TGIF: Je unaijua Misingi iliyoliunda Taifa letu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
Kila taifa lina misingi yake. Misingi ambayo husimama kama maono ya aina ya taifa gani watu wanalitaka kujenga na wananchi wake hujitahidi kuifikia hiyo. Kwa mfano Wamarekani wanachukulia Tangazo la Uhuru na kauli za waasisi wao kuweza kuona misingi yao. Mambo kama Uhuru (liberty) na haki za mtu (individual rights) ni misingi ya Wamarekani.

Je Tanzania ina misingi gani? Je unaifahamu? Je unafahamu Kanuni Nne za mahusiano ya Tanzania? Je unajua ilimaanisha nini kusema wewe ni Mtanganyika au Mtanzania (baada ya Muungano)?

Je umewahi kujifunza misingi hiyo ukiwa shuleni au chuoni?

PICHA ZA IGUNGA

igunga1.JPG gavana_wa_bot2.jpg naibuwaziri.jpg wodi.jpg

Picha za Igunga Mgongoro, Kata ya Igunga

igunga3.jpg igunga4.jpg igunga5.jpg
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
Hivyo vilikuwa vinajibu swali la "ili tuendelee tunahitaji victus vingapi?". Mambo mengi tunayoyaona leo kuhusu viongozi wetu yanahusiana na kuacha misingi ya taifa. Naweza kuweka dau dogo la dola mia na hakuna mtu anaweza kusema misingi hiyo ilianishwa wapi na ni ipi hasa. Azimio la Arusha lilikuja baadaye baada ya misingi hiyo kuanishwa karibu miaka mitano nyuma.
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
Mkuu kabla ya azimio la arusha tulikuwa na misingi kweli? Labda uhuru ni kazi
 
Obe

JF-Expert Member
Dec 31, 2007
9,654
33,169
Kutokujua misingi ya taifa letu (siyo tatizo la vijana pekee) hata waliopo madarakani sasa hawajui misingi inayounda taifa letu, misingi ya USAWA (HAKI) na UMOJA. na ni kutokana na hali hii hakuna anayewajibika kwani, kwanza, hatujitambua zaidi ya kuongea kiswahili
 
Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
729
Kila taifa lina misingi yake. Misingi ambayo husimama kama maono ya aina ya taifa gani watu wanalitaka kujenga na wananchi wake hujitahidi kuifikia hiyo. Kwa mfano Wamarekani wanachukulia Tangazo la Uhuru na kauli za waasisi wao kuweza kuona misingi yao. Mambo kama Uhuru (liberty) na haki za mtu (individual rights) ni misingi ya Wamarekani.

Je Tanzania ina misingi gani? Je unaifahamu? Je unafahamu Kanuni Nne za mahusiano ya Tanzania? Je unajua ilimaanisha nini kusema wewe ni Mtanganyika au Mtanzania (baada ya Muungano)?

Je umewahi kujifunza misingi hiyo ukiwa shuleni au chuoni?

Misingi yetu ni Uhuru na Umoja
Dira yetu ni Ujamaa na Kujitegemea
Mimi na wewe tunakumbuka tumefundishwa sana mashuleni na kipindi tuko JKT. Labda vijana wa kizazi cha hivi karibuni watueleze wanafundishwa nini siku hizi?
 
Entrepreneur

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
1,087
612
Kwa ninavyokumbuka, miaka hyo tulikuwa na party suprimacy.

Sasa misingi ya utaifa ilikuwa reflected kwenye mambo ya kichama zaidi (ccm).

Nadhan kadi ya uanachama ya ccm (upande wa nyuma) inatoa misingi hiyo kwa muhtasari. Mwenye hiyo kadi atuwekee hiyo mistari hapa. Mimi ninakumbuka mmoja.
1. Binadamu wote ni Sawa.
2.
3.
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
Misingi yetu ni Uhuru na Umoja
Dira yetu ni Ujamaa na Kujitegemea
Mimi na wewe tunakumbuka tumefundishwa sana mashuleni na kipindi tuko JKT. Labda vijana wa kizazi cha hivi karibuni watueleze wanafundishwa nini siku hizi?

