Thank God for giving us Magufuli aka Jiwe aka Chuma!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Ni miaka miwili na miezi kumi tangu ndugu John Joseph Pombe Magufuli aapishwe kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni mengi ya kutafakarisha yametokea tangu Magufuli awe Rais, na kila siku wengi wetu tunajifunza mapya na kukumbuka mengi.

Nasema ni shukrani maana katufungulia na kutufunulia mengi kuhusu Tanzania na zaidi kuhusu sisi kama Taifa na wananchi wake.

Natambua sitaeleweka kama jinsi sikueleweka miaka 10 iliyopita nilipoandika "Thank God for giving us Kikwete" lakini naamini safari hii wenye juhudi na upeo wa ufahamu na uelewa watanielewa.

Tuendelee kutafakari!
 
Ni miaka miwili na miezi kumi tangu ndugu John Joseph Pombe Magufuli aapishwe kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni mengi ya kutafakarisha yametokea tangu Magufuli awe Rais, na kila siku wengi wetu tunajifunza mapya na kukumbuka mengi.

Nasema ni shukrani maana katufungulia na kutufunulia mengi kuhusu Tanzania na zaidi kuhusu sisi kama Taifa na wananchi wake.

Natambua sitaeleweka kama jinsi sikueleweka miaka 10 iliyopita nilipoandika "Thank God for giving us Kikwete" lakini naamini safari hii wenye juhudi na upeo wa ufahamu na uelewa watanielewa.

Tuendelee kutafakari!
Kweli tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa sababu kupitia utawala wa JIWE ndipo wananchi watazinduka usingizini kwamba hatima ya nchi iko mikononi mwao na bila kuchukua hatua na kuwaachia wanasiasa peke yao ni kuzidi kujizika shimoni.
 
Ni mengi ya kutafakarisha yametokea tangu Magufuli awe Rais, na kila siku wengi wetu tunajifunza mapya na kukumbuka mengi.

Nasema ni shukrani maana katufungulia na kutufunulia mengi kuhusu Tanzania na zaidi kuhusu sisi kama Taifa na wananchi wake.
!
Nimerejea kauli yako nikabaini ilikuwa na maana pana kuliko ufupi wa mistari yake

Tunajifunza mapya. Kwa walioishi kipindi cha Mwalimu na waliofuata kuna mengi wanapaswa kujifunza kuliko waliyojifunza

Nimekumbuka hili la mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa(RC)

Kiuhalisia kamati ni utaratibu wa kiutawala katika ulinzi na usalama (admin)
RC ni mjumbe kama alivyo kamanda wa mkoa au kanda na wanakamati wengine

Kamati ni chombo cha kiutawala siutendaji. Watendaji ni pamoja na vyombo vya dola kama Polisi
Polisi wana utaratibu wa mamlaka zao na zimeanishwa kuanzia ngazi ya chini hadi ya Juu

RC anapoingia ''barracks' na kuchukua majukumu ni jambo jipya la kujifunza

RC kama m/kiti angeweza kupeleka salam kwa kutumia wajumbe kutoka vyombo vya dola ndani ya kamati yake. Hao wangeweza kuwasiliana na 'timu' zao kupokea salaam
Polisi ni sehemu ya wizara ya mambo ya ndani. Taratibu za maeneo hayo zipo

Tunaposikia kuna msemaji wa wizara, katibu mkuu, waziri, IGP,Msemaji wa Polisi, RPC, OC n.k. si jambo la bahati mbaya. Viongozi hao wapo kwasababu maalumu za kisheria na kiungozi

Leo askari wanaposerebuka kambini na RC, viongozi wa wizara na jeshi wanakuwa katika hali gani! Pengine ndiyo maana hawazungumzii au hawaoni umuhimu wa tukio au wamekwazika

Hata hivyo, busara ingetumika zaidi kuliko ilivyotokea. Kupongeza si jambo baya, lakini je, linafanyika kwa wakati gani?Je, kitendo kile kilifanyika sehemu, wakati na watu muafaka?

Je, ni busara kuipongeza Simba kwa kuwafunga Bacelona wakati Askofu anasoma misa ya mazishi? Wakati sheikh anafanya hitma ya msiba?

Sherehe wakati wa matokeo kutangazwa Ukonga na Monduli zinatoa picha mpya ya zama hizi

Kuna hisia hisia katika jamii kuhusu mahusiano ya Polisi, wananchi, wanasiasa na jamii.
Ni hisia tu zinazoweza kutokuwa na ukweli au kuwa na ukweli

Aliyewahi kuwa IGP kabla, alikemea tabia ya wananchi kusherehekea maafa kama yale ya mkoa wa Pwani. Zile hisia za mahusiano ya jeshi na wananchi zikaanza kuonekana na ufa wake

Kuna hisia kuhusu Tume ya uchaguzi na uendeshaji wa chaguzi nchini

Ukikusanya mazonge zonge yoote hayo utabaini RC amesaidia kuondoa shaka dhidi ya hisia(doubts). Kwanza, ameikwaza serikali na kutoa picha isiyopendeza.

Pili, ameikwaza wizara na kuleta mkanganyiko wa madaraka. Tatu, amelikwaza jeshi kwa ''ushahidi' dhidi ya hisia, na Mwisho ameikwaza tume ya uchaguzi kwa kuijengea taswira tofauti

Haya yote tunajifunza, kwa miaka 23 ya Mwl pengine yalifanyika, lakini sasa yanafanyika hadharani mchana bila hofu tena kwa kugonga glass bila kusoma hisia au uso wa jamii.

