Thadei Kweka aachiwa huru

Thadei Kweka aachiwa huru

AMERICA means PROTECTION of God-given RIGHTS that everybody possess by virtue of being a HUMAN BEING made by God, and no other country articulates that princple as forcefully.

Tucker Carlson
 
Nani kapiga simu? Ubalozi ulimpa support kama raia wake na wakataka asaini zile documents huko mahakamani lakini mkazuia, mkakataa hata mawakili wake wasihudhurie kesi, mkaisikiliza kesi upande mmoja, leo weekend ghafla mmemuachia

Ni uoga wenu tu ndio umefanya mmemuachia.
Comment #16
 
Hii kitu wahuni watakupinga
AMERICA means PROTECTION of God-given RIGHTS that everybody possess by virtue of being a HUMAN BEING made by God, and no other country articulates that princple as forcefully.

Tucker Carlson
 
Unajichanganya, hapa watu wanaonyesha ni kwa kiwango gani mahakama zetu zinapewa maagizo. Inaonekana ww umeumia kwanini huyu imepigwa simu akaachiwa. Hii ni proof ya alichosema Rostam.
Hapana mkuu, quinine cmnt#16 amesema "imepigwa simu moja tu...." Sasa ndio nikauliza je kama alivyosema rostam? Ingawa ya rostam ni kashfa na hii ya usa ni sahihi?
Double standard
 
Taarifa ya hivi punde...

Mmarekani mwenye asili ya Tanzania ambaye alikamatwa huko Kilimanjaro kwa ‘maagizo toka juu’, ameachiwa huru jioni ya leo.

View attachment 3524678

KWA KINA:

Thadei Kweka ameachiwa huru leo January 3, 2026 baada ya kushikiliwa Polisi kwa siku 6 kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kupitia group la "What sup".

Thadei ambaye ni raia wa Marekani mwenye asili ya Tanzania alikamatwa December 28, 2025 usiku na kushikiliwa kituo kikuu cha Polisi (Central) Moshi. December 31, 2025 alipandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kupewa AMRI ya kutoa password ya simu yake ili polisi waweze kupekua hilo group la "What sup" alikokuwa akifanya uchochezi.

Hata hivyo Thadei alisema hatambui "What sup" ni kitu gani na hana application ya aina hiyo kwenye simu yake. Pia alisema kutokana na unyanyasaji aliofanyiwa na polisi, alipoteza kumbukumbu ya mambo yake mengi ikiwemo password ya simu yake.

Ubalozi wa Marekani ulituma fomu maalumu (Consular Notification and Access Form) ambayo Thadei alitakiwa kusaini ili Serikali ya Marekani iweze kuwa "involved" kwenye kesi yake. Ni kawaida Marekani kufuatilia kesi yoyote inayohusu raia wake. Lakini polisi walikataa asisaini.

Jana Mawakili wa Thadei wali-file "Habeas corpus" ili kuwalazimisha Polisi wamfikishe mahakamani. Pia Ubalozi wa Marekani ukataka kujua kwanini Thadei hajasaini "Consular Notification and Access Form" ili waweze kufuatilia kesi yake. Haraka sana Tahdei akapewa fomu ya ubalozi akasaini jana, na leo ameachiwa huru
Kama ameachiwa basi tanzania raia wake wanaonewa kweli. Yaani tunaonewa na vionvozi wetu wanaotutawala. Mtanzania anakamatwa kwa twitter tu aliyoposti watu wanakaa kuamua afe au aishi. Huyo kweka wamemwacha kwa sababu anapassport ya marekani. Aisee watanzania lazima hili jambo litufikirishe sana. Vijana wengi wanateswa nakupotezwa kwa msg za kwenye mitandao tu. ingekuwa hizo msg zina madhara nadhani usalama wa marekani ungekuwa hatarani kuliko nchi yoyote duniani maana raia wake wanaongoza kwa kumpiga madongo rais wao. Wakina chaula wanakufa tu hivihivi kisa kuchoma karatasi alilochora mwenyewe. Nchi yetu watu wa usalama ndo wanaamua mtu aishi au afe. Hii kitu inaumiza sana.
 
She is everything, utasikia pesa ya mama, barabara ya mama kwanini akwepe hii ishu, mama ndiye alitoa order ya kukamatwa.
Ukamataji, mauaji, utesaji na ufiraji ni AMRI YA MAMA pia
 
Huyu nae vipi
G58PaCoXIAESJ1H.jpg
 
Back
Top Bottom