Testing KLH Live!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,597
40,372
Tunakesha tukifanya majaribio ya kutangaza "live" kutoka studio zetu mpya... pembezoni mwa jiji la Detroit. Ukiingia kwenye KLH News upande wa kulia chini ya video kuna mahali panasema sikiliza "Live" na chagua player yako halafu nipe feedback.
 
Nasikia wazulu wakiimba.. Je kuna taarifa ya habari ya saa mbili asubuhi kwa saa za TZ?
 
mkuu nasikiliza huruma ya bwana hapa. anasema siatasahau huruma ya bwana iko safi

na qaswiida utuwekee mkuu si mambo haya tu.

halafu mkuu matangazo yako unalipia hapa JF au ndio unapenda dezo
 
Mkuu Mwanakijiji safi sana inapatikana vizuri huku mashariki. Natumaini itakuwa murua kabisa. Tatizo kubwa lililopo ni sauti, unapoongea wewe volume inakuwa kubwa sana tofauti na unaporusha matangazo au muziki. Hali hiyo inanifanya kushika vitufe vya spika mara kwa mara ili kuweka sauti sawa. Otherwise, iko safi hakuna background (is clear bila miungurumo isiyo na maana.)

keep it to the best.
 
hapo sasa hapo ukitutilia na qaswida moja hivi itakuwa shwari nnaomba mkuu ili jumamosi ipite vizuri nikiwa na jagi langu la mtindi mkononi
 
yeah iko shuwari mwanawane hapa mie ndio inasindikiza jagi langu taratiibu u made my day
 
Nashukuru Nziku na nimenotice pia.. mic yangu ina nguvu sana... na nilikuwa naizungumzia karibu.. ni tofauti na ninayotumia kwa matangazo ya kawaida...

Mtu wa Pwani.. ngoja nikuangalizie hapa..
 
mkuu umenikosha

anta nuru ala nuru, anta misbaaah sudurii

maalim asante kama culture wamekataa hata hapa pametosha asante mwanawane


wajaba shukuri alayna
 
Nilikuwa nakupata vizuri... naona mitambo yangu imekatika najaribu kujiunga tena .....
 
sasa hivi kwangu limetokea tatizo inapiga kisha inabuffer muda mrefu au tatizo ni la kwangu
 
jaribu kuliiconnect... ninatangaza kwenye bitrate za juu sana.. wenye high speed ndio watakuwa wanajinoma..
 
Safi kabisa naona tunapata buruduni saaaaaafi hapa! Congrats and keep flying! We can't wait to see this radio taking the lead!
 
Back
Top Bottom