Ni jambo la kujifunza, kwamba, tunadhani tunaelewa kumbe yapo mengi tusiyoyaelewa.

Tunajifunza kuwa, tunaweza kuwa na amani na utulivu, tukaamua kufikia maendeleo yetu haraka kwa njia za mkato bila kuwa na ukiritimba wa nidhamu (discipline)


Namshukuru Rev. Kishoka kwa mada yake, tunajifunza
 
WATANZANI HAWAJUI KUJENGA AU KUBOMOA HOJA
YA Dr BASHIRU NA MEMBE YANAELEZA HATARI YA KAULI ZA VIONGOZI

Mjadala unaoendelea wa kauli ya KM wa CCM Dr Bashiru dhidi ya Membe unatufungulia mengi
Bandiko # 3 nilisema hivi QUOTE]'Ni jambo la kujifunza, kwamba, tunadhani tunaelewa kumbe yapo mengi tusiyoyaelewa''[/QUOTE]

Ni mjadala unaeleza weledi wa Wanzania na hatari inayoweza kwa kauli but za hasa viongozi Tunajifunza viongozi wawe waangalifu wa kauli zao

Watanzania wana tatizo la kuelewa mada (topic), mantiki (semantic), maudhui (contents) na kusudio (context). Ni rahisi sana kupotoka, kupotosha au kuchanganyikiwa

Kauli ya Dr Bashiru haina tatizo katika mada(topic) aliyozungumzia kuhusu tambo za uchaguzi
Haina tatizo katika maudhui(contents) alipozungumzia taarifa za mikutano ya siri

Kauli ya Bashiru ilikuwa na matatizo makubwa katika kusudio(context) na maana (semantic)
1. Kusudio lilikuwa kumsema Membe hadharani. Angeweza kuongelea tatizo la vikao bila kumtaja. Kitendo cha kumtaja kilimpa haki asiyokuwa nayo na kumnyang'anya Membe haki aliyokuwa, yaani kumhukumu mbele ya court of public opinion bila yeye kujieleza

2. Dr Bashiru hakutumia utaratibu wa Chama chake wa kushughulikia matatizo.
CCM wanahimiza, na yeye alisema ''mambo ya chama yanaongelewa katika vikao'

Bashiru alimwita Membe ofisini kwa njia ya mikutano. Hakuanza na vikao anvyohuviri

Haikuwa tofauti na kutumia mitandao anayoilaani kila siku. Taratibu za CCM angemwita rasmi wakaongea huko mambo yao na kumalizana. Hilo ni tatizo lao

3. Dr Bashiru hakutumia kanuni ya asili ya kusikiliza pande husika kupata ukweli kabla ya kutoa 'hukumu ' mbele ya umma.

Kauli limegeuka hukumu, kwamba Membe anafanya vikao bila ushahidi kwasababu ya misleading (upotoshaji) ya Dr Bashiru. Kwamba, kauli yake imekuwa hukumu

Hoja ya Dr Bashiru kuhusu songomibingo za vikao na wagombea CCM ni za CCM. Haituhusu

Hata hivyo kuna public interest pale kauli zake zinapouchanganya umma kwasababu tu alishindwa kuwa na mawasiliano bora, kutojua taratibu za ofisi kwa kiwango chake cha elimu.

Huyu ni KM wa chama tawala, sera za nchi zinasimamiwa na CCM zinatugusa sote
Inapotokea KM haelewi ubora wa mawasiliano tena na Sr. CCM cadre/Cabinet kuna tatizo.

Vizazi vinavyokuja vitafuata utaratibu mbovu vikidhani ndio utaratibu sahihi
Ndiyo maana KM wa Zamani Makamba anamuunga mkono eti kwasababu aliwahi kufanya au kufanyiwa hivyo. Tunaweza kutoa ''benefit of doubt'' kwa Makamba, kwa Dr Bashiru ni no no!

Kwasababu Watanzania hawaelewi mada, maudhui, maana , na hawajui kujenga au kubomoa hoja tunaona vijana tunaodhani ni wasomi wakimtuhumu Membe kwa kutaka kugombea

Vijana hao hawana ushahidi , KM Bashiru hana ushahidi hajakutana na mtuhumiwa.

Hoja imeondoka kutoka mawasiliano mabaya ya KM na kuwa Membe na kugombea wakitumia kauli ya Dr Bashiru dhidi ya Membe aliyoitoa hadharani.

Madhara ya kauli ya Dr Bashiru yanamchafua Membe bila kuwa na ukweli au ushahidi.
Wawili hao hawajakutana, KM hajamsikiliza, ni vipi basi jamii imefikia hitimisho dhidi ya BM?

Tuhuma zinazorindima ni Membe kugombea. Just tuhuma tu bila ushahidi kwasababu KM amesema. Hakuna anayeona mapungufu ya mawasiliano yaliyozaa mjadala usio na ulazima

Dr Bashiru angewasiliana na Membe nje ya mikutano, wangeyamaliza wenyewe.
Dr angekuwa na upande wa pili, ushahidi au la,na angetumia vikao kuyamaliza na si mikutano

Dhalili , aibu mashambulizi na fedheha anayopata Membe ni kutokana na upungufu wa kufuta taratibu na ubovu wa mawasiliano. Bila kumsikiliza au ushahidi ni hukumu isiyo na kesi

Watu warudi kwenye tatizo la mawasiliano, kugombea au vikao si tatizo la msingi
Hoja ipo namna KM wa CCM alivyoliangalia suala bila kufuata taratibu

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3,

Nimekusoma kwenye mabandiko yako mawili na hitimisho langu ni moja: CCM haijapevuka kuwa na uhuru wa ndani na uwezo wa kukosoana hata kuwajibishana!

Haya ni matokeo ya kusinyaa na kuzibwa pumzi kwa Demokrasia ndani ya CCM, jambo ambalo limeanza tangu TANU na hata kuzaa kauli mbiu ya "zidumu fikra za mwenyekiti" na mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambaye miaka yote ni ama Rais au Rais mstaafu atakayempasia kigoda aliye Rais amekuwa akitukuzwa kama "omnipotent" the absolute righteous power almighty!

Nyuma ya pazia hili, ni mvutano na uhasama wa ndani ya chama ambao hautokani na ushindani wa Itikadi, Sera au falsafa za uongozi bali ni maslahi binafsi na fursa za kuwezeshana!

Hili limezaa makundi na mitandao ambayo iko tiyari kuingia vitani na kumtetea mtu wao at any cost na ashindapo, humwekea ulinzi at any cost na ole wako yule atakayethubutu kuhoji, kukosoa au kupingana na "jemedari" wa kikosi kipya!

Ni mfumo wa "kutesa kwa zamu" ambao huhakikisha Rais wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wake wa Taifa anajengewa ngome kubwa ya ulinzi wa kutokuhojiwa, kupingwa, kukosolewa au kuwekwa katika ushindani wa ndani (au nje ya chama) chama ambapo mwenye kumletea ushindani anaweza kuja na mtazamo tofauti na bora zaidi na kumng'oa kwenye nafasi ya kuwa mgombea na Rais kupitia CCM.

Alichofanya Bashiru ni kuwaambia wana CCM kuwa kundi-genge lililoko madarakani ndani ya Chama na lenye nguzu za maamuzi na utendaji limeridhia na utendaji wa aliye Rais wao na ole wao (wake) yeyote ambaye atataka kuleta ushindani wa aina yeyote (sera, itikadi, mipango) ambao ni kumpinga Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa atashughulikiwa kwa utovu wa nidhamu, ili kuulinda "utamaduni" wa kumwachia aliye Rais apete ndani ya chama (na hata nje ya chama0 bila kupingwa!

Anayeumia kutokana na "falsafa" hii ya Bashiru na wenzake ambao ni wapambe wenye kusifia na kulazimisha kukubalika kwa Mwenyekiti wao ni Tanzania kama Taifa na zaidi ni maana na matiki ya Demokrasia!

Msuguano huu wa ndani ya Chama (si mara ya kwanza, upo tangu enzi za TANU) umezaa mazingira ya Rais na "walinzi" wake kujiwekea mazingira ya kuwa unopposed by anyone! Leo hii hata Bunge lenye mamlaka kikatiba na kisheria kumwajibisha Rais na Serikali limewekwa kwenye mazingira ya kuogopa kufanya kazi zao kwa uadilifu kwa mujibu wa katiba kwa hofu ya kushughulikiwa Kichama!

Ni mazingira ya kumfanya Rais awe Sultani, Mwinyi, Mfalme ambaye hapingwi! Ni mazingira ambayo yameleta utendaji wa kuridhia na kumfurahisha mtu aliye Rais na kwamba asipingwe, kataliwe au kukosolewa. Ni mfumo ambao umishia kumjengea Rais kingo za ngome ya ulinzi kwa kutunga sheria za kuwaadhibu na kuwadhibiti wote wenye kuhoji maamuzi ya Rais au kumkosoa.

Ni mfumo ambao umelazimisha Mbunge wa CCM akiuke bila hiari katiba ya Chama chake na hata Katiba ya nchi ili kutimiza matakwa ya genge lenye madaraka na mamlaka, ambalo ndilo linalotawala nchi!

Hii, ni hatari, hatari kwa uhai wa kweli ndani ya CCM na hata Taifa!

leo mtu mwenye mawazo tofauti ndani ya CCM anatolewa kauli za kashfa, anatolewa vitisho na hatua za "kinidhamu" zinachukuliwa kumnyamazisha asiongee lolote. Tunaliona Bungeni na hata kwenye vikao vya chama na hata mivutano ya chini chini ya chama.

Haki ya dhati kisheria na kikatiba ya mwanachama wa CCM kukosoa uongozi wake au kuingia ushindani wa hoja, sera na uongozi dhidi ya aliye Mwemnyekiti wa Taifa inazimwa kwa nguvu za dola na za kichama na mwenye nia hiyo, huandamwa kama msaliti!

Badala ya kuruhusu ushindani wa ndani wenye afya na kukiimarisha chama ili kiwe na uwezo wa kiitikadi na kisera kuendelea kulitumikia Taifa kwa manufaa ya Taifa, dhana ya "kuridhika" na utendaji wa Rais na Mwenyekiti wa Chama imekuwa ni yamini ya kulazimisha kwa wanacham wa CCM, watendaji wa CCM na hata Taifa. Ole wako wewe unayehoji kwa maana ni msaliti, adui na kuwadi wa wanaopinga maendeleo ya Taifa!

Inawezekana kabisa kuna WanaCCM ambao wana weledi wa uongozi na mtazamo tofauti kabisa wa kiuongozi na kisra na wenye sera na mipango mbadala yenye kuliletea Taifa la Tanzania na CCM yenyewe manufaa makubwa kabisa. Lakini kutokana na mfumo huu wa Rais hapingwi, hakosolewi na kuwa yeye ni absolute righteous, hivyo inabidi msubiri aondokapo madarakani!

Tanzania inaumia kutokana na mfumo huu wa kifisadi wa madaraka, na maendeleo yake kitaifa huchukua mtazamo mmoja na pale inapotokea kuwa kuna makosa ni vigumu kurekebika kutokana na ngome hii ya kuzuia Rais na MWenyekiti wa Chama kuwajibishwa na kuwa challenged!

Nilitarajia kauli kutoka kwenye CCM Mpya ingekuwa ni kuwakaribisha wote ambao wana mawazo mbadala kuanza kunadi sera na mipango yao ilinganishwe na anachofanya Rais na Mwenyekiti wa CCM na mwishowe kwenye mkutano mkuu, demokrasiaichukue mkondo wake kwa mwenye kujinadi awe mshindi wa kupewa dhamana na si mfumo ulioko wa genge kuamua nani agombee, aliyeko asipingwe na kiuhalisia kuendeleza mfumo wa kikoloni wa kutawala na kunyamazisha sauti zote zisizofanana na sauti "pendwa"!

Waswahili husema Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza! Kama ushawishi wa Rais ni mzuri kiasi hicho, hakuna sababu ya kuhofia yeye kupingwa na mwanachama wa ndani au hata nje ya chama ambapo Sheria kukandamiza upinzani zinaboreshwa!
 
Katiba ya Tanzania uchaguzi wa rais ni kila baada ya miaka mitano. Huu utaratibu wa kumpisha aliyeko madarakani aendelee ni utaratibu waliojiwekea CzCM na dr Bashiru anaulinda.
 
CCM haijapevuka kuwa na uhuru wa ndani na uwezo wa kukosoana hata kuwajibishana!
Mkuu Rev, hapa nina mtazamo tofauti. CCM ilishapevuka kinachoendelea sasa ni CCM kudumaa. Nasema hivi kwa kuangalia NEC na CC za CCM miaka ya nyuma. Hata wananchi walisubiri sana kusikia hoja zitajadiliwa vipi katika vikao hivyo kwa kuelewa kulikuwa na kukosoana kwa mantiki. Unakumbuka hoja ya Marehemu Nyalali na Nyerere kuhusu mahakama? Unakumbuka sakata la mauaji ya Pemba, JK , BWM na wajumbe wa CC?
Akina mzee Warioba, Malecela, Msuya n.k. wanaeleweka kwa misimamo yao mingine dhidi ya CCM
Wakati wa JK na akina Sitta hali ilikuwa tofauti na sasa. Ndiyo maana nasema imedumaa
 
Mkuu Rev, hapa nina mtazamo tofauti. CCM ilishapevuka kinachoendelea sasa ni CCM kudumaa. Nasema hivi kwa kuangalia NEC na CC za CCM miaka ya nyuma. Hata wananchi walisubiri sana kusikia hoja zitajadiliwa vipi katika vikao hivyo kwa kuelewa kulikuwa na kukosoana kwa mantiki. Unakumbuka hoja ya Marehemu Nyalali na Nyerere kuhusu mahakama? Unakumbuka sakata la mauaji ya Pemba, JK , BWM na wajumbe wa CC?
Akina mzee Warioba, Malecela, Msuya n.k. wanaeleweka kwa misimamo yao mingine dhidi ya CCM
Wakati wa JK na akina Sitta hali ilikuwa tofauti na sasa. Ndiyo maana nasema imedumaa

Mkuu,

Upevu ulikuwa wa kinafiki!

Nasema wa kinafiki kwa maana ulilenga kutuliza kundi moja kufurukuta kwa kuwa na final unanimous consensus huku watu bado wana hasira zao!

Mauaji ya Pemba, upambe wenye kusimamia haki na uliopata uchungu ulikubali kwa shingo upande bila uwajibikaji wa kweli hata kama ungekimegua chama! Maana yalipotokea ya MwembeYanga, chama kilikaa kimya kumwajibisha ipaswavyo Rais na Mwenyekiti wake.

Ndio maana nasema hakijapevuka. Ni mfumo wa kufa kufaana na kulindana. CCM walivyokutana Butiama kuvuana magamba, matokeo yaliyotakikana kutokea yalizimwa kimya imya. Kama chama kingekuwa kimepevuka, wangemvua gamba kasa mkuu na hata kukubali matokeo yake ambayo kiuhalisia yangetikisa nchi lakini haki ingesimama.

Ndio tunaweza kusema 1984 na Mzee Jumbe ilikuwa ni ukomavu, lakini ulikuwa ni wa kinafiki na kimaslahi kwa maana baada ya hapo, emphasis imekuwa kumezeana.

Hivyo balehe ya kutoka manii kama 1984 haina maana sasa Chama kimepevuka.
 
