Arafat
JF-Expert Member
- Nov 17, 2009
- 2,581
- 758
... Je Watanzania tunasimamia vipi kupigania utu wa watu wetu? should we? au nani atatukumbusha kusimamia utu wa watu wetu wakinyanyaswa, wakidhalilishwa na kupata ubutu wa utawala wa kifisadi? Je ufisadi si adui mkubwa wa utu wa mtu? Isn't corruption the greatest enemy of the dignity of man?It is, for sure; na ndio maana mara zote tumesema tunapambamba kujinasua kutoka katika mikono ya hawa wakoloni weusi.
Mwanakijiji nimekupata, na hapo ndipo baadae palipo zaa siasa ya kutofungamana na upande wowote, maana sisi msingi wetu umejengwa juu ya utu wa mtu na si siasa za magharibi wala mashariki!
Usawa wa Kiutu ambao pia hata wakomunisti walikiri kuwa aina ya ujamaa wa Mwalimu Nyerere ni wa kipekee haufanani na wao, yeye mwenyewe akiupambanuwa kuwa ni ujamaa wenye asili ya ubinadamu unajengwa juu ya utu na misingi ya familia moja. Nadhani familia moja leo aipo na hakuna kiongozi anaye jali shida za wananchni wake kama za familia yake. Mwalimu yeye akisema kama watanzania wanalala njaa basi na watoto wangu watalala njaa, aina ya elimu wanayosoma watanzania ndio pia watoto wangu wataisoma; leo tumeona hawa watawala wetu wakitoa elimu duni hapa ndani ya nchni na watoto wao wakisoma ng'ambo! Leo tumeona watoto wao wanapomaliza shule tu wanakuwa mamilionea na wanamiliki mitaji mikubwa wakati watoto wa wakulima na wafanyakazi wakizeeka bila hata mitaji ya kukaangia vitumbuwa.
Heshima yako Mkuu umenirudishia hisia lakini kila nikikumbuka napata hasira na kulia.