Thadei Ole Mushi; The Hero of Freethinking

Anaonekana Pombe ilikula Inni naziona dalili zote.
 
ULIMWENGU ni jukwaa la mateso kwa watu huru kifikra. Wenye kutumia akili zao kupokea, kutafsiri na kujenga hoja. Wanaounda mitazamo na misimamo baada ya kujiridhisha kwa tafakuri binafsi.

"The essence of the independent mind lies not in what it thinks, but in how it thinks." - "Msingi wa fikra huru hauegemei katika nini unafikiri, bali kwa jinsi unavyofikiri." Ndivyo alisema mwandishi wa UK, Chris Hitchens.

Watu wenye kujitegemea kifikra na kuamua kufuata jambo kwa utashi wa fikra binafsi, mara nyingi hugeuka wapweke. Upo wakati utafikiri tofauti na wengine. Utajikuta upo peke yako. Si ajabu ukazodolewa, hivyo kuifanya dunia kuwa ngumu upande wako.

Dunia ni nyepesi kwa wafuata mkumbo. Upepo unapovuma na wao wanaunga. Hawaumizi kichwa, wakisikia mayowe wanafuata. Akisema fulani, naye anaamini hata kama huyo msemaji ni Kizabizabina.

Thadei Ole Mushi. Mwalimu kitaaluma. Mwandishi na mmoja wa wajenga hoja huru ninaowafahamu na kuwatambua. Soma makala za Thadei. Andiko kwa andiko. Posti zake. Alivyojenga hoja na misingi aliyosimamia. Thadei ni mantiki ya fikra huru.

Hakuona aibu kujisema yeye ni kada wa CCM. Hata sare za chama alivaa. Shughuli za CCM alishiriki waziwazi. Kisha, ungemsoma Thadei akiikosoa serikali, vilevile chama chake. Ni kwa sababu msingi wa fikra zake, haukuegemea alichofikiri, bali jinsi alivyofikiri.

Tembelea akaunti zake, soma posti kwa posti. Kuna mahali aliandika, watu kwa wingi wao, walimpongeza. Kwingine alijenga hoja, watu kwa wingi kabisa walimshambulia, walimpinga na kumpa majina mabaya. Hiyo ndiyo gharama ya kuushughulisha ubongo kwa utofauti.

Abraham Lincoln, alifundisha kusimamia unachokiamini, hata kama kila mtu anafuata mkumbo. Ni somo zuri, ila linaweza kusababisha ugonjwa wa moyo. Fikiria unauona ukweli ambao kila mtu hauoni. Halafu wewe mwenye ukweli, unaitwa majina mabaya.

Nilifahamu Thadei alikuwa katika hali ya kupigania maisha yake kutokana na maradhi ya moyo. Nilijua angenyanyuka akiwa imara. Leo nikapokea habari kuwa Thadei amepumzika. Sikuamini. Binadamu hatujawahi kukikubali kifo.

Kwangu, Thadei ni shujaa wa ufikiri huru. He's a freethinking hero!

Ndimi Luqman MALOTO.
Uzi mzuri sana
 
Kula yule suijui anajiita Malisa ameharibiwa na lugha ya matusi anayotumia
 
SSa
Mkuu,
Lini
Sikuwai kumjua thadei ole mushi personally..

Ila nilisoma makala zake akiwa Mwanza alikua teacher

Nimehuzunika thadei alikua kama Lucas
[QUOTE="Dr am 4 real PhD, post: 49264951, member: 373194"]
Mkuu,
Lini
Sikuwai kumjua thadei ole mushi personally..

Ila nilisoma makala zake akiwa Mwanza alikua teacher

Nimehuzunika thadei alikua kama [USER=674699]Lucas mwashambwa
MWENYEZ MUNGU ampe pumziko jema....

Kumfananisha Thadei na Mwashambwa ni kumkosea Thadei, tofauti yao kubwa ni kwamba Thadei alitoa hoja kutoka Central Nervous System lakini huyu mwingine anatumia digestive system
 
Aliniudhi kudhihaki waliopigwa risasi,kutekwa na kupotezwa, akasahau kwamba sheitwan Hanaga RAFIKI
Hii ni contradiction, Wewe ni mfuasi kindakindaki na shabiki wa kutupwa wa Putin
 
Gilbert Masawe dhambi uliyofanya kumuua Thadei Ole Mushi kwa kumlisha sumu itakutafuna daima
 
Back
Top Bottom