Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,740
- 36,248
Hawa wapenda kiki dawa ni kuwapa kitumbo tu bila kujali jinsia zao
Walishapewa muda, kama unakumbuka mwaka 2016 TCU walifungia baadhi ya vyuo, vigezo vya kufungua vyuo ni muwe hata na PhD holder hata wawili kutegemea na ukubwa wa chuo.kwa hiyo kuwaweka ndani ndiyo wanafunzi watapata vyeti? issue ilikuwa kuwapa muda wahakikishe kila kitu kimekaa sawa
Kamatakamata ina raha yake kwa viongozi wa CCM.Vipi hawawezi wakawa assisted ili wapate hizo requirements ?
Sababu hizi kamata kamata mwisho wa siku tunakwenda kuwalisha kwa kodi zetu
Ukivunja sheria unafanywaje sasa?kwa hiyo kuwaweka ndani ndiyo wanafunzi watapata vyeti? issue ilikuwa kuwapa muda wahakikishe kila kitu kimekaa sawa
Hizo zipo chini ya NACTE na VETAWalishapewa muda, kama unakumbuka mwaka 2016 TCU walifungia baadhi ya vyuo, vigezo vya kufungua vyuo ni muwe hata na PhD holder hata wawili kutegemea na ukubwa wa chuo, sasa leo hii kuna watu wanafungua vyuo unakuta mtu anayesoma bachelor anafungundishwa na bachelor mwenzake au mtu mwenye mastaers, wapi na wapi? Siyo sahihi, chuo kinafundisha hakina vifaa, ni lazima chuo kijipange maana kinaelimisha watu wa Taifa la kesho.
Sheria no ngapi wamevunja?Ukivunja sheria unafanywaje sasa?
Hao Jamaa siasa uchwara za mitandaoni zimeharibu sana akili zao, inamaana wanataka nchi iongozwe kwa leissez fair leadership ambapo kwa 99.9% haikuwahi kuwa na matokeo chanya kimaendeleo.Ukivunja sheria unafanywaje sasa?
Kwani hakuna sheria? Bila shaka sheria zimeelekeza hatua za kuwachukulia. Haya mambo ya wakuu wa wilaya kuagiza watu wawekwe mahabusu ni ujinga. Tunakose sana tunapoangalia mambo kama haya kijuujuu bila kuchimba mizizi yake.Kama watu wanakosea unataka wafanywe nini? Wale wanafunzi baada ya kumaliza Chuo ina maana vyeti vyao havitatambulika na hawatapata ajira. Hili likiachwa na Serikali ikakaa kimya ni sawa na kuwapotezea muda wale vijana ambao wamewekeza muda wao na pesa zao kwa kitu ambacho hakina faida. Wezi ni wengi sana, ache ni tu Mhe DC Jokate asimamie majukumu yake.
Hawa mimi huwaita vinyamkera. Wapo kuongeza matumizi ya serikali tu na hawana msaada wowote kwenye maendeleo ya nchi. Matokeo yake wananchi ndiyo wanakamuliwa kwa kuongezewa tozo zisizo na maana yoyote.Hawa wapenda kiki dawa ni kuwapa kitumbo tu bila kujali jinsia zao
PhD holder ana msaada gani kwenye ujasiliamali wa kitaaluma? Tatizo mmeweka mkazo kwenye vyeti kama kwamba ndivyo vinavyotoa elimu. Kuna PhDs lundo nchi hii hawana kabisa msaada zaidi ya kutumia vile vyeti kama kitegauchumi wakati wanapwaya kwenye nafasi walizopewa kusimamia.Walishapewa muda, kama unakumbuka mwaka 2016 TCU walifungia baadhi ya vyuo, vigezo vya kufungua vyuo ni muwe hata na PhD holder hata wawili kutegemea na ukubwa wa chuo, sasa leo hii kuna watu wanafungua vyuo unakuta mtu anayesoma bachelor anafungundishwa na bachelor mwenzake au mtu mwenye mastaers, wapi na wapi? Siyo sahihi, chuo kinafundisha hakina vifaa, ni lazima chuo kijipange maana kinaelimisha watu wa Taifa la kesho.
Wewe ulitakiwa uwe kiongozi.Vipi hawawezi wakawa assisted ili wapate hizo requirements ?
