Thank God for giving us Magufuli aka Jiwe aka Chuma!

Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,076
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,076 2,000
"Zakumi, post: 30002653, member: 12016"]Actually kuna nchi za kiafrika ambazo hazikuanza kama Tanzania zimeanza kupata identities za utaifa ambazo Tanzania ilimekuwa nazo toka mkoloni.
Kwa mfano nchi nyingi zilizokuwa chini ya Mwingereza, tayari zina local english ambayo ni ya kwao pekee yao. Hata zile zinazozungumza kifaransa zina kifaransa chao. Hile advantage tuliyokuwa nayo miaka ya 60. 70 na 80 sio big deal tena.
Mkuu, ''nchi nyingi' ni general term. Tueleze zipi kwa mifano halisi

Pili, nchi hizo zikitafuta identity kupitia London au Paris sisi tulikuwa nayo. Hivyo advantage yetu ya miaka ya 60, 70,80 nayosema si big deal huenda ni kweli, lakini haiondoi ukweli kuwa ni kazi ya Nyerere

Nimejaribu sana kukufahamisha kuwa Nyerere ana mazuri na mabaya yake kutokana na mtazamo wa mtu
Huwezi kufuta credit zake kirahisi, hata maadui zake wanajua hilio.

Nyerere alikuwa mwanadamu na hatutetegemei utimilifu 100%. Tusichoweza kufuta ni ukweli kuhusu yeye. Kwamba, ndiye aliyepokea Uhuru kutoka kwa Mwingereza. Wapo wasiokubali lakini huo ni ukweli hata kama si big deal tena kwavile nchi nyingi zimejitawala. Kwamba, allifanya tuwe tulivyo , ni ukweli hata kama mtu hataki

Pamoja na matatizo yao, Nigeria is largest economy in Africa. Kenya is the largest economy in our region. Cameroon vilevile wako mbali. Nchi hizo ulizotaja wametuzidi per capital. Wametuzidi ya namba ya dispora inayosaidia nchi zao. Na wametuzidi katika matrix zingine unazozijua.
Nigeria kwa population, muda wa uhuru na historia ya Afrika ilipaswa kuwa ndiyo Taifa kama South Afrika. Ina utajiri wa mafuta wa muda mrefu
Kuilinganisha na Tz kunaeleza jinsi taifa hilo lilivyo sasa hivi.
Matatizo ya ukabila , udini n.k. ni makubwa kuliko Tanzania sijui kama hilo umeliangalia

Kenya na Cameroon wana matatizo yale yale ya Ukabila na udini.
Sijui kama uchifu umeweza kusaidia lolote katika maendeleo ya mataifa hayo

Pengine tofauti kidogo ni kuwa mimi nimeishi na Kenyata na Nyerere na waliofuata. Hii EA ikifa sisimuliwi

Tanzania imepiga hatua kubwa sana kiuchumi, kijamii kwa miaka 25 iliyopita kulinganisha na Kenya wakati huo
Unazungumzia diaspora! mbiona huzungumzii kandambili za matairi, wengine tumeishi

Kuhusu diaspora, wingi wao unatokana na siasa zao za mwanzo na si uchifu. Kenya ilikuwa na open market miaka nenda rudi. Sisi tulikuwa na ujamaa uliotufunga. Guess what speed yetu sasa hivi inatupeleka at par
Tanzania haina diversity kubwa kuliko Marekani. Makabila mengi yanazungumza the same f@cking languages. Wasukuma na wanyamwezi ni watu walewale. Mpare, mzigua, msambaa wanazungumza lugha moja. Mpogoro na mdengeleko wanasikilizana. Wakinga na wahehe ni watu walewale.
Diversity si makabila!!! hiyo inaitwa misnomer .
Tunapoongelea diversity tuna definition tofauti.Makabila ni sehemu tu lakini si diversity.
 
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,849
Points
1,500
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,849 1,500
Mkuu, ''nchi nyingi' ni general term. Tueleze zipi kwa mifano halisi

Pili, nchi hizo zikitafuta identity kupitia London au Paris sisi tulikuwa nayo. Hivyo advantage yetu ya miaka ya 60, 70,80 nayosema si big deal huenda ni kweli, lakini haiondoi ukweli kuwa ni kazi ya Nyerere

Nimejaribu sana kukufahamisha kuwa Nyerere ana mazuri na mabaya yake kutokana na mtazamo wa mtu
Huwezi kufuta credit zake kirahisi, hata maadui zake wanajua hilio.

Nyerere alikuwa mwanadamu na hatutetegemei utimilifu 100%. Tusichoweza kufuta ni ukweli kuhusu yeye. Kwamba, ndiye aliyepokea Uhuru kutoka kwa Mwingereza. Wapo wasiokubali lakini huo ni ukweli hata kama si big deal tena kwavile nchi nyingi zimejitawala. Kwamba, allifanya tuwe tulivyo , ni ukweli hata kama mtu hataki

Nigeria kwa population, muda wa uhuru na historia ya Afrika ilipaswa kuwa ndiyo Taifa kama South Afrika. Ina utajiri wa mafuta wa muda mrefu
Kuilinganisha na Tz kunaeleza jinsi taifa hilo lilivyo sasa hivi.
Matatizo ya ukabila , udini n.k. ni makubwa kuliko Tanzania sijui kama hilo umeliangalia

Kenya na Cameroon wana matatizo yale yale ya Ukabila na udini.
Sijui kama uchifu umeweza kusaidia lolote katika maendeleo ya mataifa hayo

Pengine tofauti kidogo ni kuwa mimi nimeishi na Kenyata na Nyerere na waliofuata. Hii EA ikifa sisimuliwi

Tanzania imepiga hatua kubwa sana kiuchumi, kijamii kwa miaka 25 iliyopita kulinganisha na Kenya wakati huo
Unazungumzia diaspora! mbiona huzungumzii kandambili za matairi, wengine tumeishi

Kuhusu diaspora, wingi wao unatokana na siasa zao za mwanzo na si uchifu. Kenya ilikuwa na open market miaka nenda rudi. Sisi tulikuwa na ujamaa uliotufunga. Guess what speed yetu sasa hivi inatupeleka at par
Diversity si makabila!!! hiyo inaitwa misnomer .
Tunapoongelea diversity tuna definition tofauti.Makabila ni sehemu tu lakini si diversity.
Nguruvi3:

Tanganyika ilikuwa na amani wakati wa mkoloni. Chama kilichodai uhuru TANU, kilikuwa na wanachama kutoka pande zote za nchi. Hivyo tulikuwa na changamoto zingine kuliko hizo nchi unazotaja. Ukienda Kenya, wajaluo wana timu yao ya mpira, wana vilabu vyao vya pombe, wana bendi zao za muziki. Ukienda Nigeria, waibo wanaoshi Kaskazini wana vitongoji vyao na mambo yao.

Huku kweli tumeshabikia Simba na Yanga toka 1936. Tumecheza wote muziki wa Tabora, Morogoro Jazz. Ukija Dar Es Salaam, mjini kulikuwa na wamanyema, wanyamwezi kuliko wazaramo. Kama sehemu unayotoka ilisubiri Nyerere kuelewa kuishi na watu wa makabila mengine, basi utakuwa ni sehemu ndogo ya population na usitujumlishe na watanzania wote.

My point is watanzania tulikuwa na changamoto zingine baada ya kupata. Kuvunja uchifu kuondoa changamoto hizi. Kuna maana gani ya kuvunja uchifu na badala yake kuweka mkuu wa mafunzo ya siasa anayeimba ujamaa siku nzima bila kuwa na mafanikio? Kuimba siasa hakuleti kitumbua mezani.

Makabila na miundo yao ya uchifu yangeweza kuachwa. Na hii isingeweza kuharibu utaifa wetu. Nyerere katawala kwa miaka 23. Miaka 23 haitoshi kuondoa ukabila na mgawanyiko wa kijamii. Hivyo hata ukipa credits, alikaa madarakani kwa muda mfupi. Kama unataka kumpa sifa mpe kwa sababu ulisubiri Nyerere upate mabadiliko.

Tukirudi kwenye kamili. Tanzania ni nchi yenye watu wenye asili zao na maeneo yao. Sio nchi ya wahamiaji. Hivyo tunapozungumza masuala ya katiba na maendeleo, inabidi wakati mwingine tukumbuke asili zetu.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,076
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,076 2,000
Nyerere katawala kwa miaka 23. Miaka 23 haitoshi kuondoa ukabila na mgawanyiko wa kijamii. Hivyo hata ukipa credits, alikaa madarakani kwa muda mfupi. Kama unataka kumpa sifa mpe kwa sababu ulisubiri Nyerere upate mabadiliko.
Miaka 23 katika utawala hasa nchi masikini ni muda mefu sana. Katika miaka 23 Nyerere hakumaliza ukabila au udini, alijenga misingi imara ya watu kuviona vitu hivyo kama tatizo. Ndivyo tulivyo leo na hili ni wazi.
Mwinyi, Mkapa, Kikwete wana 30 years , nani anawaongelea?

