Thank God for giving us Magufuli aka Jiwe aka Chuma!

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,498
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,498 2,000
Kushindikana kuandikwa kwa katiba mpya baada ya kazi za muda mrefu sana iliyofanywa na Tume wa Warioba lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa nchi.

Hali hiyo ilitokana na katiba hiyohiyo inayompa rais madaraka ya kuamua lolote, na ndiyo aliyotumia Kikwete kuunda tume hiyo, halafu akayatumia pia kuua muendelezo huo wa kuandikwa kwa katiba mpya.

Swala la kurekebishwa kwa Katiba mpya lilitakiwa lianzie bungeni kusudi liwe na nguvu ya kisheria, siyo kuwa ni utashi wa rais tu.
Nakubaliana nawe 100%. Nakumbuka JK alipotanganza ile Dec kuanza kwa mchakato wa katiba, Wapinzani walimpongeza kwa hatua hiyo. Lile lilikuwa kosa na tuliwatahadharisha
1. Tuliwaambia ili mchakato ufanikiwe ni lazima uondoke katika mikono ya CCM ambao hawakutaka suala hilo
Niliwaeleza hapa jamvini, hoja ilitakiwa kwenda Bungeni ili ipate uhalali tu wa kisheria na si vinginevyo
Kisha, ilitakiwa mchakato mzima utazamwe na mkutano wa kitaifa ili kuondoa uCCM
Katika hilo Bunge la Katiba lisingehusu CCM kama ilivyokuwa kwa katiba ya 1977 n.k.
2. Kwasababu namba 1 haukizingatiwa, CCM wakatumia nguvu yao kisiasa na si kiuzalendo na nchi kuupiga ngwara mchakato mzima. Na Rais alitishwa na CCM na kwavile alikuwa na nguvu akanywea

Kuharibika kwa mchakato wa katiba kwa sehemu kubwa sana kulichangiwa na Wapinzani kutoelewa mchezo wa siasa za CCM na kuamini kuwa CCM ni Wazalendo wanaoweza kufanya nao kazi, siyo!
 
Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,703
Points
2,000

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,703 2,000
Mkuu Kichuguu, long time Mkuu. Tume miss sana michango yako kama huu
Nakubaliana nawe 98% ya uliyoeleza. Ninatofautiana nawe kwa hizo 2% katika hayo niliyo bold hapo juu
Rais kutumia madaraka yake yote kwa mujibu wa katiba kama alivyopewa siyo tatizo na si sidhani ni hoja
Hoja ni kwamba je, matumizi hayo yanatumika kama yalivyoaanishwa na katiba? Kwa malkia wanasema 'to the letter''. Hapa naomba nitoe mifano
- Sioni tatizo kama Rais atasaini wafungwa wote waliohukumiwa kifo kunyongwa siku moja. Katiba inamruhusu
-Sioni tatizo kama Rais atatumia 'decree au executive order' kwa mambo kama yalivyoanishwa kikatiba, sioni!
-Leo akiamua kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi sioni tatizo. Katiba inamruhusu
-Sioni tatizo kama wateule wake watakuwa watu wa familia yake na majirani. Katiba inamruhusu

Naoliona tatizo ikiwa Rais atatumia mamlaka na madaraka yake kutenda jambo nje ya katiba
Kwa mfano, ikiwa katiba na sheria za nchi zinaruhusu jambo, na Rais akatumia madaraka yake yote ya kikatiba kulizuia jambo hilo bila kutumia sheria zinazompa madaraka hayo , hapo kuna tatizo na si suala la 'madaraka yote aliyopewa na katiba'
Ukiisoma katiba hiyo kwa makini, utagundua kuwa haiweki limit ya jinsi rais atakavyotumia madaraka yake hayo. Katiba yote inategemea zaidi busara na hekima za rais kuamua namna ya kuyatumia vizuri. Madaraka mengine yametolewa indirectly kabisa; kwa mfano katiba hiyo inamruhusu rais kuingilia mamlaka ya bunge!
 
Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,856
Points
1,500

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,856 1,500

Kichuguu za mwaka mpya. Kwa kuongezea point yako ya mwanzo na hii. Kuna matatizo ya kimuundo ambayo kwa kiasi kubwa inachangiwa na mapungufu ya kikatiba. Lakini pamoja na mapungufu ya kikatiba, kwa maoni yangu kuna mapungufu ya kimwamko (enlightenment) ndani ya jamii yetu. Huwezi kuwa na jamii isiyo na mwamko na ikaja kuwa na katiba nzuri. na huwezi kuwa na jamii isiyo na mwamko na ikadai ubora (excellence ) kutoka kwa viongozi wake.

Awali umesema matatizo ya 1983, yalisababisha mfumo mbovu unaoendelea mpaka sasa. Hupo sahihi na uchambuzi wako. Hila naona matatizo haya yalianza mapema zaidi ya hapo. Kulikuwa na matatizo ya kiuchumi yaliyokuwa nje ya uwezo wa Tanzania. Lakini vilevile kulikuwa na matatizo ya kimuundo ambayo nchi ilishindwa kuyafanyia kazi.

Moja ya matatizo ya kimuundo: siasa ilikumba kila nyanja ya jamii na uchumi. Na ulifika wakati tuliamini kuwa siasa yetu ilikuwa ni bora kuliko miundo mingine ya siasa duniani. Katiba ya nchi ilikuwa haina nguvu kama katiba ya chama. Vikao vya chama vilikuwa vina nguvu kuliko mamlaka za kiserikali. Kibaya zaidi katiba ya nchi ilifanyiwa marekebisho hili ikidhi itikadi za chama.

Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi yaliyotoka Ulaya Mashariki mwanzoni mwa 90 hayakutegemea na Tanzania haikujitayarisha na mabadiliko hayo. Kwa mfano kulikuwa na watu wengi walioacha taaluma zao na kujikita kwenye siasa. Ghafla bin vuu, hawa hawakuwa na hoja.
 
Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,856
Points
1,500

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,856 1,500
Nakubaliana nawe 100%. Nakumbuka JK alipotanganza ile Dec kuanza kwa mchakato wa katiba, Wapinzani walimpongeza kwa hatua hiyo. Lile lilikuwa kosa na tuliwatahadharisha
1. Tuliwaambia ili mchakato ufanikiwe ni lazima uondoke katika mikono ya CCM ambao hawakutaka suala hilo
Niliwaeleza hapa jamvini, hoja ilitakiwa kwenda Bungeni ili ipate uhalali tu wa kisheria na si vinginevyo
Kisha, ilitakiwa mchakato mzima utazamwe na mkutano wa kitaifa ili kuondoa uCCM
Katika hilo Bunge la Katiba lisingehusu CCM kama ilivyokuwa kwa katiba ya 1977 n.k.
2. Kwasababu namba 1 haukizingatiwa, CCM wakatumia nguvu yao kisiasa na si kiuzalendo na nchi kuupiga ngwara mchakato mzima. Na Rais alitishwa na CCM na kwavile alikuwa na nguvu akanywea

Kuharibika kwa mchakato wa katiba kwa sehemu kubwa sana kulichangiwa na Wapinzani kutoelewa mchezo wa siasa za CCM na kuamini kuwa CCM ni Wazalendo wanaoweza kufanya nao kazi, siyo!
Toka siasa za vyama vingi zianze. Wapinzani (na wanasiasa kutoka CCM) wamegombea nafasi mbali mbali bila kusoma na kujua katiba ya nchi. Sidhani kama Mrema alisoma na kujua katiba ya nchi wakati alipogombea mwaka 1995.

Wengi wanagombea kwa kutumia umaarufu wao. Na kama wangejua mapungufu ya kikatiba basi wasingejaribu kuingia kwenye uchaguzi wa 1995 na kuendelea.

Pili, pamoja na mapungufu yake, katiba sio tatizo. Waingereza hawana katiba iliyoandikwa. Lakini wanafuata taratibu walizojiwekea. Leo waziri mkuu akishindwa kura ya maoni, anaondoka haraka na kumwachia mwingine. Na yakitokea matatizo wanakwenda mahakama kupata sheria. Kwa maneno mengine wanavyo taasisi na vyombo vinavyolinda katiba.

Tanzania hakuna taasisi inayolinda katiba. Vitu vinafanyika kwa hekima na busara za Rais, kwa kuheshimiana au kwa ubabe. Kwa mfano ya Tanzania inasema mwenyekiti wa tume ya uchaguzi akishatangaza matokeo ya urais, matokeo hayatenguliwi. Lakini ndani ya katiba hiyo hiyo, wananchi wapewa haki ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao. Hivyo si sahihi kwa tume kumpa urais mgombea ambaye hakuchaguliwa na wananchi.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,498
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,498 2,000
"Zakumi, post: 29963705, member: 12016"]Toka siasa za vyama vingi zianze. Wapinzani (na wanasiasa kutoka CCM) wamegombea nafasi mbali mbali bila kusoma na kujua katiba ya nchi.
Sidhani kama Mrema alisoma na kujua katiba ya nchi wakati alipogombea mwaka 1995
Nakubaliana, na inaonekana hawakuweza kukaa na kutafakari. Laiti wangekaa chini na kujiuliza nini kilitokea Zanzibar mara zaidi ya 3 wangetambua tatizo si kura au kupata kura, ni endapo kura hizo zinathamani
Na kama wangejua mapungufu ya kikatiba basi wasingejaribu kuingia kwenye uchaguzi wa 1995 na kuendelea.
Wana matumaini hisani iliyotokea Zambia na Kenya inaweza kutokea Tanzania
Pili, pamoja na mapungufu yake, katiba sio tatizo. Waingereza hawana katiba iliyoandikwa. Lakini wanafuata taratibu walizojiwekea. Leo waziri mkuu akishindwa kura ya maoni, anaondoka haraka na kumwachia mwingine. Na yakitokea matatizo wanakwenda mahakama kupata sheria. Kwa maneno mengine wanavyo taasisi na vyombo vinavyolinda katiba.
Sidhani kama ni uwezo wa kwenda mahakamani.
Kiwango cha elimu kwa wananchi ni kikubwa mno. Leo utasikia Labour wanatawala, kesho conservative n.k
Wananchi wanachagua sera si vyama ili kuleta mabadiliko katika maisha yao
Ukiangalia wanavyojadili Brexit, iwe kwa namna yoyote kuna jambo moja utakalojifunza, wanajielewa
Tanzania hakuna taasisi inayolinda katiba.
Hii ni siri kubwa wengi hawaijui
Vyombo vya kulinda katiba ni sehemu ya utawala, kinachoonekana ni kiini macho
Kupingwa rasimu ya Warioba na CCM si kwamba CCM hawaoni tatizo lililopo, wanaliona sana
Hofu yao ni kuwa kufumua katiba hii kutajenga mazingira ya wazi ya mifumo inayolinda katiba
Katika hilo CCM wanatambua hawawezi kusimama kidete tena
Kwa mfano ya Tanzania inasema mwenyekiti wa tume ya uchaguzi akishatangaza matokeo ya urais, matokeo hayatenguliwi.
Kwa maana kuwa Mwenyekiti wa tume ana ''kura'' na uwezo mkubwa kuliko wapiga kura.

Ni suala la yeye kutaka nani awe nani asiwe. Hana shaka na gharama za hatua hizo
Ndiyo maana hapo juu nimeeleza, suala si kura ni thamani ya kura kama kweli ipo
Lakini ndani ya katiba hiyo hiyo, wananchi wapewa haki ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao.
Hivyo si sahihi kwa tume kumpa urais mgombea ambaye hakuchaguliwa na wananchi
Hoja isiyo na majibu ni kama tume ya uchaguzi ipo huru. Tuliona uchaguzi uliopita Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais alibadilisha wajumbe wa tume siku chache kabla ya uchaguzi! Majibu yalikuwa rahisi, Rais ana mamlaka hayo

Yaani motive ya kubadilisha na muda haikuwa na nguvu kuliko mamlaka aliyopewa Rais
Ikitokea tume ya uchaguzi ikaitwa katika mdahalo na kuulizwa kama ipo huru, nina uhakika mdahalo utaishia hapo