Sababu hizi kamata kamata mwisho wa siku tunakwenda kuwalisha kwa kodi zetu
Serikali ilishatoa muda kwa vyuo kama hivi kwenda kujisajili na kufuata taratibu zote ila wamiliki hawakufuata taratibu. Shida inakuja pale wamiliki hawataki kujulikana ili wasilipe kodi na kwa sababu wanajua uwezo wao kuwa kujiendesha ni mdogo ndiyo wanaamua kujifichaficha sana, mwisho wa siku elimu wanayotoa inakuwa haitambuliki na inakuwa ni hasara kwa wahitimu hasa wanapoambiwa vyeti vyao havitambuliki.Viongozi wetu naona huwa wanapenda kukurupuka sana. Ukiona chuo, hospitali au shule binafsi inaendeshwa kimya kimya bila usajili ujue kwa asilimia mia kuwa mamlaka za udhibiti zinawakwamisha mahali fulani ili Serikali isipate halali yake bila watendaji kupata chochote.
Cha kufanya siyo kukifungia chuo,bali ni kukirasimisha kwanza na kukiwezesha kufanya kazi maana kina wanafunzi tayari... Kisha kuchunguza chanzo cha kufanya shughuli zake bila vibali, uhalali na stahili ya vyeti vya kitaaluma. Baada ya kujiridhisha chanzo cha mtafaruku ndio adhabu itolewe kwa anayestahili.
Hata wewe unatakiwa uwe kiongoziWewe ulitakiwa uwe kiongozi.
Mungu akubariki.
Wanawekwa ndani kisha wanachukuliwa dhamana...faili linapelekwa kwa mwanasheria mkuu in a one kana mashtaka hayakidhi kupelekwa mahakamani kesi inamalizwa juu kwa ju...uhasama mpya unazaliwaMkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. JOKATE MWEGELO Aagiza Kuwekwa Chini ya Ulinzi Mkali Viongozi wa Chuo cha LUBANDO TRAINING COLLEGE
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ameagiza kuwekwa chini ya ulinzi kwa Viongozi wa Chuo cha Lubando Training College kilichopo Mtaa wa Butiama, Kata ya Mtoni Kijichi baada ya kubaini Chuo hicho kinaendeshwa kinyume cha Sheria.
DC Jokate ametoa agizo hilo wakati alipoungana na Wataalamu katika ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ambapo aliambatana pia na Mkurugenzi-Uthibiti, Ufuatiliaji na Tathmini kutoka NACTE Dkt. Joefrey Oleke.
Baada ya kufanya mahojiano na Mkuu wa Chuo hicho, DC Jokate alibaini kuwa kwa muda sasa Chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo bila kupata usajili, pamoja na kutoa mafunzo kwenye mazingira yasiyo rasmi .
"Hamna kitu kibaya kama kufanya utapeli halafu ukadhani hutagundulika, Serikali ina macho kila sehemu, NACTE kaeni hapa na Polisi, lazima tupate 'information', Chuo hakijasajiliwa lakini hata mandhari yake haistahili, kuna Watu wanatoa huduma ambazo kiuhalisia hawastahili kutoa, tushirikiane katika ufuatiliaji, hawa wachukuliwe hatua kali huu ni utapeli"———-DC Jokate
Kwa upande wake Dkt. Jofrey Oleke amesitisha shughuli zote zinazoendelea katika chuo hicho, huku akielekeza taratibu nyingine za kisheria kufuatwa huku akisema kwa ukaguzi uliofanyika, chuo hicho hakitambuliki NACTE wala VETA.
View attachment 1919666
Hayo yote unayoyasema yalishafanywa na kutolewa maelekezo, sema wabongo ni wagumu kutii sheria na kufuata utaratibu uliowekwa na Mamlaka zao. Serikali kwa upande wake ilishajitahidi kuweka utaratibu wa kumiliki taasisi za Elimu binafsi. DC JOKATE amefanya kwa mujibu wa Sheria.Viongozi wetu naona huwa wanapenda kukurupuka sana. Ukiona chuo, hospitali au shule binafsi inaendeshwa kimya kimya bila usajili ujue kwa asilimia mia kuwa mamlaka za udhibiti zinawakwamisha mahali fulani ili Serikali isipate halali yake bila watendaji kupata chochote.
Cha kufanya siyo kukifungia chuo,bali ni kukirasimisha kwanza na kukiwezesha kufanya kazi maana kina wanafunzi tayari... Kisha kuchunguza chanzo cha kufanya shughuli zake bila vibali, uhalali na stahili ya vyeti vya kitaaluma. Baada ya kujiridhisha chanzo cha mtafaruku ndio adhabu itolewe kwa anayestahili.
Mh.Jokate yuko sahihi....Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. JOKATE MWEGELO Aagiza Kuwekwa Chini ya Ulinzi Mkali Viongozi wa Chuo cha LUBANDO TRAINING COLLEGE