Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,362
- 1,130
Nitarudi kujibu baadhi ya maswali ya Mwijage hapo juu.
Kuhusu swali la msingi kwa ufupi jibu ni kuwa Tanzania imejengwa katika msingi wa UTU wa MWANADAMU (THE DIGNIqTY OF MAN). Hii ni falsafa ya juu kidogo kuliko wale waliopigania tu "USAWA NA HAKI ZA WATU". Fikiria kidogo; mtu anaweza kukubali kuwa uko sawa naye mbele ya haki (equality in justice) lakini asikuthamini kama mtu mwenzie. Kwa mfano, mtu anaweza akasema "binadamu wote ni sawa" lakini inapokuja swali la kukuozesha binti yake au binti yako kuolewa kwao anakuona hauko sawa kwa sababu ya rangi, dini, hadhi, cheo n.k Kimsingi anakubali mko sawa kisheria lakini hamna utu sawa! !
MMM,
Umegusa kwenyewe kabisa!!
Na nilazima jaribio lolote la kuikomboa hii nchi kuirudisha kwenye HESHIMA na USTAWI wake wa Kweli kwa kila Mwanachi Lianzie hapo ...lipitieee hapo na kumalizikia hapo!! ...KWENYE UTU!!
Inatakiwa Tafakari ya Kitaifa kuhusu hasa maana ya UTU,*Lazima kuwa na MJADALA WA KITAIFA KUHUSU UTU NI NINI
Unajua nini ... Ingawa UTU ni tunu muhimu kwa mwandamu ... Ni ajabu tukisema tujadii UTU ni Nini ...Utasikia Kuna mtu hajui kuwa UTU ni Nini,...Ambayo Its shame...Mtu kutojitambua kiasi hicho.... UTU hauko kwa mnyama yeyote ila kwa mtu tu!! Na hilo ndilo linaufanya Ubinadamu na Unyama kuwa Tofauti ..Ndio ..UTU NI UUNGU NDANI YA MTU ...Thamani ambayo hakuna kiumbe chcochcote kinachoweza kutambua na kufikia. Hivyo , Lazima hiyo dhamani ijitokeze kwenye kila nyanja ya Ustawi na maisha ya jamii ya kitanznaia.
NB .. Ni Muhimu kuwepo tafakari ya kitaifa kuhusu DHANA YA UTU!! Mjadala wa kitaifa kuhusu UTU NI NINI KAMA MSINGI NA NGUZO YA UJENZI WA TAIFA!!
Hivi kweli Tunajidili vipi kuhusu Kupata katiba ya Nchi Huku Hatujui FOUNDING PRINCIPLE za TAIFA... I am telling you we will miss it all again!*Maana hiyo katiba kwa kifupi ni ingekuwa ni Tafsiri ya utu kwenye nyanja zote za katiba hiyo!!
Vinginevyo tutatengeneza katiba inayowafaa Nyani na tumbili wa mwituni kwani Pasipo na UTU kuna ufisadi usio na tofauti kubwa na unyama wa porini.
Lakini katiba iliyosimamia misinigi ya UTU ni katiba iliyosimamia UUNGU na kutupa kiburi kuimba MUNGU ibariki Tanzania. Na UTU hauna dini, hauna itikadi ya chama, UTU hauna Kabila , UTU hauna JINSIA, UTU hauna Kanda, UTU ni MMOJA KWA KILA MTU ...Nani haoni maana ya Utanzania_
Utanzania ni UTU ...Utanznaia ..sio kabila, Utanznaia, sio dini, Utanznaia sio Ukanda, Utanzania sio Jinsia UTANZANIA NI UTU!!
MIMI NAABUDU KWENYE UTU NA DINI YANGU NI UTANZANIA ... !!