Kitu kimoja kizuri au kibaya kuhusu Nyerere ni kuwa hahitaji msaada wa kusifiwa au kulaumiwa

Nyerere anatetewa na historia na alichofanya kibaya au kizuri

Ukitaka kumbomoa Nyerere huwezi kwa hisia tu au chuki, ukitaka kumjenga pia huwezi kwa hisia au mahaba

Hicho ndicho kinamtofautisha na viongozi wengi nchini na duniani.
Kwamba, hata waliomchukia kuna mahali husema hapa alikuwa sahihi bila shurti.

Kwamba aliweka misingi ya sisi kujitambua kama taifa, alitujengea umoja 'is unequivocal'

Ukitaka kumfahamu Nyerere kwa merits or demerits, kwanza unatakiwa uwe 'sober minded' pili, usiwe na prejudice. Hili litasaidia sana kuona vitu kwa 'eagle eye'
Vinginevyo itakuwa hadithi ya wanaoamini aliyepewa Uhuru kutoka kwa Mwingireza ni Abdul Sykes

Yaani wapo deluded. They hate Nyerere to the core, that, the best remedy to them is delusion
 
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,515
Points
1,500
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,515 1,500
Kichuguu za mwaka mpya. Kwa kuongezea point yako ya mwanzo na hii. Kuna matatizo ya kimuundo ambayo kwa kiasi kubwa inachangiwa na mapungufu ya kikatiba. Lakini pamoja na mapungufu ya kikatiba, kwa maoni yangu kuna mapungufu ya kimwamko (enlightenment) ndani ya jamii yetu. Huwezi kuwa na jamii isiyo na mwamko na ikaja kuwa na katiba nzuri. na huwezi kuwa na jamii isiyo na mwamko na ikadai ubora (excellence ) kutoka kwa viongozi wake.

Awali umesema matatizo ya 1983, yalisababisha mfumo mbovu unaoendelea mpaka sasa. Hupo sahihi na uchambuzi wako. Hila naona matatizo haya yalianza mapema zaidi ya hapo. Kulikuwa na matatizo ya kiuchumi yaliyokuwa nje ya uwezo wa Tanzania. Lakini vilevile kulikuwa na matatizo ya kimuundo ambayo nchi ilishindwa kuyafanyia kazi.

Moja ya matatizo ya kimuundo: siasa ilikumba kila nyanja ya jamii na uchumi. Na ulifika wakati tuliamini kuwa siasa yetu ilikuwa ni bora kuliko miundo mingine ya siasa duniani. Katiba ya nchi ilikuwa haina nguvu kama katiba ya chama. Vikao vya chama vilikuwa vina nguvu kuliko mamlaka za kiserikali. Kibaya zaidi katiba ya nchi ilifanyiwa marekebisho hili ikidhi itikadi za chama.

Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi yaliyotoka Ulaya Mashariki mwanzoni mwa 90 hayakutegemea na Tanzania haikujitayarisha na mabadiliko hayo. Kwa mfano kulikuwa na watu wengi walioacha taaluma zao na kujikita kwenye siasa. Ghafla bin vuu, hawa hawakuwa na hoja.
You nailed it Zakumi!

1. Balance ya mgongano na tofauti za mawazo ndani ya Serikali na Chama yalizimwa kwa rungu la Chama. Mfano. Vyama vya Wafanyakazi badala ya kusimamia kwa nguvu ustawi wa maslahi ya wafanyakazi (serikalini na sekta binafsi) ili kuchochea kukua kwa uhakika daraja la kati, Vyama hivi viligeuka kuwa matarumbeta ya Chama Tawala na zaidi kukomoana ndani katika kugombea vyeo na madaraka. Hata Umoja wa Vijana, Washirika, UWT na Wazazi, vilishindwa kujenga misingi imara ya kijamii na kuwa satelite units za maamuzi ya Chama. Mbaya zaidi ni pale Chama kilipoamua kuchukua vyombo vya ulinzi na usalama na kuunda "mkoa wa majeshi" katika mfumo wa utendaji wa Chama.

2. Kulikuwa na jitihada zenye nia nzuri, lakini mipango mibovu katika kujenga Taifa na kusogeza maendeleo kwa watu. kwa mtazamo wangu, tulipaswa kuwa na maeneo maalum kama vituo vikuu vya maendeleo ya miji na vijiji (development centers). Mfano Mwanza ingewekwa kuwa kituo kikuu kwa mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, na Shinyanga (kabla ya kumegwa kwa Geita na Simiyu). Iringa iwe center kwa Mbeya Dodoma na Morogoro, Lindi iwe na Ruvuma, Mtwara na Pwani, Tabora iwe na Rukwa, Kigoma na Singida, Arusha ibebane na Kilimanjaro na Tanga. Natumia hizi kama mfano wa kujenga major economic hubs pamoja na social services. Huko kungejengwa Hospitali za Rufaa, Vyuo Vikuu na kuondokana na kila kitu Dar au leo hii kila kitu Dodoma. Aidha encouragement ilipaswa kuwekwa kwa kila eneo kuwa na rights za mapato walau hata 30% ya income kujiendesh na maendeleo ya ndani. nadhani tulikosea sana kujaribu kujenga kila kona kwa uharaka huku tukiwa hatuna uwezo wa kifedha na kukosekana mipango imara.

3. Dhana ya kauli mbiu "Uhuru! Kazi ya TANU" na kuwa TANU (CCM) vitaleta maendeleo vilidumaza Watanzania na kujiona ni wamilikiwa wa TANU (CCM) na hivyo kusalimisha kila kitu na kuitegemea TANU-CCM kuleta "ukombozi, maendeleo, haki, usawa, kufuta Ujinga, maradhi na umasikini.

4. Ndani ya CCM, hapakuwa na afya bora ya upinzani wa ndani wa kiitikadi. Kwenye kila itikadi ya siasa kuna mirengo ya kati, uhafidhina, uliberali na taffsiri tofauti ambazo huchochea ushindani bora wa hoja na sera. Sisi tulimpa kila kitu Mwenyekiti wa Chama ambaye ni Rais, hata kusifia "Zidumu Fikra za Mwenyekiti" something following Stalinism, Maoism and such... leo ni vigumu hata kwenye vyama vya upinzani kuonyesha upinzani wa wazi kwa aliye mwenyekiti wa Chama.

HIvyo, ni lazima tufike mahali tulazimishe haya mabadiliko ya kulijenga Taifa letu upya na si mabadiliko ya Chama cha siasa pekee au fursa za kupokezana vijiti kutawala.

Tuanze kwa kusitisha matumizi na fikra zinazosema "Chama tawala"!
 
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,515
Points
1,500
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,515 1,500
Toka siasa za vyama vingi zianze. Wapinzani (na wanasiasa kutoka CCM) wamegombea nafasi mbali mbali bila kusoma na kujua katiba ya nchi. Sidhani kama Mrema alisoma na kujua katiba ya nchi wakati alipogombea mwaka 1995.

Wengi wanagombea kwa kutumia umaarufu wao. Na kama wangejua mapungufu ya kikatiba basi wasingejaribu kuingia kwenye uchaguzi wa 1995 na kuendelea.

Pili, pamoja na mapungufu yake, katiba sio tatizo. Waingereza hawana katiba iliyoandikwa. Lakini wanafuata taratibu walizojiwekea. Leo waziri mkuu akishindwa kura ya maoni, anaondoka haraka na kumwachia mwingine. Na yakitokea matatizo wanakwenda mahakama kupata sheria. Kwa maneno mengine wanavyo taasisi na vyombo vinavyolinda katiba.

Tanzania hakuna taasisi inayolinda katiba. Vitu vinafanyika kwa hekima na busara za Rais, kwa kuheshimiana au kwa ubabe. Kwa mfano ya Tanzania inasema mwenyekiti wa tume ya uchaguzi akishatangaza matokeo ya urais, matokeo hayatenguliwi. Lakini ndani ya katiba hiyo hiyo, wananchi wapewa haki ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao. Hivyo si sahihi kwa tume kumpa urais mgombea ambaye hakuchaguliwa na wananchi.
I hate to repeat myself... you nailed it again!

Wanasiasa wengi wa Tanzania (both CCM na Upinzani) hawana uelewa wa kutosha wa Katiba ya nchi. Mfano, leo hi kuna kesi mbili au tatu za kikatiba ambazo zimeanzishwa na Watu binafsi na taasisi (NGO), LHRC, TLS na hata kesi ya Jamii Forums versus AG. Wanasiasa wetu hasa wa Upinzani walikataa kuangalia na kutumia Katiba kuwasilisha kesi Mahakamani kama ya tume ya Uchaguzi au kurekebisha mfumo wa Tume walipokutana na Kikwete 2010 na kuridhia kuwepo kwa bunge la Katiba.

Ubabe wa RC na DC haujaanza na kina Makonda, umeanza siku nyingi sana ambapo Dola kwa uwazi bila kificho tangu 1995 imekuwa ikiipendelea CCM (quoting Shibuda juzi kuwa Mwalimu Nyerere aliuliza kwa nini watu wanakamatwa kwa kumbeba Mrema : Wacheni wafu wabebane").

Haya yalihitaji mabadiliko ya Sheria yanayoendana na mabadiliko ya katiba ya 1992.

