Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source:Habari Radio Tumaini.
Akili za kutumwa achanganye na zake kwani nguvu ya umma ilimfika Mubadaraki, Ghadaf, na wengine. Kwa tanzania haiko mbali hata kidogo.
 
kachanganyikiwa anadhani polisi ni chama cha siasa
 
sasahivi itv news (saa 2 kamili usiku huu)

ndugu zangu, nadhani mpango wa kuifuta chadema umewadia, john tendwa( msajili wa vyama vya siasa) anasema, kama chama cha siasa kitakuwa ndio chanzo cha mauaji ya mtu yeyote katika mikutano yake, anasema kwa mamlaka yake aliyonayo atakifuta (Bila shaka anakilenga chadema, na bila shaka ni kuzidi kuwapa nguvu polisi-Bila shaka polisi wataua watu wengi sana katika mkutano wowote ujao wa chadema ili kuhalalisha hili azimio). Baasi naona kweli serikali ya sisiemu wamedhamilia kukifuta chadema, daah nimeishiwa na nguvu ndugu zangu kwa huu ubabe.
 
Kwa mujibu wa msajili wa vyama mh Tendwa chama cha siasa kinachosababisha mauaji atakifutia usajili mara moja hivi anachelewa nini akifutilie mbali chadema ss hv wameshasema wenyewe kuwa wanataka watu wafe kwa kuwaambia polisi waandae silaha mxiiiiiii
 
Na yeye ATAFUTWA. Hilo wala lisikupe wasiwasi.
 
Nami nimeona na nadhani ni njama ya ccm baada ya kuona wamezidiwa nguvu na cdm
 
Ataifuta chadema TZ lakini yeye atafutika duniani au anadhan yeye ataish milele kwanza m2 mwenyew kashazeeka.atutolee bp zake hapa
 
Sio rahisi kiivyo,shaihidi zote zinaonesha polisi ndiop wauaji.Hana lolote,thubutu yake!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kutokana na habari ya saa mbili ya ITV, Kuwa Mheshimiwa Tendwa ambaye ni msajili wa vyama vya siasa nchini, amesema kuwa atakifuta chama cha siasa ambacho kitabainika kukiuka agizo pingamizi kutoka kwa polisi.....KIDUMU CHAMA CHA MAGAMBA.....
 
aifute cdm aone timbwili timbwili la asha ngedere. ni kama vile unipige teke kati kati ya miguu huo uchungu wake!
 
Atafutwa yeye kabla ya kukifuta hicho chama maana kitachomkuta atajuta....
 
MSAJILI WA VYAMA WAO, POLISI WAO ,MAHAKAMA WAO,TUME YA UCHAGUZI WAO,TUME ZA UCHUNGUZI WAO, SILAHA ZAO. refaree wao, wachezaji wao, malaizimeni wao, watangazaji wao, washangiliaji wao,watangazaji matokeo wao.CHADEMA INA KAZI KUBWA SANA
 
kwa akili walizonazo wanaweza kukifuta lakini hawataweza maana kina mizizi mikuu sana.
 
Wanajizungusha tu...!

Kauli hii ya Tendwa inakamilisha mzingo wa tulichokuwa tunakihisi toka mwanzo....

Ni hi hiki, wahujumu mikutano ya CDM, wafanye mauaji, waunde Tume feki ambayo mwishoni itakihukumu CDM then mpira utarudi kwa Tendwa, atakamilisha alichokisema....

Fumbo mfumbie mjinga mwenzio Tendwa, hapa JF tunawaangalia tu hadi mtakapo ingia kwenye kumi na nane.
 
nahisi tendwa anataka kuharakisha mageuzi nchini. asilogwe kulisema hilo tena kwana hasira za wananchi kwa police ni kubwa sana huku yeye na wapambe wake wakiwabeba tu.
 
Back
Top Bottom