TFF imemfungia Nyoso kwa miaka miwili kucheza mpira wa miguu

Kumfungia miaka miwili si kumuua kabisa jamaa.Mi naona angefungiwa miezi kadhaa lakini apewe counselling ya nguvu katika muda huo.Maana jamaa inaonekana ni kawaida kwake kufanya vitendo vya kihuni.Jamaa inaonesha kapata malezi mabovu utotoni

kamati imekuwa linient Sana kwa huyu shetani, alistahili life ban na faini ya 10m na kufunguliwa shtaka la shambulio la aibu. Wananchi wamfuatilie kwa karibu huyu shetani nyoso Ni hatari kwa watoto mitaani!! Kama anathubutu kuwafanyia hivyo watu wazima kama Bocco! He is a pervert! Atengwe kwenye jamii.
 
Mara ya tatu hiyo. Alianza na Amir Maftah,Maguli then Bocco

duh! hafai kabisa kuwa mchezaji! sheria ipo vipi kwa kosa kama hilo haswa baada ya adhabu ya TFF maana sioni kama inamtisha wala hajatendewa haki kwa kosa alilofanya halisemeki' watu alio wakosea wana familia wana ndugu wana majamaa na mabosi huoni kuwa ame wafedhehesha wenzake kiasi kisicho ongeleka
 
duh! hafai kabisa kuwa mchezaji! sheria ipo vipi kwa kosa kama hilo haswa baada ya adhabu ya TFF maana sioni kama inamtisha wala hajatendewa haki kwa kosa alilofanya halisemeki' watu alio wakosea wana familia wana ndugu wana majamaa na mabosi huoni kuwa ame wafedhehesha wenzake kiasi kisicho ongeleka

Angepelekwa mahakamani iwe somo kwa wavuta bange wengine
 
Hiyo faini hailipiki Mkuu. Jamaa kafungiwa miaka miwili kucheza soka, hakuna shaka faini hiyo inatakiwa ilipwe baada ya hiyo miaka miwili kutimia ili arudi uwanjani. Ukimwangalia Nyosso pale alipo baada ya miaka miwili atakuwaje? Huyu hatacheza tena hivyo hana sababu ya kulipa faini ya hiyo milioni mbili. Labda TFF imbane sasa hivi ailipe, lakini najiuliza tayari ameshafungiwa asipolipa atapewa adhabu gani?

Kwa maoni yangu adhabu pekee inayotekelezeka ni kufungiwa kucheza soka miaka 2 hiyo ya fedha haitekelezeki!

ungekuwa umetiwa ww dole ungempa hiyo adhabu na faini kiasi gani!? upopobawa huo! wazazi, watoto, ndugu, jamaa, marafiki, mabosi wenzako wote na wananchi wenzio wameshudia ulivyo fanyiwa upopobawa hadharani alafu unasema adhabu aliyopewa ni kubwa' naamini mbali na mpiga dole kutokucheza kama ni ww ungepigwa dole ungesha chimba kaburi either la aliye kupiga au lako maana hapo adhabu alizo pewa hazina maana!
 
Sikubaliani kabisa na vitendo vichafu vya Nyosso lakini tuambiwe kanuni gani imetumika kutoa adhabu ya miaka miwili na faini ya million mbili.
Kama kanuni ni dhaifu zifanyiwe kazi haraka. Kimsingi Nyosso kafungiwa maisha labda kwenye ndondo.

KANUNI ZA TFF
Kanuni ya 37 Kifungu cha 24 cha Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2015 kinasema: “Mchezaji yeyote atakayepatikana na hatia ya kufanya makosa makubwa ya kimaadili au kinidhamu, au ya kibaguzi au ya kidhalilishaji au yatakayotafsiriwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za mchezo na ubinaadamu atatozwa faini kati ya shilingi milioni moja mpaka milioni tatu au/na kusimamishwa kushiriki michezo mitatu mpaka kumi ya klabu yake yoyote atakayoitumikia katika Ligi Kuu na mashindano mengine rasmi ya TFF au kufungiwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miwili.”
 
Mimi naona haitoshi,angefungiwa maisha kucheza soka.
Mpuuzi mkubwa huyo.