Lingine; katiba tuliyonayo sasa hivi pamoja na kuruhusu vyama vingi, bado inatakmka wazi kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa. Sasa ni vipi chama kisicho na mtazamo wa kijamaa kikapewa ridhaa na wananchi ambao ni rahisi kuaminishwa kuwa Chama hiki hakistahili kwa kuwa Katiba inasema Tanzania nchi ya kijamaa na hawa ni mabepari...?
 
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,515
Points
1,500
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,515 1,500
Hii ni hoja inayopaswa kuzungumzwa sasa hivi
Tunapoambiwa hakuna pesa za kusimamia mchakato wa katiba, inashangaza

Katiba ni nyaraka na tunu ya nchi. Ni chombo cha juu kabisa kinachoeleza Uzalendo

Tuna wasomi na wananchi wenye uelewa kuliko wakati mwingine
Mchakato wa katiba ufanywe kwa Uzalendo bila kutanguliza pesa

Kinachoitajiwa sasa hivi ni mchakato na uitishwe kwa mbiu ya Uzalendo
Kwamba watakaoshiriki watapewa vitendea kazi na si malipo kama ule ''uvundo''

Hatuhitaji sana wasomi, tnahitaji watu wenye weledi,mapenzi na nchi na wazalendo

Mchakato unawezekana bila pesa na hilo ndilo liwe kipimo cha 'uzalendo'
Uzalendo wa Tanzania unapimwa kwa mafao na posho. Kazi ya kuandika Katiba ilipaswa kuwa jambo la kujitolea, uzalendo wa kweli na si mahesabu ya per diem allowance!

Hii dhambi ya Watunga Sheria ililetwa na Spika Sitta wakati wa vita vyake na Lowassa na Kikwete akavipa baraka kwa kuwapa Wabunge mafao na mishahara waliolilia ili wapitishe miswaada na bajeti zake.

Talks about Executive Hongo!
 
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,515
Points
1,500
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,515 1,500
Mkuu utaifa ulikuwepo, kuujenga ni kitu tofauti kidogo
Nigeria walikuwa na utaifa kama ilivyo Kenya, Cameroon, Rwanda , Burundi n.k.
Swali ni je, hali yao ipoje sasa kwa kuzingatia utaifa wao kama ulivyokuwa wetu?

Ni kweli hatukuwa tumegawanyika kwasababu haikuonekana hadharani.
Sote tulikuwa katika minyororo ya Mjerumani na Mwingereza tukililia hali zetu.

Baada ya uhuru tofauti zingelikuwa wazi kama kungekuwa hakuna mtu wa kuzingalia.

Nyanza cooperation ya kanda ya ziwa ilikuwa na nguvu sana
Kwa kuangalia makabila, Nyanza ingeweza kutawala kwa njia ya kura bila kuiba hata kura moja

KNCU kule Kilimanjaro ilikuwa chini ya makabila madogo .
Ukubwa na influence ilikuwa kwa Wasomi ambao wangeweza kabisa kuwa na upper hand katika siasa za nchi
Ukiuuangali hakuna mahali unaweza kusema tuna mfumo sahihi na hii ni kwasababu hatuna ''mfumo mama'' unaojenga mifumo mingine. Kuzorota kwa taasisi zetu za umma ni zao la mfumo mbaya
I think tatizo letu was more economical then than uzalendo wa Utaifa. Nyanza na KNCU zilikuwa na msukumo mkubwa sana wa kiuchumi wa kujitegemea na walichangia kwa kiasi kikubwa uendeshaji wa TANU na Taifa. Remember Kahawa, Pamba, Tumbaku, Dhahabu na Almasi zote zilikuwa kwenye "himaya' za NYanza na KNCU. Na zaidi, hii arable land yao ilikuwa inazalisha food crops... hivyo ilikuwa ni rahisi sana wka Nyanza na KNCU kuwa huru na wanaojitegema kiuchumi na kuwa na nguvu kubwa kwenye kura zao kuliko wengine.

Kosa la mwalimu ni kushindwa kuwatumia kina Nyanza na KNCU kujenga mfumo bora wa uzalishaji na ushindani ndani ya nchi katika maeneo mengine bila kusukumizia siasa ya Ujamaa na kupiga vita "mabwanyenye" wa ndani.
Nafikiri it would have been safe to have mabwanyenye wa kiuzalishaji mali hasa kilimo na viwanda kuliko mabwanyenye na mamwinyi wa kimadaraka na utawala ambao ndio wamehakikisha badala ya kujenga uchumi, wanakineemesha CCM kiendelee kutawala!
 
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,515
Points
1,500
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,515 1,500
Nguruvi3:

Tanganyika ilikuwa na amani wakati wa mkoloni. Chama kilichodai uhuru TANU, kilikuwa na wanachama kutoka pande zote za nchi. Hivyo tulikuwa na changamoto zingine kuliko hizo nchi unazotaja. Ukienda Kenya, wajaluo wana timu yao ya mpira, wana vilabu vyao vya pombe, wana bendi zao za muziki. Ukienda Nigeria, waibo wanaoshi Kaskazini wana vitongoji vyao na mambo yao.

Huku kweli tumeshabikia Simba na Yanga toka 1936. Tumecheza wote muziki wa Tabora, Morogoro Jazz. Ukija Dar Es Salaam, mjini kulikuwa na wamanyema, wanyamwezi kuliko wazaramo. Kama sehemu unayotoka ilisubiri Nyerere kuelewa kuishi na watu wa makabila mengine, basi utakuwa ni sehemu ndogo ya population na usitujumlishe na watanzania wote.

My point is watanzania tulikuwa na changamoto zingine baada ya kupata. Kuvunja uchifu kuondoa changamoto hizi. Kuna maana gani ya kuvunja uchifu na badala yake kuweka mkuu wa mafunzo ya siasa anayeimba ujamaa siku nzima bila kuwa na mafanikio? Kuimba siasa hakuleti kitumbua mezani.

Makabila na miundo yao ya uchifu yangeweza kuachwa. Na hii isingeweza kuharibu utaifa wetu. Nyerere katawala kwa miaka 23. Miaka 23 haitoshi kuondoa ukabila na mgawanyiko wa kijamii. Hivyo hata ukipa credits, alikaa madarakani kwa muda mfupi. Kama unataka kumpa sifa mpe kwa sababu ulisubiri Nyerere upate mabadiliko.

Tukirudi kwenye kamili. Tanzania ni nchi yenye watu wenye asili zao na maeneo yao. Sio nchi ya wahamiaji. Hivyo tunapozungumza masuala ya katiba na maendeleo, inabidi wakati mwingine tukumbuke asili zetu.
Nafikiri tunakosea sana na kudhulumu wengine wote wasioitwa TANU katika kudai Uhuru wa Tanganyika.

Hii dhana ya kuwa "Uhuru, Kazi ya TANU0 pekee kunamfanya Mtemvu aonekane msaliti (just like how Upinzani leo unafanywa kuwa ni wasaliti), kunawafutia kiana Sheikh TEWA na EAMWS sehemu yao ya kugombea uhuru pamoja na maandiko ya Mohammed Dai kuonyesha Waswahili na Waislamu wa Mwambao (Pwani, Tanga na Mzizima) kuonyesha hivyo, bado jamii inayakataa.

Tuanze kuacha kudai TANU pekee ndio ilileta Uhuru wa Tanganyika!
 
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,849
Points
1,500
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,849 1,500
Miaka 23 katika utawala hasa nchi masikini ni muda mefu sana. Katika miaka 23 Nyerere hakumaliza ukabila au udini, alijenga misingi imara ya watu kuviona vitu hivyo kama tatizo. Ndivyo tulivyo leo na hili ni wazi.
Mwinyi, Mkapa, Kikwete wana 30 years , nani anawaongelea?

Kitu kimoja kizuri au kibaya kuhusu Nyerere ni kuwa hahitaji msaada wa kusifiwa au kulaumiwa

Nyerere anatetewa na historia na alichofanya kibaya au kizuri

Ukitaka kumbomoa Nyerere huwezi kwa hisia tu au chuki, ukitaka kumjenga pia huwezi kwa hisia au mahaba

Hicho ndicho kinamtofautisha na viongozi wengi nchini na duniani.
Kwamba, hata waliomchukia kuna mahali husema hapa alikuwa sahihi bila shurti.

Kwamba aliweka misingi ya sisi kujitambua kama taifa, alitujengea umoja 'is unequivocal'

Ukitaka kumfahamu Nyerere kwa merits or demerits, kwanza unatakiwa uwe 'sober minded' pili, usiwe na prejudice. Hili litasaidia sana kuona vitu kwa 'eagle eye'
Vinginevyo itakuwa hadithi ya wanaoamini aliyepewa Uhuru kutoka kwa Mwingireza ni Abdul Sykes

Yaani wapo deluded. They hate Nyerere to the core, that, the best remedy to them is delusion
Nguruvi3;

Utanzania wangu ni wa kuzaliwa. Haki zangu za kikatiba haziusiani kabisa na mchango wa Nyerere kwa nchi. Katika haki za kikatiba na haki za kibinadamu ninaruhusiwa kuwa na mawazo binafsi. Na mawazo yangu ni kuwa Tanzania ilipopata uhuru tayari ilikuwa na identity ya kitaifa kuliko mataifa mengine ya Africa. Kama historia yako inakwambia identity yetu inatokana juhudi za Nyerere, hayo ni mawazo yako na katiba na mkataba wa haki za binadamu unakulinda kuwa na mawazo yako binafsi. Unachotakiwa usiwahite watu wengine delusional. Kwanini watu wawaze na kuamini kama wewe katika vitu ambavyo vina mawazo mbadala?

