahusiano ya binadamu. Falsafa hii inaitwa Red String Of Fate (Yīnyuán hóngxiàn).

Kwamba, kuna 'uzi' usioonekana unawaunganisha watu tangu siku wamezaliwa, watu ambao maishani wanatakiwa kuja kukutana, au kusaidiana au kuwa pamoja.

Uzi huu usioonekana unalindwa na kusimamiwa na aina ya Mungu/roho anayeitwa Yuè Xià Lãorén (au kwa kifupi Yuè Lão).

Tafsiri rahisi ya jina la "mungu/roho" huyu ni "matchmaker god"
Yeye anasimamia uzi huu unaowaunganisha watu hawa usikatike daima mpaka pale watakapokuja kukutana.

Nchini china wanaamini uzi huu unafungwa kwenye viwiko vya mkono, na nchini Japan wao wanaamini uzi huu unafungwa kwenye kidole kidogo cha mwisho na kwamba uzi huu unaowaunganisha watu hawa, unaweza kupinda (tangle) au kunyooka zaidi (stretch) lakini kamwe hauwezi kukatika mpaka watu hawa wakutane.

Kwa kifupi, imani hii ya watu Asia inarandana na imani ya watu wa magharibi kuhusu 'Soulmate'.

Mimi na Nifah: Historia fupi

Nikiwa sekondari nilikuwa naisikia sikia kitu kinaitwa "jambo forums" na 'kasheshe' zake lakini sikuijua sana kwa undani.

Baadae mwaka 2009 nikiwa kidato cha tano nikaichungulia ndani kujua yaliyomo, kipindi hiki ilikuwa imeanza kuitwa "Jamii Forums".

Kipindi hiki kulikuwa na mijadala 'mizito mizito' sana na karibu yote ilihusu siasa.
Japokuwa nilikuwa 'mtoto wa sekondari' nilivutiwa nayo sana, napenda sana mijadala, hasa mijadala mizito (yenye hoja sio matusi).

Mwaka 2011 nikajiunga rasmi (kwa ID nyingine) lakini baadae nikasahau password ya ile ID. Ndipo hapa mwaka 2013 nikafungua ID hii ya The bold.
Mwanzoni nilikuwa nasoma tu, sikuwa mchangiaji sana, lakini kuanzia 2014 nikaanza kuwa active zaidi na hata kuanzisha threads.

Kwa sababu zangu binafsi, nikaepuka mijadala ya jukwaa la siasa, na nikajikuta navutiwa zaidi na Jukwaa la Jamii Intelligence. Na nikitaka kupumzika nikawa naingia Celebrities Forums… na huko ndiko mambo yalikoanzia.

Binafsi nina maslahi fulani fulani na pia ni shabiki mkubwa wa vijana wa WCB. Huko Celebrities Forum nikakutana na bibie Nifah mkosoaji mkubwa wa WCB.
Taratibu tukaanza kukwaruzana kwenye mijadala. Ugomvi huu ukawa mkubwa zaidi na kufikia pabaya mwaka 2015 na mwanzoni kwa 2016. Ulikuwa ni ugomvi mkubwa haswaaa kiasi kwamba tulikuwa tunatoleana lugha Kali za aibu kabisa. Ugomvi huu ukaendelea na kukua siku baada ya siku, kiasi kwamba Nifah akawa adui yangu namba 1 humu JF na mimi nikawa hivyo kwake.

Lakini ukweli ni kwamba rohoni nilikuwa namkubali sana huyu bibie na nilikuwa navutiwa nae sana, IQ yake, ujengaji hoja wake na niliamini ni mtoto mrembo haswaaa!!

Kwahiyo mara kwa mara nilikuwa nafanya ule mchezo wa kutembelea profile yake na kuanza kuangalia replies zake kwenye threads mbalimbali. Nikazidi kuvutiwa naye zaidi na nikajikuta naanza kulike posts za huyu "adui" yangu.