Tume inachaguliwa na M/Kiti wa CCM ambaye ni Rais. Uteuzi hauhojiwi ni chombo chochote kile
Haiwajibiki kwa chombo kingine chochote kile na haiwezi kushtakiwa popote pale
Maana yake ni moja, Tume inawajibika kwa aliyeiunda na inalindwa na aliyeiunda
 
Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,703
Points
2,000

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,703 2,000
Kichuguu za mwaka mpya. Kwa kuongezea point yako ya mwanzo na hii. Kuna matatizo ya kimuundo ambayo kwa kiasi kubwa inachangiwa na mapungufu ya kikatiba. Lakini pamoja na mapungufu ya kikatiba, kwa maoni yangu kuna mapungufu ya kimwamko (enlightenment) ndani ya jamii yetu. Huwezi kuwa na jamii isiyo na mwamko na ikaja kuwa na katiba nzuri. na huwezi kuwa na jamii isiyo na mwamko na ikadai ubora (excellence ) kutoka kwa viongozi wake.

Awali umesema matatizo ya 1983, yalisababisha mfumo mbovu unaoendelea mpaka sasa. Hupo sahihi na uchambuzi wako. Hila naona matatizo haya yalianza mapema zaidi ya hapo. Kulikuwa na matatizo ya kiuchumi yaliyokuwa nje ya uwezo wa Tanzania. Lakini vilevile kulikuwa na matatizo ya kimuundo ambayo nchi ilishindwa kuyafanyia kazi.

Moja ya matatizo ya kimuundo: siasa ilikumba kila nyanja ya jamii na uchumi. Na ulifika wakati tuliamini kuwa siasa yetu ilikuwa ni bora kuliko miundo mingine ya siasa duniani. Katiba ya nchi ilikuwa haina nguvu kama katiba ya chama. Vikao vya chama vilikuwa vina nguvu kuliko mamlaka za kiserikali. Kibaya zaidi katiba ya nchi ilifanyiwa marekebisho hili ikidhi itikadi za chama.

Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi yaliyotoka Ulaya Mashariki mwanzoni mwa 90 hayakutegemea na Tanzania haikujitayarisha na mabadiliko hayo. Kwa mfano kulikuwa na watu wengi walioacha taaluma zao na kujikita kwenye siasa. Ghafla bin vuu, hawa hawakuwa na hoja.
Mkuu Zakumi, kukosekana kwa huo mwamko ndiko nilikojaribu kueleza kuwa ni kutokana na watu kuzowea maisha ya kimkato mkato, na ndiyo inayokamilisha hilo duara jeuri!!
 
Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,703
Points
2,000

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,703 2,000
Nakubaliana, na inaonekana hawakuweza kukaa na kutafakari. Laiti wangekaa chini na kujiuliza nini kilitokea Zanzibar mara zaidi ya 3 wangetambua tatizo si kura au kupata kura, ni endapo kura hizo zinathamani
Wana matumaini hisani iliyotokea Zambia na Kenya inaweza kutokea Tanzania
Sidhani kama ni uwezo wa kwenda mahakamani.
Kiwango cha elimu kwa wananchi ni kikubwa mno. Leo utasikia Labour wanatawala, kesho conservative n.k
Wananchi wanachagua sera si vyama ili kuleta mabadiliko katika maisha yao
Ukiangalia wanavyojadili Brexit, iwe kwa namna yoyote kuna jambo moja utakalojifunza, wanajielewa
Hii ni siri kubwa wengi hawaijui
Vyombo vya kulinda katiba ni sehemu ya utawala, kinachoonekana ni kiini macho
Kupingwa rasimu ya Warioba na CCM si kwamba CCM hawaoni tatizo lililopo, wanaliona sana
Hofu yao ni kuwa kufumua katiba hii kutajenga mazingira ya wazi ya mifumo inayolinda katiba
Katika hilo CCM wanatambua hawawezi kusimama kidete tenaKwa maana kuwa Mwenyekiti wa tume ana ''kura'' na uwezo mkubwa kuliko wapiga kura.

Ni suala la yeye kutaka nani awe nani asiwe. Hana shaka na gharama za hatua hizo
Ndiyo maana hapo juu nimeeleza, suala si kura ni thamani ya kura kama kweli ipo
Hoja isiyo na majibu ni kama tume ya uchaguzi ipo huru. Tuliona uchaguzi uliopita Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais alibadilisha wajumbe wa tume siku chache kabla ya uchaguzi! Majibu yalikuwa rahisi, Rais ana mamlaka hayo

Yaani motive ya kubadilisha na muda haikuwa na nguvu kuliko mamlaka aliyopewa Rais
Ikitokea tume ya uchaguzi ikaitwa katika mdahalo na kuulizwa kama ipo huru, nina uhakika mdahalo utaishia hapo

Tume inachaguliwa na M/Kiti wa CCM ambaye ni Rais. Uteuzi hauhojiwi ni chombo chochote kile
Haiwajibiki kwa chombo kingine chochote kile na haiwezi kushtakiwa popote pale
Maana yake ni moja, Tume inawajibika kwa aliyeiunda na inalindwa na aliyeiunda
Mkuu Nguruvi3 uko correct kabisa kwa analysis hii, ila chimbuko la yote ni kukosekana kwa katiba inayotoa dira nzuri ya nchi bila kujali chama au mtu aliyeko madarakani.
 
Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,856
Points
1,500

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,856 1,500
Mkuu Nguruvi3 uko correct kabisa kwa analysis hii, ila chimbuko la yote ni kukosekana kwa katiba inayotoa dira nzuri ya nchi bila kujali chama au mtu aliyeko madarakani.
Wakati Mwalimu Nyerere alipokuwa hai, kubadilisha katiba ilikuwa ni kama kufanya njama za kufuta legacy yake. Hivyo hakuna aliyejaribu jambo hilo bila kupata baraka zake. Katiba ya sasa ilikuwa ni framework ya kujenga nchi ya kijamaa na chama kimoja. Ilikuwa ni nyongeza ya katiba ya CCM na Azimio la Arusha. Tukitaka katiba itakayokidhi mahitaji na wakati wa sasa, ni lazima legacy za Ujamaa, Chama kimoja na Azimio la Arusha viwekwe kando.

