Thank God for giving us Magufuli aka Jiwe aka Chuma!

Zakumi, post: 30046023, member: 12016"]I have a full time job. Hivyo siwezi kuiga mifano yako ya ku-quote na kujibu.
No body is interested to know about your personal affairs
Kama huwezi ku quote then kuwa mkweli, usiandike maneno yako ukasema ni yangu dishonest.
Kimya si kufeli, ni kutafakari
Katika posti yangu ya mwisho nilikuwa naonyesha kuwa Nyerere alipokuwa na umri kati ya miaka 0-30, alikuwa professional student na michango yake kwa TAA ulikuwa mdogo sana na wa kutojulikana.
Nyerere alizaliwa 1922, 30 yrs later ilikuwa mwaka 1952. Nini kigumu kuelewa hapa?

Alikuwa katibu wa tawi la Tabora kwasababu alikuwa anafanya kazi, rejea kitabu cha MS
Uwepo wake Tabora hakuwa shuleni au mafunzoni, alikuwa kazini. Rejea MS

Rejea kitabu cha MS, mwaka 1953 alimbwaga Abdul katika mkutano mkuu wa chama pale Arnatouglo
Huyu ni ''professional student'' kwa mujibu wako aliyeweza kuangusha Nguli wa siasa! real, then alikuwa genius.

Akiwa na miaka 39 alipewa nchi! kama Rais wa kwanza wa Tanganyika huru!
 
No body is interested to know about your personal affairs
Kama huwezi ku quote then kuwa mkweli, usiandike maneno yako ukasema ni yangu dishonest.
Kimya si kufeli, ni kutafakari
Nyerere alizaliwa 1922, 30 yrs later ilikuwa mwaka 1952. Nini kigumu kuelewa hapa?

Alikuwa katibu wa tawi la Tabora kwasababu alikuwa anafanya kazi, rejea kitabu cha MS
Uwepo wake Tabora hakuwa shuleni au mafunzoni, alikuwa kazini. Rejea MS

Rejea kitabu cha MS, mwaka 1953 alimbwaga Abdul katika mkutano mkuu wa chama pale Arnatouglo
Huyu ni ''professional student'' kwa mujibu wako aliyeweza kuangusha Nguli wa siasa! real, then alikuwa genius.

Akiwa na miaka 39 alipewa nchi! kama Rais wa kwanza wa Tanganyika huru!

What I was telling you is I am not here to waste my time. I have other important things to do in life and I can't sit here and quote every paragraph you write.

Now with regard to the topic at hands, karibu vyama vyote vya wapigania uhuru barani Africa viliwapokea watu waliorudi nyumbani na kuwapa nafasi za kuongoza. Hiyo ilitokea kwa Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Kamuzu Banda etc etc. Hivyo kulikuwa hakuna U-genius wowote.

Pili ndani ya TAA kulikuwa makundi ya vijana na wazee. Vijana walitaka msukumo kutoka kwa vijana waliokuwa wanarudi kutoka masomoni.

Tatu kama yeye alikuwa Nguli na Genius kwanini alitaka kuacha na kurudi kufundisha pale alipoambiwa achague kazi au siasa?

Nne, uchaguzi ulifanyika kidemokrasia. Na walioshindwa walikubali kushindwa na waliendelea kumsaidia. Kwanini hiyo demokrasia haikuendelea wakati anatawala?

Tano, Tanganyika ilikuwa Jamuhuri mwaka 1962. Hivyo alikuwa rais wa kwanza 1962 akiwa na miaka 40 na sio 39 kama ulivyoandika. Kasome tena historia na ujue urais ulianza lini.

Sita, Tanganyika ilikuwa sio koloni kamili la mwingereza. Hivyo tulichotakiwa ni kuonyesha kuwa tuna watu wanaoweza kuongoza nchi na ku-negotiate tarehe ya uhuru. Hivyo hakuna u-genius wowote wa uhuru wa Tanganyika na ndio maana watu walikuwa wanabadilisha katiba wanavyotaka.
 