Pasipo mimi kujua, kumbe naye anafanya mchezo huu wa kutembelea profile ya mimi "adui" yake na ghafla nikaanza kuona likes kutoka kwake.
Baadae tension kati yetu ikaanza kupungua na tukawa tukikutana kwenye threads yoyote lazima tuchit chat.
Kipindi cha uchaguzi wa marekani nakumbuka tulibet, yeye akaweka 100K kwa Clinton, mimi nikaweka 100K kwa Trump, [emoji23].. Alijuta [emoji23][emoji23]

Chit chat kwenye threads zikaendelea…

Kisha tukahamia PM. Huko PM kilichoendelea sitaki kuwasimulia… ila kwa ufupi mwana wane sikutaka ujinga, nikajitutumua, nikafanya yangu… and the rest is history.!

Tangu hapo… we have been crazily in love together!

Najivunia kumpata mwanamke wa dizaini yake, ana heshima, mnyenyekevu, big IQ, beautiful, anajua kukalangiza jikoni na mwenye kujua haswa mapenzi ya dhati… bila kusahau usiku tukizima taa huwa najihisi tumeenda kutalii sayari ya Mars!! Mashallaaahh…

Nafurahi pia ndugu zake wanajivunia mimi kuwa na binti yao, na ndugu zangu pia wanajivunia mimi kuwa na huyu binti.!

Mwenyezi Mungu akutunze white masai wangu… na wakuu mtuombee soon tunataka kufanya halal..

Imekuwa six months sasa tuko pamoja… let's make it to six more years, and then 60 years na hatimaye 600 years!! Let's make this forever...

Happy six months anniversary soulmate...
Nakupenda sana Cheupe!

The Bold
-----------
Jangid plaza chali
 
Nnatamani kuuuliza swali fulani lakini naogopaa🤣🤣🤣🤣......mrs none, coca, trudie wote alituweka kwenye mstari 🤣🤣🤣
😂😂😂😂😂
Jamaniii mie hawezi kuniweka kwenye mstarii, ni vile nimeamua kuacha mambo ya flow vile anataka.

Na anajua.
 
😂😂😂😂😂
Jamaniii mie hawezi kuniweka kwenye mstarii, ni vile nimeamua kuacha mambo ya flow vile anataka.

Na anajua.
Si ndio anasema jeshi la mtu mmoja eti 😀😀😀
 
Inasikitisha sana mkuu.

Ndio maana Mimi nimeridhika ya maisha ya ukapuku nafanya yangu tu tukikwaruzana na mtu kwenye nyuzi tunazichapa hapo hapo inaisha na sio kuhifadhi mpaka kufikia kwenye kufuatiliana personal life na privacy.
Maisha ni yako Ila mazishi ni yetu. Lazima tukufatilie😅
 
Jamaa anafuatilia sana maisha ya member wa kike humu...

ana tabia zote za kupoteza ubingwa...

hivi mwanaume uliyekamilika, mwenye mambo yako binafsi unaumia nini juu ya mahusiaono ya wanawake na watu wao?
Achana na hayo dogo, niweke hapo kwa nifah😅
 
Kufuta post dalili tosha kuwa jamaa mgaigai , tapeli na sio wa kuaminika na mtu wa kumtilia mashaka .

Bahati nzuri Jf watu usiwaone kimya wana akili wanaweza kukuchimba na kukufuatilia kiundani na kugundua janjajanja zako bila kukujua na wanaweza kukuumbua mpaka kuona Jf hii chungu na historia humu inaonyesha watu wengi matapeli na WA kufake life wameumbuliwa na wengine kukimbia Jf mazima.

Jamaa nilimuona kipindi Cha nyuma kwenye nyuzi kadhaa ni mtu wa Shari na baadhi ya members haswa wa Kike mpaka kufika stage za kuanikana privacy.
Post zangu humu nilifuta toka mwaka juzi, nilikuaga chawa Ila sasa hivi nimepanda grade😅😅
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom