Gilbert A Massawe
JF-Expert Member
- May 14, 2015
- 4,686
- 3,398
RAIS wangu Samia Suluhu Hassan, kwa unyenyekevu mkubwa mama yetu mpendwa, leo ni siku yako ya kuzaliwa. Keki zimekatwa kila mahali nchi nzima kukusherehekea. Hongera sana Rais Samia kwa miaka aliyokuruhusu Allah uendelee kuishi na kuvuta pumzi chini ya jua. Hiyo ni zawadi ya Mungu.
Lakini mama yetu yupo kijana wako, Thadei Ole Mushi ambaye anaishi kwa kutumia mashine hapa KCMC. Moyo wake una-fail kufanya kazi. Ukichomoa tu ile mashine baada ya dakika 20 Ole Mushi atakuwa amefariki. Chumba alicho ninaambiwa ni zaidi ya ICU. Huduma ya kumponya ni Aircraft Ambulance kumpeleka Nairobi ili aokolewe roho yake.
Rais Samia, unaweza kujiuliza Ole Mushi ni nani hasa? Ni wachache sana nchi hii watumiaji wa mitandao ya kijamii wasimjue Thadei Ole Mushi. Huyu ni kada wa kindaki-ndaki wa CCM. Ole Mushi ni muibuaji wa mada na mijadala anuai iliyoisaidia sana CCM akiwa ni Mwalimu kitaaluma. Katika mgogoro wa mkataba wa Bandari na DP World Ole Mushi alisimama na wewe mwanzo mwisho. Maandiko ya Ole Mushi kwa CCM hakuna mwenye shaka nayo.
Ole Mushi moyo umesimama. Anaishi kwa msaada wa mashine hapa KCMC. Msaada ni ama amepelekwe India au Nairobi. Mawaziri wako Ridhiwan Kikwete, David Kihenzile, Dotto Biteko (NW/Mkuu) wametoa msaada wa Hali na mali kasoro Waziri Ummy Mwalimu aliyeshindwa kufanya nafasi yake kama wizara.
Nakusihi Mama yetu sema neno moja kada mwenzetu apone. Ole bado ni kijana na mchango wake kwa Taifa ni mkubwa sana. Walimu wa CWT walipojaribu kukudhalilisha kwa uteuzi wako Ole Mushi alisimama na wewe. Mama mpe keki ya Uhai Ole Mushi naye aishi kukumbuka birthday yako.
Vijana wa upinzani wanavumisha uongo wa kukataa kumchangia Ole Mushi kwamba alipewa sumu na watu wa "mfumo" kwamba afe. Kwamba "mfumo" utafurahi akifa. Hii kashfa mbaya Kwa chama chetu. Mama yetu okoa kwanza maisha ya Thadei Ole Mushi kwa kila unaloweza kufanya kama raia namba moja nchi.
Itakuwa ni faraja ukimpigia wewe mwenyewe mke wa Thadei Ole Mushi kupitia simu namba 0714 742 243 au 0620 300000 Victor Tesha ambaye ndiye yuko pembeni mwa kitanda alikolazwa Thadei Ole Mushi ambaye ameishi na tatizo la moyo kwa muda mrefu bila kujua.
Kama mwenye upendo na utu, sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo Hadi umfikie mama yetu Samia Suluhu Hassan na huo unaweza kuwa mchango wako. Tumuombee Thadei Ole Mushi.
27/1/2024
Mungu Amlinde Thadei