Thanks God for Giving us Kikwete

Tumshukuru M/Mungu kwa kutupa uhai na nguvu - ili kuendeleya kuishi tukiwa wazima na wenye afya. Na tumshukuru M/Mungu pia kwakutubainishiya Mazuri na Mabaya.

M/Mungu anapotauambiya "Sisi tupange yetu, na wao wanapanga yao; ila mwisho wake la M/Mungu ni bora"

Kwahiyo kuwepo kwa JK pale alipo ni M/Mungu - ila tu, anayomengi moyoni mwake (ambayo sisi hatuyajui) - ila M/Mungu kwa kipindi hichi anatuleteya yale waTanzania tunotaka kuyaona na kuyasikia!

Ila kwakutumia dhana kwa kujaribu kubashiri yaliyokuwemo ndani ya Moyo wa Raisi wetu - ndo hayo hayo ambayo wananchi tunataka kuyaona na kuyasikia.

Tumwombe apate nguvu kuyafikiria na kuyajua M/Mungu na Watanzania wanayo yataka ili ayatende.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
lengo tumeanza kuliona, manake ingekuwa enzi za BMK hapa angethubutu kufungua mtu mdomo kushutumu ufisadi??!!
 
Mchungaji soma alama za nyakati,Huyu JK una hisa naye ama? Unadhani kuwa yeye ndiye anayekuruhusu kusema haya? Naomba ujue wakati wa bwana umefika, jiulize mbona hapo mwanzo haikuwa hivyo? Mungu wetu kaona atutoe utumwani, si kikwete wala yeyote yule
 
Mchungaji soma alama za nyakati,Huyu JK una hisa naye ama? Unadhani kuwa yeye ndiye anayekuruhusu kusema haya? Naomba ujue wakati wa bwana umefika, jiulize mbona hapo mwanzo haikuwa hivyo? Mungu wetu kaona atutoe utumwani, si kikwete wala yeyote yule

Kama M/mungu alivyomtia moyo mgumu Farao kuwaachilia wana wa Israel, ili kuonyesha kuwa yeye anaweza yote, na ili litimie kwa Tanzania! Ameni
 
Pale mwadadamu anapofikia kikomo cha kufikiria ndipo Mungu huingilia kati ili kuonyesha ukuu wake. Tanazania ilikuwa imekata tamaa hasa wakati huu wa kiongozi wetu JK. So, yawezekana Mungu akamuweka makusudi ili aproove failure na ndipo Yeye Mungu anaingilia kati na kuonyesha Ukuu wake
 
I still send praise to the Most High kwa sababu...Kupitia kwenye utawala wa huyu JK tumeweza kushuhudia wakongwe wenye majigambo na misifa wakianguka!!!
 
I still send praise to the Most High kwa sababu...Kupitia kwenye utawala wa huyu JK tumeweza kushuhudia wakongwe wenye majigambo na misifa wakianguka!!!
Glory glory glory....to the MOST HIGH
 
Kwani ni Mungu "alitupa" Kikwete? Kumshukuru Mungu kwa kufanya kitu ambacho labda hakukifanya haiwezi kuwa kumdhihaki? Wewe Carmalenge ambaye unatangazia dunia "Habeamus Papam" unaamini kweli Mungu angetupa Kikwete? Kwani tumemkosea nini?

Mungu alijua, kabla ya wakati, kwamba JK agekuwa Rais wetu. Alijua hivyo hata kabla baba yake JK hajazaliwa. Lakini unataka kusema ni yeye alichora dili la kuchukua fedha BoT kwa ajili ya takrima za kumfanya JK akubalike? Hapana, Mungu hakutupa JK. Tumejitwalia huyu ndugu wenyewe baada ya kunogewa na takrima.

Kilichobaki ni kumwomba Mungu aendelee kumpa JK ujasiri wa kuruhusu mafisadi wafichuliwe. Ampe hata nguvu ya kuwavaa Mkapa, Yona na Rostam Aziz. Akiwavaa hao basi hata mimi nitaanza kudhani labda ni Mungu ametupa huyu mwenzetu.


Moshi,

Just curious , in the past you have said that Mkapa was the best president Tanzania has ever had . Knowing what you know now , i was wondering if you still stand by that statement.
 