Natoka Morogoro, sehemu iliyokuwa na mashamba makubwa ya mkonge. Kabla ya uhuru kulikuwa na wazawa (waluguru na wasagara etc). Baadaye walikuja wanyamwezi, wamanyema, waarabu wakati wa biashara ya utumwa na kujenga reli. Wakati mashamba ya mkonge walikuja warundi, wafipa, wamanda, wamakonde, wagiriki, wahindi etc. Watu hawa wameishi na wanaishi kwa amani kwa miaka mingi wakizungumza kiswahili. Kwenye uchaguzi wa uhuru, Kambona aligombea ubunge na akapewa. Tulikuwa na wabunge wahindi, waarabu. Na mpaka sasa wapo.

Swali langu, kwanini unataka mtu aliyezaliwa Morogoro aamini kuwa bila Nyerere, tungekuwa tunapiga vita vya kikabila? As a matter of fact watu wanaoleta matatizo Morogoro ni waMasaai waliohamia miaka ya 70.
 
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,849
Points
1,500
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,849 1,500
Nafikiri tunakosea sana na kudhulumu wengine wote wasioitwa TANU katika kudai Uhuru wa Tanganyika.

Hii dhana ya kuwa "Uhuru, Kazi ya TANU0 pekee kunamfanya Mtemvu aonekane msaliti (just like how Upinzani leo unafanywa kuwa ni wasaliti), kunawafutia kiana Sheikh TEWA na EAMWS sehemu yao ya kugombea uhuru pamoja na maandiko ya Mohammed Dai kuonyesha Waswahili na Waislamu wa Mwambao (Pwani, Tanga na Mzizima) kuonyesha hivyo, bado jamii inayakataa.

Tuanze kuacha kudai TANU pekee ndio ilileta Uhuru wa Tanganyika!
Rev. Nilikutana na wanafamilia moja kutoka Arusha. Familia hii inamiliki biashara na ilikuwa hipo mbali kimaendeleo kabla ya uhuru. Nyerere, Obote na Kenyatta walikuwa wakifanya mikutano Arusha walikuwa wanakutana kwenye hoteli iliyomilikiwa na familia hii free of charge. Uhuru ulipopatikana hakuna aliyewakumbuka. Ukienda Kagera utaambiwa kuna mhaya aliyechagia. Ukienda Mwanza utaambiwa kuna msukuma aliyechangia. Hile ofisi ya CCM pale Lumumba, ilikuwa ni nyumba ya mtu.

Hivyo tukija kwenye suala zima na uhuru, kuna watu walijitolea. Na inashangaza sana kwa suala la kihistoria la kuandika katiba, watu wanalipwa na hakuna wanachokitoa.

Ukija kwenye suala la Mtemvu, alikuwa anapigania uzawa. Moja ya vitu ambavyo hakutaka ni kuwakaribisha wazungu kwenye chama cha waafrika. Tulikaribisha wazungu na matokeo yake lengo zima la kupigania uhuru likawa kujenga Ujamaa na sio kumpa mwafrika uhuru.
 
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,849
Points
1,500
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,849 1,500
I hate to repeat myself... you nailed it again!

Wanasiasa wengi wa Tanzania (both CCM na Upinzani) hawana uelewa wa kutosha wa Katiba ya nchi. Mfano, leo hi kuna kesi mbili au tatu za kikatiba ambazo zimeanzishwa na Watu binafsi na taasisi (NGO), LHRC, TLS na hata kesi ya Jamii Forums versus AG. Wanasiasa wetu hasa wa Upinzani walikataa kuangalia na kutumia Katiba kuwasilisha kesi Mahakamani kama ya tume ya Uchaguzi au kurekebisha mfumo wa Tume walipokutana na Kikwete 2010 na kuridhia kuwepo kwa bunge la Katiba.

Ubabe wa RC na DC haujaanza na kina Makonda, umeanza siku nyingi sana ambapo Dola kwa uwazi bila kificho tangu 1995 imekuwa ikiipendelea CCM (quoting Shibuda juzi kuwa Mwalimu Nyerere aliuliza kwa nini watu wanakamatwa kwa kumbeba Mrema : Wacheni wafu wabebane").

Haya yalihitaji mabadiliko ya Sheria yanayoendana na mabadiliko ya katiba ya 1992.

Lingine; katiba tuliyonayo sasa hivi pamoja na kuruhusu vyama vingi, bado inatakmka wazi kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa. Sasa ni vipi chama kisicho na mtazamo wa kijamaa kikapewa ridhaa na wananchi ambao ni rahisi kuaminishwa kuwa Chama hiki hakistahili kwa kuwa Katiba inasema Tanzania nchi ya kijamaa na hawa ni mabepari...?
Katiba ya nchi ni mwongozo wa nchi na sio mwongozo wa itikadi. It's ok kama katiba ya CCM itasema tunataka kujenga ujamaa.

Utangulizi wa katiba ya nchi unatakiwa kuangalia misingi ya kuanzishwa kwa nchi. Kwa Tanzania inatakiwa irudi kwenye harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Na vilevile ichukue harakati za kupigania uhuru wa Zanzibar na mapinduzi yaliotokea.

Kwa kifupi jukumu la katiba iwe ni kulinda haki na uhuru wa mtanzania kitu ambacho alinyimwa wakati wa mkoloni na akahamua kudai uhuru na kufanya mapinduzi. Ujamaa, kununua ndege, kujenga reli ya STG, kupata Phd hayo ni matokeo tu uhuru.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,076
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,076 2,000
Nafikiri tunakosea sana na kudhulumu wengine wote wasioitwa TANU katika kudai Uhuru wa Tanganyika.

Hii dhana ya kuwa "Uhuru, Kazi ya TANU0 pekee kunamfanya Mtemvu aonekane msaliti (just like how Upinzani leo unafanywa kuwa ni wasaliti), kunawafutia kiana Sheikh TEWA na EAMWS sehemu yao ya kugombea uhuru pamoja na maandiko ya Mohammed Dai kuonyesha Waswahili na Waislamu wa Mwambao (Pwani, Tanga na Mzizima) kuonyesha hivyo, bado jamii inayakataa.

Tuanze kuacha kudai TANU pekee ndio ilileta Uhuru wa Tanganyika!
Na hii ndiyo 'point of contentions' kati yangu na Mohamed. Siku zote nimesimama na kusema Wazee wetu wote waliopigania uhuru wanastahili heshima. Hii ni pamoja na wazee anaowataja Mohamed Said na wengine wasiotajwa

Hakuna hata siku moja nitakejeli mchango wa mtu yoyote, tena nasikitika hata kumbu kumbu zao hazipo

Tatizo kubwa ni pale historia inapopindishwa ili 'ku 'fit' narrative fulani.
Kuna wanaosema waliopigania Uhuru ni watu wa Pwani. Ukisoma historia upinzania dhidi ya mkoloni ulianza maeneo mengi na miaka mingi. Akina Mkwawa, Mirambo, Wapare na kodi ya Mbiru n.k n.k

Mfano wa hoja tunazopingana na baadhi ni kuhusu katiba ya vyama. Niliwahi kuuliza kabla ya TANU kulikuwa na vyama vilivyotangulia AA na TAA. Je vilikuwa na katiba iliyoandikwa? Jibu likawa ni hapana

Nikauliza baada ya hapo nani aliandika katiba? Watu wakagoma kusema ni Nyerere kwa hoja kuwa alinukuu kutoka maeneo mengine. Hapa ni katika kuondoa credit hata kama ukweli ni kuwa yeye ndiye ''aliyekusanya''

Dhulma ya historia inafanywa kwa kuficha ukweli kuwa kule Mbeya, Tunduru, Bukoba na Ujiji kulikuwa na watu waliochangia sana katika harakati. Hata hivyo, Dar es salaam kuwa jiji na makao ya gavana kulitoa picha kubwa zaidi kwa wale walioishi hapo. Advantage hiyo isistumiwe kudhulumu haki za wapigani uhuru wengine

Dhulma hiyo inaendelea kwa watu kutokuwa na mtazamo mpana. Wanaongozwa na prejudice na grudge na hayo yanawafanya wanakuwa na 'delusion' . Wapo katika state of denial hata kama ukweli unawaongoza

Mfano, tukipata uhuru tulikuwa Watanganyika na utaifa wetu uliojengwa juu ya kujitawala. Baada ya Uhuru watu walikuwa 'malimbukeni' kwa maana ya kuwa misguided wakidhani Uhuru ilikuwa open season hasa kwa wenye nguvu. 1964 Mutiny inaeleza vema, 1967 iliyopelekea Africanization inaeleza

Kazi ya kuwafanya watu waelewe maana ya Uhuru na Umoja wetu ilifanywa na Nyerere.
Nikatoa mfano wa Nigeria ambako walipata Uhuru kabla yetu wakiwa na utaifa, lakini kwa kukosa kuinganisho wamepitia wakati mgumu. Sasa inapokuja suala la Nyerere kama mwanadamu kuna merits na demerits zake

Watu ukiwaambia Nyerere alijenga bwawa la nyumba ya mungu wanakataa kwa hoja kuwa mto Ruvu (K'njaro) ulikuwepo kabla ya Nyerere kufika. Hii ndiyo naita state of denial, kwa kitu rahisi tu kutaka kuondoa credit
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,076
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,076 2,000
Uzalendo wa Tanzania unapimwa kwa mafao na posho. Kazi ya kuandika Katiba ilipaswa kuwa jambo la kujitolea, uzalendo wa kweli na si mahesabu ya per diem allowance!

