Tetesi: Jimbo la Kawe Wazi!. Ubunge wa Gwajiboy Kwenye Hati Hati!. Umehang Kwenye Utando wa Buibui!. Ama Achanje Asalimike, Akikomaa, Amwagwa!.

Katika ile list ya kina Dr Mashinji, Paskali,mwijaku, Kayuni, Yusufu mwenda hakuna anaeuweza moto wa sauti ya zege Halima James Mdee. Hakuna hata wa kusimama nae kwenye podium na kufanya mdahalo. Halima ni mashine na kawe walimkubali japo alikuwa na mapungufu ya ubishoo lakini CCM ya mama inahitaji team ya Ushindi na Halima ndio mpiga ngoma mwenyewe sasa.
Ndugu yangu bado hujaifahamu nguvu (clout) ya CHADEMA ilivyokuwa nyuma ya “sauti ya zege”. Leo hii huko bungeni anafanyiwa madharau na kina Tulia kama mtoto aliyeokotwa mitaani. Anaongea point nzito lakini anazimwa na kukumbushwa kumshukuru mwendazake kwa kuwepo kwake bungeni.

Ajaribu kuvaa kijani halafu apite mitaa ya Kawe utauona huo mrejesho. Ataangaliwa kama msukule wa mtukufu Rashid. Itabidi dola itumike na kura za viroba ziletwe kumpa angalau uhai fake wa kisiasa.
 
Leo nikaita Bolt fulani, kumbe ni bolt ya kada. Kada akaona jina langu, hivyo nilipoingia tuu ndani ya gari, dereva akanisalimia kwa kunichangamkia, na kuniuliza, vipi haujaribu tena?, jimbo limeisha tangazwa kichini chini liko wazi!. Askofu Gwajima amemwagwa rasmi, ila haijatangazwa rasmi!.

Mtoaji habari wangu akasema Salama pekee ya Askofu Gwajima kuendelea na ubunge wake wa Kawe ni kujitokeza kuchanjwa hadharani, vinginevyo, it's a gone case!.

"Hivyo kama bado uko interested na Kawe jimbo liko wazi wewe tuu!.

Nilimweleza ukweli wangu, I'm not interested!.
Kiini cha uzi hiki apa!! Yani uzi ungekua hivi tu tayari umebeba maana ya hayo maneno yoote uliyoandika.

Nyuzi zako zina vitu ila maneno yasiyo na tija unaweka mengi mno yanachosha.
 
Back
Top Bottom