Mmmh.....Mchungaji analo jambo ngoja tusubiri nafikiri ufunuo bado unaendelea...............Mungu bariki wana JF
 
wakti wowote mheshimiwa ataikimbia nchi, kule airport wamwulize anakwenda wapi kila wakati...! ebo!

Wanyonge wengi wakiamua wana nguvu kuliko silaha za mangamizi, (wale wafuasi wa maksi, kuliko lile bomu la atomic.
 
Naomba niwashukuru wote mliochangia na mliochungulia.

Najua hii sauti ya kichungaji imekuwa si ile ya ki-Romero, bali ni ya Yohani Pauli, yenye upole na kutokueleweka.

KUna wengi wamechukulia jambo hili na bandiko langu kwa masikhara, na kuona kuwa ni utani na kiroja.

Naomba mpekue magazeti yote ya leo, angalieni thread zote za leo na hata siku zilizopita, kisha mjiulize where and when in Tanzania kulikuwa na uwezo wa "kuitikisa" serikali?

Angalieni kinachotokea Bungeni, mitaani na hata katika nafsi zetu.

Ndiyo maana nimemshukuru Mungu, pamoja na gadhabu zangu za kutokuona hatua madhubuti zikifanyika kutoka kwa Rais wetu.

Kile kilio cha maono ya wapanda farasi wanne, na ile ahadi ya vazi jeupe, vitatimilika bila sisi kujua na kw kupitia njia ambazo hatutegemei au hatuzitaki.

Tunakoelekea ndiko tunakotaka, ila njia na mbinu ni tofauti kidogo, tuvumiliane.
 
Kwani ni Mungu "alitupa" Kikwete? Kumshukuru Mungu kwa kufanya kitu ambacho labda hakukifanya haiwezi kuwa kumdhihaki? Wewe Carmalenge ambaye unatangazia dunia "Habeamus Papam" unaamini kweli Mungu angetupa Kikwete? Kwani tumemkosea nini?

Mungu alijua, kabla ya wakati, kwamba JK agekuwa Rais wetu. Alijua hivyo hata kabla baba yake JK hajazaliwa. Lakini unataka kusema ni yeye alichora dili la kuchukua fedha BoT kwa ajili ya takrima za kumfanya JK akubalike? Hapana, Mungu hakutupa JK. Tumejitwalia huyu ndugu wenyewe baada ya kunogewa na takrima.

Kilichobaki ni kumwomba Mungu aendelee kumpa JK ujasiri wa kuruhusu mafisadi wafichuliwe. Ampe hata nguvu ya kuwavaa Mkapa, Yona na Rostam Aziz. Akiwavaa hao basi hata mimi nitaanza kudhani labda ni Mungu ametupa huyu mwenzetu.

Mwalimu Augustine,

Mimi nimempa Mungu tukuzo. Nimempa shukrani, soma magazeti ya tangu mwaka huu uanze, mpaka leo, soma mijadala ya watu kama sisi JF na wengine, ni ishara wazi kuwa mapenzi ya Mungu kulipa Taifa letu neema yanatimilika, ila si kwa utashi wetu au kwa umahiri wa kiongozi wetu.

Yanayotokea ni dhahiri kuwa hata kama kwa nafsi zetu tunamuona JK hafai na ni batili, lakini ni JK huyohuyo ambaye katupa nafasi (kwa kudhamiria au hata bila kudhamiria) kuyazungumza yale ambayo yalikuwa hayazungumziki.
 
Rufiji,

Baada ya kujua haya ya sasa, nimebadilisha maoni yangu kuhusu Mkapa. Ni kweli alifanya mengi ya kujenga uchumi, lakini kama alijiuzia mwenyewe KIWIRA COAL MINE, basi hawezi kuwa Rais bora.

Kinachotumaliza ni huu mtindo wa serikali kuwekeana mikataba ya siri na wawekezaji. Hili Mkapa aliliridhi kwa waliomtangulia, lakini inaelekea alilitumia vibaya sana.

Kikwete hajakubali kusahihisha hii dosari. Katiba yetu inasema wazi kwamba Bunge linatakiwa liidhinishe mikataba mikubwa kati ya serikali na makampuni binafsi. Lakini JK na serikali yake wanazidi kudanganya kwamba ni lazima mikataba iwe ya siri.