Mimi Naona Angefungiwa Mechi Moja Tu Tena Iwe Ni Kipindi Cha Kwanza Na Kipindi Cha Pili Aingie Kukipiga Na Kama Ni Faini Basi Apigwe Tsh 1,500/ Tu ILI Kulinda Kipaji Chake. Beki Ya Nyosso Inanikumbusha Mno Beki Yangu Nikiwa UMISETTA Shighatini Ngome Ya UKAWA Mkoa Wa WANAONGOZA KWA UBAHILI Nchini Tanzania, Bugema Na Kabojja Secondary Nchini Uganda Huku Tukiwakomaza Watu Kama Akina Andrew Mukasa, Henry Mwesigwa Na John Nsubuga Wakati Huo Akina Owino, Okwi, Kiiza, Brian Majwega, Sentongo Wakiwasumbua Tu Mama Zao Ktk Mabeseni Ya Kuoga. Natamani Nirudi Tena Ktk Kandanda Tuka JumaNyossoane Vizuri.
 
John Bocco nae alistahili adhabu..Mtt wa kiume unapigwaje kidole halafu unatulia tu..

Nyosso Alikuwa Anawaweka Sawa Vijana Tena Hasa Kupitia Kwa Nahodha Msaidizi Huyo Wa Taifa Stars Kuwa Lazima AGANGAMALE Ili Mechi Zijazo Za Timu Ya Taifa Asiwe Anacheza NYORONYORO. Nyosso Alikuwa Anasambaza UJUMBE Tu Wa KIUMENI Kwa Vitoto Vya Siku Hizo Vibishoo Vinavyocheza Soka Kwa Maringo. Tuliocheza Mpira Wala Hatulalamiki. Watu Mlivyo WANAFIKI Humu Leo Nyosso MNAMLAUMU Hivi Mbona HAMLALAMIKI Tambwe ALIVYOMCHOMA VIDOLE VYA MACHONI YULE MCHEZAJI Wa JKT Ruvu Hadi AKATOKWA Na Damu? Kama Hiyo Mmesahau Mbona HAMPIGI KELELE Kitendo Cha Juzi Ktk Kariakoo Derby Ambapo Mshambuliaji Wa Yanga Ambae Ni BWABWA Donald Ngoma Alimpiga KICHWA Tena Kwa MAKUSUDI Beki Namba Mbili Bora Kwa Sasa Nchini Tanzania Ramazan Hassan Kessy Hadi Nusura AMTOE JICHO? Mmeiona Hii Tu Ya Nyosso? Wanafiki Wakubwa Nyie MLIOTUKUKA.
 
Huyu Nyoso ni mvuta bange. Wangemfungia hata maisha. Hatuhitaji vichaa kama hawa kwenye mpira wetu.

Kwani Bangi/Bange Ni Mbaya Mkuu? Mbona WAFUASI Wengi Wa UKAWA Tena Wale Wanaoandamana HUITUMIA Sana Ktk Amsha Amsha Yao?
 
Naunga mkono hoja yako 100%.

Michezo ni furaha na si kudhalilishana wala uhasama.

Watu wanaoharibu jina la "mchezo" kama huyo mjinga wafungiwe maisha. Anashindwa kuelewa kuwa wanamichezo hususan mpira hapa kwetu wana influence kubwa sana kwa vitendo vyao kwa watoto.

Kuna siku mjukuu wangu alinambia "nataka kunyoa kama Baloteli", nilikuwa simjuwi ndiyo nani, akanambia ntakuonesha akioneshwa kwenye TV, mimi sikusubiri anioneshe nikaenda ku google, nikamuona Baloteli na alivyonyoa, kwanza nilicheka nikamwambia mjukuu wangu hapo utanisamehe sana, sikupeleki ukanyoe kiwazimu namna hiyo. Akanambia "mbona Baloteli kanyoa hivyo kwani yeye mwenda'zimu?". Nikakosa la kumjibu.

Nimeelezea hicho kisa kuonesha ni vipi hawa wachezaji wanaweza kuathiri jamii.