"
Rev. Kishoka, post: 29534178, member: 18"]Haya ni matokeo ya kusinyaa na kuzibwa pumzi kwa Demokrasia ndani ya CCM, tangu TANU na hata kuzaa kauli ya "zidumu fikra za mwenyekiti" na mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambaye miaka yote ni ama Rais au Rais mstaafu atakayempasia kigoda aliye Rais amekuwa akitukuzwa kama "omnipotent" the absolute righteous power almighty!
Utamaduni huo ulifanikiwa kwa nyakati hizo.
CCM watambue kuwa nyakati zinaelekeza aina ya siasa.
Kizazi hiki kina mtazamo tofauti. UNIP na KANU wanaelewa vizuri madhara ya uhafidhina
Hili limezaa makundi na mitandao ambayo iko tiyari kuingia vitani na kumtetea mtu wao at any cost na ashindapo, humwekea ulinzi at any cost na ole wako yule atakayethubutu kuhoji, kukosoa au kupingana na "jemedari" wa kikosi kipya!
Madhara ya ke yanagusa demokrasia ya nchibi. Kuminywa kwa upinzani ni matokeo ya kufanikiwa ''sera' hiyo ndani ya CCM
Alichofanya Bashiru ni kuwaambia wana CCM kuwa kundi-genge lililoko madarakani ndani ya Chama na lenye nguzu za maamuzi na utendaji limeridhia na utendaji wa aliye Rais wao na ole wao (wake) yeyote ambaye atataka kuleta ushindani wa aina yeyote (sera, itikadi, mipango) ambao ni kumpinga Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa atashughulikiwa kwa utovu wa nidhamu, ili kuulinda "utamaduni" wa kumwachia aliye Rais apete ndani ya chama (na hata nje ya chama0 bila kupingwa!
Huko ndiko tunakoelekea kwa kuangalia madhila yanayoukumba upinzani nchini.

Wiki iliyokwisha CCM wametangaza kushinda chaguzi ndogo za vijiji na mitaa 46 bila kupingwa
Msuguano ndani ya Chama (si mara ya kwanza, upo tangu enzi za TANU) umezaa mazingira ya Rais na "walinzi" wake kujiwekea mazingira ya kuwa unopposed by anyone! Bunge lenye mamlaka kikatiba na kisheria kumwajibisha Rais na Serikali limewekwa kwenye mazingira ya kuogopa kufanya kazi zao kwa uadilifu kwa hofu ya kushughulikiwa Kichama!
Wametengeneza ''Caucus' inayotumika kama chaka la kujificha.

Kwamba, Caucus inalinda serikali ya chama na chama kinalinda caucus
Kwa mantiki hiyo wananchi wamepoteza uwakilishi, kwamba, caucus ndiyo inayowakilisha wananchi na siyo Wabunge na kuzaa ubutu wa Bunge.

Mwanachama wa Upinzani anapohamia CCM hapewi ukuu wa Mkoa au Wilaya.
Ni ngumu kumdhibiti.Anapewa Ubunge awe ndani Caucus atakapoweza kudhibitiwa vema
Ni mfumo ambao umelazimisha Mbunge wa CCM akiuke bila hiari katiba ya Chama chake na hata Katiba ya nchi ili kutimiza matakwa ya genge lenye madaraka na mamlaka, ambalo ndilo linalotawala nchi!
Hata kuwasaliti wapiga kura
Hii, ni hatari, hatari kwa uhai wa kweli ndani ya CCM na hata Taifa!
Hasa Taifa.

Leo Wabunge wa CCM wametelekeza jukumu lao la kuisimamia serikali na uwakilishi

Wamekuwa loyal kwa Caucus si nchi au wananchi.
Wakati wa chama kimoja ilikuwa bora kulik. Bunge limepoteza maana ya asili ya kazi zake
leo mtu mwenye mawazo tofauti ndani ya CCM anatolewa kauli za kashfa, anatolewa vitisho na hatua za "kinidhamu" zinachukuliwa kumnyamazisha asiongee lolote.
Tunaliona Bungeni na hata kwenye vikao vya chama na hata mivutano ya chini chini ya chama.
Hata pale wanapotimiza wajibu wao wa kibunge.
Adhabu inayowasubiri ni kuondolewa majina yao kwa kosa la kuwakilisha wananchi wao badala ya kutetea ''vanguard au Politburo'
Haki ya dhati kisheria na kikatiba ya mwanachama wa CCM kukosoa uongozi wake au kuingia ushindani wa hoja, sera na uongozi dhidi ya aliye Mwemnyekiti wa Taifa inazimwa kwa nguvu za dola na za kichama na mwenye nia hiyo, huandamwa kama msaliti!
Haki hiyo imezimwa ndani ya vikao, mfano ni mkutano mkuu, baadhi waliwekwa mahabusu kwasababu tu walikuwa na maoni tofauti

Kwasasa CCM siyo chama kinachoongoza dola ni chama kinachoongozwa na dola

Matumizi ya vyombo vya dola kwa CCM yanaeleza udhaifu mkubwa ndani yake

Kwamba, CCM haina sera, wala ushawishi wa hoja pasi matumizi ya dola

Mswada wa sheria ya vyama unaeleza jinsi gani matumizi ya vyombo na taasisi za dola yanavyoandaliwa ili kuua upinzani baada ya kumaliza upinzani wa ndani
Udhaifu wa CCM si sera, ni kukosa ushawishi kunakotokana na kuminywa demokrasia
Badala ya kuruhusu ushindani wa ndani wenye afya na kukiimarisha chama ili kiwe na uwezo wa kiitikadi na kisera kuendelea kulitumikia Taifa kwa manufaa ya Taifa, dhana ya "kuridhika" na utendaji wa Rais na Mwenyekiti wa Chama imekuwa ni yamini ya kulazimisha kwa wanacham wa CCM, watendaji wa CCM na hata Taifa. Ole wako wewe unayehoji kwa maana ni msaliti, adui na kuwadi wa wanaopinga maendeleo ya Taifa!
Ni dhana ya unafiki kwa kuelewa upo upinzani wenye hoja unaoweza kutoa mabadiliko.

