Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
- Thread starter
- #261
Rev Kishoka,
Kuna mengi sana umeandika na kwa kuwa kwa busara zako na cheo chako umeandika ukiwa na mantiki nzuri ILA BILA SHAKA ULISAHAU NENO ZAMA. KWANI SOTE TUNAAMINI KILA MTU NA ZAMA ZaKE.
Ni msingi mkuu kwenu sasa KUCHAGUA VIONGOZI SAHIHI NA SIO VIONGOZI BORA ILI WAFANYE MAAMUZI SAHIHI kwa mustakabali wa kukuza uchumi wenu.
Shukran
Siku zote, nia ya mtoa hoja ni kuleta mahojiano na ubadilishano wa fikra na mawazo. Kama wengi tungelipokea hili kwa chachu na kwa niliyoyanukuu hapo, basi ni wazi ingekuwa ni rahisi sana kwa dhamira yangu kueleweka pamoja na hoja nyingi nilizojengwa kwa umahiri kumkosoa Kikwete.
Ukweli ni kwamba leo tunapoangalia watangaza nia, kampeni chafu ndani ya chama tawala, lundo la tuhuma na uchafu wa kila namna, kwa nini basi tusishukuru "madhaifu" ya Kikwete kutufunulia Watanzania aina ya watu wanaotaka tunu na dhamana ya kuongoza Taifa ilhali si watu wanaofaa?
Ni moaka lini au kwa ishara gani Watanzania tuendelee kuwa wanyonge na wadanganyika wa kauli tamu huku utendaji hakuna na ukweli hawa wote wanataka kutumikia na kuneemesha matumbo yao na whya wafuasi wao?