Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Katika hiki Kitab Alf Layla wa Layla, napenda kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Subhana Wataala kwa kutupa Jakaya Mirisho Kikwete kuwa Raisi wetu.
We need to thank God for so much blessings to have Kikwete as man in charge.
Yes I have been critical of his leadership, I have mocked him, I have challenged him for his in-activeness and forgot that it was blessings in disguise from our Lord God!
Mungu ni wa ajabu sana, na nafikiri ni mapenzi yake tumepewa Kikwete awe kiongozi wetu. Ni mapenzi ya Mungu leo hii tupo hapa tukipiga kelele na baragumu tukitumia vinubi, zumari na tarumbeta kufukuta hasira zetu, vilio vyetu, aibu yetu na umoja wetu.
Si kwa mapenzi yake Jakaya Kikwete, bali ni mapenzi ya Mungu, kuwa yanayotokea sasa hivi, yalipangwa mapema na Mola.
Nasi tumkubali Jakaya Mrisho Kikwete kwa mapungufu yake yote, ukimya, uzembe, uvivu, uzubaaji, kutokuchangamka, kutokuwajibika na dhana kuwa analinda wale wahujumu. Mapungufu yake, ndiyo ngao na silaha yetu tuliyopewa na Mungu dhidi ya wale wenye kutaka kutufanyia dhuluma na kutuumiza.
Kuporomoka kwa Mawaziri wakubwa na mashuhuri wanne si mapenzi yake Kikwete, maana alitoa machozi. Lakini ni mapenzi ya Mungu leo hii nchi nzima si vilio kuhusu ufisadi tuu, bali mazungumzo ya kutaka uwajibikaji, mazungumzo ya kuimarisha ufanisi, na kulitakia Taifa letu maisha mema na Baraka za Mungu ndiyo yaliyotawala.
Tunataka mshikamano, tunataka uongozi madhubuti, tunataka tufaidi matunda ya utajiri wetu wa asili, uhuru wetu na matunda ya jasho letu bila kunyonywa, kudhulumiwa, kuonewa au kudhihakiwa.
Haya yote yasingetokea kama Kikwete wetu, mtalii, Vasco Da Gama, Sinbad, Chekacheka, Kisura asingekuwa madarakani.
Najiuliza je tungekuwa na mwamko mkubwa namna hii wa kutetea haki zetu kama tungekuwa chini ya Nyerere? Labda ungekuwako, lakini tungekuwa na woga.
Najiuliza je tungekuwa na ukali namna hii wakati wa Mwinyi, yawezekana, lakini bado tungekuwa na woga.
Najiuliza tena tungekuwa na uwezo wa kuchambua mambo muhimu kwa Taifa letu, kuishupalia Serikali, kutafuta ushahidi na hata kuimbua Serikali yetu wakati wa Mkapa? tungeweza, lakini angetupuuza na angetumia ujeuri na dharau zake kutokutusikiliza.
Sidhani kama Kikwete ni msikilizaji mzuri, ila ni baraka za Mungu kuwa kujivuta vuta kwake ambao wengine wamekuita Uyakhe yakhe, Ukwerekwere na Usaigon, ndio umetusaidia sana.
Yeye mwenyewe sijui kama analijua hili, lakini tafadhali sana wewe uliye mwakilishi wa Mheshimiwa Kikwete unayepita kuchungulia JF wamesema nini, mnapoamka Ijumaa hii na kujiandaa na Gwaride la Muungano, mwambie Mheshimiwa Raisi, tunamshukuru Mungu kwa kuwa yeye ni Raisi wetu.
Mapambano yetu bado hayajaisha. Tuendelee kutumia kudra, rehema na baraka hizi za Mwenyezi Mungu, kuendeleza Libeneke la kutaka uwajibikaji, ufanisi, umahiri kupiga vita Uhujumu, Uzembe, Dhuluma, Umasikini, Ujinga na Maradhi.
Kila jamii ina njia yake ambayo Mungu kawatengenezea. Njia yetu ya Ukombozi ni wakati huu wa ndugu yetu Muungwana akiwa Raisi!
Tutumie fursa hii kupigana na wale mahasidi wasiotutakia mema, tuendeleze shinikizo letu kwa viongozi wetu wawe watii wa sheria, walinzi wa katiba, wafuata haki na wanaothamini utu.
Through Jesus Christ our Lord, Amen, Amen, Amen
Through Muhamed our Lord, Amen, Amen Amen
By the Grace of Allmighty Lord, Amen, Amen, Amen
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Tubariki watoto wa Tanzania.