DOLA YA WACHAGGA MIAKA MICHACHE KABLA YA UHURU.
By Malisa GJ,
Wakati wazungu wanagawana bara la Afrika, walipokuja walikuta baadhi ya maeneo kuna tawala zenye nguvu, zilizokua na mfumo rasmi wa uongozi. Wao waliziita tawala za jadi (Chiefdoms).
Moja ya tawala iliyokua na nguvu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ni dola ya wachagga (Chagga state). Zilikuwepo nyingine zenye nguvu kama Himaya ya Sultani wa Zanzibar, Dola ya Buganda, Nyamwezi, Ngoni, Haya, Hutu, Tutsi, Hehe, etc.
Dola ya wachagga imetamalaki eneo la pembezoni mwa mlima Kilimanjaro kuanzia maeneo ya Rongai hadi Siha.
Eneo hili lilikua na mtawala mkuu mmoja (aliyeitwa Mangi Mkuu). Huyu alikua kama Rais ama Mfalme wa jamii hiyo. Chini yake walikuwepo watawala wakuu wawakilishi wa majimbo. Hawa waliitwa 'Mangi Waitori'. Chini yao walikuwepo watawala wa wa maeneo madogo, hawa waliitwa Mangi kama vile Mangi Meli wa Old Moshi, Mangi Sina wa Kibosho, Mangi Salakana wa Useri etc.
Kwa mfano eneo kama Rombo lilikuwa na Mangi wengi. Alikuwepo Mangi wa Keni, Mangi wa Mashati, Mangi wa Mengwe etc. Lakini wote waliunganishwa na Mangi Mwitori wa Rombo. Vivyo hivyo katika maeneo ya Kibosho, Machame, Siha, Old Moshi, Marangu etc.
Mangi mdogo aliripoti kwa Mangi Mwitori. Mangi Mwitori naye aliripoti kwa Mangi Mkuu aliyeunganisha wachagga wote.
Kwa mfano kufikia mwaka 1953 Mangi Mwitori wa Vunjo alikua Petro Itosi Marealle, Mangi Mwitori wa Hai alikua Abdiel Shangali, Mangi Mwitori wa Rombo alikua James Selengia Kinabo kabla ya kustaafu mwaka 1952 na John Maruma kuchukua nafasi yake.
Mangi Mwitori alichaguliwa na wamangi wadogo. Kisha wamangi wadogo na wamangi waitori waliunda baraza kuu la uongozi (Supreme council) ambalo lilimchagua Mangi Mkuu.
January 1952 kulifanyika uchaguzi wa kumchagua Mangi Mkuu wa Wachagga. Wagombea walikua watano. Abdieli Shangali wa Machame, Jackson Kitali wa Mbokomu (Old Moshi), Petro Marealle wa Vunjo, John Maruma wa Rombo, na Thomas Marealle wa Marangu.
Baada ya kila mgombea kunadi sera zake, hatimaye kura zilipigwa na Mangi Thomas Marealle kutangazwa mshindi, akifuatiwa kwa mbali na ndugu yake Mangi Petro Itosi Marealle, aliyekuwa Mangi Mwitori wa Vunjo.
Mangi Mkuu ndiye aliyekuwa Kiongozi mkuu wa dola ya wachagga. Baraza la uongozi (Supreme council) ndicho kilikua chombo cha juu kinachosimamia utendaji wa serikali.
Kwahiyo Mangi mkuu alijitahidi sana kushirikiana mangi waitori na mangi wadogo kuhakikisha jamii nzima ya wachagga inajiletea maendeleo.
Kila Mangi alikua na baraza lake la ushauri lililojulikana kama 'baraza la wachili', ambalo lilifanya kazi kama baraza la mawaziri kwa sasa.
Ushirikiano huu ulifanya dola ya Wachagga kupiga hatua kubwa kimaendeleo kuliko jamii nyingi za wakati huo.
Kwa mfano kufikia mwaka 1920 dola ya wachagga ilikua ya kwanza kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kuanzisha na kumiliki gazeti lake (Komkya). Miaka 10 baadae dola ya Buganda (Buganda Kingdom) nayo ilianzisha gazeti lake (Buruuli) na mwaka 1940 Himaya ya Sultani wa Zanzibar (Zanzibar Sultanate) nayo ikaanzisha jarida lake (Imperial).
Si hivyo tu, huduma za maji, umeme, miundombinu ya barabara, hospitali na shule vilifika mapema kulinganisha na maeneo mengine ya nchi. Ikulu ya kisasa ya Mangi Mkuu wa wachagga, iliyojengwa karibu miaka 100 iliyopita ndiyo inayotumika hadi sasa kama Ikulu ndogo ya Rais kwa mkoa wa Kilimanjaro.
Zilizokuwa ofisi za watendaji wa serikali ya Mangi mkuu (eneo la KDC Moshi) ndio ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Moshi kwa sasa.