Tukumbuke vile vile kwamba kuna habari za mtu aliyedai kuwa mtoto wa Karume alikwenda India na kutaka "kuuza" mkataba wa kununulia Mchuchuma Iron and Coal Deposits kwa fedha chache sana, mradi awekewe kiasi kwenye akaunti yake. Wezi wetu bado wanazunguka huku na huko wakijaribu kuuza nchi kwa sarafu 30.

Camerlengo,

Mimi nadhani una point. Huenda JK akawa ndiye Rais atakayetugeuza kutoka kuzama kwenye ufisadi. Niliwahi kusema huyu Bwana ni mvumilivu sana wa criticism. Mzee Mwinyi alihangaika kufungia magazeti lakini JK humsikii akifanya hivyo. Anataka tuanze kukosoana bila woga.
 
Last edited by a moderator:
Rev Kishoka,

Hapo mkuu ndipo utanishinda!...

Ukiingiza maswala ya Mungu hapa mkuu inakuwa ngumu kwangu kwani imani yangu inapinga sana maswala ya kumshukuru Mungu kwa sababu ya kina Pharaoh na Pilate kuwepo kwao ndiko kumetuongeza imani ya dini na uwezo wa mitume.

Kweli kabisa bila Ramse 11 (Pharaoh) tusingeweza kuyaona maajabu ya Mussa lakini kweli inaingia akilini kumshukuru Mungu kuwepo kwa Ramse?..mbona leo hii tunaamini zaidi dini zetu kuliko wakati ule hali hakuna kina Pharaoh na Pilate!..wala hakuna maajabu ya mitume tena ila tunaamini kwa record kubwa Uungu wake.

Je, zile hesabu ya watoto, wanawake na watumwa (walalahoi) waliokufa katika process nzima ya kuwepo kwa mtu kama huyo unaweza kusema ni rehma za Mungu?..Mnnnnh! hivi huyo shetani ana nafasi gani ktk matukio kama haya!...

Binafsi mkuu naamini kwamba Mungu alisha fanya kazi yake kamaliza na mtihani ni wetu sisi wenyewe.. kusuka ama kunyoa na yeye kazi yake ni kuutazama mtihani wetu na kutoa points za vema na makosa.

Kila tunachokifanya kinatokana na sisi wenyewe kwani katupa mtaji mkubwa wa akili...
Siamini kabisa kwamba Mungu ndiye aliyetupa Kikwete isipokuwa Mungu amejalia maombi yetu (Kura) na pia aliyejalia kina Hitler ktk mitihani ya wao kuongoka lakini shetani alikuwa na kazi yake pia.

Tumemweka sisi wenyewe, yeye (Mungu) kajalia yale tuliyokusudia na shetani huingia ktk nafsi moja moja kughiribu. Sasa kazi ni akili zako vises shetani, Mungu ni msimamiaji wa mtihani huo!
Naogopa sana wale wanaoamini tafsiri za kiswahili kuwa - Ni kazi ya Mungu!

Mbali na yote haya mkuu lazima nikubali wewe mwandishi mzuri sana!... unda team na MKJJ mtashtua!
 
Augustine Moshi ,

Nimefurahishwa sana na mtazamo wako wa sasa kuhusu Mkapa . Kusema ukweli hata vile vitu vichache alivyovifanya hizi kashfa zinazomwandama zinafuta kabisa kila kitu alichokifanya ...Huyu mtu alikuwa mlafi na ambaye aliweka maslahi yake mbele .
 
mmeanza kunifanya nifikiri kitu ambacho sikutaka kufikiri.. shetani atatetemeka. Ningekuwa mimi ni mteuliwa wa Rais wakati huu ningekuwa nakaa karibu na choo.
 
Mchungaji,
Nakumbuka mzee Ruksa aliwahi kuwaita viongozi wa kidini wakati wa utawala wake akawakumbusha aya isemayo;
Heshimu kila mamalaka
iliyoko duniani
maana hakuna mamlaka
isiyotoka kwa Mungu
amwasiye mwenye mamlaka
anapingana na Mungu

Hata hivyo naamini aya hiyo haimaanishi mamlaka inapokosea isiambiwe ukweli. Kumbuka hata Daudi alipoiba mke wa mtu,nabii kwa heshima zote alikwea kwenda Ikulu kumpa vidonge vyake.
 
Back
Top Bottom