Mkuu usipopata hiyo dollar 100 mimi nitaandamana. Uhuru na Umoja ndio hasa manake upo kila mahala. Nembo ya Taifa letu imebeba maneno hayo mujarabu.
 
Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,615
Kila taifa lina misingi yake. Misingi ambayo husimama kama maono ya aina ya taifa gani watu wanalitaka kujenga na wananchi wake hujitahidi kuifikia hiyo. Kwa mfano Wamarekani wanachukulia Tangazo la Uhuru na kauli za waasisi wao kuweza kuona misingi yao. Mambo kama Uhuru (liberty) na haki za mtu (individual rights) ni misingi ya Wamarekani.

Je Tanzania ina misingi gani? Je unaifahamu? Je unafahamu Kanuni Nne za mahusiano ya Tanzania? Je unajua ilimaanisha nini kusema wewe ni Mtanganyika au Mtanzania (baada ya Muungano)?

Je umewahi kujifunza misingi hiyo ukiwa shuleni au chuoni?
Swali zuri sana MMM na kusema kweli tunapoanza kubabaika na swali kama hili inaonyesha wazi kwamba tumeupoteza Uhuru wetu.
Kama sikosei jibu lako lipo ktk - Nembo ya Taifa...
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,371
2,471
Uhuru na umoja, uhuru ni kazi, binadamu wote ni sawa, rushwa ni adui wa haki.......
 
Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,582
755
Duh Mwana Kijiji! Let me bet: - Before Arusha declaration I think our moral was laid on
  1. Work and Self-reliance: That our development will depend on our own resources!
  2. Equality: Only on that basis we can work cooperatively.
  3. Freedom: Freedom to all; because the individual is not served by the society unless it is his society.
  4. Unity: Unified society where members live and work cooperatively in peace, security and well being.
If my bet is true then the 100$ prize should be donated to the JF.
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Kila taifa lina misingi yake. Misingi ambayo husimama kama maono ya aina ya taifa gani watu wanalitaka kujenga na wananchi wake hujitahidi kuifikia hiyo. Kwa mfano Wamarekani wanachukulia Tangazo la Uhuru na kauli za waasisi wao kuweza kuona misingi yao. Mambo kama Uhuru (liberty) na haki za mtu (individual rights) ni misingi ya Wamarekani.

Je Tanzania ina misingi gani? Je unaifahamu? Je unafahamu Kanuni Nne za mahusiano ya Tanzania? Je unajua ilimaanisha nini kusema wewe ni Mtanganyika au Mtanzania (baada ya Muungano)?

Je umewahi kujifunza misingi hiyo ukiwa shuleni au chuoni?

Wasiwasi wangu ni kwamba utaishia ku-quote speeches na maandiko za mwana jumuia mwenzako (a.k.a. mtakatifu nyerere) kama mising ya taifa...too late no going back..

Taifa letu si yeye na wala yeye siyo authority ya kuunda taifa letu..

Tutaandaa mising yetu yenyewe wala si matokeo ya ccm ya nyerere a.k.a chadema
 
Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,552
774
RUSHWA
UBADHIRIFU
UBWANYENYE
UFISADI
USIRI KWENYE KILA KITU (KUTOKUWA WAWAZI)
SIASA KUENDESHA UCHUMU

hiyo ndio misingi ya taifa letu na ndio imetufikisha hapa tulipo
 
We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
797
363
MM mimi nadhani kama taifa, tulikuwa hatuna misingi, ila tu tumekuwa na misingi ya kiitikadi na kichama zaidi na imekuwaikibadilika siku hadi siku, ndiyo maana watanzania wengi hatujui maana ya Uzalendo au utaifa wetu kama watanzania. Hakuna anayeweza kusisimama kutoka chama chochote kile, Dini yoyote ile au Kabila lolote lile akaonyesha uzalendo wa Mtanzania ni upi. Tofauti na wenzetu wa Taifa kama Marekani, popote utakapo kutana na mmarekani, cha kwanza ni kuuonyesha uzalendo kuwa yeye ni Mmarekani bila kujali antoka ktk kabila, Dini au chama gani. Kwa hiyo Mzee Mwanakijiji, mimi nadhani Msingi mkuu ulikuwa ni ule Uzalendo kuwa Mtanzania, ambao kwa kweli hatukukua nao na wala hata sasa haupo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Top Bottom