Pamoja na legacy za mwalimu, CCM ni chama cha wanasiasa wa kulipwa. Katiba ya kweli itawafanya CCM kupoteza nguvu na kukosesha kazi watu waliozoea kupata ulaji kupitia CCM. Sababu ya CCM kuvumiliana, sio kuonyesha upevu wa kisiasa. Bali kusubiriana hili wale kwa zamu.
 
Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,856
Points
1,500

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,856 1,500
Mkuu Zakumi, kukosekana kwa huo mwamko ndiko nilikojaribu kueleza kuwa ni kutokana na watu kuzowea maisha ya kimkato mkato, na ndiyo inayokamilisha hilo duara jeuri!!
Mchambuzi wako unasoma mawazo yangu. Nilipokuwa shule, wenzangu walikuwa wanaangalia nafasi za juu kama chanzo cha kuleta mabadiliko (Top down approach). Kwa upande wangu, niliangalia kwa kuanzia chini na nilipopata nafasi nilianza kusaidia jamaa zangu walio chini wanyanyuke kielimu na kibiashara. Katika kipindi cha miaka kumi za experiments zangu, nimehitimisha kuwa hawa watu wa chini wana nia na tamaa zilezile kama wale waliopo katika ngazi za juu au tunaowaita mafisadi. Kila mtu anataka short cuts.

Kuhusu Magufuli, pamoja kwamba Magufuli ana mapungufu yake, nadhani ni kiongozi muafaka kwa katiba na muundo wa kiserikali uliopo sasa. Katiba ya sasa na muundo huu wa serikali, Magufuli ni bora kuliko Nyerere. Hii ni kwa sababu katiba na muundo wa kiserikali wa sasa, unampa rais madaraka makubwa hili afanye kama anavyopenda kwa manufaa ya watu. Ni Magufuli pekee yake anayefanya mabadiliko kama anavyopenda.

Pia, Magufuli anachukua majukumu ya kile anachofanya (takes ownership). Viongozi waliomtangulia walikuwa hawachukui majukumu ya maamuzi yao. Mtu anatangaza Azimio la Arusha lakini na baadaye atasema haya ni maazimio ya chama au kamati kuu imesema hivi na vile.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,498
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,498 2,000
"Zakumi, post: 29975965, member: 12016"]Wakati Mwalimu Nyerere alipokuwa hai, kubadilisha katiba ilikuwa ni kama kufanya njama za kufuta legacy yake. Hivyo hakuna aliyejaribu jambo hilo bila kupata baraka zake.
Mkuu kuna wakati namwelewa Mwalimu Nyerere hasa kuhusu katiba
Mwl alipochukua nchi ni kama mtu aliyekadhiwa kijiji kisicho na shule

Kazi ya kwanza ilikuwa kujenga utaifa, kisha kuwaunganisha watu.

Tunaweza kutokubaliana na sera zake nyingi lakini ukweli utabaki pale pale yapo aliyoyafanya tusiyoyaona na tusiyoyajua ndiyo yanatuweka tuwe kama tulivyo

Nchi ikipata uhuru ilikuwa na makabila 120 na dini mbali mbali.

Kazi ya kuunganisha watu haikuwa rahisi, ilihitaji mwelekeo na kuvumiliana
Leo miaka 50 tunaona matatizo Kenya na kwingine ambako makabila si zaidi ya 30

Nigeria imekuwa katika mapinduzi kuanzia Nandi Azikiwe hadi leo hii.

Katika miaka 50 tu iliyopita nchi hiyo haikuwa na utulivu licha ya utajiri wa mafuta, watu na rasilimali nyingine. Tunaona tofauti za udini na ukabila 'in black and white'

Ukitaka kuona matatizo yaliyokuwepo na ambayo kama Mwalimu asingekuwa imara yangetuacha baya ni ''1964 Mutiny', askari hawakujua wanataka nini

Kwamba sasa mzungu kaondoka ni wakati wao, jaribio lililoshindwa
Kuundwa kwa Azimio la Arusha ilikuwa ni sehemu ya suluhu ya ''Africanization'

Hivyo Mwl alihitaji katiba itakayompa madaraka makubwa ili kukabili upinzani uliotishia utaifa. Hilo kama ni kosa au la ni suala la mjadala

Hata hivyo miaka mingi baadaye Mwl alionekana kuridhika na uwezo wa watu kuhimili vishindo vya siasa za upinzani. Tena ukianzia ndani ya chama chake

Upinzani ukianza ali 'set tone nzuri' sana. Unakumbuka aliposema 'mtu abebwe kuna kosa gani? Unakumbuka aliposema maandamano yana matatizo gani

Ni 'tone hiyo' ndiyo iliwazuia waliofuata kukubali siasa za ushindani bila kuhasimiana
Tukitaka katiba itakayokidhi mahitaji na wakati wa sasa, ni lazima legacy za Ujamaa, Chama kimoja na Azimio la Arusha viwekwe kando.
Haya mambo yamewekwa kando siku nyingi sana.

Ujamaa haupo ulifutika wakati wa Mwinyi , Mkapa akapigilia msumari na akina JK wakasawazisha tu

Azimio la Arusha lilipigwa mweleka kule Zanzibar siku nyingi na ndilo chimbuko la ubadhirifu na ufujaji wa mali za umma. Chama kimoja kilifutwa baada ya upinzani

Hata hivyo CCM ni wazuri sana wa kutumia hoja za ujamaa, Azimio na chama kimoja pale ambapo masilahi yao yanapokuwa matatani

Ni kama wanavyomtumia Mwalimu pale wanapohitaji kujenga hoja na si kumuezi

Ukiwakusanya CCM katika kamati kuu , Halmashauri kuu na makada wazoefu ukauliza nini itikadi ya chama, nakuhakikishia utapata itikadi tofauti zaidi ya 100 kwa saa 1.