Kitendo alichokifanya si chema kabisa hafai kurudi uwanjani ukichukulia kuwa si mara yake kwanza kufanya hivyo, nimesoma sehemu kuwa alishawahi kufungiwa kwa kitendo kama hicho, hajakoma.

Kinachofatia atakuambia anataka afanywe kama bocco kitu ambacho cyo kizuri, heshima ianzie nyumbani
 
Kumfungia miaka miwili si kumuua kabisa jamaa.Mi naona angefungiwa miezi kadhaa lakini apewe counselling ya nguvu katika muda huo.Maana jamaa inaonekana ni kawaida kwake kufanya vitendo vya kihuni.Jamaa inaonesha kapata malezi mabovu utotoni

Donald Ngoma Kumpiga Kichwa Cha MAKUSUDI Ramazan Kessy Na Amis Tambwe Kumchoma VIDOLE Vya Machoni George Mikael Wao Walipata MALEZI MAZURI UKUBWANI?
 
KANUNI ZA TFF
Kanuni ya 37 Kifungu cha 24 cha Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2015 kinasema: "Mchezaji yeyote atakayepatikana na hatia ya kufanya makosa makubwa ya kimaadili au kinidhamu, au ya kibaguzi au ya kidhalilishaji au yatakayotafsiriwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za mchezo na ubinaadamu atatozwa faini kati ya shilingi milioni moja mpaka milioni tatu au/na kusimamishwa kushiriki michezo mitatu mpaka kumi ya klabu yake yoyote atakayoitumikia katika Ligi Kuu na mashindano mengine rasmi ya TFF au kufungiwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miwili."

Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu. Nadhani wametoa adhabu kwa kuzingatia kanuni /sheria.
Kwa umri wake mpira ndiyo kwa heri tena. Atafute kazi nyingine lakini ajue kila kazi ina maadili yake pia.
 
Hata ndondo hachezi? Bas ccm wamchukue awafanyie kampeni tu, mbona basata imemfungia shilole lkn ccm imemchukua awakatie mauno??
 
hupendezi na uzuri wako kuwa na roho ya kikatili kama hiyo...usisahau nyoso ana mke na watoto wanamtegemea acheze mpira wale wavae wasome...maisha ni adhabu kubwa sana...sawa na kuuwa familia yake.

Nilichogundua Ni Kwamba Wengi Mnaojifanya Kulalamika Humu Hamjacheza Na Hamjui Mpira Zaidi Tu Ya Kuwa Mashabiki Na Kuukodolea Ktk Runinga. Luis Suarez Aling'ata Mara Ya Kwanza Akaadhibiwa Na Akarudia Tena Je Alipoadhibiwa ALIPEWA ADHABU Ya Miaka Miwili Kama Hii Ya Beki Wangu NINAYEMKUBALI Kiboko Ya Vijana NYORONYORO Juma Nyosso? Naomba Nipate Justification Yenye HOJA Ya KUTUKUKA ITAKAYONISHAWISHI Ya Kitendo Cha Kung'ata Cha Suarez Na Kupiga Ndole Wachezaji Cha Nyosso. Adhabu Ya Nyosso IMECHAGIZWA Mno Na Media Ambazo Hizo Hizo Huacha Matukio Ya Wachezaji Wa Timu Kubwa Hapa Nchini Wenye Hizo Tabia Chafu. Nani Ambae Hajui Kuwa Mchezaji Kama Kelvin Patrick Yondani Ndiyo Kinara Wa NYOSSO Formula Ktk Ligi Ya Hapa Bongo? Huyo Mpiga Picha Saleh Ally Kwanini Kamera Yake Huwa Pia HAILEKEZI Kwa Yondan? Tuache UNAFIKI Na Tuwe Fair. Nyosso Angekuwa Anachezea Simba au Yanga TUNGETOKWA NA MISHIPA Ya SHINGO Hivi KULALAMIKA?
 
Anajua sana kutumia vidole so atanunua kapu na rangi za kucha aanze kusugua wadada miguu na kuwaremba. . . . ..

Au mchukue mpeleke kozi ya kufuma huko wanatumia zaid vidole. . . . .

Acha apotee . . . .
Jibu lako nimelipenda mkuu. Inakera kuona watu wanaleta utani kwenye tabia za kukemea :angry:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom