HILI NI TATIZO LA KATIBA, CCM Msajili wa vyama wao, Tume ya uchaguzi wao, mahakama yao, Speaker wa bunge wao, Jeshi la Polisi wao. Referees wao, Laizimen wao, wachezaji wao, washangiliaji wao, watangazaji wao na Uwanja wao. SISI NI TIMU PINZANI TUU. panakazi kubwa kweli hapo
msajili wa vyama vya siasa nchini john tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya cdm na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.
Katika hali ya kushangaza tendwa ameshauri vyama visubiri nyajati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.
Source:habari radio tumaini.
Ule vi Mbaya sana huu
Kunywa Gongo
Kuvuta Bangi ( Tena Kuvutia Bangi Chooni)
Kuvuta Bangi iliyochanganywa na Majani ya Chai na Mapapai
Ugoro
Chibuku na Tambaku
Ni Ulevi Mbaya sana
Acha jazba wewe, ndo siasa hiyo
Huyu naye ana matatizo kichwani kama anafikiri anaweza kukifuta chama cha siasa kwanini asikifute?
Nakumbuka maneno ya marehemu Nyerere aliwahi kusema "ULEVI WA MADARAKA" ndio huu, yaani ameshajiona anaweza akafikiria lolote likawa atakavyo yeye.
Huwa najiuliza inakuwaje raia mwema katika nchi anabadilika na kuwa gaidi!! ukandamizaji demokrasia kama huu ndio unapelekea mtu kuwa gaidi.
Msameheni bure kizee cha watu kinatetea ugali wake!
Wamekosa kitu kimoja tu, nguvu ya umma ambayo ikiamua kuadabisha watawala ni balaa.