Hakuna anayeweza kueleza nini chama kinasimamia
Pamoja na legacy za mwalimu, CCM ni chama cha wanasiasa wa kulipwa. Katiba ya kweli itawafanya CCM kupoteza nguvu na kukosesha kazi watu waliozoea kupata ulaji kupitia CCM. Sababu ya CCM kuvumiliana, sio kuonyesha upevu wa kisiasa. Bali kusubiriana hili wale kwa zamu
Absolutely! Ni chama ambacho ima unasubiri muda wako au unataka masilahi yako yalindwe

Sababu kubwa ya kuipiga vita rasimu ya Warioba na kutotaka kuzungumzia katiba ni hofu ya kupoteza madaraka, nadhani si kukosa nguvu haipo hata muda huu.

Nguvu ya CCM imebaki katika kulindwa na dola ni si wanachama
Rais Kikwete aliwaambia wazi, ni lazima chama kipendwe na si kulindwa
 
Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,856
Points
1,500

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,856 1,500
Nakubaliana, na inaonekana hawakuweza kukaa na kutafakari. Laiti wangekaa chini na kujiuliza nini kilitokea Zanzibar mara zaidi ya 3 wangetambua tatizo si kura au kupata kura, ni endapo kura hizo zinathamani
Wana matumaini hisani iliyotokea Zambia na Kenya inaweza kutokea Tanzania
Sidhani kama ni uwezo wa kwenda mahakamani.
Kiwango cha elimu kwa wananchi ni kikubwa mno. Leo utasikia Labour wanatawala, kesho conservative n.k
Wananchi wanachagua sera si vyama ili kuleta mabadiliko katika maisha yao
Ukiangalia wanavyojadili Brexit, iwe kwa namna yoyote kuna jambo moja utakalojifunza, wanajielewa
Hii ni siri kubwa wengi hawaijui
Vyombo vya kulinda katiba ni sehemu ya utawala, kinachoonekana ni kiini macho
Kupingwa rasimu ya Warioba na CCM si kwamba CCM hawaoni tatizo lililopo, wanaliona sana
Hofu yao ni kuwa kufumua katiba hii kutajenga mazingira ya wazi ya mifumo inayolinda katiba
Katika hilo CCM wanatambua hawawezi kusimama kidete tenaKwa maana kuwa Mwenyekiti wa tume ana ''kura'' na uwezo mkubwa kuliko wapiga kura.

Ni suala la yeye kutaka nani awe nani asiwe. Hana shaka na gharama za hatua hizo
Ndiyo maana hapo juu nimeeleza, suala si kura ni thamani ya kura kama kweli ipo
Hoja isiyo na majibu ni kama tume ya uchaguzi ipo huru. Tuliona uchaguzi uliopita Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais alibadilisha wajumbe wa tume siku chache kabla ya uchaguzi! Majibu yalikuwa rahisi, Rais ana mamlaka hayo

Yaani motive ya kubadilisha na muda haikuwa na nguvu kuliko mamlaka aliyopewa Rais
Ikitokea tume ya uchaguzi ikaitwa katika mdahalo na kuulizwa kama ipo huru, nina uhakika mdahalo utaishia hapo

Tume inachaguliwa na M/Kiti wa CCM ambaye ni Rais. Uteuzi hauhojiwi ni chombo chochote kile
Haiwajibiki kwa chombo kingine chochote kile na haiwezi kushtakiwa popote pale
Maana yake ni moja, Tume inawajibika kwa aliyeiunda na inalindwa na aliyeiunda
Nguruvi3:

Vitu vyote vizuri tunavyoviona duniani havikuporomoka kutoka mbinguni kama chakula cha wana wa Israeli. Vitu vingine ni utamaduni wa kujijengea na haviusiani sana na uwezo mkubwa wa kielimu.

Nilifanya utafiti wa kulinganisha katiba ya Tanzania na Marekani. Wakati wamarekani wanatunga katiba yao zaidi ya miaka 200 iliyopita, watungaji wengi walikuwa na elimu ya kujiendeleza wenyewe. Kwa mfano Benjamin Franklin alienda shule rasmi kwa miaka miwili tu. Hata Harvard University, ilikuwa haitohi elimu ya kiwango kikubwa. Hivyo kielimu pekee yake, watanzania wa sasa wanaelimu kubwa kuliko wamarekani wa miaka 200 iliyopita.

Tofauti kubwa ni mwamko. Sisi tunasoma uli upate kazi ya ajira na wenzetu walisoma hili wapate mwamko. Bunge la katiba la Tanzania lilikuwa na wasomi kuliko wamarekani waliokutana Philadephia kuandika katiba. Wabunge wa bunge la katiba walikwenda kulipwa na hawakujali matokeo ya kazi yao. Wakati watunzi wa katiba ya Marekani walifanya kazi wakijua wanaandika historia ya nchi yao.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,498
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,498 2,000
Lakini pamoja na mapungufu ya kikatiba, kwa maoni yangu kuna mapungufu ya kimwamko (enlightenment) ndani ya jamii yetu. Huwezi kuwa na jamii isiyo na mwamko na ikaja kuwa na katiba nzuri. na huwezi kuwa na jamii isiyo na mwamko na ikadai ubora (excellence ) kutoka kwa viongozi wake.
Hili ni tatizo kubwa kuliko katiba yenyewe
Watanzania si kuwa wanataka njia za mkato, ingalikuwa hivyo wangetumia njia hizo kupata katiba. Watanzania ni watu wanaosubiri kila kitu 'in silver plate'
 
Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,498
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,498 2,000
Bunge la katiba la Tanzania lilikuwa na wasomi kuliko wamarekani waliokutana Philadephia kuandika katiba. Wabunge wa bunge la katiba walikwenda kulipwa na hawakujali matokeo ya kazi yao. Wakati watunzi wa katiba ya Marekani walifanya kazi wakijua wanaandika historia ya nchi yao.
Hii ni hoja inayopaswa kuzungumzwa sasa hivi
Tunapoambiwa hakuna pesa za kusimamia mchakato wa katiba, inashangaza

Katiba ni nyaraka na tunu ya nchi. Ni chombo cha juu kabisa kinachoeleza Uzalendo

Tuna wasomi na wananchi wenye uelewa kuliko wakati mwingine
Mchakato wa katiba ufanywe kwa Uzalendo bila kutanguliza pesa

Kinachoitajiwa sasa hivi ni mchakato na uitishwe kwa mbiu ya Uzalendo
Kwamba watakaoshiriki watapewa vitendea kazi na si malipo kama ule ''uvundo''

Hatuhitaji sana wasomi, tnahitaji watu wenye weledi,mapenzi na nchi na wazalendo

Mchakato unawezekana bila pesa na hilo ndilo liwe kipimo cha 'uzalendo'
 
Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,856
Points
1,500

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,856 1,500
Mkuu kuna wakati namwelewa Mwalimu Nyerere hasa kuhusu katiba
Mwl alipochukua nchi ni kama mtu aliyekadhiwa kijiji kisicho na shule

Kazi ya kwanza ilikuwa kujenga utaifa, kisha kuwaunganisha watu.