Maendeleo haya na mengine mengi, wachagga waliamini yalitokana na elimu. Kwahiyo mwamko wa elimu ulikua mkubwa hasa baada ya wamisionari kujenga shule na huduma za afya kila walipojenga kanisa. Vitu hivi vitatu viliambatana. Kanisa, Shule, na Kituo cha afya.
Kwahiyo hata kwenye kuchagua viongozi, yule aliyekuwa na elimu nzuri ndiye aliyepewa nafasi kubwa ya kushinda ikiaminika kwamba elimu yake itachochea kasi ya maendeleo. Na hii ni moja ya sababu iliyomfanya Thomas Marealle kushinda kiti cha umangi mkuu mwaka 1952, kwani kati ya wagombea wote yeye ndiye aliyekua na shahada ya uzamili (masters degree) kwa wakati huo.
Kabla ya uhuru kulikua wachumi wawili tu wazawa ambao ni Thomas Marealle na mzee Fredrick Mchauru ambaye walisoma pamoja London School of Economics, kabla ya Marealle kupata ufadhili Cambridge University (Trinity College).
Iliaminika pia kwamba Uingereza ilitaka dola ya wachagga ijitenge kutoka Tanganyika na itafute uhuru wake yenyewe, kama Rwanda na Burundi zilivyojitenga kutoka Tanganyika baada ya vita vya kwanza vya dunia, wakati huo zikiitwa Ruanda-Urundi.
Hata hivyo mpango huo ulishindikana kwa kuwa Tanganyika ilikua 'Trusteeship colony' ya Umoja wa mataifa, na Uingereza alikabidhiwa tu aisimamie hadi iweze kujitawala. Kwahiyo hoja ya Muingereza ilitupwa kwa maelezo kwamba wakati wa kugawanya bara la Afrika pale Berlin mwaka 1884/85 hakuna nchi inayoitwa 'Chagga state' iliyogawanywa. Hivyo uhuru unaopaswa kuwa wa Tanganyika kwa ujumla na sio wa jamii moja moja.
Baada ya jaribio hilo kushindwa, inadaiwa shirika la ujasusi la Uingereza (M16) lilimpendekeza Mangi Thomas Mareale kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika baada ya uhuru.
Katika moja ya barua za Richard Turnbull (Gavana wa mwisho wa Uingereza) kwenda kwa shirika la ujasusi la nchi hiyo (M16) ilieleza mapendekezo hayo kwa Thomas Mareale.
Sehemu ya nyaraka hiyo iliyoandikwa mwaka 1958 ilisema 'I consider Thomas Marreale an outstanding Chagga leader. I dont know him personally but he would be the leader of Tanganyika if British had to leave. However he lack support from other tribes'
Turnbull alikua akiwaelezea M16 kuhusu Mangi Thomas Marealle na umahiri wake katika uongozi. Hata hivyo alionesha hofu kuwa Marealle hakuwa na ushawishi mkubwa kwa makabila mengine nje ya wachagga.
Na hii ni moja ya hofu kubwa aliyokua nayo Mwalimu Nyerere wakati wa kudai uhuru. Alipofika uchaggani alikuta dola ya wachagga ina mamlaka kamili. Ilikua na 'well defined leadership structure', bendera yake, wimbo wake, na askari wake.
Nyerere alisema ili Tanganyika iwe uhuru lazima dola ya wachagga ife kwanza, kwa sababu hatuwezi kuwa na taifa moja ndani ya taifa jingine. Mwaka 1961 Nyerere aliagiza bendera ya Tanganyika isipandishwe kabla bendera ya wachagga haijashushwa kwanza. Tarehe 8 December 1961 saa 5 usiku bendera ya wachagga ilishushwa katika Ikulu ndogo ya Moshi, na muda mfupi baadae (saa 6 usiku, December 9) bendera ya Tanganyika ikapandishwa.
Hata hivyo hofu ya Nyerere haikua na mashiko kwa sababu Mareale mwenyewe alimpa ushirikiano mkubwa wakati wa kudai Uhuru. Na ili kuonesha kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumhujumu, aliamua kujiuzulu nafasi yake ya umangi mkuu mwaka 1960, na kuruhusu askari wake kujiunga na jeshi la Tanganyika.
Pichani ni wagombea watatu kati ya watano walioshiriki uchaguzi wa Mangi Mkuu mwaka 1952. Kutoka kushoto ni Mangi Thomas Mareale aliyeshinda uchaguzi huo), Mangi John Maruma (Mangi Mwitori wa Rombo), na Abdieli Shangali (Mangi Mwitori wa Machame).
Malisa GJ
01/01/2019
Moshi.!