Hii dhambi ya Watunga Sheria ililetwa na Spika Sitta wakati wa vita vyake na Lowassa na Kikwete akavipa baraka kwa kuwapa Wabunge mafao na mishahara waliolilia ili wapitishe miswaada na bajeti zake.

Talks about Executive Hongo!
Ni makosa makubwa sana kazi za kizalendo kuzifanya kazi za kulipwa
Bunge la katiba ni kazi ya kizalendo, kama kuna atakayepata fursa ya kulitumikia mtu huyo atakuwa amepewa heshima kubwa ya nchi.

Hicho ndicho kilicholeta tatizo. Hoja ilikuwa kuwepo Bunge la katiba. Wakaazi wa ''Dodoma' wakaona ulaji utapita pembeni wakafanya kila wawezalo wawe ndani ya Bunge. Fadhila walizopewa walizilipa kwa kitu kinaitwa ''caucus' kwamba misimamo ya vyama juu ya katiba badala ya misimamo wa wabunge wa bunge la katiba

Tunaweza kuita mkutano wa kitaifa bila malipo. Wazalendo wakaja kujadili hatma ya nchi kwa gharama zao
Wasiofika ni wale ''wafanyabiashara''. Mkutano wa kitaifa ndio utakaondaa mchakato mzima wa katiba

Sioni, mahali ambapo kunahitajika gharama zaidi ya kuwepo ulinzi ambao tayari unalipiwa kila siku

Na ili tupate katiba bora, ''wafanyabiashara'' wa mjengo Dodoma wakae pembeni
Washiriki nao wakubali kuwa kwa namna yoyote watafaidika kama raia baada ya kazi yao na si vyeo
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,076
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,076 2,000
Natoka Morogoro, sehemu iliyokuwa na mashamba makubwa ya mkonge. Kabla ya uhuru kulikuwa na wazawa (waluguru na wasagara etc). Baadaye walikuja wanyamwezi, wamanyema, waarabu wakati wa biashara ya utumwa na kujenga reli. Wakati mashamba ya mkonge walikuja warundi, wafipa, wamanda, wamakonde, wagiriki, wahindi etc. Watu hawa wameishi na wanaishi kwa amani kwa miaka mingi wakizungumza kiswahili. Kwenye uchaguzi wa uhuru, Kambona aligombea ubunge na akapewa. Tulikuwa na wabunge wahindi, waarabu. Na mpaka sasa wapo.
Thank you! thank you! thank you!
Ulichokieleza hapo ndicho kitu kinaitwa '' Diversity and inclusion''

Kwa mfano wako hao juu, tunarudi nyuma niliposema Tanzania ina diversity kubwa
Lakini si diversity tu ni diversity and inclusion
 
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,849
Points
1,500
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,849 1,500
Na hii ndiyo 'point of contentions' kati yangu na Mohamed. Siku zote nimesimama na kusema Wazee wetu wote waliopigania uhuru wanastahili heshima. Hii ni pamoja na wazee anaowataja Mohamed Said na wengine wasiotajwa

Hakuna hata siku moja nitakejeli mchango wa mtu yoyote, tena nasikitika hata kumbu kumbu zao hazipo

Tatizo kubwa ni pale historia inapopindishwa ili 'ku 'fit' narrative fulani.
Kuna wanaosema waliopigania Uhuru ni watu wa Pwani. Ukisoma historia upinzania dhidi ya mkoloni ulianza maeneo mengi na miaka mingi. Akina Mkwawa, Mirambo, Wapare na kodi ya Mbiru n.k n.k

Mfano wa hoja tunazopingana na baadhi ni kuhusu katiba ya vyama. Niliwahi kuuliza kabla ya TANU kulikuwa na vyama vilivyotangulia AA na TAA. Je vilikuwa na katiba iliyoandikwa? Jibu likawa ni hapana

Nikauliza baada ya hapo nani aliandika katiba? Watu wakagoma kusema ni Nyerere kwa hoja kuwa alinukuu kutoka maeneo mengine. Hapa ni katika kuondoa credit hata kama ukweli ni kuwa yeye ndiye ''aliyekusanya''

Dhulma ya historia inafanywa kwa kuficha ukweli kuwa kule Mbeya, Tunduru, Bukoba na Ujiji kulikuwa na watu waliochangia sana katika harakati. Hata hivyo, Dar es salaam kuwa jiji na makao ya gavana kulitoa picha kubwa zaidi kwa wale walioishi hapo. Advantage hiyo isistumiwe kudhulumu haki za wapigani uhuru wengine

Dhulma hiyo inaendelea kwa watu kutokuwa na mtazamo mpana. Wanaongozwa na prejudice na grudge na hayo yanawafanya wanakuwa na 'delusion' . Wapo katika state of denial hata kama ukweli unawaongoza

Mfano, tukipata uhuru tulikuwa Watanganyika na utaifa wetu uliojengwa juu ya kujitawala. Baada ya Uhuru watu walikuwa 'malimbukeni' kwa maana ya kuwa misguided wakidhani Uhuru ilikuwa open season hasa kwa wenye nguvu. 1964 Mutiny inaeleza vema, 1967 iliyopelekea Africanization inaeleza

Kazi ya kuwafanya watu waelewe maana ya Uhuru na Umoja wetu ilifanywa na Nyerere.
Nikatoa mfano wa Nigeria ambako walipata Uhuru kabla yetu wakiwa na utaifa, lakini kwa kukosa kuinganisho wamepitia wakati mgumu. Sasa inapokuja suala la Nyerere kama mwanadamu kuna merits na demerits zake

Watu ukiwaambia Nyerere alijenga bwawa la nyumba ya mungu wanakataa kwa hoja kuwa mto Ruvu (K'njaro) ulikuwepo kabla ya Nyerere kufika. Hii ndiyo naita state of denial, kwa kitu rahisi tu kutaka kuondoa credit

Nguruvi3:

Kazi za utafiti wa Mohamedi Saidi zipo nzuri tu. Kachukua thesis zake na kaonyesha. Na wewe unaweza kufanya utafiti wako na kuongezea au kupinga.

Kwanini Mohamedi Saidi aandike kama wewe unavyotaka? Kila siku hupo hapa unaimba demokrasia. Lakini demokrasia inataka mawazo mbadala. Au unafikiri ni kitu cha afya watu kuimba Nyerere Nyerere kila siku. Kama kwenu kuna watu waliofanya vitu unavyoona vina mchango wa kitaifa au mchango katika kabila yako, wewe andika. Wapo watakaokubaliana na wewe na watakaopinga.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,076
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,076 2,000
"Zakumi, post: 30037452, member: 12016"]Nguruvi3:
Kazi za utafiti wa Mohamedi Saidi zipo nzuri tu. Kachukua thesis zake na kaonyesha.
Na wewe unaweza kufanya utafiti wako na kuongezea au kupinga.
Hatuendi hivyo kwamba usipokubaliana na kitu lazima uandike kitabu.

Kinachotakiwa ni critical thinking, kwamba, kwanini kuna abacd? Mhusika ndiye anapaswa kujibu

Wattson alipoandika kuhusu IQ za waafrika, si kila mawanasayansi aliandika kitabu

Katika mijadala ambayo sijui kama ulishiriki, Mohamed ameshindwa kutetea baadhi ya hoja
Hiyo haifanyi kazi yake iwe na makosa, hapana! inasaidia kuonyesha palipo na mapungufu

Nimeeleza mara nyingi kuhusu historia yake ambayo mengi hayakujulikana au yalifichwa
Hata hivyo, kuna maeneo ambayo ima 'facts' zimefichwa au kuondolewa kwasababu zisizo na msingi

Nitakupa mfano. Katika kitabu Mohamed anasema aliyemtambulisha Nyerere kwa mara ya kwanza Dar es Saalaam na aliyemwingiza katika siasa ni Abdul Sykes mwaka 1953 kama sikosei

Kitabu hicho hicho kinaeleza Nyerere alikuwa katiba wa TAA tawi la Tabora na alihudhuria mkutano wa TAA 1948

Kwa mtu anayesoma between the lines, kuna tatizo.
Kwanza, Nyerere alikuwa katika siasa akiwa Makerere na kuandika barua za mawasiliano za chama cha wanafunzi

Pili, katibu wa TAA Tawi kubwa kama la Tabora zama hizo alikuwa na mawasiliano na makao makuu
Tatu, kama alihudhuria mkutano mkuu Dar es Salaam 1948 ni wazi alikutana na viongozi akiweme Abdul

Haya si maneno yangu ni maandiko ya Mohamed yanayopingana.
Ukisoma kwa uyakinifu, hoja ni kuonyesha Nyerere hakujua siasa, alifunzwa na akina Abdul na alifika Dar 1953

Yote yanakinzana katika kitabu na hoja kubwa ni kutaka ku'degrade' Nyerere na kumu'elevate' Abdul hata kwa kupindisha ukweli.