Tunaweza kutokubaliana na sera zake nyingi lakini ukweli utabaki pale pale yapo aliyoyafanya tusiyoyaona na tusiyoyajua ndiyo yanatuweka tuwe kama tulivyo

Nchi ikipata uhuru ilikuwa na makabila 120 na dini mbali mbali.

Kazi ya kuunganisha watu haikuwa rahisi, ilihitaji mwelekeo na kuvumiliana
Leo miaka 50 tunaona matatizo Kenya na kwingine ambako makabila si zaidi ya 30
Nguruvi3:

Ni kweli tulikuwa backward. Lakini katiba ilianza kuaribiwa kwa design na sio kwa sababu Nyerere alikabidhiwa kijiji kisicho na shule. Hivi ni visingizio tu baada ya watu kushindwa kazi.

Mwingereza hakutoa uhuru moja kwa moja. Alianza na madaraka ya ndani ambayo yaliandaa watu kupata uhuru. Hivyo uhuru tulipopata, tulikabidhiwa bandera na katiba. Tatizo ni kwamba kila kiongozi wa kiAfrika alitaka kuacha uwaziri mkuu na kuwa raisi hili asipingwe na bunge na kuwa na madaraka makubwa.

Kwa mfano Robert Mugabe alirudia vilevile walivyofanya viongozi wengine na yeye hakuachiwa kijiji kisicho na shule. Nkwame Nkrumah alikuwa waziri kiongo kwa miaka mitano kabla Ghana kupata uhuru kamili. Na Ghana ilipopata uhuru alianza kupangua pangua katiba hili awe na madaraka mengi.

Kama anavyosema Kichuguu, katiba iwe dira ya kuwaongoza watu bila kujali itikadi za chama na isitungwe na walio madarakani.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,498
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,498 2,000
Ni kweli tulikuwa backward. Lakini katiba ilianza kuaribiwa kwa design na sio kwa sababu Nyerere alikabidhiwa kijiji kisicho na shule.
Mtu anayeharibu 'design' si tatizo
Tatizo ni je, kulikuwa na watu waliom 'challenge'? Jibu ni hapana
Hilo tunaliona kuanzia katiba ya Uhuru 1961, ya mpito 1964 na 1977

Nilikupa mfano wa 1964 Mutiny, kwamba, askari pengine waliokuwa na fursa ya kufanya mabadiliko walijikita kupinga kwanini wanaongozwa na Mzungu Kwanini hawapewi vyeo

Hili la Nyerere niliweka wazi, tunaweza kuwa na mitazamo mbali mbali kuhusu kufanikiwa au kufeli kwake.

Tusichoweza kupingana ni suala la kutujengea Utaifa kama tulivyo leo
Ni ukweli kuwa alifanya kazi katika mazingira yasiyo na rasilimali watu
 
Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,856
Points
1,500

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,856 1,500
Mtu anayeharibu 'design' si tatizo
Tatizo ni je, kulikuwa na watu waliom 'challenge'? Jibu ni hapana
Hilo tunaliona kuanzia katiba ya Uhuru 1961, ya mpito 1964 na 1977

Nilikupa mfano wa 1964 Mutiny, kwamba, askari pengine waliokuwa na fursa ya kufanya mabadiliko walijikita kupinga kwanini wanaongozwa na Mzungu Kwanini hawapewi vyeo

Hili la Nyerere niliweka wazi, tunaweza kuwa na mitazamo mbali mbali kuhusu kufanikiwa au kufeli kwake.

Tusichoweza kupingana ni suala la kutujengea Utaifa kama tulivyo leo
Ni ukweli kuwa alifanya kazi katika mazingira yasiyo na rasilimali watu
Tanganyika ilipopata uhuru ilikuwa na utaifa. Hatukuwa tumeganyika. Hata makabila makubwa ya Tanganyika hayakuwa na vyama vyao tofauti vya kisiasa. Haya mambo ya kuwa utaifa umejengwa baada ya kupata uhuru yanatoka wapi?

CCM na wale wasiotaka mabadiliko ya kweli siku zote wanatumia hoja ya utaifa kutofanya mabadiliko. Utaifa tulikuwa nao kwa sababu ya lugha moja na makabila madogo madogo yasio na mvutano.

Changamoto za Tanzania sio utaifa. Na utaifa haikuwa changamoto wakati tumepata uhuru.

Kama utaifa sio changamoto yetu, ni nini chagamoto yetu. Kwa maoni wangu changamoto kubwa ni mfumo mbovu wa kisiasa na uongozi ambao umeshindwa kunyanyua jamii kwa kutumia utaifa na amani iliyokuwepo.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,498
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,498 2,000
"Zakumi, post: 30000075, member: 12016"]Tanganyika ilipopata uhuru ilikuwa na utaifa. Hatukuwa tumeganyika.
Mkuu utaifa ulikuwepo, kuujenga ni kitu tofauti kidogo
Nigeria walikuwa na utaifa kama ilivyo Kenya, Cameroon, Rwanda , Burundi n.k.
Swali ni je, hali yao ipoje sasa kwa kuzingatia utaifa wao kama ulivyokuwa wetu?

Ni kweli hatukuwa tumegawanyika kwasababu haikuonekana hadharani.
Sote tulikuwa katika minyororo ya Mjerumani na Mwingereza tukililia hali zetu.

