Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Kweli tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa sababu kupitia utawala wa JIWE ndipo wananchi watazinduka usingizini kwamba hatima ya nchi iko mikononi mwao na bila kuchukua hatua na kuwaachia wanasiasa peke yao ni kuzidi kujizika shimoni.Ni miaka miwili na miezi kumi tangu ndugu John Joseph Pombe Magufuli aapishwe kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ni mengi ya kutafakarisha yametokea tangu Magufuli awe Rais, na kila siku wengi wetu tunajifunza mapya na kukumbuka mengi.
Nasema ni shukrani maana katufungulia na kutufunulia mengi kuhusu Tanzania na zaidi kuhusu sisi kama Taifa na wananchi wake.
Natambua sitaeleweka kama jinsi sikueleweka miaka 10 iliyopita nilipoandika "Thank God for giving us Kikwete" lakini naamini safari hii wenye juhudi na upeo wa ufahamu na uelewa watanielewa.
Tuendelee kutafakari!
Nimerejea kauli yako nikabaini ilikuwa na maana pana kuliko ufupi wa mistari yakeNi mengi ya kutafakarisha yametokea tangu Magufuli awe Rais, na kila siku wengi wetu tunajifunza mapya na kukumbuka mengi.
Nasema ni shukrani maana katufungulia na kutufunulia mengi kuhusu Tanzania na zaidi kuhusu sisi kama Taifa na wananchi wake.
!
TulichaguliwaMjifunze Kuchagua Ndugu Zangu
Mimi Niiteni Majina Yote MnayotakaTulichaguliwa
Mkuu Rev, hapa nina mtazamo tofauti. CCM ilishapevuka kinachoendelea sasa ni CCM kudumaa. Nasema hivi kwa kuangalia NEC na CC za CCM miaka ya nyuma. Hata wananchi walisubiri sana kusikia hoja zitajadiliwa vipi katika vikao hivyo kwa kuelewa kulikuwa na kukosoana kwa mantiki. Unakumbuka hoja ya Marehemu Nyalali na Nyerere kuhusu mahakama? Unakumbuka sakata la mauaji ya Pemba, JK , BWM na wajumbe wa CC?CCM haijapevuka kuwa na uhuru wa ndani na uwezo wa kukosoana hata kuwajibishana!
Mkuu Rev, hapa nina mtazamo tofauti. CCM ilishapevuka kinachoendelea sasa ni CCM kudumaa. Nasema hivi kwa kuangalia NEC na CC za CCM miaka ya nyuma. Hata wananchi walisubiri sana kusikia hoja zitajadiliwa vipi katika vikao hivyo kwa kuelewa kulikuwa na kukosoana kwa mantiki. Unakumbuka hoja ya Marehemu Nyalali na Nyerere kuhusu mahakama? Unakumbuka sakata la mauaji ya Pemba, JK , BWM na wajumbe wa CC?
Akina mzee Warioba, Malecela, Msuya n.k. wanaeleweka kwa misimamo yao mingine dhidi ya CCM
Wakati wa JK na akina Sitta hali ilikuwa tofauti na sasa. Ndiyo maana nasema imedumaa
Utamaduni huo ulifanikiwa kwa nyakati hizo.Rev. Kishoka, post: 29534178, member: 18"]Haya ni matokeo ya kusinyaa na kuzibwa pumzi kwa Demokrasia ndani ya CCM, tangu TANU na hata kuzaa kauli ya "zidumu fikra za mwenyekiti" na mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambaye miaka yote ni ama Rais au Rais mstaafu atakayempasia kigoda aliye Rais amekuwa akitukuzwa kama "omnipotent" the absolute righteous power almighty!
Madhara ya ke yanagusa demokrasia ya nchibi. Kuminywa kwa upinzani ni matokeo ya kufanikiwa ''sera' hiyo ndani ya CCMHili limezaa makundi na mitandao ambayo iko tiyari kuingia vitani na kumtetea mtu wao at any cost na ashindapo, humwekea ulinzi at any cost na ole wako yule atakayethubutu kuhoji, kukosoa au kupingana na "jemedari" wa kikosi kipya!
Huko ndiko tunakoelekea kwa kuangalia madhila yanayoukumba upinzani nchini.Alichofanya Bashiru ni kuwaambia wana CCM kuwa kundi-genge lililoko madarakani ndani ya Chama na lenye nguzu za maamuzi na utendaji limeridhia na utendaji wa aliye Rais wao na ole wao (wake) yeyote ambaye atataka kuleta ushindani wa aina yeyote (sera, itikadi, mipango) ambao ni kumpinga Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa atashughulikiwa kwa utovu wa nidhamu, ili kuulinda "utamaduni" wa kumwachia aliye Rais apete ndani ya chama (na hata nje ya chama0 bila kupingwa!