2
 
Zakumi, post: 30050889, member: 12016"]What I was telling you is I am not here to waste my time. I have other important things to do in life and I can't sit here and quote every paragraph you write.
Hatuna interest ya kujua ratiba zako za maisha au uko busy au lazy kiasi gani .

If you can't respond appropriately because you're busy then don't spend your time writing the page and paragraphs on fabrications, dishonest!
Vyama vyote vya wapigania uhuru barani Africa viliwapokea watu waliorudi nyumbani na kuwapa nafasi za kuongoza. Hiyo ilitokea kwa Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Kamuzu Banda etc etc. Hivyo kulikuwa hakuna U-genius wowote.
Ndiyo maana nakushauri ujaribu kusoma na si kusoma tu bali kuelewa zikiwemo alama za maandishi, na semantic.

Sijasema Nyerere ni genius, nilichosema ni kuwa kwa kauli yako kuwa at 30 yrs alikuwa ''professional student'' licha ya kuwa mwalimu, na aliweza kwenda from no where kumbwaga nguli Abdul, then he should be a genius!
Pili ndani ya TAA kulikuwa makundi ya vijana na wazee. Vijana walitaka msukumo kutoka kwa vijana waliokuwa wanarudi kutoka masomoni.
Kwanini Abdul aliondoka na kuanzisha AMNUT! Je, alikubali uwepo wa vijana na mabadiliko unayosema?
Tatu kama yeye alikuwa Nguli na Genius kwanini alitaka kuacha na kurudi kufundisha pale alipoambiwa achague kazi au siasa?
Sijasema alikuwa nguli, sijasema alikuwa genius, nimeonyesha kuwa kwa hoja yako kuwa alikuwa 'professional student' na kwenda kuwabwaga nguli na wazee, then atakuwa ni genius! alama ! ina maana
Nne, uchaguzi ulifanyika kidemokrasia. Na walioshindwa walikubali kushindwa na waliendelea kumsaidia. Kwanini hiyo demokrasia haikuendelea wakati anatawala?
Well, kabla ya utawala wake Abdul Sykes (Ref; MS) alikwenda AMNUT! Je, alikubali demokrasi!
Tano, Tanganyika ilikuwa Jamuhuri mwaka 1962. Hivyo alikuwa rais wa kwanza 1962 akiwa na miaka 40 na sio 39 kama ulivyoandika. Kasome tena historia na ujue urais ulianza lini.
Dec 9 1961? Iwe ilikuwa na madaraka ya ndani au Jamhuri, hoja inabaki pale pale Nyerere alianza kuongoza 1961 akiwa na 39 yrs kama PM. Si mwingine yoyote yule

Hii ni miaka 9 baada ya kile unachosema 'professional student'. Hili linaeleza uwezo wake kwani akiwa ''professional student'' kwa mujibu wako aliibuka miaka 9 na kuchukua uongozi wa nchi akiwa Waziri mkuu
Sita, Tanganyika ilikuwa sio koloni kamili la mwingereza. Hivyo tulichotakiwa ni kuonyesha kuwa tuna watu wanaoweza kuongoza nchi na ku-negotiate tarehe ya uhuru. Hivyo hakuna u-genius wowote wa uhuru wa Tanganyika na ndio maana watu walikuwa wanabadilisha katiba wanavyotaka.
Again sijawahi kusema alikuwa genius, umechukua neno ''genius'' bila kuelewa 'semantic'

Tufanye assumption kuwa kilichotakiwa ni kuonyesha tuna watu wanaoweza kuongoza.
Well, aliyeonyeshwa anaweza ni Nyerere!