Haya ndiyo ninayokataa kwa maana kuwa huwezi kukataa historia ya Kivukoni iliyoandikwa kishabiki halafu ukaandika historia katika upotofu wa kusahihisha upotofu. Nadhani utanielewa hadi hapo
Kwanini Mohamedi Saidi aandike kama wewe unavyotaka? Kila siku hupo hapa unaimba demokrasia. Lakini demokrasia inataka mawazo mbadala.
Absolutely, demokrasia ni pana sana

Sitaki wala sijafikiri aandike kama ninavyotaka. Sina kitabu cha historia nilichoandika, iweje nimtake aandike kwa namna isiyokuwepo? Katika uandishi wake ninaupenda, ni orator mzuri, lakini hilo halizuii kufanya 'critic'

Tatizo nililo nalo na ambalo nimelibaini lakini sijui suluhu yake ni kuwa mimi si mtu wa kumeza.
Huwa napenda kutafuna, kukamua ili nipate ladha wakati naishibisha akili yangu.
Au unafikiri ni kitu cha afya watu kuimba Nyerere Nyerere kila siku. Kama kwenu kuna watu waliofanya vitu unavyoona vina mchango wa kitaifa au mchango katika kabila yako, wewe andika. Wapo watakaokubaliana na wewe na watakaopinga.
Hey, Nyerere ni mwanadamu na ana mapungufu yake.

Katika watu walioandika mapungufu nipo. 1. Kuua vyama vingi 2. Kutoafikiana na wenzake wa zama zake baada ya uhuru 3. Kuua vyama ushirika 4. Kuanzisha UPE iliyozaa kizazi kilichopo 5. Kujenga utamaduni wa kuhamisha watumishi na si kuwaadhibu 5. Kuifanya serikali isimamie biashara kama ilivyokuwa RTC, n.k n.k

Mapungufu hayo na mengine mengi nisiyoyataja kwa muono wangu, hayanifanyi niondoe credit za kile kizuri alichofanya. Hata Idd Amin Waganda wanamkumbuka kwa mazuri licha ya uharamia aliokuwa nao

Sasa kuandika kitabu kuhusu makabila wapo walioandika na sote hatuwezi kuwa wanahistoria
Kutokuwa mwanahistoria hukuzuii kusoma, kuielewa na kuichambua historia

Muhimu ni kuwa kupinga hoja katika historia si kuikataa historia.

Kitabu kinapowekwa katika hadhira kinakuwa subject of discussions and scrutiny.

Kitabu cha historia hakisomwi kama noval ya Chase hasa kwa wanaotumia vichwa
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,076
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,076 2,000
I think tatizo letu was more economical then than uzalendo wa Utaifa. Nyanza na KNCU zilikuwa na msukumo mkubwa sana wa kiuchumi wa kujitegemea na walichangia kwa kiasi kikubwa uendeshaji wa TANU na Taifa. Remember Kahawa, Pamba, Tumbaku, Dhahabu na Almasi zote zilikuwa kwenye "himaya' za NYanza na KNCU. Na zaidi, hii arable land yao ilikuwa inazalisha food crops... hivyo ilikuwa ni rahisi sana wka Nyanza na KNCU kuwa huru na wanaojitegema kiuchumi na kuwa na nguvu kubwa kwenye kura zao kuliko wengine.

Kosa la mwalimu ni kushindwa kuwatumia kina Nyanza na KNCU kujenga mfumo bora wa uzalishaji na ushindani ndani ya nchi katika maeneo mengine bila kusukumizia siasa ya Ujamaa na kupiga vita "mabwanyenye" wa ndani.
Nafikiri it would have been safe to have mabwanyenye wa kiuzalishaji mali hasa kilimo na viwanda kuliko mabwanyenye na mamwinyi wa kimadaraka na utawala ambao ndio wamehakikisha badala ya kujenga uchumi, wanakineemesha CCM kiendelee kutawala!
Nyanza na KNCU zilikuwa na mwamko sana katika masuala ya kicuhumi na kijamii.

Mfano, KNCU walijenga sekondari ya Lyamungo wakiwa na ambition ya kuwa na chuo kikuu. Huko Nyanza nako nguvu ya chama ilikuwa kubwa sana hasa kiuchumi

Mwalimu aliona nguvu ya kiuchumi inaweza kuwa tishio katika utawala.
Utakumbuka akina Chief Marealle walivyohangaishana nyakati hizo. Kumbu kumbu hiyo haikuwa nzuri kwake

Kwasababu hiyo, Mwl akaua vyama hivyo kwa makosa kabisa.

Laiti angeviacha vingechangia katika maendeleo ya maeneo yao na kuipa serikali nguvu ya kuhudumia maeneo mengine

Kwa mfano, zao la kahawa KNCU ilikuwa inatoa pembejeo kama dawa na zana za kutumia kwa wakulima

Ilikuwa ina uwezo wa kuwakopesha wakulima ili wazalishe zaidi na pembejeo halikuwa tatizo kabisa

Kahawa iliponunuliwa kwa ''Sh 5'' kwa kilo, chama kiliuza katika soko la dunia.
Kuna wakati bei ilipanda baada ya mauzo na chama kilirudi kuwafidia wakulima kwa kilichoitwa 'mabaki'

Lakini pia KNCU ilikuwa inatafuta masoko na ilijihusisha na shughuli za kijamii.
Viongozi walichaguliwa na wanachama kwa sifa zao na waliwajibika kwao kikamilifu

Tukitazama leo, pembejeo ni tatizo mbolea inaozea katika maghala.

Wasimamizi ni wakuu wa Wilaya ambao majukumu yao ya kisiasa ni zaidi ya kiuchumi.
Hawana 'say' katika shughuli za uzalishaji na hawawajibiki kwa Wazalishaji.
Hilo limepelekea kuua kilimo kwa sehemu kubwa sana

Badala ya decentralization iliyoacha serikali kuwa na majukumu machache, centralization inaifanya serikali kuwa mkulima, mfanyabiashara na mkusanya kodi.
Haiwezekani ! hiyo si kazi ya serikali na ndiyo tunayoyaona sasa
 
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,849
Points
1,500
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,849 1,500
Hatuendi hivyo kwamba usipokubaliana na kitu lazima uandike kitabu.

Kinachotakiwa ni critical thinking, kwamba, kwanini kuna abacd? Mhusika ndiye anapaswa kujibu

Wattson alipoandika kuhusu IQ za waafrika, si kila mawanasayansi aliandika kitabu

Katika mijadala ambayo sijui kama ulishiriki, Mohamed ameshindwa kutetea baadhi ya hoja
Hiyo haifanyi kazi yake iwe na makosa, hapana! inasaidia kuonyesha palipo na mapungufu

Nimeeleza mara nyingi kuhusu historia yake ambayo mengi hayakujulikana au yalifichwa
Hata hivyo, kuna maeneo ambayo ima 'facts' zimefichwa au kuondolewa kwasababu zisizo na msingi

Nitakupa mfano. Katika kitabu Mohamed anasema aliyemtambulisha Nyerere kwa mara ya kwanza Dar es Saalaam na aliyemwingiza katika siasa ni Abdul Sykes mwaka 1953 kama sikosei

Kitabu hicho hicho kinaeleza Nyerere alikuwa katiba wa TAA tawi la Tabora na alihudhuria mkutano wa TAA 1948

Kwa mtu anayesoma between the lines, kuna tatizo.
Kwanza, Nyerere alikuwa katika siasa akiwa Makerere na kuandika barua za mawasiliano za chama cha wanafunzi

Pili, katibu wa TAA Tawi kubwa kama la Tabora zama hizo alikuwa na mawasiliano na makao makuu
Tatu, kama alihudhuria mkutano mkuu Dar es Salaam 1948 ni wazi alikutana na viongozi akiweme Abdul

Haya si maneno yangu ni maandiko ya Mohamed yanayopingana.
Ukisoma kwa uyakinifu, hoja ni kuonyesha Nyerere hakujua siasa, alifunzwa na akina Abdul na alifika Dar 1953

Yote yanakinzana katika kitabu na hoja kubwa ni kutaka ku'degrade' Nyerere na kumu'elevate' Abdul hata kwa kupindisha ukweli.

Haya ndiyo ninayokataa kwa maana kuwa huwezi kukataa historia ya Kivukoni iliyoandikwa kishabiki halafu ukaandika historia katika upotofu wa kusahihisha upotofu. Nadhani utanielewa hadi hapo
Absolutely, demokrasia ni pana sana

Sitaki wala sijafikiri aandike kama ninavyotaka. Sina kitabu cha historia nilichoandika, iweje nimtake aandike kwa namna isiyokuwepo? Katika uandishi wake ninaupenda, ni orator mzuri, lakini hilo halizuii kufanya 'critic'

Tatizo nililo nalo na ambalo nimelibaini lakini sijui suluhu yake ni kuwa mimi si mtu wa kumeza.
Huwa napenda kutafuna, kukamua ili nipate ladha wakati naishibisha akili yangu. Hey, Nyerere ni mwanadamu na ana mapungufu yake.

Katika watu walioandika mapungufu nipo. 1. Kuua vyama vingi 2. Kutoafikiana na wenzake wa zama zake baada ya uhuru 3. Kuua vyama ushirika 4. Kuanzisha UPE iliyozaa kizazi kilichopo 5. Kujenga utamaduni wa kuhamisha watumishi na si kuwaadhibu 5. Kuifanya serikali isimamie biashara kama ilivyokuwa RTC, n.k n.k

Mapungufu hayo na mengine mengi nisiyoyataja kwa muono wangu, hayanifanyi niondoe credit za kile kizuri alichofanya. Hata Idd Amin Waganda wanamkumbuka kwa mazuri licha ya uharamia aliokuwa nao

Sasa kuandika kitabu kuhusu makabila wapo walioandika na sote hatuwezi kuwa wanahistoria
Kutokuwa mwanahistoria hukuzuii kusoma, kuielewa na kuichambua historia

Muhimu ni kuwa kupinga hoja katika historia si kuikataa historia.

Kitabu kinapowekwa katika hadhira kinakuwa subject of discussions and scrutiny.

Kitabu cha historia hakisomwi kama noval ya Chase hasa kwa wanaotumia vichwa

Ngoja nionyeshe mapungufu ya uchambuzi wako. Nyerere kazaliwa 1922. Hivyo mwaka 1948 alikuwa na miaka 26 tu. Hivyo bado alikuwa kijana sana kusema kwamba alikuwa na mchango mkubwa kwa TAA.

Pili Nyerere alikuwa masomoni Makerere mwaka 1943 - 1947. Hivyo aliondoka akiwa na miaka 21 na kurudi akiwa na miaka 25. Hivyo katika kipindi ambacho alikuwa masomoni, alikuwa nje ya TAA. Hivyo huwezi kusema alikuwa anajulikana vizuri ndani ya TAA.

Tatu, wakoloni walifuatilia wanafunzi walioanza kuwa radicalized na kuwanyima nafasi za kuendelea. Kwa mfano Odinga Oginga naye alisoma Makerere na alionyesha u-radical wake na matokeo yake hakupewa nafasi za kuendelea. Hakuna sehemu zinazoonyesha Nyerere was radicalize akiwa mwanafunzi. Na kama angekuwa radical, nafasi ya kusoma Scotland asingepewa.

Nne, Nyerere alikuwa Masomo Scotland kuanzia 1949-1952. Hivyo ukiondoa kipindi alichokuwa Masomoni Makerere, utaona kuwa Nyerere alijitokeza sana kwenye siasa akiwa na zaidi ya miaka 30. Alianza shule akiwa na miaka 12. Alimaliza O level akiwa na miak 20 (1942). Baada ya hapo alikuwa Makerere mpaka 1947. Hivyo katika kipindi cha miaka yake 30 ya mwanzo ni mwaka 1948 alikuwa mfanyakazi anayejitegemea na ambaye angeweza kushiriki kwenye masuala ya kisiasa. Zaidi ya hapo alikuwa ni mwanafunzi.

Tano, Nyerere aliporudi kutoka masomoni (Scotland) alitaka kuanzisha chama chake. Kama yeye alikuwa anajulika ndani ya TAA kwanini alikuwa na nia ya kuanzisha chama chake? Ni wakina Kambona walioshawishi ajiunge na TAA na watu wakamwachia nafasi.

Sita, kwa mujibu wa Kambona. Na maneno haya aliyesema aliporudi 1992 na hakuna mtu aliyekataa. Kambona alisema kuwa baada wakoloni kumwambia Nyerere achague kazi ya kufundisha au kuwa mwanasiasa, Nyerere alitaka kurudi kufundisha na kuacha TANU. Ni baada ya wazee kumwambia kuwa watamlipa posho na kumwakikishia maslahi yake ndipo aliondelea na shughuli.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,076
Points
2,000
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,076 2,000
Mkuu Zakumi, with due respect this is anachronism. Usiniwekee ''maneno mdomoni'' ndiyo maana hufanyi 'quote' ili iwe rahisi kumchanganya mtu anayesoma bila kujua nini kilisemwa (dishonest)
Nilichokieleza kuhusu Mohamed kimetoka katika kitabu chake nikionyesha 'contradiction'
"Zakumi, post: 30038204, member: 12016"]Ngoja nionyeshe mapungufu ya uchambuzi wako. Nyerere kazaliwa 1922. Hivyo mwaka 1948 alikuwa na miaka 26 tu. Hivyo bado alikuwa kijana sana kusema kwamba alikuwa na mchango mkubwa kwa TAA.
Sijasema, nimekariri maneno ya kitabu na mijadala tuliyokuwa nayo na Mohamed. Nilimuuliza swali, ilikuwaje Nyerere akiwa katibu wa TAA Tabora alifika katika mkutano mkuu Dar, halafu Nyerere huyo huyo akaandikwa kufika Dar kwa mara ya kwanza 1953? wewe unajibu?

Nikauliza alipokuja katika mkutano mkuu ambao viongozi walikuwa akina Abdul hakukutana nao akiwa katibu wa Tawi kuu la Tabora? angalia kuna alama ya kuuliza, si kauli.
Haya yapo katika kitabu chake na mijadala, sikutafiti, sijaandika. Mohamed hakuwa na jibu!
Pili Nyerere alikuwa masomoni Makerere mwaka 1943 - 1947. Hivyo aliondoka akiwa na miaka 21 na kurudi akiwa na miaka 25. Hivyo katika kipindi ambacho alikuwa masomoni, alikuwa nje ya TAA. Hivyo huwezi kusema alikuwa anajulikana vizuri ndani ya TAA.
Sijaandika anajulikana TAA.
Nilichosema ni kuwa akiwa katibu mkuu wa Tawi la Tabora, definite alijulikana. Kulikuwa na matawi mangapi? Tabora ilikuwa na nafasi gani? Again nilimuuliza mwanahistoria hakujibu. Hayo unayoandika na maneno yako
Tatu, wakoloni walifuatilia wanafunzi walioanza kuwa radicalized na kuwanyima nafasi za kuendelea.
Kwa mfano Odinga Oginga naye alisoma Makerere na alionyesha u-radical wake na matokeo yake hakupewa nafasi za kuendelea. Hakuna sehemu zinazoonyesha Nyerere was radicalize akiwa mwanafunzi. Na kama angekuwa radical, nafasi ya kusoma Scotland asingepewa.
The same thing! Hakuna mahali nimeandika kuhusu unayosema hapo!
Nilichofanya ni nukuu ya kitabu ndiyo maana nimetumia neno ''critic' kwa kuonyesha kuna kitu kinahojiwa
Nne, Nyerere alikuwa Masomo Scotland kuanzia 1949-1952. Hivyo ukiondoa kipindi alichokuwa Masomoni Makerere, utaona kuwa Nyerere alijitokeza sana kwenye siasa akiwa na zaidi ya miaka 30. Alianza shule akiwa na miaka 12. Alimaliza O level akiwa na miak 20 (1942). Baada ya hapo alikuwa Makerere mpaka 1947. Hivyo katika kipindi cha miaka yake 30 ya mwanzo ni mwaka 1948 alikuwa mfanyakazi anayejitegemea na ambaye angeweza kushiriki kwenye masuala ya kisiasa. Zaidi ya hapo alikuwa ni mwanafunzi.
Well, unamueleza Mwanahistoria si mimi. Mimi natumia kitabu kilichoandikwa

Pengine nikusaidie hoja, Mwl alizaliwa 1922, kwa miaka 30 unayosema ilikuwa mwaka 1952, mwaka mmoja kabla ya kupewa uongozi. Hii ni tafakuri tu na ndipo ninapoweza kuonyesha matundu ya hoja (between the lines)

Tano, Nyerere aliporudi kutoka masomoni (Scotland) alitaka kuanzisha chama chake. Kama yeye alikuwa anajulika ndani ya TAA kwanini alikuwa na nia ya kuanzisha chama chake? Ni wakina Kambona walioshawishi ajiunge na TAA na watu wakamwachia nafasi.
Kitabu kinasema alikuwa katibu wa TAA Tabora. Na kitabu kinawataja akima Mwapachu ndio waliomshawishi kuingia siasa za TAA.

Sasa kama kuna Kambona hiyo ni sehemu ya historia unayotueleza pengine tusioijua.
Narudi kule kule maelezo yangu yanatokana na mijadala na kitabu cha MS
Sita, kwa mujibu wa Kambona. Na maneno haya aliyesema aliporudi 1992 na hakuna mtu aliyekataa. Kambona alisema kuwa baada wakoloni kumwambia Nyerere achague kazi ya kufundisha au kuwa mwanasiasa, Nyerere alitaka kurudi kufundisha na kuacha TANU. Ni baada ya wazee kumwambia kuwa watamlipa posho na kumwakikishia maslahi yake ndipo aliondelea na shughuli.
Ahsante kwa maelezo, lakini haijawa hoja yangu popote pale

Naheshimu sana mawazo yako, hata hivyo ni vema ukifanya 'quote' kila unapojibu hoja badala ya kutunga maneno na kisha kusema ni yangu.