Haya tunayoyaona yakina BM ni dalili ya moshi na kuchoka mapenzi ya unafiki.
Ni vicious circle, walikuwa ndani wakilinda mfumo bila kujua ipo siku utawaacha njia panda
Waswahili husema Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza! Kama ushawishi wa Rais ni mzuri kiasi hicho, hakuna sababu ya kuhofia yeye kupingwa na mwanachama wa ndani au hata nje ya chama ambapo Sheria kukandamiza upinzani zinaboreshwa!
Hakuna jibu na anayeweza kuelewa. Wanajificha katika kauli ya 'utamaduni'
Kukeketa ni utamaduni, je, tuache tu wakeketwe kwasababu ni utamaduni hata kama ni mbaya
 
Ndugu Nguruvi,

Leo kikao cha NSB, TRA, Rais na appointees wake kimeniacha very much confused......
 
Ndugu Nguruvi,

Leo kikao cha NSB, TRA, Rais na appointees wake kimeniacha very much confused......
Kuna mambo yanayohitaji tafakuri
1. NBS, TRA, na Exec branch ilikuwepo katika mkutano.
Swali lililozuka ni kuhusu idadi ya walipa kodi ambayo ni chini ya 3M katika 45M population
Kwanini hili liwe mjadala katika 'public"? Kulikuwa na plan na strategy kulenga ukusanyaji kodi?

a)Je, kuna mfumo wa kubaini watu wanaopaswa kulipa kodi na kama wanalipa kodi?
b)Inawezekanaje kukusanya kodi bila kujua 'catchment area' uliyo nayo?
c) Tatizo la walipa kodi wachache limeanza leo?

Nitaanza kujadili na (c) hapo juu.
Tatizo ni la muda mrefu lililoendekezwa kwa kutegemea kodi za wafanyakazi wa serikali na Private sectors.

Kwa mtazamo wa haraka makundi hayo yanachangia zaidi ya 1/3 ya ukusanyaji kodi

Tukirudi (b) catchment area, hakuna mfumo unaombaini kila mmoja na kodi anayolipa inapobidi. Kutokana na hilo kuna 'informal sector' isiyotambuliwa katika ulipaji kodi

Kutokuwa na mfumo mzuri kunalazimisha wafanyakazi na wafanyabiashara kuwa walipa kodi wakubwa, sehemu kubwa ya walipa kodi katika informal sector ikiachwa huria

Wafanyakazi hawana choice, wanakatwa kodi bila kushika pesa zao.

Wafanyabiashara hawana choice wanataka leseni, tofauti na wafanyakazi wao wana 'alternative'.

Mfanyabiashara anaweza kupunguza gharama za uendeshaji kwa kupunguza wafanyakazi

Kupungua kwa biashara kuna 'impact kubwa' katika ukusanyaji kodi.Spill over effect inafinywa. Biashara inayojiri watu 50 ina walipa kodi wengi kwa 'spill over effect yake''

Siyo mchumi ni gula gula wa mtaani, nashangaa debate ni ya nini kuhusu walipa kodi!

Kama hawajui nani anapaswa kulipa kodi katika watu watu 45M, kodi tutegemee nini?

Je, wanatambua sekta isiyo rasmi na inachangia vipi katika kodi?
Je, kuna mfumo wa kubaini walipa kodi?
Je, biashara ambayo ni sehemu kubwa ya walipa kodi ni 'vibrant'?

Wakiwa na 'tool zote' nilitegemea waje na majibu na si public debate! Inahusu vipi wananchi?

Wangekaa behind the door, wakajadili na kuja na majibu.Sisi wananchi ktk hili tunasaidiaje?
 
BENDERA NA WIMBO WA TAIFA
JE, NI DALILI ZA 'KUSUSIA' TARATIBU?

Takribani mwezi sasa mjadala ni kauli ya KM-CCM kumwita Bw Membe kwa njia ya mikutano.

Ingawa mjadala ulipindishwa kuwa haki ya kumwita, baadhi tulisimama kusema 'taratibu' za kiofisi na hata CCM haziruhusu mawasiliano katika mikutano. Hiyo ni vurugu si taratibu

Hoja ni kwamba, KM Bashiru ana kila uwezo na sababu za kuwasiliana na Membe kwa njia za kiofisi kupata ukweli kabla hajamsomea ''hukumu'' bila kumsikiliza au ushahidi wa tuhuma.

Jambo hili tulilieleza kama dalili ya kukosa 'taratibu' kutoheshimu taratibu na pengine ufahamu finyu ukichagizwa na ushabiki badala ya hekma.

