TFF imemfungia Nyoso kwa miaka miwili kucheza mpira wa miguu

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,146
13,216
Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.

Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.

Klabu ya Young Africans imepigwa faini ya shiligi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.

Wachezaji waliopata kadi za njano wa Young Africans katika mchezo huo ni ni Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.

Aidha klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya shilingi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.

Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.

Simba pia inapigwa faini baada ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.

Mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.

Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=

Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)

Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).

Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports kocha wa Stand United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.

Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni

i. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari

ii. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon

iii. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na

iv. Sultani Kasiras badala ya Adam Said

Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo.

Safi sana. Nashauri hiyo faini apewe John Bocco kama kifuta jasho chake cha kudhalalishwa.

Iwe fundisho kwa wengine.

jamaa kapendelewa sana, afungiwe maisha ili akili imkae sawa, hajui kuwa mpira ajira ndo tatizo la kukosa elimu+nidhamu kwa baadhi ya watu, mpumbavu sana huyu mchezaji. SINTOTEGEMEA KUONA KUNA MTU ANAM SUPPORT KWA TUKIO KAMA HILI.

jamaa kapendelewa sana, afungiwe maisha ili akili imkae sawa, hajui kuwa mpira ajira ndo tatizo la kukosa elimu+nidhamu kwa baadhi ya watu, mpumbavu sana huyu mchezaji. SINTOTEGEMEA KUONA KUNA MTU ANAM SUPPORT KWA TUKIO KAMA HILI.

Ana miaka mingapi Nyosso

Hiyo faini ya wachezaji wa yanga kushangilia upande wa simba ni ya kikoloni

Huyu Nyoso ni mvuta bange. Wangemfungia hata maisha. Hatuhitaji vichaa kama hawa kwenye mpira wetu.

Sikubaliani kabisa na vitendo vichafu vya Nyosso lakini tuambiwe kanuni gani imetumika kutoa adhabu ya miaka miwili na faini ya million mbili.
Kama kanuni ni dhaifu zifanyiwe kazi haraka. Kimsingi Nyosso kafungiwa maisha labda kwenye ndondo.

adhabu aliyopewa haijitoshelezi na kosa kalirudia kwa mara ya pili! hafai kuwa Mchezaji

Sikubaliani kabisa na vitendo vichafu vya Nyosso lakini tuambiwe kanuni gani imetumika kutoa adhabu ya miaka miwili na faini ya million mbili.
Kama kanuni ni dhaifu zifanyiwe kazi haraka. Kimsingi Nyosso kafungiwa maisha labda kwenye ndondo.

Kweli zifanyiwe kazi ili afungiwe miaka mitano na faini milioni kumi. . . .Na aliyefanyiwa kitendo hiko apewe uhuru wa kumpeleka mahakamani kwa mashtaka zaid ya udhalilishaji

atakula lichopanda maana hakuna namna, kumbuka hii ni mara ya pili anafanya kitu ichoicho cha kifedhuri, na mimi nasema nawapongeza sana TFF kwa kumfungia huyu firauni ila alitakiwa kufungiwa maisha

Atakula nini?

Mimi namtetea nyosso khaaaaa!!

Hata mimi hilo limenishangaza...

Hawa watu waTFF sijui wanatumia kanuni za wapi na nani aliyezitunga...

Hiyo faini ya wachezaji wa yanga kushangilia upande wa simba ni ya kikoloni

Similar Discussions

Back
Top Bottom