Baada ya uhuru tofauti zingelikuwa wazi kama kungekuwa hakuna mtu wa kuzingalia.

Tofauti ni kama ile ya 1964 Mutiny ambapo jeshi lilidhani lina haki ya kuwa na viongozi waafrika
Hali ile ilikuwepo kwingineko na kilichokuwa kinafuata kama si ukabila ni udini kwa wale wasio na silaha

Nigeria, Kenya, Rwanda , Camaeroon nyufa za kutoshughulikia umoja wa kitaifa zinarindima kila uchao
Je, unadhani kwetu ilikuwa ni bahati au kulikuwa na jitihada mahususi na nani yupo nyuma ya hilo
Hata makabila makubwa ya Tanganyika hayakuwa na vyama vyao tofauti vya kisiasa.
Haya mambo ya kuwa utaifa umejengwa baada ya kupata uhuru yanatoka wapi?
Makabila makubwa yalikuwepo yakiwa na influence katika siasa.

Nyanza cooperation ya kanda ya ziwa ilikuwa na nguvu sana
Kwa kuangalia makabila, Nyanza ingeweza kutawala kwa njia ya kura bila kuiba hata kura moja

KNCU kule Kilimanjaro ilikuwa chini ya makabila madogo .
Ukubwa na influence ilikuwa kwa Wasomi ambao wangeweza kabisa kuwa na upper hand katika siasa za nchi

Tofauti za miaka hiyo huwezi kuziona sasa hivi kwa uhalisia bali kwa hisia.
Hii habari ya ''Kanda fulani watusubiri' si bahati mbaya.
Ni kauli zinazorindima zikialeza dukuduku lililokuwepo. Kama utakuwa umenielewa
CCM na wale wasiotaka mabadiliko ya kweli siku zote wanatumia hoja ya utaifa kutofanya mabadiliko. Utaifa tulikuwa nao kwa sababu ya lugha moja na makabila madogo madogo yasio na mvutano.
Lugha moja ilikuwepo, kulikuwa na jitihada za kuifanya ituunganishe.

Again angali nani alikuwa nyuma ya hilo?Uchifu ulifutwa kwasababu mahususi vinginevyo tungekuwa katika wakati tofauti
Changamoto za Tanzania sio utaifa. Na utaifa haikuwa changamoto wakati tumepata uhuru.
Hakuna anayesema changamoto zetu ni utaifa. Hoja hiyo imekuja kueleza kuwa iwe iwavyo kwa ubaya au wema wa Nyerere kuna mambo hayana mjadala na hili la utaifa ni moja kwa moja
Kama utaifa sio changamoto yetu, ni nini chagamoto yetu. Kwa maoni wangu changamoto kubwa ni mfumo mbovu wa kisiasa na uongozi ambao umeshindwa kunyanyua jamii kwa kutumia utaifa na amani iliyokuwepo.
Huko kwenye changamoto za utaifa tulishavuka
Mfumo wetu mbaya ndiyo changamoto kubwa tuliyo nayo

Tumeshindwa kutumia umoja wetu wa kitaifa kubadili hali na mwelekeo wetu kwa masilahi binafsi
Hapo nyuma tulijadili kuwa tatizo ni CCM ambayo imekuwa chama cha siasa za kulipwa na siyo siasa za utaifa

Katika mambo niliyowahi kuyazungumzia hadi kuitwa ''Mfumo'' hapa jamvini ni hilo la mfumo wetu

Ukiuuangali hakuna mahali unaweza kusema tuna mfumo sahihi na hii ni kwasababu hatuna ''mfumo mama'' unaojenga mifumo mingine. Kuzorota kwa taasisi zetu za umma ni zao la mfumo mbaya
 
Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,856
Points
1,500

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,856 1,500
Mkuu utaifa ulikuwepo, kuujenga ni kitu tofauti kidogo
Nigeria walikuwa na utaifa kama ilivyo Kenya, Cameroon, Rwanda , Burundi n.k.
Swali ni je, hali yao ipoje sasa kwa kuzingatia utaifa wao kama ulivyokuwa wetu?

Ni kweli hatukuwa tumegawanyika kwasababu haikuonekana hadharani.
Sote tulikuwa katika minyororo ya Mjerumani na Mwingereza tukililia hali zetu.

Baada ya uhuru tofauti zingelikuwa wazi kama kungekuwa hakuna mtu wa kuzingalia.

Tofauti ni kama ile ya 1964 Mutiny ambapo jeshi lilidhani lina haki ya kuwa na viongozi waafrika
Hali ile ilikuwepo kwingineko na kilichokuwa kinafuata kama si ukabila ni udini kwa wale wasio na silaha

Nigeria, Kenya, Rwanda , Camaeroon nyufa za kutoshughulikia umoja wa kitaifa zinarindima kila uchao
Je, unadhani kwetu ilikuwa ni bahati au kulikuwa na jitihada mahususi na nani yupo nyuma ya hilo Makabila makubwa yalikuwepo yakiwa na influence katika siasa.

Nyanza cooperation ya kanda ya ziwa ilikuwa na nguvu sana
Kwa kuangalia makabila, Nyanza ingeweza kutawala kwa njia ya kura bila kuiba hata kura moja

KNCU kule Kilimanjaro ilikuwa chini ya makabila madogo .
Ukubwa na influence ilikuwa kwa Wasomi ambao wangeweza kabisa kuwa na upper hand katika siasa za nchi

Tofauti za miaka hiyo huwezi kuziona sasa hivi kwa uhalisia bali kwa hisia.
Hii habari ya ''Kanda fulani watusubiri' si bahati mbaya.
Ni kauli zinazorindima zikialeza dukuduku lililokuwepo. Kama utakuwa umenielewa Lugha moja ilikuwepo, kulikuwa na jitihada za kuifanya ituunganishe.