Ingawa linahusu CCM, tulieleza,viongozi wasipokemewa wataweza kulitia taifa katika misuko suko isiyo na ulazima kama si tayari wameshafanya hivyo baadhi yao

Wiki hii mjadala wa Bendera na wimbo wa Taifa ulipamba tena majadiliano.
Rais Magufuli ameingilia kati na kufuta barua kutoka wizara ya mambo ya ndani- Elimu

Bendera na wimbo wa Taifa ni alama za Taifa bila kujali itikadi za kisiasa.
Ni masula yanayohitaji 'consultation' na wajuzi kabla ya kuyatolea matamko

Viongozi waliotoa amri hawakuzingatia taratibu kama alivyokuwa kwa KM wa CCM.
Wametoka 'solo' pengine kuonyesha tu wanafanya kazi hata kama hawazingatii taratibu

Bendera na Wimbo wa Taifa si alama za Utaifa tu bali ni chachu za uzalendo.
Ni vitu vinavyomuunganisha mtu na nasaba yake, vinavyomfanya mhusika ajivunie nchi yake

Yupo kijana wa Kitanzania anayefanya vema katika eneo la IT (Harnandez?) yeye kila anapotokea hubeba bendera ya Tanzania kwa furaha na kujivuna akiitangaza nchi
Kuna kosa gani kufanya hivyo? Je, tunasubiri watalii waje kubeba bendera yetu kujivunia?

Wimbo wa Taifa nao kama alama ya Mtanzania inapaswa kujivunia.
Vipi leo kijana wa Tanzania akitokea mbele ya dunia bila kujua wimbo wake wa Taifa, ni nani atatuelewa katika dunia ya leo

Kichotakiwa ni kuhimiza kuheshimu alama hizo, bila kuzitumia vibaya.
Hakukuwa na sababu ya kuzuia kuzitumia, ni haki ya raia wa na haitolewi na mtu au watu

Ikibidi kufanyika mabadiliko, zipo taratibu za kufuata si kuamka asubuhi na kuachia tamko

Haya yanatokea kwasababu kitu kinachoitwa taratibu au mwongozo sasa hivi kipo katika mkabarasha ya zamani pale maktaba kuu. Tunakwenda kwenda tu bila kufuata taratibu
 
Nahisi kuna jitihada za makusudi kabisa kuvuruga mtazamo na focus ya wananchi kwenye mambo ya msingi, mfano ni hili s?\uala la Wimbo wa Taifa au maamuzi ya DC wa Arumeru kwenda kukagua hospitali na vituo vya afya usiku wa manane na kuamuru wauguzi na madaktari wasilale huku kimfumo wa kikazi wanapaswa kupumzika overnight!

Cha kujiuliza ni inakuwaje huu uholela wa wateuliwa wa Rais hasa ma-RC na DC kuwa mstari wa mbele kuvurunda vitu na si kufuata sheria, kanuni au mfumo halisi wa kazi na kanuni? na la zaidi kwa nini wanaendelea na "vurugu" zao bila kuadhibiwa?

Ikiwa PM ilimbidi kupeleka mawaziri Kilimanjaro ili kutuliza mfarakano kati ya RC na ma-DC wake wawili, what does that say?
 
Tatizo kubwa la Tanzania siyo Magufuli wala CCM. Rais Magufuli siyo malaika, ni binadamu kama binadamu wengine wote, ana mazuri yake na mapungufu yake- unaweza kushangaa kuwa mapungufu yake ni mchache kuliko mapungufu ya baadhi ya marais waliomtangulia. Halafu CCM ni chama cha siasa kama kama ilivyo kwa CHADEMA na CUF, vyote malengo yao ya kwanza ni kushika madaraka- vitajitahidi kutumia mbinu zozote kuweza kushika madaraka.

Tanzania ya leo ina matatizo mawili tu ambayo yanaiacha nchi katika vicious circle: tatizo moja linasababisha tatizo la pili ambalo lijirudia kwenye lile tatizo la kwanza kama ifuatavyo.

(a)Katiba mbovu:
Katiba ya Tanzania leo ni viraka viraka vya katiba ya Tanganyika iliyoandikwa na Nyerere mwenyewe mwaka 1961 huku ikiwa inakaribia ile katiba ya Lancaster House iliyoandikwa mwaka 1960 kwa ajili ya uhuru wa Tanganyika chini ya serikali iliyoongozwa na Governor General akimwakilisha ya Malkia- raia wote walikuwa wanajulikana kama subjects wa malkia. Nyerere alirekebisha vipengele kadhaa kusudi iwe ni kwa Jamhuri ya Tanganyika chini ya serikali inyoongozwa na Rais aliyechaguliwa na wanachi, na ikaanza kutumika mwaka 1962; katiba hiyo ya Nyerere nayo inherently iliacha raia wawe kama subjects wa rais kwa kumpa madaraka mengi sana kuhusu maisha yao ya kila siku. Katiba hiyo hiyo ndiyo imekuwa inawekewa viraka viraka viraka kufiti serikali ya TANU, na tena baadaye serikali ya CCM na baadye vyama vingi. Vifungu vikubwa vya katiba hiyo vimebaki kuwa vile vile na hivyo kuwa vinamfanya rais awe mamlaka kama yale aliyokuwa nayo malkia wakati wa katiba ya Uhuru. Sasa tunapopata rais ambaye anaamua kutumia madaraka yake yote kama alivyopewa na katiba tusimlaumu.

Kushindikana kuandikwa kwa katiba mpya baada ya kazi za muda mrefu sana iliyofanywa na Tume wa Warioba lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa nchi. Hali hiyo ilitokana na katiba hiyohiyo inayompa rais madaraka ya kuamua lolote, na ndiyo aliyotumia Kikwete kuunda tume hiyo, halafu akayatumia pia kuua muendelezo huo wa kuandikwa kwa katiba mpya. Swala la kurekebishwa kwa Katiba mpya lilitakiwa lianzie bungeni kusudi liwe na nguvu ya kisheria, siyo kuwa ni utashi wa rais tu..

