Mkuu Pasco,
Tuweke record sahihi, Mkapa amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje 1977-80 under Nyerere, then 1984 - 1990. Baada hapo alikuwa Balozi Diria (RIP). Kwa kufuata hiyo mantiki yako, then Rais angekuwa Marehemu Diria. Maana kipindi cha 1990 - 1992, Mkapa alikuwa Habari na Utangazaji, then 1992 - 1995 akaenda Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.
Kuhusu Membe, naomba usijenge hoja kwa kutumia Wizara ya Mambo ya Nje, maana itakuwa haina mashiko. Kutumia kigezo cha Kikwete kukaa MFA kwa miaka 10, bado Membe atakuwa hajafikisha miaka 10, maana kuna miaka 2 ya mwanzo alikuwepo Bibie Asha-Rose Mtengeti-Migiro.
Bottom line ni kwamba it is too early kuanza kuongelea mitandao ya kumuweka mtu kwenye hiyo nafasi. Sana sana kwa mtu kama Michuzi ni kujiwekea maadui bure na siasa za Bongo siku hizi ni za visasi. Waulizeni waliokuwa wapambe wa Sumaye leo hii wako wapi na wanafanya nini? Hiyo ndio siasa ya Bongo.
Pia siasa za CCM hazieleweki, leo hii watu wanaweza kuhisi kwamba JK yuko upande wa Membe na ukaja kushangaa dakika za majeruhi 2014 kuelekea 2015 jamaa anahamisha kambi kama ilivyokuwa kwa Mkapa ambaye alibadilisha mawazo dakika za majeruhi. Ni Mkapa huyu huyu na Philip Mangula ambao walisema wamestaafu siasa, ujio wao kwenye kampeni za Igunga should be a signal kwamba they are up to something. Uchaguzi wa CCM wa 2007, Mangula aliambulia patupu akaamua kuendelea na kilimo cha viazi huko kwao. Ilikuwaje juzi kule Igunga akakumbukwa na ni nani aliyemwita aende kupiga kampeni? Hali halisi ndani ya chama iko slippery hakuna ambaye ana uhakika na kitakachotokea 2015 on mgombea wa chama. Lakini uchaguzi wa ndani ya chama wa mwakani unaweza kutoa mwanga wa mwelekeo.