Uwezo wake ulijidhihiri kuanzia alipoandika katiba ya chama cha siasa

Uwezo wake ulijidhihiri alipoongoza Watanganyika na kukabidhiwa nchi.

Hoja yako inaeleza uwezo wake zaidi ya kuonyesha udhaifu
 
Mkuu Rev
Kuna mambo mengi tunayojifunza sasa, huko nyuma hatukuyaona kwa umuhimu wake
Nimeshngaa kusikia kuna watu wanajipanga kwa nafasi za Urais 2020 kutoka vyama vya siasa

Ninaendelea kujiuliza, hivi kuna kitu nisichokijua au nisicho kiona kwa hali ya siasa iliyopo?
Kwa kutumia katiba hii iliyopo nani anaweza kufikiri tofauti kuhusu ukweli wa CCM kuendelea kutawala!

Katiba iliyopo ilisukwa kiasi cha kutoa uhalali popote pale hata pasipostahili tena kisheria kabisa
Mzozo uliopo kati ya Msajili wa vyama na Wapinzani unaeleza ugumu unaowakabili wapinzani

Msajili ni mlezi wa vyama, hivi anashindwaje kukaa nao kutafuta suluhu kama 'mlezi' na waelelewa?
Nimemsikiliza katibu mkuu wa CCM akisema 'mswada' haupaswi kuondolewa hata koma katika maandishi

Ukitazama kwa upana, kuna 'ushirikiano' wa utatu kati ya Msajili, serikali na CCM
Utatu huu unaanzia pale Msajili anapoteuliwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM bila kuwajibika popote

Utatu huo unaonekana katika tume ya uchaguzi ya Taifa kuanzia makao makuu hadi majimboni

Utatu huu ni halali kabisa kisheria, swali ni je, kama unatumika ilivyokusudiwa au unatumika kinyume

Katika mazingira hayo nani anaweza kudhani sanduku la kura linaweza kumpa matokeo tofauti na tunayoyajua
 
ok, ok, Time out Zakumi na Nguruvi3.. turudi kwenye hoja halisi... ;)

Time out taken !!!. Nimemaliza kumsikiliza Prof. Mussa Assad, mkuu wa CAG. Naona ameitwa na bunge kujieleza kwa kauli zake alizotoa.

Naona watanzania wasipoangalia na kuwa makini, nchi itaenda pabaya. Ni kweli Magufuli anataka asukume vitu fulani vya maendeleo kwa manufaa ya wananchi. Lakini juhudi hizi zisilete blind spots ambazo watu wakazitumia kukiuka taaribu za kazi zao, kunyima haki ya watu kujieleza katika taaluma zao, au kunyima haki ya kukosoa.

Kwa mfano ofisi ya CAG ina kazi ya kutoa maoni kuhusu matumizi ya pesa baada ya ukaguzi. Maoni hayo yanaweza kusema pesa zimetumiwa vibaya. Maoni hayo yanaweza kusemwa kuwa taratibu za kihasibu hazikufuatwa. Na maoni yanaweza kusifia kama taratibu zote zimefuatwa. Kwa ujumla nia ya CAG ni kuboresha na kudumisha taratibu za matumizi ya serikali.

Kwa maoni yangu binafsi. Naona watendaji wengi katika awamu ya tano wamekazania sana juhudi kuongeza ufanisi. Ni kweli ufanisi katika vyombo vya umma ulikuwa mbovu. Lakini Ufanisi wa kazi na huduma za serikali hauji kwa kuongeza juhudi tu. Juhudi nayo ina kikomo chake. Juhudi ni sawa na nguvu za kulima. Kama una nguvu za kulima, unaweza kulima shamba kubwa. Lakini shamba kubwa bila mbolea, linaweza litoe kitu
 
Mkuu Rev
Kuna mambo mengi tunayojifunza sasa, huko nyuma hatukuyaona kwa umuhimu wake
Nimeshngaa kusikia kuna watu wanajipanga kwa nafasi za Urais 2020 kutoka vyama vya siasa

Ninaendelea kujiuliza, hivi kuna kitu nisichokijua au nisicho kiona kwa hali ya siasa iliyopo?
Kwa kutumia katiba hii iliyopo nani anaweza kufikiri tofauti kuhusu ukweli wa CCM kuendelea kutawala!