Udhaifu wangu ni ule ule kwamba, huwa siongozwi na grudge, naheshimu kazi ya mtu bila kujali dini, kabila au rangi. Kwangu ''intellect'' ni muhimu sana na hilo linanisaidia kutosoma vitu kama noval, kujenga hoja kwa mantiki na kubwa zaidi kutumia vizuri kaubongo kangu kadogooo

Mjadala na MS unajulikana hapa JF, tumekuwa naye miaka mingi. Vitabu vyake vimesaidia sana kufungua sehemu ya historia ambayo haikuwa wazi hasa kwa watu wa Pwani.

Lakini pia kupitia mijadala na MS, tuliweza kuonyesha uimara na udhaifu wa alichoandika, hasa kuonyesha matundu kwa nia njema ya kumsaidia na kusaidia wasomaji ambao wengi walibebwa na udini zaidi ya historia, wakashindwa kusoma between the lines, wakajenga chuki bila kujua

Nitakupa mfano. MS anasema baada ya Uhuru Nyerere aliwatupa wenzake wote aliokuwa nao katika harakati na aliowakuta katika harakati hasa Waislam.

Ni kweli kabisa, kwasababu hakuna mahali Abdul Sykes alionekana tena katika siasa baada ya Uhuru na wengine wengi. Apparently Nyerere ni mtu mbaya kwa wanaosoma tu bila kujua

Tulimuuliza MS, baada ya Uhuru, 98% ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya TANU walikuwa Waislam, nini ilikuwa role yao katika kukabiliana na mwenendo wa Mwalimu? MS hakuwa na jibu hata moja

Je, kwanini AMNUT na Abdul hawakufanikiwa? Kwanini hakuungwa mkono na Waislam katika hilo?

Akahamia kwenye EAMWS ilivyo uawa na Mwl. Tukamuuliza hayo yakitokea 98% ya halmashauri kuu ya TANU ilikuwa waislam, walifanya nini? Hakuwa na jibu.

Maswali haya si kupinga au kumkomoa MS, ilikuwa kumuonyesha matundu, kwamba, kuna chuki dhidi ya Nyerere, could be right or wrong, hata hivyo kuna matundu katika historia kwa kushindwa kuonyesha Halmashauri kuu na udhaifu uliopelekea Mwl kuwa na nguvu zaidi ya 98% ya wajumbe. Usaliti miongoni mwa wazee wake!!!

Mtu akiongozwa na prejudice ,reservations etc, anapunguza intellectual capacity, hawezi kuona tofauti
Mapungufu hayo yanakuwa compensated na fabrications and hyperbole.
Wazungu wanasema '' the devil is in the detail'' you will never see it if you don't read between the lines with sober mind
 
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,849
Points
1,500
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,849 1,500
Mkuu Zakumi, with due respect this is anachronism. Usiniwekee ''maneno mdomoni'' ndiyo maana hufanyi 'quote' ili iwe rahisi kumchanganya mtu anayesoma bila kujua nini kilisemwa (dishonest)
Nilichokieleza kuhusu Mohamed kimetoka katika kitabu chake nikionyesha 'contradiction'
Sijasema, nimekariri maneno ya kitabu na mijadala tuliyokuwa nayo na Mohamed. Nilimuuliza swali, ilikuwaje Nyerere akiwa katibu wa TAA Tabora alifika katika mkutano mkuu Dar, halafu Nyerere huyo huyo akaandikwa kufika Dar kwa mara ya kwanza 1953? wewe unajibu?

Nikauliza alipokuja katika mkutano mkuu ambao viongozi walikuwa akina Abdul hakukutana nao akiwa katibu wa Tawi kuu la Tabora? angalia kuna alama ya kuuliza, si kauli.
Haya yapo katika kitabu chake na mijadala, sikutafiti, sijaandika. Mohamed hakuwa na jibu!
Sijaandika anajulikana TAA.
Nilichosema ni kuwa akiwa katibu mkuu wa Tawi la Tabora, definite alijulikana. Kulikuwa na matawi mangapi? Tabora ilikuwa na nafasi gani? Again nilimuuliza mwanahistoria hakujibu. Hayo unayoandika na maneno yako
The same thing! Hakuna mahali nimeandika kuhusu unayosema hapo!
Nilichofanya ni nukuu ya kitabu ndiyo maana nimetumia neno ''critic' kwa kuonyesha kuna kitu kinahojiwa
Well, unamueleza Mwanahistoria si mimi. Mimi natumia kitabu kilichoandikwa

Pengine nikusaidie hoja, Mwl alizaliwa 1922, kwa miaka 30 unayosema ilikuwa mwaka 1952, mwaka mmoja kabla ya kupewa uongozi. Hii ni tafakuri tu na ndipo ninapoweza kuonyesha matundu ya hoja (between the lines)

Kitabu kinasema alikuwa katibu wa TAA Tabora. Na kitabu kinawataja akima Mwapachu ndio waliomshawishi kuingia siasa za TAA.

Sasa kama kuna Kambona hiyo ni sehemu ya historia unayotueleza pengine tusioijua.
Narudi kule kule maelezo yangu yanatokana na mijadala na kitabu cha MS Ahsante kwa maelezo, lakini haijawa hoja yangu popote pale

Naheshimu sana mawazo yako, hata hivyo ni vema ukifanya 'quote' kila unapojibu hoja badala ya kutunga maneno na kisha kusema ni yangu.

Udhaifu wangu ni ule ule kwamba, huwa siongozwi na grudge, naheshimu kazi ya mtu bila kujali dini, kabila au rangi. Kwangu ''intellect'' ni muhimu sana na hilo linanisaidia kutosoma vitu kama noval, kujenga hoja kwa mantiki na kubwa zaidi kutumia vizuri kaubongo kangu kadogooo

Mjadala na MS unajulikana hapa JF, tumekuwa naye miaka mingi. Vitabu vyake vimesaidia sana kufungua sehemu ya historia ambayo haikuwa wazi hasa kwa watu wa Pwani.

Lakini pia kupitia mijadala na MS, tuliweza kuonyesha uimara na udhaifu wa alichoandika, hasa kuonyesha matundu kwa nia njema ya kumsaidia na kusaidia wasomaji ambao wengi walibebwa na udini zaidi ya historia, wakashindwa kusoma between the lines, wakajenga chuki bila kujua

Nitakupa mfano. MS anasema baada ya Uhuru Nyerere aliwatupa wenzake wote aliokuwa nao katika harakati na aliowakuta katika harakati hasa Waislam.

Ni kweli kabisa, kwasababu hakuna mahali Abdul Sykes alionekana tena katika siasa baada ya Uhuru na wengine wengi. Apparently Nyerere ni mtu mbaya kwa wanaosoma tu bila kujua

Tulimuuliza MS, baada ya Uhuru, 98% ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya TANU walikuwa Waislam, nini ilikuwa role yao katika kukabiliana na mwenendo wa Mwalimu? MS hakuwa na jibu hata moja

Je, kwanini AMNUT na Abdul hawakufanikiwa? Kwanini hakuungwa mkono na Waislam katika hilo?

Akahamia kwenye EAMWS ilivyo uawa na Mwl. Tukamuuliza hayo yakitokea 98% ya halmashauri kuu ya TANU ilikuwa waislam, walifanya nini? Hakuwa na jibu.

Maswali haya si kupinga au kumkomoa MS, ilikuwa kumuonyesha matundu, kwamba, kuna chuki dhidi ya Nyerere, could be right or wrong, hata hivyo kuna matundu katika historia kwa kushindwa kuonyesha Halmashauri kuu na udhaifu uliopelekea Mwl kuwa na nguvu zaidi ya 98% ya wajumbe. Usaliti miongoni mwa wazee wake!!!

Mtu akiongozwa na prejudice ,reservations etc, anapunguza intellectual capacity, hawezi kuona tofauti
Mapungufu hayo yanakuwa compensated na fabrications and hyperbole.
Wazungu wanasema '' the devil is in the detail'' you will never see it if you don't read between the lines with sober mind
I have a full time job. Hivyo siwezi kuiga mifano yako ya ku-quote na kujibu.

Katika posti yangu ya mwisho nilikuwa naonyesha kuwa Nyerere alipokuwa na umri kati ya miaka 0-30, alikuwa professional student na michango yake kwa TAA ulikuwa mdogo sana na wa kutojulikana.

Na vilevile aliporudi kutoka masomoni alitaka kuanzisha chama chake.

Hivyo kutokana na hizi conditions mbili, mtu yoyote mwenye hekima anaweza kukubali kuwa alishauriwa kujiunga na TAA.

Kwa maneno yake mwenyewe Nyerere, anasema TAA kilikuwa ni chama cha starehe.

Swala sio kumchukia Nyerere. Swala ni kuwa tuna haki ya kikatiba na kibinadamu kuwa na mtazamo tofauti kuhusu Nyerere.

Utaifa wangu haukuja kwa sababu Nyerere alitoa mchango mkubwa kwa TANZANIA. Utaifa wangu ni wa kuzaliwa.
 
Forum statistics

Threads 1,296,486
Members 498,655
Posts 31,249,917
Top