Mkuu wa Wilaya Jokate awataka wahandisi wa maji kutatua changamoto za maji Korogwe

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
DC JOKATE AWATAKA WAHANDISI WA MAJI KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAJI KOROGWE

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe Jokate Mwegelo amewataka Wahandisi wa Maji Wilayani Korogwe kutatua changamoto za maji zilizopo ndani ya uwezo wa mamlaka hiyo.

Akizungumza kwenye kikao Cha Taftishi kuhusu ombi la kurekebisha bei za huduma za majisafi za mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira - Mombo, kilichofanyika,Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.

"Tutafanya kikao na Wahandisi wa maji wote wa Wilaya ya Korogwe lakini kabla ya hicho kikao kama kuna changamoto yoyote iliyopo ndani ya mamlaka wawe wamezitatua" amesema DC. Jokate.

Aidha Mh.Jokate amesema katika kikao hicho atapenda kupokea taarifaya za hatua mbalimbali zilizochukuliwa na mamlaka katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama.

"Tukikutana kwenye kikao sitapenda blaablaa, nitaenda kupokea taarifa za utatuzi wa changamoto za upatikanaji wa maji".

Amesema kuwa Wahandisi na wote wenye mamlaka wasiwe sehemu ya kukwamisha wananchi kupata huduma wanazostahili kuzipata kutoka kwenye serikali yao.

Sambamba na Hilo Mhe. Jokate ametoa rai kwa wananchi pamoja na viongozi kushirikiana katika kutunza vyanzo vya maji, kwani maji ni uhai na ni muhimu kwenye Maisha ya mwandamu.

Kikao hicho kimefanyika baada ya mamlaka ya maji Mombo kupeleka maombi EWURA ya kuongezewa bei ya huduma ya maji, ambapo yalifanyika mabadiliko kwa mara ya mwisho mwaka 2011.

#KorongweMpya

 
Back
Top Bottom