(b)Raia kuzoeshwa maisha ya mkato mkato na yasiyoheshimu sheria.
Huu ni ugonjwa ulioanza kuingia kwenye jamii mwaka 1983 kutokana na uhaba wa baadhi ya mahitaji kutokana na ugumu wa maisha wakati huo. Ni kuanzia pale ambapo uvunjaji wa sheria ili kujipatia pesa za haraka haraka kimkatomkato ulipoanza na kumsababisha Marehemu Sokoine awe mkali sana kwa kile kilichoitwa wakati huo uhujumu uchumi na ulanguzi. Utawala wa Mwinyi ukahalalisha tabia hiyo kwa sera iliyojulikana zaidi kama "Ruksa." Ingawa lengo lilikuwa ni zuri la kuwapa watu uhuru zaidi wa kuendesha maisha yao, unintended consequences zake zilikuwa ni mbaya mno. Baada ya miaka kumi ya Mwinyi, watu walishaona kuwa hiyo ndiyo order ya maisha. Pesa zote zilizokuwa kwenye mzunguko wa nchi zilikuwa siyo proportional na uzalishaji wa kuwa nyingi zilitokana na viongozi wa serikali kuzikwapua sehemu fulani serikalini kinyume cha sheria, na kuziweka kwenye mzunguko. Alipokuja Mkapa na kuanza kurudisha order kwa kusimamia kwa karibu matumizi na mapato ya serikali watu wakalamika sana na kitu kilichoitwa "Ukapa" wakati huo. Rais Kikwete alirudisha yale ya Mwinyi kwa kulegeza tena usimamizi wa matumizi na mapato ya serikali, jambo ambalo watu walifurahia sana. Sasa magufuli amekuja na udhibiti mkubwa wa mapato na matumiz ya serikali unaona tena tumenza kulalamika kuwa vyuma na nati vimekaza. Tungekuwa na katiba imara inayoonyesha madaraka na mipaka ya watu mbalimbali, basi usimamamizi wa sheria ungekuwa mzuri na hivyo tungekuwa hatutegemei sana hela zinazotoka serikalini kwa njia haramu. Tungekuwa tumeshajijingea utaratibu mwingine wamaisha kuliko huo wa kutegema hela za haramu haramu.
 
(a)Katiba mbovu:
Katiba ya Tanzania leo ni viraka viraka vya katiba ya Tanganyika iliyoandikwa na Nyerere mwenyewe mwaka 1961 huku ikiwa inakaribia ile katiba ya Lancaster House iliyoandikwa mwaka 1960 kwa ajili ya uhuru wa Tanganyika chini ya serikali iliyoongozwa na Governor General akimwakilisha ya Malkia- raia wote walikuwa wanajulikana kama subjects wa malkia. Nyerere alirekebisha vipengele kadhaa kusudi iwe ni kwa Jamhuri ya Tanganyika chini ya serikali inyoongozwa na Rais aliyechaguliwa na wanachi, na ikaanza kutumika mwaka 1962; katiba hiyo ya Nyerere nayo inherently iliacha raia wawe kama subjects wa rais kwa kumpa madaraka mengi sana kuhusu maisha yao ya kila siku. Katiba hiyo hiyo ndiyo imekuwa inawekewa viraka viraka viraka kufiti serikali ya TANU, na tena baadaye serikali ya CCM na baadye vyama vingi. Vifungu vikubwa vya katiba hiyo vimebaki kuwa vile vile na hivyo kuwa vinamfanya rais awe mamlaka kama yale aliyokuwa nayo malkia wakati wa katiba ya Uhuru.
Sasa tunapopata rais ambaye anaamua kutumia madaraka yake yote kama alivyopewa na katiba tusimlaumu.
Mkuu Kichuguu, long time Mkuu. Tume miss sana michango yako kama huu
Nakubaliana nawe 98% ya uliyoeleza. Ninatofautiana nawe kwa hizo 2% katika hayo niliyo bold hapo juu
Rais kutumia madaraka yake yote kwa mujibu wa katiba kama alivyopewa siyo tatizo na si sidhani ni hoja
Hoja ni kwamba je, matumizi hayo yanatumika kama yalivyoaanishwa na katiba? Kwa malkia wanasema 'to the letter''. Hapa naomba nitoe mifano
- Sioni tatizo kama Rais atasaini wafungwa wote waliohukumiwa kifo kunyongwa siku moja. Katiba inamruhusu
-Sioni tatizo kama Rais atatumia 'decree au executive order' kwa mambo kama yalivyoanishwa kikatiba, sioni!
-Leo akiamua kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi sioni tatizo. Katiba inamruhusu
-Sioni tatizo kama wateule wake watakuwa watu wa familia yake na majirani. Katiba inamruhusu

Naoliona tatizo ikiwa Rais atatumia mamlaka na madaraka yake kutenda jambo nje ya katiba
Kwa mfano, ikiwa katiba na sheria za nchi zinaruhusu jambo, na Rais akatumia madaraka yake yote ya kikatiba kulizuia jambo hilo bila kutumia sheria zinazompa madaraka hayo , hapo kuna tatizo na si suala la 'madaraka yote aliyopewa na katiba'
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom