Je, hip hop ndio mziki bora wa wakati wote? Vipi kuhusu misingi yake?

Dj Aiman

Member
Dec 21, 2022
23
13
Hip hop ni aina ya muziki unaoelezea aina ya usanii na utamaduni uliyotokana na jamii ya Wamarekani Weusi na Walatino kunako miaka ya 1970 mjini New York City, hasa katika kitongoji cha Bronx na badae katika miji mikubwa yote Marekani alafu Dunia nzima.Muziki wa hip hop pia huchukua tabia (mwenendo) wa staili za muziki wa pop, yaani kama disko na reggae.

Muziki wa hip hop awali ulianzishwa na Ma-DJ waliokuwa wanatengeneza midundo kwa kutumia mtindo wa kurudirudia na kusimama (hasa katika visehemu vidogo vya muziki wa kusisitiza mwelekeo wa kigongoma) kwenye turntable mbili, hasa hujulikana kama kusampo muziki.

Hii baadaye ikaja kusindikizwa na "rap", mtindo wa wizani unaotoa maneno au mashairi yaliyo kwenye vipimo vya mstari ulalo wa nota 16 katika fremu ya muda, ikiwa sambamba na beatboxing, maujanja ya sauti hutumika hasa katika kugezea mfumo wa midundo na elementi za muziki mbalimbali na mautundu na vionjo kadhaa kutoka kwa Ma-DJ wa hip hop.

MISINGI/NGUZO TANO ZA HIP HOP
1.DJing (Hapa namuongelea DJ)
2:Uchoraji
3:MC (Msanii wa HIP HOP)
4.Dance
5:Ujumbe
Hapo kwenye ujumbe ndo kunajibu la swali letu la msingi la siku ya leo linalo uliza kuwa, Je hip hop ndio mziki bora wa wakati wote?.

Utamaduni huu ulianzia nchini marekani katika maeneo ambayo watu wa tabaka la chini walikuwa wakiishi.Waafrika wenye asili ya kimarekani ambao walikuwa wakiishi magettoni katika maeneo wanamoishi watu wa kipato au tabaka la chini waliamua kuanzisha utamaduni huu ili kuweza kuwasilisha mataizo na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili katika maisha yao kwa njia ya sauti.

Mziki huu ulilenga zaidi kuelezea maisha halisi ya watu kwenye mitaa, kama vile masuala ya ukosefu wa ajira, ubaguzi wa rangi, masuala ya wizi na unyang'anyi, ukosefu wa elimu, nk.

Baadhi ya waandishi wanadai kwamba utamaduni wa hip hop ulianzishwa na akina DJ Kool Herc pamoja na DJ Afrika Bambaataa.

Hata leo hip hop bodo ipo katika misingi inategemea tu wewe umeamua kuwasikiliza wasanii gani,Kwani kuna wanao fuata hizo nguzo tano ambayo ndiyo misingi ila kunawasio fuata,Hao ndio maMc wanao haribu Hip Hop. Pia Kuna baadhi ya mashairi ya muziki wa hip hop yanayozungumzia wahuni, uhalifu, na utumiaji haramu wa madawa ya kulevya, Hii iko nje ya misingi.

Hivyobasi Hip Hop ni maisha na maisha ni misingi, Kwaleo nakuachia jina moja tu la msanii anayefanya hip hop ya kweli Tanzania ambaye ni Edger Vicent AKA Dizasta Vina.Kupitia makala hii naamini umejua Hip Hop ni nini na misingi yake ni ipi.

Hivyo nawewe unaweza kuniandikia oroza ya wasanii 5 Tanzania wanao fanya/walio fanya Hip Hop alisi adi sasa na wengine wa5 Duniani kote.

Asante

Screenshot_20221231-101436~2.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom