msuyaeric
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 838
- 1,167
Na Mwl Udadis, Buza kwa Lulenge
Moja ya falsafa ngumu katika uongozi ni uwezo wa kuongoza watu kimageuzi. Rais Samia anaendelea kuiishi falsafa hii kwa weledi na umahiri wa hali ya juu. Nafasi za teuzi siku zote ni dhamana katika kuwatumikia watanzania, dhamana hii inaweza kukabidhiwa kwa mtumishi mwingine kadri itakavyoonekana inafaa na hili tunaliona dhahiri katika mabadiliko ya Mkurugenzi Mkuu wa idara ya usalama wa Taifa.
Kipekee nampongeza Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa anayemaliza muda wake kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa nchi yetu. Utamaduni wa mbio za vijiti ndio lugha ya uongozi wa kimageuzi. Kama ilivyo katika timu bora za soka, sasa anaingia Mkurugenzi mpya kwaajili ya kuendeleza utumishi wake kwa kasi, ari na weledi zaidi.
Baadhi ya sifa za viongozi wengi wanaoteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika utumishi wa umma;
1. Uzalendo, uchapakazi na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu.
2. Kuhakikisha uzoefu na rekodi ya utumishi iliyotukuka katika kuwatumikia watanzania.
3. Kuzingatia taaluma, ubobezi na stadi za fani mbalimbali zinazoendana na mahitaji ya majukumu.
4. Kuzingatia ujumuishi, haki na usawa katika kupewa dhamana mbalimbali za kiuongozi katika majukumu.
5. Kufuata kanuni, miongozo na taratibu za utumishi wa umma sanjari na sheria za nchi yetu.
Naungana na watanzania wote kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiishi falsafa ngumu ya kiuongozi kwa vitendo. Kujitoa katika kutekeleza falsafa ya kimageuzi ni matokeo ya uzalendo na mapenzi makubwa kwa nchi yako, Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda na kukubariki Rais wetu mpendwa ili uzidi kuitumikia nchi yetu kwa mapenzi makubwa.