Katiba iliyopo ilisukwa kiasi cha kutoa uhalali popote pale hata pasipostahili tena kisheria kabisa
Mzozo uliopo kati ya Msajili wa vyama na Wapinzani unaeleza ugumu unaowakabili wapinzani

Msajili ni mlezi wa vyama, hivi anashindwaje kukaa nao kutafuta suluhu kama 'mlezi' na waelelewa?
Nimemsikiliza katibu mkuu wa CCM akisema 'mswada' haupaswi kuondolewa hata koma katika maandishi

Ukitazama kwa upana, kuna 'ushirikiano' wa utatu kati ya Msajili, serikali na CCM
Utatu huu unaanzia pale Msajili anapoteuliwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM bila kuwajibika popote

Utatu huo unaonekana katika tume ya uchaguzi ya Taifa kuanzia makao makuu hadi majimboni

Utatu huu ni halali kabisa kisheria, swali ni je, kama unatumika ilivyokusudiwa au unatumika kinyume

Katika mazingira hayo nani anaweza kudhani sanduku la kura linaweza kumpa matokeo tofauti na tunayoyajua

Nguruvi3,

Kinachotokea sasa ni kulazimisha uwepo wa "himaya" mpya ambayo itakuwa na Uhru wa kupindukia na kuamua nani awe nani na nani aseme nini. Zakumi akinijibu kuhusu CAG kalionyesha kwa ufupi bila kuingia kwa undani sana.

Leo hii, tunadekeza mfumo wa Executive branch kujiamulia itakalo bila checks and balances au sort of accountability mpaka Rais kudiriki kusema kama Awamu yake haitapewa fursa ya kutatua matatizo, meaning kama hana free will and free hand ya kufanya analoona yeye kama ndio sahihi kwa madendelo ya Tanzania au kutatua matatizo ya Tanzania, hivyo Tanzania will never be able to be successful na hata akasema atakayemfuata hataweza.

So you have mihimili ya Checks and balances ikiwa under tight grip ya Rais ambaye anachongea kila anayempinga au kumkosoa kuwa ni adui wa maendeleo na anaichelewesha Tanzania Mpya. Bunge, Mahakama,TRA, TCRA, Msajili wa Vyama, Vyombo vya Dola, Tume ya Uchaguzi na sasa CAG, vyote vinabanwa ili kumpa absolute powers Rais afanye anavyopenda.

Sheria zinatungwa kandamizi ili kurasimisha kufutwa kwa uhuru wa maoni na kukuosoa. Leo ukikosoa unavuliwa Uzalendo, unashitakiwa Jinai na haki zako zinafutwa. Zaidi uko hatarini kupoteza kilicho halali yako kutokana na uamuzi na mamlaka ya kusema mwenye Rungu anaweza kufanya lolote kwa kuwa yeye ndio "Custodian" wa nchi.

Leo unaweza kufilisiwa, kunyang'anywa mali, kufukuzwa kazi, kufukuzwa nchi, kufungwa hata uhai wako ukapotezwa -haki yako kunyang'anywa hata kura yako ikafutiwa maana yake ili kumfurahisha "mfalme"!

Tujiulize ni Taifa gani tunajenga? je tulipotaka kuongozwa na Dikteta, tuliangalia kwa makini? tulitamani kwa umakini wa kuelewa Dikteta na Udikteta na matokeo yake?

Leo, kila senti inakusanywa kwa mabavu, kukiuka kanuni na sheria (Wavuvi kigamboni wananyang'anywa leseni, kisa wamechelewa renewal za mwaka mpya ambazo ni due March 31st 2019), senti inatumika bila kufuata kanuni na sheria na mahesabu yanasunikwa yasipitie mkondo wa uhakiki kwa kisa cha kusema tunaletewa Maendeleo.

Bunge linaona ni sawa, Mahakama inaamua kujificha.. je mwishowe ni nini? Fukuto hili la uji likipasuka nje ya chungu... uji ukammwagika... balaa lake sijui tutajificha wapi...yote kisa tunataka maendeleo tufanane na ulaya!
 
So you have mihimili ya Checks and balances ikiwa under tight grip ya Rais ambaye anachongea kila anayempinga au kumkosoa kuwa ni adui wa maendeleo na anaichelewesha Tanzania Mpya.

Bunge, Mahakama,TRA, TCRA, Msajili wa Vyama, Vyombo vya Dola, Tume ya Uchaguzi na sasa CAG, vyote vinabanwa ili kumpa absolute powers Rais afanye anavyopenda.

Sheria zinatungwa kandamizi ili kurasimisha kufutwa kwa uhuru wa maoni na kukuosoa.
Leo ukikosoa unavuliwa Uzalendo, unashitakiwa Jinai na haki zako zinafutwa.

Zaidi uko hatarini kupoteza kilicho halali yako kutokana na uamuzi na mamlaka ya kusema mwenye Rungu anaweza kufanya lolote kwa kuwa yeye ndio "Custodian" wa nchi.

Leo unaweza kufilisiwa, kunyang'anywa mali, kufukuzwa kazi, kufukuzwa nchi, kufungwa hata uhai wako ukapotezwa -haki yako kunyang'anywa hata kura yako ikafutiwa maana yake ili kumfurahisha "mfalme"!

Tujiulize ni Taifa gani tunajenga?
Mkuu haya maneno ni mazito sana.

Ninajiuliza kwanini sheria zinatungwa kwa kulenga watu au makundi na si jamii kwa ujumla wake?

Tuliambiwa gharama za 'Bunge live' ni kubwa.
Leo kila siku tunaona matukio hatujui nani analipia gharama hizo ikiwa tuliamua kupunguza!

Sheria ya mtandao ikasemwa imelenga watuamiaji hasa wa picha za ngono. Well, tunajua ililenga mitandao ili wakubwa wasisikie wananchi wao wanaeleza nini. Kila mmoja aimbe 'nyimbo' zinazoletwa

Ikaja sheria ya takwimu. Hii ilimlenga yule Mbunge ili akizungumzwa awe na takwimu zao si takwimu halisi

Tukiambia Tanzania haina malaria 99% inabidi tukubali, utapinga kwa takwimu zipi ikiwa umeambiwa utumie zile ''zinazotakiwa''

Imekuja hii sheria ya Msajili. Sheria ya vyama vingi imekuwepo tangu vyama hivyo vianzishwe

Msajili si mmiliki wa vyama, ni mlezi tena pale inapobidi. Vinginevyo ni mwangalizi tu wa mambo

Sheria inayokusudiwa imelenga kumpa nguvu ya kuamua nani awe mwanachama nani asiwe

Msajili atakuwa na uwezo wa kusema Maalim asiwe kiongozi wa CUF na ikawa tena kisheria

Msajili anaweza kusema futa Chadema, na ikafutwa tena kiuhalali kabisa, si sheria ipo?

Msajili anaweza kumfuta uongozi mtu fulani kwasababu zake tu kwasababu haruhusiwi kuhojiwa

Sheria imewalenga watu wawili watatu 'wanaoleta' ukorofi na si jamii ya wanademokrasia

Ukitaka kuona ubutu wa sheria hiyo , kwanza angalia kinga aliyopewa Msajili.

Kwamba, anaweza kufanya lolote bila kushtakiwa. Hii ni 'replica' ya sheria ya Tume ya uchaguzi

Sheria hizo zinapitishwa tu na Wabunge wa CCM bila kuangalia madhara yake

Pengine wangemuuliza yule Mbunge aliyeshinikiza kufutwa kwa Bunge live kisha kusotwa bastola
Pengine wangewauliza wale mawaziri wakuu wawili ambao leo hawawezi kuitisha mkutano

Labda wangejiuliza kidogo, hivi Msajili akiamua 'kumfuta' uanachama mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais hali itakuwaje kikatiba? Hili linaonekana haliwezekani kwasababu moja, sheria inatungwa kwa kuelewa uwezekano wa hilo kutokea haupo. Kama hakuna uwezekano, sheria imemlenga nani?

