Majok majok
JF-Expert Member
- Aug 3, 2023
- 618
- 1,570
Kwakweli Hawa watu ni makatili sijawai Kuona, walikuwa wametega mtego mbaya sana dhidi ya yanga lakini wameferi na wameshindwa vibaya sana.
Hii ratiba aikupangwa kwa bahati mbaya bali walikuwa wamedhamilia na walikuwa na Nia mbaya kabisa, yanga kacheza na Azam baada ya siku tatu kacheza na singida, baada ya siku 5 kacheza na Simba baada ya siku 3 akasafiri kwenda tanga kucheza na coast union, mechi 4 ngumu ndani ya siku 13.
Wanayejitahidi kumbeba abebeki ni Kama gunia la misumali mgongoni, kacheza jumapili lakini yeye anacheza siku inayofata na Yuko dar lakini anayesafiri ndiye kacheza kabla ni mambo ya kishamba sana haya!
Walikuwa wanajua yanga lazima adondoshe point kwa Azam wakaferi, wakajua waipange mechi ya singida karibu ili kusudi wasipodondosha kwa Azam basi wadondoshe kwa singida kwakuwa watakuwa na uchovu mwingi napo wakapigwa za uso, imekuja mechi ya Simba wakaaibishwa.
Wakapanga yanga ikutane coast union ndani ya siku 3 ili kusudi wakishindwa kudondosha kwenye derby wasafiri kwenda tanga na wakutane na UGUMU wakiwa wametoka kutumia nguvu kubwa kwenye mechi ya derby ili waache point ata sare napo wamelambishwa mchanga🤣🤣🤣
Siku zote Giza aijawai kuishinda Nuru mtaendelea kushindwa Kila mtapokuwa mnapanga mipango miovu na Yanga ni mpango wa mungu, ingekuwa ndio iyo timu yenu imekutana na hii ratiba Sasa hivi mngekuwa mnaomboleza parapanda kolowahed.