Jokate Mwegelo ateuliwa kuwa kati ya Vijana watakaowakilisha ndani ya Mtandao wa Kimataifa wa Vijana unaochagiza maamuzi makubwa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Jokate urban Mwegelo @jokatemwegelo ameteuliwa kuwa mmoja kati ya Vijana wachache mahiri watakaowakilisha ndani ya Mtandao wa Kimataifa wa Vijana unaochagiza maamuzi makubwa ulioko chini ya Club de Madrid.

Club de Madrid ni jukwa kubwa Duniani linalounganisha pamoja Marais na Mawaziri Wakuu Wastaafu pamoja na Viongozi wengine mashuhuri kutoka kona zote za Dunia na kutumia uzoefu wao mkubwa ndani ya uongozi kustawisha demokrasia na ustawi wa Watu na maendeleo kiujumla.

Club de Madrid ni chombo cha kimataifa kisichofungamana kisiasa wala kisichotengeneza faida, chombo hichi kinatumia uzoefu na ushawishi mkubwa wa Wanachama wake wasiopungua 100 kutoka Nchi zaidi ya 70 kushawishi maboresho endelevu ya sera na kupata Uongozi makini na mahiri katika kuendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali katika nyanja za Kitaifa na Kimataifa.

Katika hatua nyingine, DC Jokate, ametuliwa pia kuwa Rais wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Jukwaa la Viongozi Wanawake Afrika(Africa Women’s Movement-AWM) akiwa na jukumu kubwa la kuhakikisha Ukanda wa Afrika Mashariki unaendelea kupika na kutengeneza Viongozi Wanawake wengi zaidi katika kuchangia maendeleo endelevu na ustawi wa Mataifa yetu.
 
Kama Jokate ndio simple ya wanawake wadogo ambao wanachipukia kiuongozi then we are in for a big fall.
 
Ni kama dogo janja mwaka ule?
Makonda anasemaje?
 
Back
Top Bottom