Wabunge wanasahau kuwa sheria ikimaliza kuwahukumu wanaokusudiwa haitafutwa.
Ipo siku itawarudi wao au vizazi vyao maana ipo vitabuni

Kwanini tusielekeze nguvu zetu kwa mambo ya maana ya kusadia jamii badala yake tunajishughulisha na 'petty politics' zisizotatua kero za mahindi, machungwa, barabara au kuondoa maradhi!
 
Tukumbuke, Tanzania sheria na katiba zake zinasema mgombea wa nafasi yeyote: Udiwani, Ubunge na Urais lazima atokane na Chama. Msajili ndio mwenye kuidhinisha mtu kuwa mwanachama wa chama....!
 
Tukumbuke, Tanzania sheria na katiba zake zinasema mgombea wa nafasi yeyote: Udiwani, Ubunge na Urais lazima atokane na Chama. Msajili ndio mwenye kuidhinisha mtu kuwa mwanachama wa chama....!
Hatari iliyopo ni kuzua migogoro ndani ya vyama
Hali hiyo itamwalika Msajili ambaye kwa nia yoyote atakayokuwa nayo , uamuzi wake ni wa mwisho

Mfano, mgogoro wa CUF ambao sehemu kubwa unaonekana kuelemea upande fulani utaamuliwaje?
Ikiwa sasa hivi kuna upande ''unaopigiwa debe'' haki ya upande mwingine itapatikana wapi?
Msajili atakuwa na uwezo wa kuamua nani awe mwenyekiti wa CUF

Na kwa mamlaka atakayokuwa nayo, ataweza kuzuia baadhi ya wananchama kujiunga na vyama vingine
Hili litafanyika kwa sheria hiyo hiyo inaymtaka mtu kuhamia chama kingine kwa muda maalumu
Sheria hiyo ndiyo itakayotumika kuzuia umoja wa vyama vya siasa kisheria kabisa

Nguvu atakazokuwa nazo Msajili wa vyama 'zitategemea ' busara na hekma zake kwa mtazamo wake
Ni nguvu hizo ndizo zinazotumiwa na Tume ya uchaguzi ambayo hata kukiwa na ushahidi wa tatizo halitashughulikiwa. Tumeona Wakurugenzi wakifunga ofisi ili kutopokea fomu bila Tume kusema lolote

Hakuna sheria inayomzuia Rais na M/Kiti wa CCM kuteua Wakurugenzi kwa maana hakuna mwongozo.

Haki na mamlaka yanapatikana kikatiba na hivyo anaweza kupanga makada wa CCM kila jimbo ambao pia ni wawakilishi wa Tume ya uchaguzi! Hapa uhuru wa tume na uchaguzi huru unapatikana kwa njia ipi?

Sasa ukichukua nguvu anazotaraji kupewa msajili,ukachanganya na nguvu ilizo nazo tume ya uchaguzi, ukatoa nguvu ''iliyoporwa ya mahakama'' unabaki na jibu moja tu, '' ushindi ni lazima' tena kwa kutumia sheria

Sheria zitatumika vizuri kuhalalisha matokeo ya uchaguzi, lakini, sheria hiyo hiyo imewekewa uzio kwamba haiwezi kutafsiriwa na mahakama kwasababu vyombo hivyo viwili vitakuwa na haki ya kutohojiwa mahakamani

Kitakachotokea ni kuwa na 'wadai haki' na 'watoa haki, wakiwekewa uzio mzito wa 'Msajili na tume'
Haiwezekani kudai haki iliyozuiliwa kufika mahakamani, na hapo kutazaa kitu kinaitwa 'desperation'

Desperation(kukata tamaa) siyo demoralization (kuvunjika moyo).

Desperation hulazimisha mhusika kutafuta namna ya kujinasua. Ni pale mhusika anapoamua kumpiga simba ngumi ili kujiokoa. Si kwamba amekata tamaa, la hasha, ni kwamba hatua yoyote kwake ni halali na ukombozi

Ndicho imekuwa chanzo cha matatizo sehemu nyingi duniani
 
NI lazima tufike mahali tuache kutengeneza sheria kukidhi matakwa na utashi wa mtu mmoja ambaye ni Rais na hata kuweka mazingira ya kuhalalisha ubinafsi huo na ujanja wa kumwekea kinga!
 
Back
Top Bottom