Miaka 20 ya Maranatha: DC Jokate ashiriki ibada, aomba viongozi wa dini kuombea serikali

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
MIAKA 20 YA MARANATHA DC JOKATE ASHIRIKI IBADA, AOMBA VIONGOZI WA DINI KUOMBEA SERIKALI.

Na Miko Luoga Tanga

Mkuu wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Jokate Mwegelo amewaomba viongozi wa dini na waumini wilayani humo kuwaombea viongozi wa serikali na ardhi ya Tanzania ili Taifa liendelee kuwa salama.

Jokate amesema hayo leo jumapili aprili 16, 2023 katika ibada ya shukurani ya kutimiza muda wa miaka 20 ya huduma ya kwaya ya Maranatha iliyofanyika kwenye Kanisa Anglikana mtakatifu Andrea Manundu Korogwe.
Katika Ibada hiyo iliyoambatana na kuchangia mfuko wa kununua gari ya kwaya hiyo Jokate alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba na kutoa salamu za serikali kwa niaba yake.

Aidha amewaeleza waimbaji wa kwaya hiyo na waumini walioshiriki kuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri kindamba ameahidi kuchangia mfuko huo kiasi cha shilingi milioni tano nae akiahidi kuunga mkono zoezi hilo kiasi cha shilingi milioni tatu.

Hatahivyo Kanisa Anglikana Mtakatifu Andrea Korogwe limefanya ibada maalumu ya kumuombea mkuu wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake.

Kasisi Canon Dominic Singano kutoka Kanisa Anglikana mtakatifu Andrea Magomeni Dar es Salaam amewatia moyo wa matumaini waumini na waimbaji kuwa wakiungana zoezi la ununuzi wa gari hilo litakamilika kwa wakati ili injili ya Kristo ihubiriwe kote nchini.

Kwa upande wake Kasisi kiongozi wa mtaa wa Mtakatifu Andrea Manundu Korogwe Canon Aidan Kamote amesema waumini wa Kanisa hilo wameendelea kuunga mkono matukio yote ya kwaya zinazohudumu kanisani hapo ili ziweze kutimiza malengo husika.

Zoezi la kuchangia mfuko wa ununuzi wa Gari la Kwaya ya Maranatha jumla ya fedha taslimu za kitanzania kiasi cha milioni nne la laki tano 4,500,000 zimepatikana na ahadi zikiwa milioni 17,400,000 milioni kumi na saba na laki nne hata hivyo zoezi hilo ni endelevu ili kufikia lengo la kukusanya milioni sabini.

Niwaombee viongozi, mi nateseka hivi, eti wawe salama ili wafanye ubadhirifu kama alivyoainisha CAG,waaapi, siwezi. Na mbaya zaidi hawanipi hata ajira na vigezo ninavyo, nà kinachokera nilihitimu 2016, na Kiingereza nimesoma, lakini wanakuja kuajiri wa 2020, 2021 na 2022, waaapi, mi siwezi kuwaombea.
 
Yesu mwenyewe alisema jililieni wenyewe na watoto zenu, unaanzaje kuwalilia wazee wa mavi8! hata mimi sina upuuzi huo, hivi kwanza bado wanamatumaini kuwa wataionja pepo! Labda pepopunda…
 
MIAKA 20 YA MARANATHA DC JOKATE ASHIRIKI IBADA, AOMBA VIONGOZI WA DINI KUOMBEA SERIKALI.

Na Miko Luoga Tanga

Mkuu wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Jokate Mwegelo amewaomba viongozi wa dini na waumini wilayani humo kuwaombea viongozi wa serikali na ardhi ya Tanzania ili Taifa liendelee kuwa salama.

Jokate amesema hayo leo jumapili aprili 16, 2023 katika ibada ya shukurani ya kutimiza muda wa miaka 20 ya huduma ya kwaya ya Maranatha iliyofanyika kwenye Kanisa Anglikana mtakatifu Andrea Manundu Korogwe.
Katika Ibada hiyo iliyoambatana na kuchangia mfuko wa kununua gari ya kwaya hiyo Jokate alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba na kutoa salamu za serikali kwa niaba yake.

Aidha amewaeleza waimbaji wa kwaya hiyo na waumini walioshiriki kuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri kindamba ameahidi kuchangia mfuko huo kiasi cha shilingi milioni tano nae akiahidi kuunga mkono zoezi hilo kiasi cha shilingi milioni tatu.

Hatahivyo Kanisa Anglikana Mtakatifu Andrea Korogwe limefanya ibada maalumu ya kumuombea mkuu wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake.

Kasisi Canon Dominic Singano kutoka Kanisa Anglikana mtakatifu Andrea Magomeni Dar es Salaam amewatia moyo wa matumaini waumini na waimbaji kuwa wakiungana zoezi la ununuzi wa gari hilo litakamilika kwa wakati ili injili ya Kristo ihubiriwe kote nchini.

Kwa upande wake Kasisi kiongozi wa mtaa wa Mtakatifu Andrea Manundu Korogwe Canon Aidan Kamote amesema waumini wa Kanisa hilo wameendelea kuunga mkono matukio yote ya kwaya zinazohudumu kanisani hapo ili ziweze kutimiza malengo husika.

Zoezi la kuchangia mfuko wa ununuzi wa Gari la Kwaya ya Maranatha jumla ya fedha taslimu za kitanzania kiasi cha milioni nne la laki tano 4,500,000 zimepatikana na ahadi zikiwa milioni 17,400,000 milioni kumi na saba na laki nne hata hivyo zoezi hilo ni endelevu ili kufikia lengo la kukusanya milioni sabini.

Mbagala tunamshukuru mama kwa kututua ndoo, alianza kuivuruga Mbagala kwa uroho wa pesa.
Ni vizuri zaidi kama ataiombea yeye ili tusimchanganye Mungu.
 
Back
Top Bottom