Again angali nani alikuwa nyuma ya hilo?Uchifu ulifutwa kwasababu mahususi vinginevyo tungekuwa katika wakati tofauti Hakuna anayesema changamoto zetu ni utaifa. Hoja hiyo imekuja kueleza kuwa iwe iwavyo kwa ubaya au wema wa Nyerere kuna mambo hayana mjadala na hili la utaifa ni moja kwa moja
Huko kwenye changamoto za utaifa tulishavuka
Mfumo wetu mbaya ndiyo changamoto kubwa tuliyo nayo

Tumeshindwa kutumia umoja wetu wa kitaifa kubadili hali na mwelekeo wetu kwa masilahi binafsi
Hapo nyuma tulijadili kuwa tatizo ni CCM ambayo imekuwa chama cha siasa za kulipwa na siyo siasa za utaifa

Katika mambo niliyowahi kuyazungumzia hadi kuitwa ''Mfumo'' hapa jamvini ni hilo la mfumo wetu

Ukiuuangali hakuna mahali unaweza kusema tuna mfumo sahihi na hii ni kwasababu hatuna ''mfumo mama'' unaojenga mifumo mingine. Kuzorota kwa taasisi zetu za umma ni zao la mfumo mbaya
Nguruvi:

Kuna kitu kinachoitwa diversity. Kilichofanyika Tanzania ni viongozi kuogopa diversity. Msukuma siku zote ataendelea kuwa msukuma. Hiyo ni DNA yake kwa sababu akuchagua mzazi.

Wakati mwingine tunashindwa kuwa na katiba nzuri kwa sababu tunashindwa kutambua diversity zetu. Na tunatumia muda mwingi kujaribu kujenga taifa lenye identity moja.

Katiba ya Marekani inadumu kwa sababu walikubali diversity. Diversity ya mawazo. Diversity ya kuabudu. Diversity ya maeneo yao. Huku Tanzania kabila kuwa na chifu ni dhambi.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,498
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,498 2,000
Nguruvi:

Kuna kitu kinachoitwa diversity. Kilichofanyika Tanzania ni viongozi kuogopa diversity. Msukuma siku zote ataendelea kuwa msukuma. Hiyo ni DNA yake kwa sababu akuchagua mzazi.

Wakati mwingine tunashindwa kuwa na katiba nzuri kwa sababu tunashindwa kutambua diversity zetu. Na tunatumia muda mwingi kujaribu kujenga taifa lenye identity moja.

Katiba ya Marekani inadumu kwa sababu walikubali diversity. Diversity ya mawazo. Diversity ya kuabudu. Diversity ya maeneo yao. Huku Tanzania kabila kuwa na chifu ni dhambi.
Mkuu, Kenya wana machifu, Nigeria wana machifu, Cameroon wana machifu n.k. Je, wamefanikiwaje kuliko sisi?

Kuhusu diversity, sisi tunayo kubwa kuliko Marekani kwa kila eneo unalotaka kuzungumzia

Kupatikana kwa katiba bora si suala la diversity, ni matokeo ya ulafi na ubinafsi uliofunikwa katika mwamvuli mzuri sana uliousema huko nyuma '' CCM ni chama cha siasa za kulipwa'

Ndani ya CCM wanajua na mfano mzuri ni wale washiriki warasimu ya Warioba ambao baada ya kupata fursa za kulipwa sasa wameacha kile walichoamini na kuwa 'wanasiasa wa kulipwa' wakiponda suala la katiba

Kubwa zaidi ni wananchi ambao sijui kama wana uelewa kuhusu katiba na kama wanao wanamwamko sahihi, sijui!
 
Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,856
Points
1,500

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,856 1,500
Mkuu, Kenya wana machifu, Nigeria wana machifu, Cameroon wana machifu n.k. Je, wamefanikiwaje kuliko sisi?

Kuhusu diversity, sisi tunayo kubwa kuliko Marekani kwa kila eneo unalotaka kuzungumzia

Kupatikana kwa katiba bora si suala la diversity, ni matokeo ya ulafi na ubinafsi uliofunikwa katika mwamvuli mzuri sana uliousema huko nyuma '' CCM ni chama cha siasa za kulipwa'

Ndani ya CCM wanajua na mfano mzuri ni wale washiriki warasimu ya Warioba ambao baada ya kupata fursa za kulipwa sasa wameacha kile walichoamini na kuwa 'wanasiasa wa kulipwa' wakiponda suala la katiba

Kubwa zaidi ni wananchi ambao sijui kama wana uelewa kuhusu katiba na kama wanao wanamwamko sahihi, sijui!
Actually kuna nchi za kiafrika ambazo hazikuanza kama Tanzania zimeanza kupata identities za utaifa ambazo Tanzania ilimekuwa nazo toka mkoloni.

Kwa mfano nyingi za kiafrika zina lugha za taifa ambazo zinaeleweka na taifa nzima. Kwa mfano nchi nyingi zilizokuwa chini ya Mwingereza, tayari zina local english ambayo ni ya kwao pekee yao. Hata zile zinazozungumza kifaransa zina kifaransa chao. Hile advantage tuliyokuwa nayo miaka ya 60. 70 na 80 sio big deal tena.

Pamoja na matatizo yao, Nigeria is largest economy in Africa. Kenya is the largest economy in our region. Cameroon vilevile wako mbali. Nchi hizo ulizotaja wametuzidi per capital. Wametuzidi ya namba ya dispora inayosaidia nchi zao. Na wametuzidi katika matrix zingine unazozijua.

Tanzania haina diversity kubwa kuliko Marekani. Makabila mengi yanazungumza the same f@cking languages. Wasukuma na wanyamwezi ni watu walewale. Mpare, mzigua, msambaa wanazungumza lugha moja. Mpogoro na mdengeleko wanasikilizana. Wakinga na wahehe ni watu walewale.

Jamii inaundwa na common values. Hivyo watu wanaweza kuwa na tofauti zao lakini wakawa na bonds zinazowafanya waheshimu taifa lao. Na misingi ya katiba ni kuwafanya watu waheshimu na kulinda common values zao. Hakuna tatizo kama wachagga watakuwa na chifu wao. Kama unaone machifu ni wabaya, mbona tunaruhusu watu kama Gwajima kuwa na makanisa na misikiti.
 
Thread starter Similar threads Forum Replies Date
Suriya Great Thinkers 1

Forum statistics

Threads 1,391,115
Members 528,361
Posts 34,073,982
Top