Wametengeneza ''Caucus' inayotumika kama chaka la kujificha.Msuguano ndani ya Chama (si mara ya kwanza, upo tangu enzi za TANU) umezaa mazingira ya Rais na "walinzi" wake kujiwekea mazingira ya kuwa unopposed by anyone! Bunge lenye mamlaka kikatiba na kisheria kumwajibisha Rais na Serikali limewekwa kwenye mazingira ya kuogopa kufanya kazi zao kwa uadilifu kwa hofu ya kushughulikiwa Kichama!
Hata kuwasaliti wapiga kuraNi mfumo ambao umelazimisha Mbunge wa CCM akiuke bila hiari katiba ya Chama chake na hata Katiba ya nchi ili kutimiza matakwa ya genge lenye madaraka na mamlaka, ambalo ndilo linalotawala nchi!
Hasa Taifa.Hii, ni hatari, hatari kwa uhai wa kweli ndani ya CCM na hata Taifa!
Hata pale wanapotimiza wajibu wao wa kibunge.leo mtu mwenye mawazo tofauti ndani ya CCM anatolewa kauli za kashfa, anatolewa vitisho na hatua za "kinidhamu" zinachukuliwa kumnyamazisha asiongee lolote.
Tunaliona Bungeni na hata kwenye vikao vya chama na hata mivutano ya chini chini ya chama.
Haki hiyo imezimwa ndani ya vikao, mfano ni mkutano mkuu, baadhi waliwekwa mahabusu kwasababu tu walikuwa na maoni tofautiHaki ya dhati kisheria na kikatiba ya mwanachama wa CCM kukosoa uongozi wake au kuingia ushindani wa hoja, sera na uongozi dhidi ya aliye Mwemnyekiti wa Taifa inazimwa kwa nguvu za dola na za kichama na mwenye nia hiyo, huandamwa kama msaliti!
Ni dhana ya unafiki kwa kuelewa upo upinzani wenye hoja unaoweza kutoa mabadiliko.Badala ya kuruhusu ushindani wa ndani wenye afya na kukiimarisha chama ili kiwe na uwezo wa kiitikadi na kisera kuendelea kulitumikia Taifa kwa manufaa ya Taifa, dhana ya "kuridhika" na utendaji wa Rais na Mwenyekiti wa Chama imekuwa ni yamini ya kulazimisha kwa wanacham wa CCM, watendaji wa CCM na hata Taifa. Ole wako wewe unayehoji kwa maana ni msaliti, adui na kuwadi wa wanaopinga maendeleo ya Taifa!
Hakuna jibu na anayeweza kuelewa. Wanajificha katika kauli ya 'utamaduni'Waswahili husema Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza! Kama ushawishi wa Rais ni mzuri kiasi hicho, hakuna sababu ya kuhofia yeye kupingwa na mwanachama wa ndani au hata nje ya chama ambapo Sheria kukandamiza upinzani zinaboreshwa!
why? Rev!Ndugu Nguruvi,
Leo kikao cha NSB, TRA, Rais na appointees wake kimeniacha very much confused......
Mkuu,why? Rev!
Kuna mambo yanayohitaji tafakuriNdugu Nguruvi,
Leo kikao cha NSB, TRA, Rais na appointees wake kimeniacha very much confused......
Mkuu Kichuguu, long time Mkuu. Tume miss sana michango yako kama huu(a)Katiba mbovu:
Katiba ya Tanzania leo ni viraka viraka vya katiba ya Tanganyika iliyoandikwa na Nyerere mwenyewe mwaka 1961 huku ikiwa inakaribia ile katiba ya Lancaster House iliyoandikwa mwaka 1960 kwa ajili ya uhuru wa Tanganyika chini ya serikali iliyoongozwa na Governor General akimwakilisha ya Malkia- raia wote walikuwa wanajulikana kama subjects wa malkia. Nyerere alirekebisha vipengele kadhaa kusudi iwe ni kwa Jamhuri ya Tanganyika chini ya serikali inyoongozwa na Rais aliyechaguliwa na wanachi, na ikaanza kutumika mwaka 1962; katiba hiyo ya Nyerere nayo inherently iliacha raia wawe kama subjects wa rais kwa kumpa madaraka mengi sana kuhusu maisha yao ya kila siku. Katiba hiyo hiyo ndiyo imekuwa inawekewa viraka viraka viraka kufiti serikali ya TANU, na tena baadaye serikali ya CCM na baadye vyama vingi. Vifungu vikubwa vya katiba hiyo vimebaki kuwa vile vile na hivyo kuwa vinamfanya rais awe mamlaka kama yale aliyokuwa nayo malkia wakati wa katiba ya Uhuru.
Sasa tunapopata rais ambaye anaamua kutumia madaraka yake yote kama alivyopewa na katiba tusimlaumu.